NUSU FAINALI KAGAME
KIINGILIO BUKU TATU TU
Hatua
ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
(Kagame Cup) inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Taifa, huku kiingilio
cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni shilingi elfu tatu (3,000).
Viingilio
vingine vya michezo hiyo ya kesho ni VIP
A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi
(10,000) na sehemu nyingine ya uwanja
iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu,
kijani na rangi ya chungwa.
Timu
nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor
Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu
fainali itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya ijumaa.
Mchezo
wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya
itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta
nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya
makundi.
Katika
mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na
Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali
ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji
nafasi ya kusonga mbele hatua ya fainali.
Gor
Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi
ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita,
sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.
Kocha
Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere
Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha
Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi dhidi ya
Khartoum.
Kwesi
Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu,
Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin
Ibrahim.
Vita
kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman wote
wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili
kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.
Nusu
fainali ya pili itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi ya Mamlaka ya jiji la Kampala (KCCA), mchezo
utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na Kati katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Mchezo
huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa
hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na
nahodha wake John Bocco.
KCCA
chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo
huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi
utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.
Kocha
Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio
Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na
Muzamil Mutyaba.
Azam
FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na
kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Kocha
wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo
haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji
ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.
Hall
atashuka dimbani akiwategema nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey
Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na
mlinda mlango Aishi Manula.
TFF YAIPONGEZA AZAM FC
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za
pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu
fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salam.
Katika
salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na
kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya
fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti
wawakilishi pekee wa nchi kwenye michuano hiyo
TFF
kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam
FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.
TFF YATUMA SALAM ZA
RAMBIRAMBI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya
Moshi Shaban, kufutia kifo cha Moshi kilichotokea jana jijini Dar s salaam na
mazishi kufanyika leo jijini Dar es salaam.
Katika
salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Moshi, TFF imewapa pole wafiwa,
ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha
maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu
Moshi Shaban ni baba wa wachezaji waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya
Tanzania, Haruna Moshi “Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).
TFF YAANDAA KOZI YA WAAMUZI
WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2015/2016
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa kozi ya waamuzi wa mpira
wa
miguu watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza 2015/2016,
kozi hiyo itafanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21 -24/08/2015.
Washiriki
wa kozi hii ni waamuzi waliochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
msimu wa 2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45 kwa wanawake na
miaka
23 – 45 kwa wanaume.
Waamuzi
wote wanatakiwa kuripoti tarehe 21/08/2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume
Ilala Dar es salaam na wawasilishe vyeti halisi vya kuzaliwa na nakala
zake.
Pamoja
na cheti cha kuzaliwa kwa kila mwamuzi ni lazima alete kadi ya kupigia kura au
passport ya kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa umri wake.
Washiriki
wa kozi watafanya mitihani ya kupima afya, utimamu wa mwili na sheria za mpira
wa miguu Trivia (kuandika), video clips (offside na match analysis).
Waamuzi
watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi arobaini (40) na
waamuzi
wasaidizi sabini (70) watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
kwa
msimu wa 2015/2016. Shirikisho
linawatakia wote maandalizi mema.
Baada
ya kozi ya waamuzi kutakuwa na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi
Daraja la Kwanza ambayo itafanyika kuanzia tarehe 24/08/2015 hadi tarehe 25/08/2015.
Makamisaa
wote wanatakiwa kuripoti tarehe 23/08/2015 saa 10:00 alasiri uwanja wa Taifa,
Makamisaa watakao husika na kozi hii ni wale wote walio simamia michezo ya Ligi
Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2014/15.
Makamisaa
watafanya mtihani wa sheria za mpira wa miguu (Trivia, offside, match analysis)
na kupima mwamuzi anapochezesha (evaluation).
Wale watakaofaulu ndiyo watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
--
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania