WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK. KIGWANGALA WARIPOTI WIZARANI LEO

WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK. KIGWANGALA WARIPOTI WIZARANI LEO

December 12, 2015
IMG_8317
Gari la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu likiwasili Makao Makuu ya wizara hiyo na kupokelewa kwa saluti mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_8321
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando mara tu baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.
IMG_8324
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) kuelekea ofisini kwake.
IMG_8325
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8329
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akishuhudia tukio hilo.
IMG_8346
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika wizara ya hiyo moja kwa moja akitokea Ikulu baada ya kula kiapo.
IMG_8347
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8350
IMG_8354
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimkaribisha Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwake.
IMG_8356
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8359
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8374
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja.

Updates za dada Joyce Richard Mwambepo wa mbeya aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuvunjika miguu ajalini

December 12, 2015
Ankal akiwa wodini kumtembelea dada Joyce 
 Dada Joyce alipowasili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita

Dada Joyce akiwa wodini MOI

Ndugu Wasamaria Wema,
Tunapenda kutumia fursa hii kuwashirikisha tena habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Rishard Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo dereva hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo pamoja na pesa  za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa pesa  za vipimo na matibabu.
Hadi  Msamaria mwema na Mpiganaji Deo Kakuru anakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
Hivyo Deo Kakuru, kwa msaada mkuwa wa michango ya Wasamaria Wema,  amefanikiwa kumsafirisha dada Joyce kwa Fast Jet kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya  hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI jijini Dar es salaam ambako alipokelewa na kulazwa katika jengo jipya liitwalo Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu wodi namba 2.
--------------------------------------
UPDATES:
Baada ya Deo Kakuru kuweka mitandano tatizo la dad Joyce, Wasamaria Wema kadhaa wakajitokeza kumsaidia.  Hatuna uhakika kwamba wote wangependa majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).

Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zilikusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa. KUTOA NI MOYO.

Aidha, kwa kiasi kilichopatikana tayari dada Joyce ameshafanyiwa vipimo vya MRI  Alhamisi  iliyopita na hivi sasa yanasubiriwa majibu siku ya Jumatatu ambapo baadaye Jopo la Madaktari Bingwa litaka na kuamua nini kifanyike kimatibabu. Tunashukuru madaktari na watumishi wote wa MOI kwa kuhitimisha hilo, nasi tunaendelea kuwaomba waendelee na huduma hiyo hadi dada Joyce atapopata matibabu.
Vile vile tunamshukuru sana Msamaria Mwema Mama Rozi aliyejitolea kumhudumia dada Joyce pale wodini ambako mama yake mzazi amelazwa na ana matatizo karibu sawa na ya dada yetu. Bila kuchoka mama Rozi amekuwa akimletea chakula na vinywaji dada Joyce kila siku na kumfanyia huduma za usafi kila siku. Ubarikiwe sana Mama Rozi.
Shukurani pia ziwaendee wasamaria wema wengine pamoja na wadau ambao baada ya kuguswa na matatizo ya dada Joyce wamekuwa wakimtembelea hapo wodini na kumfariji. Asanteni sana.

Wito wetu tunaomba tuendelee kumsaidia kwa hali na mali dada Joyce kwani mara baada ya majibu ya vipimo yatapotoka Jumatatu, ni dhahiri kutakuwa na mahitaji zaidi katika matibabu yake. 

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal anaendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Mratibu mwenza Deo Kakuru naye anaendelea kusaidia kwa kumtunza bibi yake Joyce na mwanae mwenye umri wa miaka 4 huko Mbeya.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema



Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri wanyakua Tuzo mbalimbali

December 12, 2015


 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrisa Mshoro akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa nne aliyefanya vizuri katika masomo yake kwa mwaka 2014/2015  wakati wa leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya Taaluma wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Gabriel Kassenga akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo kwa wahitimu wa chuo hicho waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, wawakilishi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali waliochangia tuzo mbalimbali na Wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi ya utoaji wa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri waendelea kupokea tuzo zao. Takribani wanafunzi 126 wamepata Tuzo na zawadi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kike 61 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
 Wanafunzi na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
 Mwanafunzi Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi ( Geomatics) Bi. Lilian Kato akipokea zawadi yake ya mashine ya kupimia Ardhi (Total Station) yenye thamani ya shilingi milioni 15 aliyozawadiwa na Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike wa mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015.
 Mwanafunzi wa mwaka wa 4 wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Bi. Beatrice Kaijage akipokea zawadi yake kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya High Tech System ya jijini Dar es salaam.
 Mwanafunzi Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi ( Geomatics) Bi. Lilian Kato akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna atakavyonufaika na  mashine ya kupimia Ardhi (Total Station) aina ya Stonex aliyozawadiwa na Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike wa mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015.
 Viongozi wa Wakuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho, viongozi wa taasisi na Makampuni mbalimbali mara baada ya hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Viongozi wa Wakuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hicho waliofanya vizuri kwa mwaka 2014/2015 , wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho, viongozi wa taasisi na Makampuni mbalimbali mara baada ya hafla ya utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.

EDITH EMILY MUDOGO, DIWANI KATA YA NYEGEZI JIJINI MWANZA NI KAZI TU.

December 12, 2015
Diwani wa Kata ya Nyegezi Jijini Mwanza kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Edith Emily Mudogo akiapa jana ili kuwatumikia wananchi wa Kata hiyo katika kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halmshauri ya Jiji la Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group (BMG)
Mudogo ni miongoni mwa Madiwani wachapa kazi ambao wanaendana na Kauli Mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya "HAPA KAZI TU" hii ikiwa ni kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka.
Kulia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza akisimamia zoezi la uapishaji Jijini Mwanza.
Madiwani wa Jiji la Mwanza wakiapa kuwatumikia wananchi
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza akiwemo diwani wa Kata ya Nyegezi (CCM) Edith Emily Mudogo.
Diwani wa Kata ya Nyegezi (CCM) Edith Emily Mudogo baada ya kuapishwa jana. Yeye kwake ni Kazi Tu.
Wananchi na wageni viongozi mbalimbali wakifuatilia kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Kwa Picha Zaidi BONYEZA HAPA

BANDARI YA TANGA YAZINDUA MATISHARI MATATU MAPYA KURAHISISHA UFANISI WA KAZI

December 12, 2015
Waandishi wa Habari mkoani Tanga wakiangalia matishari matatu mapya



Sehemu ya Matishari hayo yakiwa bandari ya Tanga jana








wa pili kutoka kushoito ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani Tanga matishari mapya matatu wakati wa uzinduzi wake.













wa pili kushoto ni ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani Tanga matishari mapya matatu wakati wa uzinduzi wake wa kwanza kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga,Bi Moni Msemo.