SERIKALI ITAENDELEA KUIPA KIPAUMBELE TMA.

September 13, 2024
WAZIRI wa Fedha, Mwigulu  Nchemba ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuipa kipaumbele kwa kuwa huduma za hali ya hewa zinasaidia katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

“Wataalam wa hali ya hewa mnafanya kazi nzuri, utabiri unaotolewa hivi sasa ni wa usahihi na umesaidia sana katika masuala ya kiuchumi na kijamii na mipango ya nchi kwa ujumla”. Alizungumza Dkt. Mwigulu alipotembelea banda la TMA katika viwanja vya AICC, Arusha wakati akifunga rasmi Jukwaa la 16 la Ununuzi la Afrika Mashariki. 

Matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa ni suala mtambuka kwani husaidia katika mipango na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamiii hususani katika kupunguza madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa kwa umma.


SERIKALI YADHAMIRIA KULIBADILI JESHI LA POLISI

SERIKALI YADHAMIRIA KULIBADILI JESHI LA POLISI

September 13, 2024



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe na Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu akizungumza na Wajumbe na Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Omar Issa akizungumza baada ya kuapa kuongoza bodi hiyo wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Omar Issa akiapa mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa kofia) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Katibu wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Dkt.Prosper Kiramuu akiapa mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa kofia) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu(wapili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Omar Issa(wakwanza kushoto),Katibu wa Bodi hiyo,Dkt.Prosper Kiramuu(kulia) na wajumbe na watendaji wa bodi na shirika hilo baada ya Hafla ya Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

………

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi,Magereza,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.

‘Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa na Jeshi la Polisi la kisasa ambalo linafanya kazi kutumia mifumo ya zamani ndio maana tunazungumzia upelekaji wa jeshi kwenye ngazi za kata na uwepo wa ofisi bora na za kisasa tukiamini uhalifu unaanzia chini,wote tumeshuhudia changamoto kubwa sana ya uhalifu uliokithiri katika nchi hii ukihusisha viungo vya watoto wadogo ili mtu apate utajiri vitu ambavyo vinaleta uhalifu katika jamii sasa katika kulipa uwezo jeshi letu kupitia Shirika la Uzalishaji Mali katika kujenga vituo na kusimamia miradi mikubwa ikiwemo mradi wa miji salama tunaiomba bodi sasa ilisimamie shirika ili lipate kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa ili hatimaye tudhibiti masuala ya uhalifu kwa njia za kisasa’alisema Masauni

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu amesema wizara iko tayari kutoa ushirikiano kwa shirika na bodi pamoja na kusimamia mambo ya kisera ili azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya jeshi letu kuwa la kisasa zaidi.

‘Mimi kama mtendaji mkuu wa wizara nimesimama kuwahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano wowote mtakaohitaji kutoka kwa wizara najua majukumu yenu yatatuhitaji kwa kiasi kikubwa ili kupata miongozo ya kisera ili muweze kutimiza shughuli za kiutendaji na matarajio ya wizara kwenye shirika letu ni makubwa na kuna matarajio mengi ya kufanya mabadiliko makubwa’ alisema Katibu Mkuu

Wakizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi,Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa na Katibu wa bodi hiyo,Dkt.Prosper Kiramuu waliishukuru serikali kwa kuwaamini na kuhaidi kutimiza malengo ya serikali yaliyokusudiwa kupitia shirika hilo.

WAZIRI KIJAJI AKUTANA NA KAMISHENI YA TABIANCHI YA BONDE LA CONGO

September 13, 2024

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Waziri wa Utalii na Mazingira wa Jamhuri ya Congo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni hiyo Mhe. Arlette Soudan – Nonault (kushto jijini Dar es Salaam. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambaye pia ni Mwakilishi wa nchi katika Mfuko wa Bluu wa Bonde la Congo Prof. Dos Santos Silayo.
Waziri wa Utalii na Mazingira wa Jamhuri ya Congo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni hiyo Mhe. Arlette Soudan – Nonault akizungumza kwenye kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa kikao cha Ujumbe wake kutoka Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Congo na Mfuko wa Bluu wa Bonde la Congo jijini Dar es Salaam



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Utalii na Mazingira wa Jamhuri ya Congo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni hiyo Mhe. Arlette Soudan – Nonault (kulia) na Ujumbe wa Kamisheni hiyo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Congo (CBCC) kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.


Amesema changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ipo kwa maana hiyo tunatakiwa kuchukua hatua kuona dunia inakuwa salama kutokana na changamoto hiyo.


Dkt. Kijaji amesema hayo wakati wa kikao na Ujumbe kutoka Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Congo na Mfuko wa Bluu wa Bonde la Congo ulioongozwa na

Waziri wa Utalii na Mazingira wa Serikali ya nchi hiyo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni hiyo Mhe. Arlette Soudan – Nonault jijini Dar es Salaam.


Aidha, amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo, Tanzania imekuja na biashara ya kaboni ambayo pamoja na mambo kadhaa inahusisha upandaji wa miti kwa wingi ambayo hunyonya hewa ya ukaa.


“Sisi kama taifa tumeanza kuchukua hatua kwenye biashara ya kaboni na tunatamani tuungane, tushirikiane na tunufaike kwa pamoja kubadilisha ujuzi ili tufikie malengo, tunahitaji maendele ambayo wenzetu wamepiga hatua huku wakiharibu mazingira na waathiriki wakubwa ni sisi nchi zinazoendelea,” amesema.


Mhe. Dkt. Kijaji amepongeza CBCC kwa kukubaliana namna wanavyoweza kuzisaidia nchi wanachama kupata fedha ambazo tayari zimewekwa katika Mfuko wa Bluu na benki mbalimbali wanazofanya nazo kazi kwa ajili ya kuendeleza shughuli za utalii na mabadiliko ya tabianchi.


Kwa upande mwingine amesema kama mawaziri wanaoshughulikia mazingira wana jukumu la kuhamasisha wananchi watumie niahsti safi ya kupikia badala ya kuni au mkaa ambazo zinatokana na ukataji wa miti holela.


Amesema kwa kutambua hilo tayari Tanzania imeaandaa Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia na Rais Mhe. Dkt. Samia aliamiwia na kupewa ukinara ili wananchi wanufaike lengo la kufika asilimia 80 ya kaya kutumia nishati safi ifikapo mwaka 2034 litimie.


Hivyo, amewapongeza wakuu wa nchi kwnye Mkutano wa COP22 kwa kuanzishwa kwa Kamisheni hiyo (CBCC) ili iangalie mabadiliko ya tabianchi na mazingira kwenye Bonde la Congo.

BASHE,MPINA USO KWA USO WAMALIZA TOFAUTI ZAO ,TUACHE SIASA KATIKA ZAO LA PAMBA

September 13, 2024

 Na Mwandishi wetu


WAZIRI wa Kilimo Husein Bashe (mb) atua kibabe Kisesa na kukutana na Mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina ana kwa ana.

Amtaka mbunge huyo kuacha siasa katika zao la Pamba Kwani Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inahitaji kuona fedha zinazotengwa zinanufaisha wakulima.

Awaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa serikali inarejesha kitalu cha mbegu kuwapatia ruzuku ya dawa za wadudu katika zao la mahindi na pembejeo na mbegu katika zao la Pamba.

Wazee wa kimila wamsimika kuwa Mtemi (Chief) wa jimbo hilo.

Kihongosi aunguruma asema hataki siasa chafu mkoani humo kwani ametumwa kazi ya maendeleo na Rais Samia hivyo hayupo tayari kuona siasa katika kilimo.

Mpina asema yuko tayari kuweka tofauti zake na Bashe pembeni na kuungana katika masuala ya maendeleo na shughuli za serikali.

Bashe ametua jimboni humo katika mkutano na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kufunga mashindano ya michezo mbalimbali ya Mwandoya na kupokelewa na mamia ya wananchi.

Ametumia fursa hiyo kukutana na Mbunge Mpina ambapo amemtaka kuacha siasa katika zao la Pamba kwa maslahi ya wananchi.

“Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kilimo Mpina amesema hapa na mimi nataka nisisitize tuweke mambo mengine pembeni aache siasa na sitaki siasa katika zao la Pamba, nafahamu zipo changamoto lakini tulipotoka sio tulipo sitakubali mtu arudishe nyuma jitihada hizi wanaoteseka wananchi,”alisema.

Aidha amekabidhi trekta 40 kwa jimbo hilo na kuwataka maafisa kilimo na ugani kuacha kukaa mjini na kuishi vijijini ili waweze kuwasaidia wakulima utaalamu na kufikia malengo ya serikali ya kilimo chenye tija.

Amewashukuru wazee wa kimila kwa kumsimika kuwa mtemi wa jimbo hilo.

“Nami leo nimesimikwa kuwa mtemi wa Kisesa hivyo Mpina akinitambia pale bungeni kwa kuingia na fimbo ya uchifu nami nitaingia na yangu,”amesema.

Naye Mkuu wa mkoa huo Kennan Kihongosi amemuhakikishia Waziri Bashe kuwa yeye ndio mwenye dhamana na mkoa huo, hivyo hawezi vumilia watu wanaotafuta umaarufu katika siasa kuingiza masuala ya maendeleo.

“Nimetumwa kazi na Rais Dk. Samia, Simiyu ni ya kwanza ama ya pili katika kuzalisha pamba hivyo kwa wananchi ni zao la kiuchumi sitaki wanasiasa watumie zao hilo kutafuta umaarufu shida zinazosemwa katika zao hilo si za kweli wananchi wa Kisesa msikubali kutumika,”amesema

Naye Mbunge Mpina ametumia fursa hiyo kumkaribisha Bashe Kisesa na kueleza kuwa wanazo tofauti zao hali iliyowafikisha hadi Mahakamani lakini yupo tayari kushirikiana naye katika masuala ya utendaji wa serikali
.
Credit-MichuziBlog



UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWENYE VYANZO VYA MAJI WAIKOSHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA

September 13, 2024


MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira Jackson Kiswaga katika akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika chanzo cha Maji Mabayani Jijini Tanga wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimueleza jambo Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika wakati akiwasili na kamati hiyo kwa ajili ya ziara ya siku moja

UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA SASA NI ZAMU YA DODOMA NA SINGIDA

September 13, 2024

 


Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu. 
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Selemani Mtibora akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,  mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.

Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Dodoma. 
Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Dodoma. 
Wazee wa kimila ni wadau muhimu wa uchaguzi kutokana  na umri, hekima na busara zao. Tume imekuwa ikishirikiana na wazee wa kimila katika kuwaelimisha na kuwashawishi wananchi kujitokeza na kushiriki kwenye michakato ya uchaguzi. Pichani ni Chifu wa Mkoa wa Singida, Mushenyi Senge Ndovu (kushoto) na Chifu wa Singida Vijijini, Kilongo Kika wakiwa katika mkutano wa wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Septemba 13,2024 mkoani Singida. 
Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Singida. 
***************
Na. Mwandishi Wetu
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Singida, sehemu ya mkoa wa Dodoma na sehemu ya mkoa wa Manyara utaanza tarehe 25 Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mstaafu, Mbarouk Salim Mbarouk ameyasema hayo leo tarehe 13 Septemba, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya zoezi hilo.

“Mzunguko wa tano wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utajumuisha mkoa huu wa Dodoma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino na Kongwa, mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya Kiteto na Simanjoro na mkoa wa Singida ambapo uboreshaji utaanza tarehe 25 Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema.

Amefafanua kuwa uboreshaji wa Daftari utahusu kuwaandikisha raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka kumi na nane na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yeyote.

Katika hautua nyingine, akifungua mkutano wa wadau mkoani Singida, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari amesema kuwa Tume katika kuhakikisha kwamba inaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kurahisisha zoezi hili la uboreshaji wa Daftari, imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao kwa mara ya kwanza utamuwezesha mpiga kura aliyepo kwenye Daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa kutumia aina zote za simu au kompyuta.

“Wanaotumia simu za kawaida (maarufu kama kitochi au kiswaswadu) nao wanaweza kutumia huduma hii kwa kupiga namba *152*00# na kisha watabonyeza namba 9 halafu wataendelea na hatua zingine kama itakavyokuwa inaelekezwa kwenye simu husika,” amesema.

Jaji. Asina amefafanua kuwa mtumiaji wa huduma hii, atatakiwa kufika kituo anachokusudia kujiandikisha ili akamilishe hatua za kupigwa picha, kuweka saini na kupatiwa kadi yake ya mpiga kura.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulizinduliwa mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 sambamba na kuanza kwa uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na mikoa ya Geit, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu na Manyara katika Halmashauri za Wilaya ya Babati, Hanang, Mbulu na Mji wa Babati.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari inatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.

TIB BENKI YAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA NZURI MAONESHO YA AFRIKA MASHARIKI

September 13, 2024

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt. Selemani Saidi Jafo, ameipongeza Benki ya maendeleo TIB kwa kuibuka mshindi wa pili katika kipengele cha Watoa Huduma za Kibiashara kwenye Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu "Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara ni kichocheo katika kukuza uchumi wa Nchi", yalianza rasmi tarehe 6 Septemba na yanatarajiwa kukamilika tarehe 15 Septemba 2024 na yametoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika mashariki kunadi bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwenye ukanda huo.

Baada ya kukabidhiwa Cheti na Waziri Jaffo wakati wa uzinduzi wa Maonesho hayo Meneja wa Benki hiyo ya TIB Kanda ya Ziwa, Bw. Zacharia Kicharo, alipo fanya mazungumzo na mwandishi wetu, amesema benki yao imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na taasisi za umma na zile za binafsi pia inafanya kazi kwa kuwawezesha mikopo wakulima wadpgo, wa kati na wakubwa.

Akiwakaribisha wananchi kutembelea maonesho hayo ya biashara ya afrika mashariki Bwana Kicharo amesisitiza kuwa zipo fursa nyingi kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujamla watakazo zipata pindi watakapo tembelea banda la TIB.

“kuna elimu ya masuala ya kiuchumi na biashara inayo tolewa hapahapa bandani kwetu na maafisa wetu hivyo ni muhimu kufika kwa na kujipatie elimu hii hususani kwa wakaazi wa Mwanza na kanda ya ziwa” alisema 

Kwa kuzingatia eneo la kimkakati la kanda ya ziwa hususani katika sekta ya uchimbaji madini na biashara ya madini ,Benki ya maendeleo ya TIB kupitia tawi lao la kanda ya ziwa inahudumia mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mwanza yenyewe lilipo tawi la benki hiyo kwa kanda ya ziwa, na kwenye maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki wameweka banda linalotoa huduma za benki hiyo kwa wananchi na wajasiriamali wa kada zote wanao fika viwanja vya furahisha yanapo fanyika maonesho hayo.

Pichani ni Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jaffo, akimkabidhi Meneja wa Benki ya Maendeleo TIB, Kanda ya Ziwa,  Zacharia Kicharo, cheti na zawadi ya mshindi wa pili katika kipengele cha Watoa Huduma za Kibiashara. Maonesho haya yenye kauli mbiu "Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara ni kichocheo katika kukuza uchumi wa Nchi", yalianza tarehe 6 Septemba na yanatarajiwa kukamilika tarehe 15 Septemba 2024.
Benki ya Maendeleo TIB inashiriki kwenye Maonesho hayo Kwa Kutoa Elimu ya Huduma mbalimbali inaayotolewa na Benki hiyo.