BREAKING NEWS.......KOCHA MPYA WA SIMBA ATUA DAR

August 13, 2014

Kocha mpya Patrick Phiri. Picha yaMaktaba.
Kocha mpya Mzambia Patrick Phiri ametua Dar muda mfupi uliopita kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuinoa Simba. Hivi sasa yupo njiani kuelekea klabuni hapo akitokea Uwanja wa Ndege.

REDD'S MISS KINONDONI 2014 NI SHIDAAAAH!

August 13, 2014

 Mratibu wa shindano la Redd's miss Kinondoni 2014 Innocent Melleck katikati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la kanda ya kinondoni litakalofanyika katika ukumbi wa Escape One ijumaa kwa kiingilio cha 10,000 kwa viti vya kawaida na 30,000 kwa VIP huku burudani za Malaika Bend chini ya Chirstian bella na Young Suma na tayari tiketi zipo mtaani. Baadhi ya warembo wa shoto ni matroni wa kambi hiyo Husna Maulid na kulia ni Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye

MAHABUSI YA WATOTO TANGA KUPATIWA FEDHA

MAHABUSI YA WATOTO TANGA KUPATIWA FEDHA

August 13, 2014

index
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
13/08/2014
Serikali imetenga fedha zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa jamii nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa cha habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”.
“Ni kweli tatizo hilo lipo ndio maana Serikali imetenga fedha tayari ambazo zitagawiwa kwenye vituo vyote nchi nzima” alisema Mwamwaja.
Mwamwaja alisisitiza kuwa deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko Tanga.
Mahabusi hiyo ni miongoni mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii ndani ya Wizara ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Matumizi ya fedha hizo ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba wa chakula kituoni hapo ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao na kufikia lengo la kuwarekebisha tabia zao ili wawe raia wema nchini.
 
Aidha, Mwamwaja aliongeza kuwa fedha zilizotengwa  si za Mkoa wa Tanga tu bali ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya wazee wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.
Mkurugenzi Idara ya Habari( MAELEZO) atembelea vitengo vya Mawasiliano Serikalini

Mkurugenzi Idara ya Habari( MAELEZO) atembelea vitengo vya Mawasiliano Serikalini

August 13, 2014


IMG_9656
Afisa Habari wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Dennis Kiilu akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi. Fatuma Malende.
IMG_9678
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambeneakiwaonesha Maafisa Habari wa Wizara ya Maji (hawapo pichani) namna Matumizi ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter unavyofanya kazi hasa katika nguvu na kasi ya upashaji habari kwenye jamii, wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelazaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9684
Baadhi ya Maafisa Uhusiano Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kutoka kushoto ni Neema Mbuja, Salama Kasamalu na Henry Kilasila wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
[PICHA NA HASSAN SILAYO]
IMG_9697
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Adrian Severin akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelzaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam
IMG_9706
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akieleza jambo kwa Maafisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (baadhi hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelzaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Adrian Severin na katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Henry Kilasila.
MWANAFUNZI ALIWA NA MBWA KARIBU NA IKULU

MWANAFUNZI ALIWA NA MBWA KARIBU NA IKULU

August 13, 2014


???????????????????????????????
Jeneza la Mwili wa Marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo likiteremshwa makaburini kwa ajili ya mazishi.
???????????????????????????????
Mchungaji akiendesha ibada ya mazishi ya Marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo
???????????????????????????????
Waomboleaji wakiuzika mwili wa marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo
???????????????????????????????
Mmoja wa Mbwa wanaodaiwa kumuua marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo ameuwawa.
???????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Bazil Makungu Ludewa
MWANAFUNZI wa shule ya msingi Ludewa mjini katika mkoa wa Njombe Iblahim Faraja Chipungahelo ameuawa na kisha kuliwa nyama na mbwa wanaosadikika kuugua kichaa kwa kukosa chakula kwa muda mrefu.
Tukio hilo la kusikitisha na lililoleta simanzi kubwa kwa wakazi wa Ludewa mjini lilitokea August 8 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo la Ikulu ambapo marehemu Chipungahelo pamoja na wenzake walikuwa wakipita njia karibu na nyumba ya mtu aliyejulikana na kwa jina la Bosco Lingalangala kwenda kuchuma mapera kama ilivyo destuli yao.
Mashuhuda wa tukio hilo mama Kumba na mama Haule wakazi wa kitongoji cha Ibani katika kata ya Ludewa kwa pamoja walieleza kuwa wakiwa nyumba walisikia kelele za watoto jirani huku wakimwita mwenzao marehemu bila mafanikio.
‘’’’ Tulipowauliza walisema kuwa mwenzao Ibrahim amekamatwa na mbwa na ndipo tulipokusanyika na kwenda kumwokoa mtoto lakini tulipofika eneo la tukio tulimkuta mbwa wakiendelea kumla marehemu huku amelala kifudifudi lakini tulishindwa kumwokoa na ndipo tukakimbia kutoa taarifa kituo cha polisi.””” walisema akina mama hao kwa uchungu
Kwa mujibu wa taarifa ya daktari Sira Rajabu wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu alisema mtoto Ibrahim alikuwa na majeraha makubwa mwili mzima huku paja la mguu wake wa kulia likiwa limeliwa na kuondolewa nyama.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Fulgensi Ngonyani alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watu mbalimbali akiwemo mmiliki wa mbwa hao ambaye inasadikika kuwa ananishi jijini Dar es salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu mganga wa mifugo Simoni Haule alisema kuwa mbwa hao wa bwana Bosco Lingalangala hawajapata chanjo zaidi ya miaka miwili sasa kwa hiyo tayari mbwa hao wanaugua ugonjwa wa kichaa ambacho hawawezi kupona tena na dawa iliyobaki ni kuuawa tu.
Mmiliki wa mbwa hao Bosco lingalangala hakupatikana ili kuzungumzia suala hilo kwa sababu simu yake ya mkononi haikupatikana.
Hata hivyo akiwa makaburini diwani wa Kata ya Ludewa Monica Mchiro aliwaambia na kuwatahadharisha waombolezaji na wananchi waliohudhuria mazishi kuwa mawasiliano yamefanywa kati yake na mmiliki wa mbwa hao lakini majibu aliyoyatoa hayana ushirikiano kwa sababu ameahidi kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakaye husika kuwadhuru mbwa wake.
Hata hivyo habari kutoka kwa majirani ambao hawakupenda kutaja majina yao walisema mbwa hao hufungiwa kwenye banda na hupewa nyama mbichi kwa kurushiwa na wahudumu lakini siku hiyo walifunguliwa na kuanza kuzagaa kwa nia ya kujitafutia chakula wenyewe baada ya kukosa kwa muda mrefu.