Rais Mstaafu Jakaya Kikwete AAGWA LEO NA BALOZI WAPYA CHIKAWE NA KISAMBA

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete AAGWA LEO NA BALOZI WAPYA CHIKAWE NA KISAMBA

May 09, 2016

J1Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
J2Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
J3Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
J4Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba,  Balozi huyo alipofika kumsalimia katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
(Picha na Bashir Nkoromo).

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA MFUKO WA PENSHENI PPF JIJINI ARUSHA

May 09, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. Picha zote na Mafoto Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
Jengo hilo lililozinduliwa leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Sehemu ya wananchi wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia.....
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mhe Rais.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na Wakurugenzi wa Mfuko wa huo wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijjah, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Wakifurahia baada ya uzinduzi huo....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja wa PPF Kanda ya Arusha, Onesmo Ruhasha, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa
Wadau wakiimba wimbo wa Taifa
Wadau wakiimba wimbo wa Taifa

TFDA YAKUTANA NA WADAU WA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO.

May 09, 2016

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Daud Ntibenda akifungua kikao kazi cha wadau wa TFDA katika sekta ya Habari mkoani Arusha.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Said Mecki Sadiki akizungumza na maafisa wa TFDA ofisini kwake walipokwenda kumtembelea ofisini kwake na kujadili masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika mkoa wake.
Picha ya Pamoja.
Wadau wa Habari mkoani Arusha wakifuatilia mada mbalimbali.  
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA bi. Charys Ugulum akitoa Maelezo ya utangulizi katika kikao kazi mkoani Arusha.
KIKOSI SERENGETI BOYS HIKI HAPA

KIKOSI SERENGETI BOYS HIKI HAPA

May 09, 2016
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi amewataka wachezaji wa timu ya soka ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama jina la Serengeti Boys kwenda kucheza soka la ushindani na kurudi na kikombe nyumbani katika mashindano maalumu ya vijana yatakayofanyika Goa, India.
Dioniz Malinzi aliyasema hayo leo Mei 9, 2016 kwenye hafla ya kukabidhi bendera timu ya Serengeti Boys inayokwenda Goa, India kushiriki mashindano hayo maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIFF).


Katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Dioniz Malinzi alisema: “Msiwe na wasiwasi, wakati wenu wa kucheza soka ndiyo huu.”

“Waziri wa Michezo, Nape Nnauye ameniagiza niwaambie kwamba Serikali itakuwa pamoja nanyi, hivyo msiwe na wasiwasi nendeni mkacheze. Mkacheze mpira wetu si kuigaiga eti mcheze kama Misri. Kachezeni mpira wenu, huu ndio wakati wenu wa kucheza mpira,” aliasa Malinzi.

Wito wa Malinzi ulipokelewa kwa mikono miwili na Nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba aliyetamba kurudi na taji hilo mwishoni mwa mwezi mara baada ya mashindano yanayofikia kikomo Mei 26, mwaka huu.

“Tunamshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa namna alivyojitahidi kutuhudumia hapa kambini. Tunaahidi tutarudi na kombe hapa,” amesema Makamba na kuongeza kikosi chako kiko vema kama alivyotangulia kusema Mshauri Mkuu wa Maendeleo kwa timu za Taifa, Kim Poulsen.

Naye, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya aliyeambatana na Naibu Balozi, Robert Shetkintong balozi amesema amefarijika kuona Tanzania imefanikiwa kupata nafasi hiyo kushiriki michuano hiyo maalumu kwa ajili ya kuiandaa India na fainali zijazo za Kombe la Vijana.

“Tunachofanya kwa sasa ni kukuza ushirikiano kati ya India na Tanzania katika michezo hasa soka. Kama tunavyofahamu soka kwa sasa ni mchezo unapendwa na watu wengi. Unagusa watu wengi na India tumeliona hilo hivyo kwa kuendeleza mchezo na uhusiano ndiyo maana tumekuwa na program za maendelo ya mpira. Tutauendeleza na ninaamini vijana hawa watakuwa chache ya kuuboresha mpira wetu,” amesema.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kwamba tangu kuanza kwa maendeleo ya soka la vijana, mashindano hayo yamekuwa ni hatua kubwa ya maendeleo ya soka Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa haijawahi kutokea timu kama hiyo ikateuliwa kushiriki michezo ya shirikisho kabla ya fainali za Kombe la Dunia kwa vijana.“Kwa kawaida au tuseme kwa mujibu wa ratiba za fainali kubwa zinazofanyika katika nchi fulani, mwaka mmoja kabla huandaliwa mashindano ya shirikisho kama haya. India mwakani wana mashindano makubwa, fainali za Kombe la Dunia kwa timu za vijana na hivyo ni wameandaa mashindano ya shirikisho ambayo Tanzania, Malaysia, Korea Kusini, Marekani na India wenyewe tumealiwa,” amesema na kuongeza kuwa Serengeti Boys inatarajiwa kusafiri kwenda India Jumatano Mei 11, mwaka huu.

Wachezaji wanaoondoka ni Ramadhan Kabwili, Kelvin Kayego, Samwel Brazio, Kibwana Shomari, Nicson Kibabage, Israel Mwenda, Nickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba, Maulid Lembe, Ally Ng'anzi, Asad Juma, Kelvin Naftari, Yasin Mohamed, Syprian Mwetesigwa, Aman Maziku, Rashid Chambo, Enrick Nkosi, Yohana Mkomola, Mohamed Abdallah, Shaban Ada na Muhsin Mkame.

Maofisa watakaosafiri na timu hiyo ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ayoub Nyenzi, Mshauri wa ufundi wa timu za vijana, Kim Poulsen, Kocha Mkuu, Bakari Shime, Kocha wa Makipa Mohamed Muharami, Daktari wa timu, Shecky Mngazija na mtunza vifaa Edward Edward.

Michuano hiyo itakayopigwa kwa mfumo wa ligi kwa timu tano kucheza mechi nne, inatarajiwa kuanza Alhamisi Mei 12, 2016 na kwamba AIFF kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Tayari Serengeti Boys imecheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa mpaka sasa, mmoja dhidi ya Burundi na miwili dhidi ya timu ya vijana wa Misri (The Pharaohs) na kupata matokeo mazuri na tangu Aprili, 2016 iliweka kambi katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa na michuano hiyo chini ya Shime, akisaidiwa na Sebastian Mkomwa.

Ratiba

Ratiba ya michuano inaonyesha kwamba Tanzania itafungua dimba na Marekani kwenye Uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa huku mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji India dhidi ya Malysia Mei 15, mwaka huu.
Serengeti Boys watashuka dimbani tena Mei 17, kucheza na wenyeji India mchezo wa kwanza, Mei 19 Serengeti Boys watacheza dhidi ya Korea Kusini na mchezo wa mwisho watamaliza dhidi ya Malysia Mei 21.

Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25 ambapo kabla ya mchezo wa fainali, utchezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa.

Maana ya mashindano

Kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo maalumu ya vijana kimataifa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Serengeti Boys, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana barani Afrika dhidi ya Shelisheli Juni 25 hadi Julai 2, 2016.

WATANZANIA KUSHUHUDIA COPA AMERICA LIVE KUPITIA STARTIMES

May 09, 2016
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Mohamed Kimweri (kushoto), akizungumza katika na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kupata haki za kuonesha michuano ya Copa Amerika moja kwa moja ambayoitafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Kulia ni Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri.
 Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya StarTimes Tanzania imefanikiwa kupata haki za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja ambayo itafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa kampuni hiyo nchini,  Zuhura Hanif alisema kuwa kupatikana kwa haki za kuonyesha michuano hiyo mikubwa na mikongwe ulimwenguni ikiwa inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni jitihada za kuhakikisha kuwa wateja wao wanafurahia vipindi bora vya michezo na burudani.

“Leo StarTimes inayo habari njema kuwataarifu kuwa tumepata haki maalum za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja kutoka nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Ninaposema haki maalumu manake ni kwamba watanzania hawataweza kushuhudia michuano hii sehemu yoyote isipokuwa kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee. 

Alisema wateja wao na wapenzi wa soka nchini wataweza kushuhudia michezo yote 32 ambapo itazikutanisha timu 16 za bara la Amerika ya Kusini na mwenyeji Marekani zitazoumana katika viwanja 10 tofauti nchini Marekani ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyikia huko.” Alisema Hanif.

Hanif aliwataka watanzania na wapenda soka kwa ujumla kujiandaa kushuhudia mechi kali za miamba ya soka kutoka bara la Amerika ya Kusini ambazo itayakutanisha majina makubwa katika ulimwengu wa mpira wa miguu kama vile; Lionel Messi, Kun Aguero (Argentina), Alexis Sanchez, Arturo Vidal (Chile), Neymar, Marcelo (Brazil), Luis Suarez, Edinson Cavani (Uruguay) na wengineo.

“Ninafahamu kuwa watanzania ni miongini mwa mashabiki wakubwa wa mchezo wa soka hivyo watafurahia zaidi kuwatazama wachezaji wanaowapenda wakiwakilisha mataifa yao katika michuano hii. Tayari tumekishashuhudia ligi mbalimbali ulimwenguni zikielekea ukingoni kama vile ligi za Bundesliga na Serie A za Ujerumani na Italia ambazo tayari timu za Bayern Munich na Juventus zimaeshatangazwa mabingwa. Na nafurahi kuwa ligi hizo zote mbili zilionekana moja kwa moja kwenye chaneli za michezo za ving’amuzi vyetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwisho wa mwezi kuanzia sh. 5,000 aliongezea

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watanzania na wateja wetu kwa ujumla kuwa michezo na burudani kwetu StarTimes ndio nyumbani. Kwa kuliona hilo baada ya kufaidi mechi za ligi kuu za Ujerumani na Italia sasa tumewaletea Copa America kuhakikisha kuwa mnafurahia vema luninga zenu. 
Mbali na michuano hii tunaahidi kuendelea kuwaletea michuano mingine kama awali tulivyofanya kwa Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Vilabu Bingwa Duniani, Kombe la Dunia la Vijana chini ya Miaka 20 na miningineyo. Nawasihi wateja wetu kukaa mkao wa kula na wasiojiunga nasi wafanye hivyo ili kufaidi uhondo huu utakaowajia hivi punde kwenye luninga zao.” Alisema Hanif.

Michuano ya Copa Amerika inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Juni kuanzia tarehe 3 mpaka 26 mwaka 2016 ni michuano mikongwe zaidi duniani ikiwa inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ambapo nchi ya Uruguay inashikilia rekodi ya kuchukua mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina mara 14. Michuano ya mwaka huu itakuwa ni ya kusisimua zaidi hasa kwa bingwa mtetezi nchi ya Chile kutetea ubingwa wake, ambapo aliuchukua mwaka 2015 baada ya kuishinda timu ya taifa ya Argentina kwa mikwaju ya penati.

TANZIA: ANKAL MICHUZI AFIWA NA MWANAE

May 09, 2016
Ankal Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

JK AMUWAKILISHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA

May 09, 2016


Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta.
Naibu Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio hilo.
Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta,Bi Margaret Kenyatta. 
Rais Mstaafu wa Kenya,Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.

Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

Fastjet Yachukua ubingwa wa bonanza la Fastjet sport extra

May 09, 2016

.Wachezaji wa Timu ya fastjet (wenye jezi nyeusi) wakichuana na wachezaji wa timu ya Diamond Trust Bank(DTB) wakati wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni

Wachezaji wa Timu ya fastjet (wenye jezi nyeusi) wakichuana na wachezaji wa timu ya Diamond Trust Bank(DTB) wakati wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni



Wachezaji wa Timu ya fastjet wakisheherekea ushindi waliopata dhidi ya timu ya Diamond Trust Bank(DTB) kwenye  mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibun

.Afisa Masoko na Mawasiliano wa fastjet, Lucy Mbogoro akionyesha cheti kilichozawadiwa kwa timu ya fastjet kama mshindi wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni


Afisa Masoko na Mawasiliano wa fastjet, Lucy Mbogoro akionyesha cheti kilichozawadiwa kwa timu ya fastjet kama mshindi wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni