POLISI TANGA YAJIPANGA UCHAGUZI JUMAPILI

October 23, 2015

Tanga, JESHI la Polisi Mkoani Tanga limesema limejiandaa kukabiliana na makundi ambayo yataonyesha kufanya fujo siku ya uchaguzi kesho na kuwataka wananchi kupiga kura na kuendelea na majukumu yao ya kujiletea maendeleo.
Akizungumz ana waandishi wa habari (leo) , kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, aliwataka wananchi kupiga kura na kurejea maeneo yao ya kazi na kudai kuwa yoyote ambaye atakiuka sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema polisi itakuwa makini na kikundi au mtu yoyote ambaye atafanya fujo na hivyo kuwataka wananchi kutekeleza haki zao za kisheria za kupiga kura na kuwataka kufuata sheria.
“Ndugu waandishi wa habari kupitia kwenu naomba kuwaomba wanachi kutumia haki yao ya kuchagua kiongozi wanaemtaka kwa amani na utulivu kama uliopo----yoyote ambaye atakiuka sheria tutamchukulia sheria” alisema Mombeji na kuongeza
“Nendeni katika vituo vya kupigia kura na kasha rejeeni katika majukumu yaenu ya kujiletea maendeleo----musiwe na wasiwasi kama eti kutatokea fujo kwa kweli tumejipanga na kujidhatiti kwa atakaeleta fujo” alisema

Kamanda Mombeji aliwataka wananchi kuepuka mikusanyiko ya watu wengi kwani siku hiyo hawataruhusu mikusanyiko na hivyo kutakuwa na doria kila pembe na mitaa.
Alisema mikusanyiko yoyote polisi itaichukulia kama ni haramu hivyo ili kuweza kuepuka ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anapiga kura na kwenda katika sehemu yake ya kazi ama kurejea majumbani.

 Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji akizungumz ana waandishi wa habari leo kuzungumzia juu ya usalama wananchi na mali zao ikiwa na pamoja na kusema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana na vurugu zozote ambazo zitatokea na hivyo kuwataka wananchi kupiga kura na kwenda katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa

MAMA SAMIA ATUA ZANZIBAR LEO, KUUNGURUMA KIBANDAMAITI NA DK. SHEIN JIONI HII

October 23, 2015

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo, kwa ajili ya mkutano wa kampeni utakaofanyika jioni hii kwenye Viwanja vya Demokrasia au Kibanda maiti.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mume wake, Hafidh Ameir, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mjukuu wake, Hamiar Ameir, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Movie alioko katika kundi la kampeni za CCM la ‘Mama Ongea na Mwanao’ Wema Sepetu alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
Baadhi ya viongozi wa CCM wakisubiri kwa hamu kusalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya viongozi alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya wasanii wa Bongo Movie alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai (Kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo

MAALIM SEIF AKUTANA NA MASHEIKH

October 23, 2015

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin, Malindi mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar wakimsikiliza Maalim Seif.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya mazungumzo yake na viongozi hao wa dini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na viongozi hao wa dini baada ya mazungumzo yao. 
(Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad, OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kushirikiana na taasisi zote za dini nchini sambamba na kuziendeleza madrasa za Kur’an, ili ziendane na wakati uliopo.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin Malindi mjini Zanzibar.

Amesema Serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar itashirikiana kwa karibu na taasisi hizo ili kuona kuwa michango yao inasaidia kuchangia juhudi za maendeleo na ustawi wa Zanzibar.

Amewataka viongozi hao wa dini kudhibiti tofauti ndogo ndogo za kimadhehebu, ili zisiwe chanzo cha kuvuruga umoja wa waislamu nchini.

Sambamba na hilo Maalim Seif amesema bado madrasa za Kur’an hazijapewa umuhimu unaostahiki, na kuahidi kulishughulikia suala hilo ili kuzijengea mazingira bora na kuangalia maslahi ya walimu wa madrasa hizo.

Amesema iwapo atachaguliwa kuongoza nchini, Serikali yake itatoa mchango wake katika kuziendeleza madrasa ili ziwe za kisasa kwa kuzipatia mahitaji yote ya msingi yakiwemo vikalio pamoja vifaa vya kusomea.

Amewakumbusha walimu wa madrasa kuweka mbele maendeleo ya watoto kwa kuwajenga kimaadili, ili waweze kuwa raia wema na viongozi bora wa baadae.

Mapema akizungumza kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo za Kiislamu, Sheikh Khamis Yussuf amesema taasisi hizo ziko tayari kuzungumza na kushirikiana na kiongozi yeyote wa serikali kwa lengo kuweka mustakbali mwema wa Zanzibar.

Amewaomba viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano katika kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa Zanzibar ili usiharibiwe na tamaduni nyengine, na kwamba utamaduni ni rasilimali muhimu kwa taifa.

Wiki iliyopita Maalim Seif alikutana na viongozi wa dini ya kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano Welezo, kuzungumzia juu ya umuhimu kutunza na kuilinda amani ya Zanzibar. 

JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA

October 23, 2015
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu kujiepusha kufika katika kituo cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au nembo ama rangi za chama cha siasa.


Aidha wametakiwa , kuepuka kutumia uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la kuwazuia wengine kwenda kupiga kura.

Pia amewataka  kuepuka kufanya kampeni katika kituo cha kupigia kura iwe kwa maneno ya ushawishi au kwa kuonyesha ishara ya chama fulani cha siasa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ahmed Msangi amesema nivema kila mwananchi anae stahili kupiga kura ahakikishe anafuata taratibu hizo ili kujiepusha na vitendo vya uvujifu wa amani katika siku hiyo muhimu.


Amesema  vyema kila mwananchi kupiga kura kwa kutumia jina na kitambulisho chake na sio cha mtu mwingine, aliyekufa au mgonjwa, kuepuka kufanya fujo ama vurugu katika kituo cha kupigia kura.


Aidha amesisitiza kuwa   kila mpiga kura mara baada ya kupiga kura kuondoka kwenye kituo cha kupigia kura na kuendelea na shughuli nyingine kwani ni kosa kupiga kura na kuendelea kubaki katika eneo la kituo cha kupigia kura.


Amesema  ni wajibu wa jeshi la polisi kuwalinda maofisa wanaosimamia uchaguzi, kuhakikisha kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa, bila vikwazo au bughudha na kuhakikisha vifaa vya kupigia kura viko salama.


Kwa mkoa wa mbeya tuna jumla ya majimbo 13 ya uchaguzi, vituo 3,899 vya kupigia kura, kila kituo kitalindwa na askari ili kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarishwa kwa kipindi chote cha zoezi la kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi.


Msangi amesema Jeshi la polisi mkoa wa mbeya limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na vituo vya kupigia kura sanjali na kuwepo kwa  na doria za magari, pikipiki, mbwa na askari ambao watakuwa wakitembea huku na kule kwa lengo la kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.JAMIIMOJABLOG





UBUNGO WAMPOKEA DK. MAGUFULI KWA FURAHA TELE, WASEMA DK. MAGUFULI NDIYO MKOMBOZI WAO

October 23, 2015
 Wakazi wa Ubungo wakimshangilia kwa shangwe mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli.
 Wananchi wakiwamtandikia apite.

NMB MOSHI WATOA KIFUNGUA KINYWA KWA WATEJA WAO.

October 23, 2015
Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Moshi mjini wa wakipata kifungua kinywa katika tawi la Benki hiyo leo asubuhi.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Moshi mjini wa wakipata chai ya asubuhi iliyoandaliwa na matawi ya Benki hiyo ya Nelson Mandela na Mawenzi yaliyopo mjini Moshi,
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki hiyo akisaidia kutoa huduma ya chai kwa wateja waliofika katika tawi la Nelson Mandela kwa ajili ya kupata kifungua kinywa leo Asubuhi.
Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini,Lameck Kehenga  akipata kifungua kinywa pamoja na watawa kutoka shule ya sekondari ya Anuarite.
Meneja Huduma kwa wateja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela,Andrew Msonga akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja waliofika katika tawi hil kwa ajili ya kifungua kinywa kilichoandaliwa na Benki hiyo mahususi kwa wateja wake.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela ,Moshi mjini akifurahia jambo na wateja waliofika katika tawi hilo kwa ajili ya kupata chai iliyoandaliwa na Benki hiyo.
Wateja walifika katika matawi ya Benk hiyo lile la Nelson Mandela na Mawenzi wamepata fursa ya kuonja keki iliyoandaliwa kwa ajili yao.
Meneja huduma kwa wateja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela,Andrew Msonga akizungumza jambo wakati wa tukio hilo lililofanyika katika tawi hilo.
Wafanyakazi wa Benki hiyo wakifurahia na wateja wao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala ni miongoni mwa wateja walifika kupata kifungua kinywa katika tawi la Nelson Mandela.
Meneja wa Benki ya NMB ,tawi la Nelson Mandela Moshi mjini,Emanue Kishosha akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala kuelekea katika meza kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.
RC Makala na Meneja wa NMB,Kishosha wakipata kifungua kinywa.
Baadhi ya wafayakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela wakizungumza na wateja wao.
Mazungumzo yakiendelea wakati wa kupata kifungua kinywa.
Mwakilishi wa Meneja wa NMB ,kanda ya Kaskazini,Lameck Kehanga akizungumza jambo marabaada ya kumaliza kupata kifungua kinywa.
Menea wa NMB ,tawi la Nelson Mandela, Emanuele Kishosha akitoa maelezo mafupi wapi Benki ya NMB imetokaa wapi ilipo sasa.
Baadhi ya wateja walifika kwa ajili ya kuapata kifungua kinywa wakifuatilia maelezo ya Meneja wa Benki hiyo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapatao Tanzania mkoa wa Kilimanjaro,Abdalah Mapembe alikuwa ni mmoja wateja walifika katika shughuli hiyo.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akizungumza mara baada ya kupata kifungua kinywa katika tawi la benki hiyo la Nelson Mandela.
Keki iliyoandaaliwa maalumu kw aajili ya wateja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wa matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi mjni Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwaongoza viongozi na wawakilishi wa wateja wa benki hiyo kukata keki.
Keki akiandaliwa vipande kwa ajili ya kugawiwa kwa wateja waliofika katika tawi hilo.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kishosha  akimlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala katka hafla hiyo.
Meneaja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kishosha akimlisha keki Mwenyekiti wa baraza la Biashara la Benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kishosha akimlisha keki ,Rose Masalu Dede kwa niaba ya wateja wa benki hiyo.
Watumishi wa Benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na badhi ya wateja wa benki hiyo.
Wateja wa benki ya NMB wakiiingia katika tawi hilo leo asubuhi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.