WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI ,MHANDISI GERSON LWENGE AZINDUA BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA).

October 15, 2016
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhanidisi Gerson Lwenge alipowasili katika Mamlaka hiyo kwa ajili ya uzinduzi wa bofi mpya ya MUWSA.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mamlak ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uznduzi wa bodi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) Prof ,Faustine Bee akizingumza katika hafla hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya utamburisho wa wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini ,Anthony Komu akisalimia mara baada ya kutamburishwa katika hafla hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akisalimia mara baada ya kutamburishwa.
Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (katikati) akiwa na wakuu wa wilaya,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakiwa katia hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa ya Mamlaka kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo.
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) Sharry Raymond (MB) akizungumza wakati wa kuaga rasmi kwa niaba ya wajumbe wenzake wa bodi waliomaliza muda wake.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael.katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA,Prof ,Faustine Bee.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaa ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Gerson Lwenge akionesha zawadi ya Tablet zilizotolewa kwa wajumbe wa bodi waliomaliza muda wake.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Tablet Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faaustine Bee.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru zawadi ya Tablet.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael aliyekuwa mjumbe wa bodi ya MUWSA , zawadi ya Tablet.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo,Hajira Mmambe zawadi ya Tablet.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya jinsia na wanawake (KWIECO) Bi Elizabeth Minde zawadi ya Tablet.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee akionesha vitendea kazi alivyokabidhiwa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru vitendea kazi kama mjumbe wa Bodi ya mamlaka hiyo .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Aisha Amour vitendea kazi kama mjumbe mpya Bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa na wajumbe wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.ya Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) . 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAJUMBE WA BODI MPYA YA MUWSA
  1. BIBI ELIZABETH MINDE
  2. ENG: ABDALLA MKUFUNZI
  3. BW: BONIFACE MARIKI
  4. BW: FILBERT KAHETA
  5. BIBI HAJIRA MMAMBE
  6. Mh. RAYMOND MBOYA
  7. Eng. AISHA AMOUR
  8. BW. MICHAEL MWANDEZI
WAJUMBE WA BODI ILIYOMALIZA MUDA WAKE
  1. Mh. SHALLY RAYMOND (MB)
  2. Mh. JAPHARY MICHAEL (MB)
  3. Eng. ALFRED SHAYO
  4. BW. JESHI LUPEMBE

UVCCM MUFINDI WATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO

October 15, 2016

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa  akikagua gwaride la vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakati wa sherehe siku ya vijana wa chama cha mapinduzi
 mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Yohannis Kaguo kushoto akiteta jambo na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga wakati kukagua mabanda ya maonyesho yaliyofanyika katika  ofisi za CCm wilaya ya Mufindi
katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na
mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga
hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.

na fredy mgunda,iringa

VIJANA wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamewataka wafanyakazi na viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kujituma ili kumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo.

Haya yalisemwa na katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo wakati akisoma lisala kwa mgeni rasmi wakati wa maazimisho ya siku ya vijana wa chama cha mapinduzi yaliyofanyika wilayani Mufindi.

viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

“nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Alisema Ngailo

Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa  uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi vijana tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Alisema Ngailo

Akiongea kwenye sherehe hizo mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo Alieleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi  kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Lwimbo


Lwimbo amebainisha kuwa  serikali itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Lwimbo

Lwimbo amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.

Kwa upande wake katibu wa CCM mkoani Iringa Hassani Mtenga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherhe hizo alisema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.



Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.

“kwa wale mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho na jua mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” alisema Mtenga

Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri wenyewe.

“Saizi unakuta vijana wengi wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo

TUNAENDELEA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA/WAFICHUENI WAFUJA FEDHA ZA SERIKALI

TUNAENDELEA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA/WAFICHUENI WAFUJA FEDHA ZA SERIKALI

October 15, 2016
mla1
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAKAMU wa rais ,Samia Suluhu Hassan,amewataka kuwafichua watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za serikali katika wilaya na mikoa wanaodhaniwa kufuja fedha za serikali na kupoteza mapato lengo ikiwa ni kuzikusanya fedha na kuzirudisha katika mikono ya wananchi waone faida yake.
Amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea na nguvu yake ya kukusanya mapato na kuziba mianya ya rushwa na kupotea kwa mapato na amewasisitiza wananchi kulipa kodi pale inapohitajika ili kusaidia na serikali kuinua mapato yake.
Aidha Samia ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kulinda  amani na usalama wa mkoa huo kufuatia  kujitokeza kwa mambo ambayo yameonekana kuhatarisha usalama wa mkoa hivi karibuni.
Katika hatua nyingine amewahakikishia wakazi wa mji wa Chalinze kutatua tatizo la maji ambalo bado ni kero kubwa ambapo ameeleza kwamba mwishoni mwa mwaka huu matunda yataanza kuonekana.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mlandizi na Chalinze,mkoani Pwani wakati aliposimama kuwasalimia akielekea mjini Dodoma kikazi,alisema wananchi waiamini serikali yao kwani imeanza kuirejesha nchi katika nidhamu ya mapato na matumizi na kazi ya maendeleo inaendelea.
“Watanzania watajenga Tanzania yao wenyewe na serikali yake na Tanzania inaweza kujiendesha yenyewe na kama itategemea misaada iwe sio kwa kiasi kikubwa.”alisema.
Hata hivyo Samia aliwataka wakulima na wafugaji kuishi kwa upendo na mshikamano baina yao pasipo kutofautiana kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha migogoro isiyo na tija na wakati mwingine kuvunja amani.
Kufuatia ombi la mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,kumeelezea kuhusu kero ya maji inayowakabili wakazi wa jimbo hilo,Samia alisema serikali inatambua hilo na kwasasa ipo katika mpango mzuri wa kumaliza tatizo la maji lililopo.
Alielezea kuwa WAMI yapo maji ya kutosha lakini tatizo ni usambazaji ,hivyo wanatarajia kuvuta maji kwa mabomba hadi eneo la Pera na kujenga matanki makubwa yenye ujazo wa lita 300,000 ,Kibiki watajenga tanki lenye ujazo wa lita 200,000 ili maji yakifungwa kuweze kuwa  na maji ya kufikisha kwa wananchi kirahisi.
Makamu huyo wa rais alisema watajenga hifadhi nyingine ya maji pale Mazizi yenye lita mil.2 ambayo itawezesha kutumia maji ndani ya wiki mbili bila kukatika ambapo mpango huo upo njia na tayari mkandarasi yupo na wametanguliza sh.bil 43 ili kazi ianze .
Samia wakati anafanya kampeni ili kuomba kuchagulia kuingia madarakani aliahidi kuwatua akinamama ndoo kichwani kwa kutatua tatizo la maji na kusema anashughulikia suala hilo hadi hapo atakapowaondolea wananachi adha ya kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo muhimu. “Nayachukua mambo yote na nitaendelea kuyafanyia kazi ,natambua kilio chenu hasa akinamama ambao huamka usiku ama kutembea umbali mrefu kutafuta maji”alisema Samia.
Akizungumzia suala la afya kuhusu vifaa tiba alisema atazungumza na wizara husika kutatua kero ya vifaa tiba,madawa na watumishi katika kituo cha afya Msoga ili kupunguza mzigo kwa hospitali za rufaa ikiwemo Tumbi.
Alisema tatizo la watumishi karibu litamalizika,kulikuwa na idadi kubwa ya watumishi hewa hivyo walikuwa wakiisafisha watumishi hao na hivi karibuni watafungua ajira mpya baada ya zoezi hilo kukamilika.
Samia aliipongeza Chalinze kumaliza tatizo la madawati ila kwenye mafanikio kunajitokeza tatizo jingine hasa kutokana na idadi ya wanafunzi imekuwa kubwa na kuzalisha tatizo la madarasa .
Aliwataka viongozi wa wilaya na mkoa kuelekeza nguvu zao kujenga ,kuongeza na kukarabati majengo ya madarasa  ili watoto waweze kusoma .
Kuhusiana na ahadi ya ujenzi wa soko na stend mjini Chalinze,amemuagiza mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo kuhakikisha anasimamia hatua ya tathmini ya eneo lililopatikana kwa ajili ya ujenzi huohadi ifikapo mwezi novemba mwaka huu.
Viwanda na uwekezaji,anasema serikali kwasasa inasuka nguvu za viwanda na uwekezaji mkoani hapo kujenga kwa ajili ya kutengeneza ajira na kukuza uchumi wa mkoa .
Alisema viwanda vikubwa 10 vitajengwa ikiwemo cha chuma na nondo,cha kutengeneza vigae na kusindika matunda  hivyo wananchi wawe tayari kupokea wawekezaji ili kupunguza tatizo la uhaba wa ajira.
Akiwa Mlandizi ,Samia aliahidi kuweka uzio kama alivyoahidi wakati wa kampeni kwenye uchaguzi uliopita katika kituo cha afya Mlandizi  kwani ni moja ya sifa ya kuandishwa kwa kituo cha afya kupanda hadhi ya wilaya na bado wanania ya kupandisha hadhi ya kvituo mbalimbali ili kuzipunguzia mzigo hospitali za rufaa .
Alisema soko la mlandizi bado ni dogo ila ana taarifa kuwa kwenye eneo la Kisabi A na B kuna maeneo yamepimwa kwa ajili ya masoko na Tamisemi wameweka mkono kidogo na kuwahakikishia kuwa atakaa na Tamisemi kuangalia uwezekeno wa kuachia maeneo hayo ili kuwepo na soko na stend kubwa .
Alieleza kupimwa kwa mji wa Mlandizi ataongea na wizara ya ardhi na sasa bahati nzuri  wizara hiyo  wamekuwa wepesi kufanya zoezi hilo hivyo ataweka msukumo kwa wizara ili waweze kupimiwa na  barabara ya Mlandizi-Mzenga ahadi ipo palepale itajengwa kwa kiwango cha lami .
Anafafanua halmashauri ya wilaya ya Kibaha Vijijini inabidi waende Kibaha mjini hivyo watajaribu kuangalia la kufanya ili halmashauri ihamie Mlandizi na ili hali wananachi wapate huduma kirahisi pasipo kwenda Kibaha mjini. Awali mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani,alisema Chalinze inashida kubwa ya maji ,hivyo serikali iangalie jambo hilo kwa jicho la huruma, TANROARS kuchelewesha tathmini ya eneo la soko na stend wakati ikiwa ni ahadi ya mh rais John Magufuli kuhakikisha kunapatikana eneo la soko na stend.
Alisema anaimani na kasi ya serikali iliyopo madarakani na chama cha mapinduzi kuwa watayashughulikia masuala hayo ili kurejesha imani kwa wananchi hao.
Ridhiwani alisema fedha zinazotolewa na serikali kutekeleza masuala ya afya na miradi mbalimbali zitoke na kufanyiwa kazi lengwa badala ya kusemwa midomoni bila kuziona na kuzifanyia kazi.

SAFARI ZA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER JIJINI ARUSHA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHIN

October 15, 2016
Moja ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier  Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakati maafisa wa Mamlaka ya Anga(TCAA) walipokua wakifanya ukaguzi kabla ya kuanza rasmi safari za kibiashara nchini.
Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)wakilakiwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ukaguzi kabla ya safari kwa ndege hizo kuanza.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ,Ibrahim Mussa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA) akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za utalii zitakazotokana na kukua usafiri wa anga nchini.
  Baadhi ya watumishi wa uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakifurahia ndege aina ya Bombadier baada ya kupata nafasi ya kuingia ndani ya ndege hiyo na kujionea mandhari yake.
  Mkuu wa kitengo cha usalama wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ,John Chaggu akijiandaa kuingia ndani ya  ndege kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi katika viwanja vingine nchini ambavyo ndege hiyo itatoa huduma.
  Baadhi ya wananchi waliokua wakipita kando ya barabara walilazimika kuishudia ndege hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.