KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA JANA KILILAZIMIKA KUAHIRISHWA BAADA YA MADIWANI KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI CUF KUGOMA KUJIORODHESHA

September 25, 2014

 Kikao cha Baraza  la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga jana kililazimika kuahirishwa baada ya  madiwani kupitia Chama cha Wananchi CUF kugoma kujiorodhesha wakipinga kitendo cha aliyekuwa diwani wa kata ya Marungu  kupitia chama chao na baadaye kuhamia CCM,Mohamed Mambeya kushiriki..

Mambeya alihamia CCM mwezi uliopita na kukabidhiwa kadi ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Abdallah Bulembo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Tangamano.

Kikao hicho ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kupokea taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG),hakikuweza kufanyika kutokana na akidi ya wajumbe kushindwa kufikia theluthi tatu  ya madiwani 35 wa Halmashauri hiyo.

Waliojisajili katika daftari la mahudhurio katika baraza hilo ni
madiwani 21 pekee wa CCM lakini wenzao wa CUF waliingia na kuketi kwenye viti bila kujiorodhesha kwenye daftari  .

Licha ya Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi kuwasihi wajiandikishe katika daftari hilo ili kikao kianze lakini madiwani hao wa CUF walikaa kimya huku nje ya jengo la Halmashauri hiyo kukiwa na ulinzi wa askari wa kikosi cha kuliza ghasia .

Baada ya kusubiri wa kwa saa moja, ndipo Meya akatangaza kuahirisha kikao hicho na kutoa sababu kwamba akidi haikutumia .

Akizungumza mara baada ya kuahirisha kikao hicho ,Diwani wa kata ya Mwanzange kupitia CUF ambaye pia ni Mwenyekiti wa c
Hama hicho Wilaya ya Tanga,Rashid Jumbe alisema wamelazimika kugomea kikao hicho kupinga kitendo cha Mambea kushiriki hali akijua kuwa si mjumbe halali kwa sababu amehama CUF.

“Mambeya anaruhusiwa kushiriki kikao cha baraza la madiwani
kumwakilisha nani wakati amejivua uanachama wa CUF iliyompa tiketi ya kuwa diwani wa kata ya Marungu?kama wanataka ashiriki waitishe uchaguzi agombee akichaguliwa kupitia CCM hatutakuwa na nongwa tena”alisema Jumbe.

Meya wa Jiji la Tanga,Guledi aliifahamisha Mwananchi kwamba
amelazimika kuahirisha kikao hicho kutokana na akidi kutotimia na kwamba ataitisha tena kikao hicho baada ya kujipanga upya.

Alisema kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea taarifa ya CAG na baada ya hapo kumuwezesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutangaza kama imepata hati safi na kwa vigezo vipi.

Kuhusu tuhuma za kumruhusu Mambeya kushiriki kikao hicho,Meya huyo alisema tatizo bado liko kwa uongozi wa CUF kwa sababu bado hawajawasilisha kwake  barua ya kumtaarifu juu ya kuhama kwake katika chama chao.

Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kuahirisha kikao hicho ,Diwani wa kata ya Mwanzange kupitia CUF ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Tanga,Rashid Jumbe alisema wamelazimika kugomea kikao hicho kupinga kitendo cha Mambeya kushiriki hali akijua kuwa si mjumbe halali kwa sababu amehama CUF.

“Mambeya anaruhusiwa kushiriki kikao cha baraza la madiwani
kumwakilisha nani wakati amejivua uanachama wa CUF iliyompa tiketi ya kuwa diwani wa kata ya Marungu?kama wanataka ashiriki waitishe uchaguzi agombee akichaguliwa kupitia CCM hatutakuwa na nongwa tena”alisema Jumbe.

Kuhusu barua,Mwenyekiti huyo alisema CUF ilishamwandikia Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Juliana Malange  ikiamini kuwa ndiye Mtendaji.

“Kama utaratibu ni kumwandikia Meya basi leo hii,tunamwandikia na kumpelekea,ila wafahamu kuwa wanachifanya ni ujanja ambao  hauna maana kwa maendeleo ya wananchi na watambue kama ataendelea kushiriki hatutakoma kufanya mgomo”alisema Jumbe.

Mwenyekiti huyo alisema CUF inaandaa maandamano makubwa yatakayoonyesha jinsi wananchi wasivyoridhishwa na kitendo cha uongozi wa Halmashauri unavyovunja sheria lakini pia CUF itaeleza jinsi fedha zinavyofujwa kupitia Mambea.

Wananchi jijini hapa jana walikuwa katika hofu kwamba ingetokea vurugu katika kikoa hicho kutokana na msimamo uliokuwa umetangazwa na CUF kwamba walikuwa tayari kuuawa na askari polisi kuliko kumwacha Mambeya ahudhurie kikao hicho.

*PRESIDENT KIKWETE MEETS QUEEN MAXIMA

September 25, 2014

 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Special Representative of the UN Secretary General on Sexual Violence in Conflict Dr.Zainab Bangura at the UN Headquarters in New York this morning.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets with Queen Maxima of the Netherlands in her capacity as United Nations Secretary General Special Advocate for Financial Inclusion for Development at the UN Headquarters in New York. Third Left is the Permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr. Servacius Likwelile and fourth left is Tanzania’s Permanent Representative in the UN Ambassador Tuvaku Manongi. Photos by Freddy Maro

*MAMA SALMA KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA AFYA KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI, MATITI NA TEZI NEW YORK

September 25, 2014


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume huko New York.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakimsikiliza Mama Salma alipokuwa anahutubia mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakimsikiliza Mama Salma alipokuwa anahutubia mkutano huo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Debby Rechler (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Yvonne Feinstein ambao ni wafanyakazi wa Tanzania Children Fund wakati wa mkutano wa Wake wa Marais uliofanyika huko New York nchini Marekani tarehe 24.9.2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Jill Bishop, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TET Foundation ya Marekani.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Penehupifo Pohamba mara baada ya kuhutubia mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika New York tarehe 24.9.2014. Katikati ni Princess Nikky Onyeri, Mmiliki wa Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative and Forum of African First Ladies Against Cervical,Breast and Prostate Cancer ya Nigeria.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Princess Nikky Onyeri (kushoto) na Gill Bishop mara baada ya mkutano. PICHA NA JOHN  LUKUWI.
*************************************

KINANA AACHA GUMZO KOROGWE MJINI

September 25, 2014


  • Ashiriki kuchavanga kwenye shamba la Skimu ya Mahenge
  • Nape awafungua vijana kuhusu siasa zisizo na tija 
  • Mrisho Gambo awa shujaa kwa kusema ukweli kwenye kila hoja iliyoletwa na wananchi wa Korogwe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
 Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw. Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza madaraka kuliko utu.

PPF YAENDESHA SEMINA KWA MAAFISA WA MAKAMPUNI MBALIMBALI KATIKA (KANDA YA KINONDONI) MKOA WA TANGA LEO

September 25, 2014

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Bw. Salum Chima akizungumza wakati akifungua semina ya Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika  (Kanda ya Kinondoni) mkoani Tanga leo

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kanda ya Kinondoni (inayojumuisha wilaya za Kibaha,Bagamoyo na mkoa wa Tanga),Bi. Zahra Kayugwa akizungumza na washiriki wa semina ya Mfuko wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika (Kanda ya Kinondoni) mkoa wa Tanga leo.
Maafisa kutoka makampuni mbalimbali katika (kanda ya Kinondoni )mkoa wa Tanga wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa leo.
wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiangalia taarifa kwenye simu ya Meneja wa PPF kanda ya Kinondoni,Mkoa wa Pwani inayojumuisha wilaya ya Kibaha na bagamoyo) na mkoa wa Tanga,Zahra kayugwa leo kabla ya kuanza semina ya mfuko wa pensheni wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika(Kanda ya Kinondoni)mkoa wa Tanga leo.
Meneja wa PPF kanda ya Kinondoni,Mkoa wa Pwani inayojumuisha wilaya ya Kibaha na bagamoyo) na mkoa wa Tanga,Zahra kayugwa (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa Mfuko huo,Mkoa wa Tanga.
washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa mfuko wa Pensheni wa PPF leo baada ya kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chima (aliyekaa katikati mwenye koti jeusi).
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Salum Chima akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF leo.Picha na Oscar Assenga,Tanga.