VIJANA 1376 IFAKARA WANUFAIKA NA MRADI WA YEE

April 01, 2017
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Jumla ya vijana 1376 wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro wamenufaika na mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) na kuratibiwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Plan International.
Takwimu hizo zimetolewa leo mkoani humo na Meneja wa Shirika hilo Wilaya ya Ifakara, Majani Rwambali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya maendeleo ya mradi huo unaotarajia  kuisha mwaka 2018.
Rwambali amesema mradi huo umeanza tangu mwaka 2015,  unatekelezwa katika Mikoa mitano ikiwemo ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro ambapo vijana wanaoishi katika mazingira magumu wanapewa elimu ya mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali ili waweze kujitegemea na kujikwamua kimaisha.
“Kwa wilaya yetu mradi huu unatekelezwa katika Kata 9 zikiwemo za Mwaya, Mkula, Mchombe, Kibaoni, Mgeta, Kiberege, Ifakara, Lumemo na Mbongo ambapo hadi sasa jumla ya vijana 1376 kati ya vijana 1490 waliokuwa kwenye lengo la mradi wameshapatiwa mafunzo na wengi wao wameshajiajiri”alisema Rwambali.
Meneja amefafanua kuwa mafunzo hayo hufanyika kwa awamu ambako mpaka sasa awamu zilizofanyika ni nne huku ikibaki awamu moja itakayohusisha vijana waliosalia kukamilisha lengo la mradi huo ambao inategemewa kuanza miezi michache ijayo kwani.
Aidha, Rwambali ameongeza kuwa mradi huo umekua na changamoto katika kuwapata vijana wenye ulemavu kwa sababu jamii bado haijatambua kuwa vijana hao wana uwezo wa kufanya kazi na kujipatia vipato sawa na vijana wengine hivyo ametoa rai kwa vijana hao kujitokeza kwa wingi katika awamu hiyo ya mwisho ya mradi huo.
Kwa upande wake Katibu wa watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani Kilombero, Hamis Liundi ameishukuru Umoja wa Ulaya kwa kuwaletea mradi huo uliowafikia hadi vijana wenye ulemavu na kuboresha maisha yao  ingawa bado kuna changamoto za vifaa vya kufanyia kazi pamoja na maeneo kwa ajili ya ofisi.
“Mradi huu ulianza wakati wa kampeni hivyo watu hawakuufatilia kutokana na kuhusisha mradi huo na mambo ya kisiasa, uchaguzi umeshapita hivyo ninawaomba vijana wenzangu hasa walemavu kujitokeza kwani fursa kama hizi zinatokea mara chache,” alisema Liundi.
Nae mmoja wa walemavu wa viungo aliyenufaika na mradi huo, Elia Limota amesema kuwa mradi huo umemuwezesha kutambulika katika jamii na kumfanya awe kijana anayeweza kujitegemea kwani baada ya mafunzo hayo yeye pamoja na walemavu wenzie wameweza kuunda kundi na kuvumbua miradi mbalimbali ikiwemo ya uchomaji wa matofali, ukodishaji wa baiskeli pamoja na kilimo cha mpunga.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KIONGOZI MKUU DUNIANI WA JUMUIYA YA KIHINDU (BAPS) MWAMINARAYAN SANSTHA MTUKUFU MAHANT SWAMI MAHARAJ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KIONGOZI MKUU DUNIANI WA JUMUIYA YA KIHINDU (BAPS) MWAMINARAYAN SANSTHA MTUKUFU MAHANT SWAMI MAHARAJ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

April 01, 2017
HIN1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Duniani Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Duniani Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi huyo Mkuu Duniani kutoka Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam.
HIN7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi huyo Mkuu Duniani kutoka Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
HIN8

MAHAFALI YA KWANZA YA TAASISI YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI TANZANIA YAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

April 01, 2017

Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Elizabeth Titus Munthali, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba
Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Honest Amedeus Matem, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 
Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Annastacia Mbunda, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO). 
Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Salim Ngailo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 
Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Lauden Cheyo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 
Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Charles Peter Moshi, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 

SEMINA YA VIONGOZI NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI LEO.

April 01, 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud mara alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika wengine alipowasili katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Baadhi ya Wahariri wa Habari na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Waandishi wa habari wakiwa katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Washauri wa Rais wa Zanzibar ni mongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 01/04/2017.

JE WEWE NI MIONGONI MWA WANAOSUBIRIA MWEZI APRILI KWA HAMU?

April 01, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Kama kuna kitu ambacho wafanyakazi wengi wanapenda kusikia basi ni sikukuu au mapumziko. Kwani hupata fursa ya kutokwenda kazini, haimaanishi kwamba ni wavivu bali kutokana na ufinyu wa likizo ukiachana na wikendi.

Kwa upande wa watanzania hali hiyo hutokea kwa baadhi ya miezi na wa Aprili ni mmojawapo. Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Jumia Travel, zifuatazo ni sababu zinazoufanya mwezi huu kupendwa zaidi nchini.

ENEO LA LEBANON SOKO LA SAMAKI LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM KINARA KWA UKATILI WA KIJINSIA

April 01, 2017
 Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Samaki la Ferry, Ali Bunda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam juzi wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo, baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Bunda alilitaja eneo la Lebanon katika soko hilo kuwa ni hatari kwa ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto.