“WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO”

November 10, 2014
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika
leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga paoo hapo.


 MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)
wilayani Muheza George Mhada kushoto akipokea fedha kutoka kwa Diwani wa Kata ya
Potwe katikati Rashid Mdachi  anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) wilayani humo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.

Afisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)kutoka Makao
Makuu Isaya Shekifu wa pili kulia akifuatilia uandikishwaji wa wanachama wapya wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) leo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika Kata ya Potwe wilayani Muheza wa kwanza kulia ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe kulikofanyika uzinduzi huo,Dr.Swalehe Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.


Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na wafanyakazi wa mfuko wa Bima ya Afya mkoani Tanga,viongozi wa Kata ya Potwe na wanafunzi wa shule ya msingi kwenye Kata hiyo leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasika na kujiunga papo hapo.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu kushoto akipokea risiti ya malipo mara baada ya kujiunga kuwa mwanachama wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF) leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye Kata ya Potwe wilayani humo anayemkabidhi risiti hiyo ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe
wilayani humo Dr.Samweli Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasika na kujiunga papo hapo.

NSSF WALIBEBA TAMASHA LA HANDENI KWETU2014

November 10, 2014
                    
NA MWANDISHI WETU, HANDENI
SHIRIKA la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Tanzania, limejitokeza tena kudhamini Tamasha kubwa la Utamaduni linalojulikana kama ‘Handeni Kwetu’, lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio (Kigoda Stadium), wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Hii ni mara ya pili kwa mfuko huo wa hifadhi kudhamini tamasha hili la utamaduni lilioanza mwaka jana, ambapo lilifanyika kwa mafanikio makubwa kwa kushirikisha vikundi vya ndani na nje ya Handeni, wakiwamo wa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kwamba kujitokeza kwa NSSF ni kitendo cha kiungwana kinacholiweka tukio lao katika kiwango kizuri na mafanikio makubwa.

Alisema kwa kuliangalia hilo, wameamua kutoa haki ya jina, ambapo sasa tamasha lao litakuwa linajulikana kama NSSF Handeni Kwetu, wakiamini kuwa ni ishara nzuri ya ushirikiano baina yao na wadau wote wa shirika hilo.

“Yapo mashirika mengi Tanzania bila kusahau kampuni ambazo zingeweza kudhamini matukio ya aina hii ambayo yana mchango mkubwa kwa taifa letu, lakini baadhi yao yamekuwa magumu mno kudhamini au hata kuyasaidia kwa namna moja ama nyingine.

“Shirika kama NSSF linapoamua kuingia kudhamini ni kuonyesha jinsi wanavyoithamini jamii yao, jambo ambalo kwetu sisi ni furaha kubwa na kuona ipo haja ya kutafuta namna ya kurudisha fadhira kwa wadau hawa muhimu nchini Tanzania,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, siku ya tamasha, kutakuwa na shughuli ya kusajili wanachama wapya wa kujiunga na NSSF, ili waweze kunufaika na huduma za mafao kwenye Shirika hilo kubwa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hapa nchini.

Wadhamini wengine wa tamasha hilo ni pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.