WIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA VYENYE THAMANI YA MILIONI 200

April 05, 2022

 


Wizara ya Afya leo imepokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi 203,550,000 kutoka Shirika la USAID kwa kushirikiana na JHPIEGO kupitia mradi wake wa Momentum Challenge Global Leadership (MCGL).

Akiongea wakati wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi ametaja vifaa hivyo kuwa ni kompyuta za mezani (Desktops) zipatazo 75 ambazo kupitia Idara yake ya Mafunzo zitasambazwa kwenye vyuo vya kada za Afya vipatavyo sita(6) pamoja na Wizara Makao Makuu.

Prof. Makubi ameishukuru USAID kwa mchango wao mkubwa ambao utakwenda kuboresha mafunzo ya TEHAMA vyuoni na itasaidia kuzalisha wataalamu wa afya wenye ujuzi na umahiri kwenye matumizi hayo nchini.

Ameongeza kuwa vifaa hivyo pia vitachangia kuboresha huduma za mafunzo na amevitaka vyuo vyote vitakavyonufaika na vifaa hivyo kuhakikisha wanatunza na kutumia kwa shughuli zilizokusudiwa.

Hata hivyo Prof. Makubi alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa vyuo vya afya nchini kuzingatia weledi na maadili ya utumishi wa umma kwa maendeleo ya Taifa .

“Ni wakati muafaka kwenu ninyi Viongozi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili yote ya kitaaluma ili mzalishe wataalamu wenye uwezo katika kusaidia utoaji wa huduma za afya zenye ubora.

Kwa upande wake Mwakilishi wa USAID Dkt. Patrick Swai amesema kuwa USAID itaendelea kuisaidia Wizara ya Afya katika kuboreaha utoaji wa huduma za afya nchini.

Dkt. Swai ameongeza kuwa Tanzania ni nchi mojawapo zilizopewa kipaumbele katika mpango wa kushughulikia vifo vinavyoweza kuzuilika vya wajawazito na watoto.

Naye Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Bi.Alice Christensen amesema kuwa Shirika lake litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na kuahidi kuwa mshirika hai katika kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

IGP SIRRO AFUNGUA KITUO CHA POLISI CHA KISASA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

IGP SIRRO AFUNGUA KITUO CHA POLISI CHA KISASA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

April 05, 2022

 

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka watendaji wa Jeshi hilo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi kwa kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu na wahalifu wanazokutana nazo.

IGP Sirro amesema hayo wakati akifungua kituo cha Polisi cha kisasa kilichopo uwanja wa ndege wa Dodoma mkoani Dodoma ambapo ambao ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi na nyumba ya Mkuu wa Kituo cha Polisi umegharimu kiasi cha milioni 115 hadi kukamilika kwake.

Kwenye ufunguzi huo IGP Sirro pia amesema kuwa, ni vyema viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kuwa macho na kuongeza umakini hasa katika kubaini wahalifu, waingizaji wa dawa za kulevya na wamakosa mengine kutokana na uwanja huo kutumiwa na watu mbalimbali kwa shughuli za usafiri wa anga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweli akimuwakilisha Mkuu wa mkoa huo Mhe, Antony Mtaka amesema kuwa, wilaya imeendelea kuhamasisha ufungaji wa kamera za usalama kwa ajili ya kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya sambamba na uhalifu mwingine.

SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NCHINI ZIMEKUA – MAJALIWA

SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NCHINI ZIMEKUA – MAJALIWA

April 05, 2022

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo wa Mwaka 2021 – 2031 baada ya kufungua Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprili 5, 2022. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za kitabu cha Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo wa Mwaka 2021 – 2031  baada ya kuuzindua kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprili 5, 2022. Wa pili kushoto ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul na kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa  Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kikao hicho kwenye ukumbi wa  Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprii 5, 2022.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma  kufungua Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara , Aprili 5, 2022. Kulia ni Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

******************************

  • Awahimiza Watanzania kufanya mazoezi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini imekuwa kwa kiasi kikubwa na imeanza kuleta tija kwa maisha ya Watanzania kutokana na miongozo thabiti inayotolewa na Serikali

“Kwenye Sanaa tumeona namna ambavyo nchi hii imeweza kutangazwa vizuri na wasanii wengi kutoka ndani ya nchi, haya yote ni matokeo ya uratibu unaofanywa na Wizara, kwenye michezo tumeona namna ambavyo leo hii Tanzania inavyopata heshima kwa kuwa na timu za michezo mbalimbali zikifanya vizuri ndani na nje ya nchi.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 5, 2022) wakati akifungua kikao kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Amesema Sekta ya  Utamaduni, Sanaa na Michezo imeonesha kuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wengi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla huku akitanabaisha kuwa sasa kwenye michezo kuna vijana wa Kitanzania wanaocheza michezo ya kulipwa katika nchi mbalimbali.

“Nitumie fursa hii kuwaasa Watanzania kuwa na moyo wa kuthamini kazi za wasanii wetu, Sanaa inatangaza taifa letu na utamaduni wetu pia unaitangaza nchi yetu.”

Waziri Mkuu amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili kuwawezesha Maafisa Utamaduni na Michezo kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Ni Muhimu sasa TAMISEMI kuhakikisha mnatambua umuhimu wa kitengo cha Michezo, Sanaa na Utamaduni katika Halmashauri kuwa ni moja kati ya vitengo muhimu ndani ya Halmashauri, na pia wapate nafasi ya kutumia taaluma yao kutekeleza majukumu ndani ya Halmashauri ili tuone mafanikio ya sekta hii”.

Aidha Waziri Mkuu ameagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha inaandaa vikao kazi vya maafisa utamaduni mara kwa mara ili kuwawezesha kupata mafunzo, kujua changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kupata muda wa kufanya tathmini ya maazimio yanayotolewa katika vikao kazi hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara hiyo kuhakikisha inaboresha uratibu na usimamizi wa mafunzo ya wataalamu wa michezo Nchini ili kuongeza idadi ya wataalam hao hususan katika mpira wa miguu kwani kumekuwa na kiwango kikubwa cha wakufunzi wa mpira kutoka nje ya nchi huku Tanzania ikikosa wakufunzi wanaofundisha nje ya Tanzania.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Maafisa Utamaduni Sanaa na Michezo kusimamia na kuratibu vikundi mbalimbali vya mazoezi vilivyo katika maeneo yao. “Ni jukumu lenu kuhakikisha kila Afisa katika eneo lake anahamasisha na kuanzisha vikundi vidogo vidogo vya mazoezi ili kuwe na hamasa ya michezo kwa watu wa rika zote pamoja na kuibua na kukuza vipaji kwa vijana mbalimbali kwa kuratibu shughuli za makundi ya wasanii.”

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Omari Mchengerwa amesema Sekta ya michezo nchini imeendelea kuimarika na imechangia zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 katika pato la Taifa na Wizara imeendelea kujipanga ili kuhakikisha mchango wa Sekta hiyo unafikisha shilingi  Bilioni 3 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Wizara imeendelea na mikakati ya kufanya maboresho ya miundombinu ya michezo, na hapa ni pamoja na maboresho ya ujenzi wa viwanja vya michezo katika shule 56 ambapo kila Mkoa utakuwa an Shule mbili za michezo, ikienda sambamba na uanzishwaji wa mkakati wa kuibua vipaji wa mtaa kwa mtaa.”

Katika kikao hicho Waziri Mkuu amezindua Mkakati wa Maboresho ya Sekta ya Michezo wa Mwaka 2021/2031 ambao utatoa muongozo wa kusimamia na kuboresha sekta ya michezo Nchini.

MWANANCHI MOMBO ASHINDA PIKIPIKI BONGE LA MPANGO

April 05, 2022

 

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi namba ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi namba ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helmet) ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (katikati) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helmet) ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (katikati) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (katikati) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mshindi wa pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).
Mshindi wa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga akitoa maneno ya shukran kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) kwa kupata zawadi hiyo. Ni baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Na ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Mombo, kabla ya kukabidhi  pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (hayupo pichani) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).



Na Yusuph Mussa, Korogwe

BENKI ya NMB imeendelea kutoa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama guta, baada ya mwananchi wa Kijiji cha Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Justin Magali (44) kuibuka mshindi.

Akizungumza leo Aprili 5, 2022 kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombo Tawi la NMB Mombo, Meneja wa  Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper alisema washindi wa fedha taslimu pamoja na pikipiki ya miguu mitatu, ni wateja wote wa benki hiyo ambao wameweka akiba angalau kuanzia sh. 100,000.

"Ndugu Watanzania zawadi tulizoziandaa kwa wateja walioweka akiba  ya walau sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB, waliingia kwenye orodha ya wanaostahili kushinda. Mpaka sasa tayari kupitia kampeni hii, tumeshatoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi mbalimbali. Pia tumepata washindi 50 wa pikipiki za miguu mitatu ya mizigo.

"Na huyu wa leo ni mshindi aliyejishindia pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya Sky Mark. Zawadi tulizotoa mpaka sasa zina thamani ya sh. milioni 300. Kikubwa leo tunatoa zawadi kwa mshindi wa Kampeni yetu ya Bonge la Mpango Awamu ya Pili ambayo tumeindesha kwa miezi mitatu iliyopita" alisema Prosper.

Prosper alisema Oktoba, 2021, walizindus kampeni maalumu yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania. Kampeni hiyo ilikuja kwa Awamu ya Pili baada ya mafanikio ya Awamu ya Kwanza iliyofanyika mpaka Juni, 2021.

"Kila wiki kulikuwa na washindi 10 wa pesa taslimu, na washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu. Kila mwisho wa mwezi kulikuwa na washindi watatu wa pikipiki za miguu mitatu, na droo kubwa ya mwisho  tumepata washindi 14 wa pikipiki hizi za miguu mitatu za mizigo" alisema Prosper.

Naye mshindi wa pikipiki hiyo, Magali, akizungumza na waandishi wa habari, amewataka Watanzania kuweka akiba Benki ya NMB, kwani pamoja na kupata zawadi ya fedha taslimu ama pikipiki ya miguu mitatu kupitia Kampeni ya Bonge la Mpango, pia fedha zao zinakuwa salama.

MWISHO.