RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA KUSHUHUDIA PEMBE ZA NDOVU 50 ZILIZOKAMATWA

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA KUSHUHUDIA PEMBE ZA NDOVU 50 ZILIZOKAMATWA

October 29, 2016
j1  j3 j5
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya
kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
j2
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya  ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
WANASHINYANGA WAOMBA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MKAA RAFIKI KWA MAZINGIRA KATIKA SIKU YA USAFI KITAIFA

WANASHINYANGA WAOMBA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MKAA RAFIKI KWA MAZINGIRA KATIKA SIKU YA USAFI KITAIFA

October 29, 2016
z1
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiru,  na Bwana Daniel Sagata Pamoja wakijiandaa kuanza zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Binzatana Mjini Shinyanga mapema leo.
z2
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luahaga Mpina akishiriki katika zoezi la kupanda miti Mjini Shinyanga leo.
z3
Viongozi pamoja na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga katka zoezi la usafi wa mazingira mjini Shinyanga leo.
z4
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiongea na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyaga katika eneo la Binzanata baada ya kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira na kupanda miti mapema leo.
z5
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Shinyanga wakishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira leo, Mjini Shinyanga.
………………………………………..
EVELYN MKOKOI SHINYANGA
Uongozi wa mkoa wa Shinyanga kupitia Mkuu wa Wilaya yake Bi Josephine Matiru umeiomba serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Kujenga kiwanda kitakacho tengeneza mkaa utokanao na mabaki ya miti ambao ni rafiki kwa mazingira ili kunusuru hali ya mkoa huo kuendelea kuwa jangwa kutokana na ukataji miti ovyo kwa matumizi ya makaa manyumbani, matumizi mengine na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu wa wilaya hiyo ametoa ombi hilo leo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliposhiriki siku ya usafi kitaifa ya mwisho wa mwezi October ambapo zoezi hilo lilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania December Mwaka jana na kuendelea kutekelezwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kama siku maalum ya usafi nchini.
Bi Materu aliendelea kusema kuwa, Mkoa wa shinyanga unakumbana na changamoto kubwa ya ukataji miti ovyo ambayo ingeweza kukabiliwa kwa kutumia mabaki ya miti, taka na maranda ya mbao kutengeneza mkaa rafiki kwa mazingira na kusema kuwa mkoa na wilaya ya shinyanga imebarikiwa kuwa na miti ya aina mbali mbali ambazo mazingira yangetunzwa vizuri na kutumia malighafi hiyo ya taka kutengeneza mkaa banifu akitolea mfano kiwanda cha kutengeneza mkaa rafiki wa mazingira cha Zanzibar.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina alikiri kupokea maombi ya mkuu wa wilaya huyo na kueleza kuwa serikali itakuwa tayari kujenga kiwanda cha kutengeneza mkaa mjini shinyanga “Na pengine katika Mbio za Mwenge Mwakani tukijaaliwa tunaweza kuzindua kiwanda hicho kama mradi wa mfano.” Alisisitiza Mpina.  “Lazima tuwe na viwanda vya mkaa rafiki kwa mazingira sasa na wafanya biashara wa gas za manyumbani sasa ufike wakati nao washushe bei ili asilimia kubwa ya watanzania waweze kutumia nishati hiyo.” Alifafanua Mpina.
Akizungumzia suala ya usafi wa Mazingira ambapo sambaba na hilo Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki zoezi la upandaji miti katika eneoa la Binzamata, alisema kuwa  watanzania wana kila sababu ya kujijengea utamaduni wa usafi wao pamoja na mazingira kwani hata vitabu vitakatifu vinasisitiza usafi wa mazingira akitolea mfano kitabu cha Biblia takatifu cha kumbu kumbu la Torati 23:11-14 na kusema kuwa “Pahala Pachafu hapana Utukufu wa Mungu na hauwezi kuonekana mahali hapo na haya siyo maneno yangu wala ya Rais Magufuli, ni maneno ya biblia hivyo watendaji katika ngazi zote mzingatie utekelezaji wa sheria yya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake na kuwachulia hatua wale wote watakao kiuka sheria hiyo.”
“Ni jukumu la kila mtu kufAnya usafi na kila wilaya na Halmashauri ijetengenezee mwongozo na sheria ndogo ndogo katika eneo hili la usafi wa mazingira na lazima watu wawajibike.”
Naibu Waziri Mpina Pia alisisitiza zoezi la upandaji miti ili kuweza kukabiliana na athari zitokanazo na Mabadiliko ya tabia nchi na kurudisha uoto wa asili.
Akitolea mfano wa kasi ya serikali ya awamu ya tano katika zoezi la usafi wa mazingira Mpina alisema “ watu walidhani Mhe. Rais alivyozindua siku ya usafi zilikuwa ni nguvu za soda, kasi tuliyonza nayo ndiyo tutakayo maliza nayo, waharibifu wa mazingira lazima sheria iwashughulikie.” Alisisitiza Mpina.
Akizungumzia wananchi wanaoabudu siku ya Jumamosi Mpina alisema Sheria ndogo ndogo za mazingira za Halmashauri na miji ni vizuri zikaona namna ya kuweza kuwapa nafasi na wao ya kuabudu na kushiriki usafi katika siku hiyo.
Siku ya kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi  imetengwa na serikali ikiwa ni maalum kwa ajili ya usafi nchini.

TAFRIJA MCHAPALO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA SERENGETI PREMIUM LAGER YAFANA

October 29, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akitoa hotuba ya  ufunguzi kwa wageni waliohudhuria tafrija mchapalo ya maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996.Pia kulizinduliwa chapa mpya ya Bia hiyo  .hafla hiyo ilifanyika siku ya alhamisi  katikaHOTELI ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara  Na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage (Mb) akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria hafla ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti premium lager .Hafla ilifanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu akitoa hotuba yake katika hafla ya kutimiza miaka 20 ya Bia ya Serengeti Premium Lager na pia kuzinduliwa kwa muonekano mupyaa wa bia hiyo mapema siku ya alhamisi.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifurahia jambo
Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie (katikati) akijadiliana jambo na Mkurungezi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyacha na Mkurungezi wa Masoko wa SBL Ceasar Mloka katka tafrija mchapalo ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti Premium Lager 
Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi akitoa ufafanuzi wa safari ya bia ya serengeti premium lager toka ilipoanzishwa miaka 20 iliyopita ikiwa ni ubunifu wa mtanzania Winston Kagusa 
Burudani maridadi ikiendelea wakati wa tafrija hiyo

Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara  Na Uwekezaji, Mh. Chrles Mwijage (Mb) (wa kwanza kushoto )akifurahia muonekano mpya wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya uzinduizi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu (katikati ) na  Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Baadh ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakiifuatilia kwa makini uzinduizi wa muoenkano mupyaa wa Serengeti Premium Lager 
Wadau wakipozi katika picha ya chui ambayo ni nembo ya bia ya serengeti

Wadau wakifurahia muonekano mpya wa bia ya Serengeti Premium lager


Wageni waalikwa wakifurahia burudani iiliyotolewa katika hafla ya  maadhimisho ya miaka 20 ya Bia ya Serengeti na pia uzinduzi rasmi wa muoenekano mpya wa bia hiyo .Hafla hiyo iliyofanyika  katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
UKAGUZI WA MAZINGIRA UFANYIKE KATIKA KAMBI YA NYARUGUSU – MAKAMBA

UKAGUZI WA MAZINGIRA UFANYIKE KATIKA KAMBI YA NYARUGUSU – MAKAMBA

October 29, 2016
m1
Mbunge wa Kasulu vijijini Mhe Augustine Vuma (Kushoto)  akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba  wakati viongozi hao walipotembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.  (Katikati ni Bw. Peter Bulugu Kaimu Mkuu wa Kambi – Nyarugusu
m4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba  akihutubia katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kagera Nkanda, Wilayani Kasulu
m2
Sehemu ya wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara baada ya kutembelea kutembelea kambi ya Nyarugusu na kutoa maelezo katika sekta ya mazingira
m3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba  akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi wakikagua uharibifu wa mazingira katika msitu wa Makere katika Wilaya ya Kasulu
…………………………………..
Na Lulu Mussa
Kasulu
Imebainika kuwa ongezeko kubwa la idadi ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu inachangia kwa kiasi kubwa la uharibifu wa mazingira kwa kuongeza matumizi ya rasilimali za asili.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa  Kambi ya Nyarugusu Bw. Peter Bulugu wakati wa kuwasilisha taarifa ya hali mazingira katika kambi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
Kaimu Mkuu wa  Kambi wa Nyarugusu Bw. Peter Bulugu amesema kuwa hali ya mazingira katika kambi si nzuri na inakabiliwa na tatizo la uharibufu wa mazingira kwakuwa wengi wa wakimbizi hao hutumia kuni kama nishati ya kupikia.
Hata hivyo Bw. Bulugu amebainisha kuwa Ofisi yake imeeanda mkakati wa upandaji miti ili kunusuru maeneo yanayozunguka, na kwakuanzia jumla ya miche 900,000 imeoteshwa katika vitalu. Pia Kambi imedhamiria kugawa majiko banifu ambayo yatatumia nishati kidogo na uzalishaji wa nishati kwa kutumia takataka za mashambani unatarajiwa kuanza mwezi Novemba.
Aidha, mkakati mwingine ni ujenzi wa nyumba za tofali mbichi na kuezeka kwa mabati badala ya miti ambapo jumla ya nyumba 800 zimekamilika na nyumba 542 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi. Alisema Bw. Bulugu
Akiwa katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Waziri Makamba ametembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kupata fursa ya kuongea na wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi hiyo.
Waziri Makamba amesema kuwa ni vema uongozi na mashirika yanayotoa misaada katika kambi hiyo kuandaa mpango mzuri wa namna ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi ili ujio wao usiathiri watanzania wanaozunguka kambi ili shughuli zao za uzalishaji mali kila siku ziwe na tija.
Waziri Makamba aliuagiza Ungozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi kutafuta pesa zaidi ili mpango wa kugawa majiko banifu uwafikie wakimbizi wote. “Kaya zilizopo hapa ni 30,000 ninyi mnataka kugawa majiko hayo kwa kaya 3000 tu, nashauri muangalie uwezekano wa kugawa kwa kaya zote” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba pia ameagiza kufanyika kwa Ukaguzi wa Mazingira (Environment Audit) ndani ya wiki mbili kwakuwa ni takwa la kisheria. Na kuwataka na kupanda miti kwa wingi. ” Pandeni miti ya aina mbalimbali mfao miti ya matunda, kuni na mbao ili kunusuru mazingira yetu”.
Waziri Makamba pia alitembelea msitu wa Makere wenye takriban ekari 75,000 ambao kwa upande wa Makere kusini kumekuwa na uharibufu mkubwa wa mazingira na kuagiza doria za mara kwa mara ili kudhibiti wananchi wanaofanya kilimo cha kuhamahama, kukata na kuchoma miti pia kudhibiti ongezeko la mifugo kwa kuiandikisha ili mgogoro uliopo baina ya hifadhi na wananchi uweze kupatiwa ufumbuzi kwa kujenga hoja madhubuti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameendelea na ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Mikoa 10 hapa nchini ambapo leo ni siku ya 13. Waziri Makamba pia atatembelea Mkoa wa Tabora.

DC MTATURU: IKUNGI MARATHON KUFANYIKA KILA MWAKA

October 29, 2016

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kulia akisistiza jambo wakati akizungumza na washiriki wa Ikungi Half Marathon kulia kwake ni MathiasCanal Mwandishi wa Habari wa mtandao wa Www.wazo-huru.blogspot.com
Afisa Michezo Wilaya ya Ikungi Aboubakary Kisuda akizungumza na awashiriki wa Ikungi Half Marathon kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Na Mathias Canal, Singida 

Mashindano ya kuibua vipaji vya wafukuza upepo kwa mbio ndefu Ikungi Half Marathon yanayotaraji kufika ukomo jumamosi hii Octoba 29, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano hayo.

Vijana takribani 60 shupavu waliochomoza kwenye mchujo wa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa  wataingia barabarani kuisaka ama heshima ya ushindi au ushiriki kwa ngazi ya Wilaya huku wengine waliokosa nafasi katika awamu hii kusubiri awamu ijayo katika mashindano ya Full Marathon yatakayofanyika Mwaka 2017.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na washiriki wote wa mbio hizo ambapo amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi jambo ambalo linaonyesha kuwa mchezo huo una wahitaji wengi.

Mtaturu amesema kuwa mashindano haya ya Ikungi Half Marathon yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa endelevu ambapo mwakani yatafanyika pia mashindano yam bio ndefu yatakayojulikana kama Ikungi Marathon 2017.

Dc Mtaturu alisema kuwa Dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hii kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yanatarajiwa kufanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 400 na mita 800.

Mashindano haya yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Octoba Mosi yalifanyika kwa ngazi ya Kata, ambapo mchujo wa ngazi ya Tarafa imemalizika Octoba 15, 2016 na hatimaye kupisha mchuano wa Kiwilaya.

Mashindano haya yatatoa fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao wa kucheza na miguu kwa kasi ya ushindani kwa maana ya manufaa ya pesa lakini pia itaimarisha ajira kupitia chama cha Riadha mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla lakini pia kuwaondoa vijana wengi katika mawazo ovu ya kushinda vijiweni badala yake kujitokeza kwa ajili ya kujihusisha na Kilimo pamoja na ufugaji.
Dc Mtaturu amewasihi washiriki wote kukimbia kwa kutumia muda mzuri ili iwe taswira ya rekodi nzuri katika ukimbiaji jambo litakalokifanya chama cha cha Riadha Taifa kuchagua vipaji vitakavyoendelezwa.

Vijana wasomi 53 wafyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni na nyumba za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani

October 29, 2016
 Vijana wasomi 53 wa grupu la Whatsapp la WAZALENDO wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 
Leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
 Mmoja wa vijana hao wasomi akielekea kazini
  Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akielekeza vijana sehemu ya kuweka matofali 
 Kazi ikiendelea
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akiwa katika picha ya pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akipungia pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akitoa maelekezo kwa vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini ambako kuna uhaba wa nafasi kiasi cha kurundikana namna hiyo
 Huko jikoni msosi unaandaliwa
 Wanafunzi wa shule hiyo wakijipanga kupata chakula cha mchana
 Wanafunzi wanapata chakula na matunda kila mlo
 Mojawapo ya nyumba chache za walimu ambamo wanakaa walimu saba
 Walimu sita kati ya saba wanaoishi kwenye nyumba hiyo
 Nishati mbadala ya solar itumiwayo na walimu hao saba
 Wanafunzi wakipata mlo wa mchana
 Vijana wasomi wanawake wanalala hapa 
 Sehemu ya vijana hao 14 wanawake wakipumzika baada ya kazi nzito
 Pamoja na kufyatua matofali baadhi ya vijana hao wasomi ambao ni walimu walikuwa wakiingia darasani kufundisha. Hapa mwalimu akiandaa kipindi baada ya kufyatua matofali
 Mwalimu akiandaa kipindi
 Sehemu ya vijana hao
 Jiwe la msingi
 Nje ya darasa
 Mandhari ya sehemu ya shule hiyo
 Bweni la vijana wasomi wanaume
 Pamoja na kazi nzito ya kufyatua matofali vijana hawa wazalendo wana nyuso za furaha na kuridhika kwa kujitolea kwao
 "....HAPA KAZI TU!" anasema kijana huyu mzalendo
 Furaha ya kumaliza kazi kwa mafanikio
 Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
 Furaha ya ushindi
 Utamu wa uzalendo ni kufanya kazi na kufurahi kwa pamoja
 Vijana mapumzikoni




  Jengo la darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
  Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
  Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Bweni kwa ajili ya wanafunzi ndani ya darasa la maabara
 Kila sehemu ya stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Hayo matofali ni alama ya kuwa upande huo wa mbele ni wa Msikiti kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Kiislamu. Wakristo na waumini wa madhehebu mengine hutumia madarasa
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakielekea bwenini
 Baada ya kazi na msosi sasa ni wakati wa kuimba wimbo wa kambi
 Wimbo wa kambi ukiimbwa na kuchezwa kwa furaha
 Kijana akishukuru kwa kuhitimishwa kwa kazi hiyo
 Mmoja wa vijana hao akishukuru Mungu kwa kumaliza kazi salama

 Sehemu ya vijana hao
 Vijana wakiwa katika kikao kidogo cha kuhitimisha kazi
  Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) akisema machache. Yeye alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
 Baada ya kazi nzito Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akijiunga kupata msosi na  vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Vijana hao wasomi 53 wakipata msosi baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.