NAMAINGO YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUKU WA KIENYEJI LIND

January 21, 2017
 Wakiwa na furaha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Limited, Ubwa Ibrahim baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji  Kuku kwa wanachama 3000 wa kampuni hiyo kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Miteja, wilayani humo juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akifungua mlango katika banda la vifaranga vya mbegu vya mradi huo
 Vifaranga vya mbegu ya kuku wa kienyeji vinavyofugwa kisasa
 Mpiga Picha wa Gazeti la Tanzania Daima,  Said Powa ambaye aliliwakilisha kundi la Wananchama Wanahabari la Kwanza One akipokea cheti cha usajili kutoka kwa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mjaka wakati wa hafla hiyo
 Kundi la Wanahabari la Kwanza One likishangilia kwa furaha baada ya kukabidhiwa cheti cha kuwa miongoni mwa wanachama watakaoshiriki kwenye mradi huo
 Mbegu za mazao zilizooteshwa kwa ajili ya kulisha kuku

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Kuu ya Shitindi Poutry Farm, Shitindi (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi, ambapo aliahidi kununua mayai ya wanachama wa ufugaji wa kuku wa Namaingo.


 Ni burudani kwa kwenda mbele
 Mtalaamu wa ufugaji kuku wa kienyeji akielezea jinsi mfugaji anavyoweza kuzalisha majani ya malisho kwa kutumia mazao mblimbali

 Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo, Ubwa Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo
 Mjaka akihutubia wakati wa hafla hiyo
 Baadhi ya Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba
 Moja ya mabanda ya kuku yaliyoandaliwa kwa ajili ya
Wanachama wakifurahia baada ya kukabidhiwa cheti cha usajiri wa Biashara cha Brela


Mwenyekiti wa Namaingo Mkoa wa Ruvuma akipokea cheti cha Brela
Dk. Hassan Kijaki Mtaalalamu wa Mifugo wa Mkoa wa Lindi akielezea kufurahishwa na kitendo cha Namaingo kuwekeza mradi wa kuku mkoani humo.
Mchumi wa Mkoa wa John Mwalongo akihutubia wakati wa hafla hiyo
Bi Ubwa na Mjaka wakikagua bidhaa mbalimbali za wAJASIRIAMALI ZILIZOFUNGWA KWA NJIA YA KISASA


MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA KILIMO NI UKOMBOZI KWA WAKULIMA NA TAIFA KWA UJUMLA

January 21, 2017
 Watafiti wakiwa lango kuu la kuingia katika  shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO), chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma. Watafiti hao walikuwa wameongoza na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kutembelea shamba hilo.

 Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada ya matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa katika sekta ya kilimo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda (kulia), akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (wa pili kushoto), alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) lililo chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma juzi. 
 Msafara ukielekea kwenye shamba hilo la majaribio.
 Waziri Tizeba (wa sita kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo mbele ya shamba hilo la majaribio ya mbegu za mahindi katika kituo cha kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma.
Watafiti na Waziri Tizeba wakijadiliana mbele ya shamba hilo.

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

MATUMIZI ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Sekta ya Kilimo nchini yataleta mafanikio makubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Hayo yalielezwa na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma. 

"Matumizi ya Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na ukame kutokana na tabia nchi" alisema Dk.Nyange.

Alisema taaluma ya uhandisi jeni inawezesha kuhamisha jeni kutoka kwa kiumbe hai kimoja na kuingiza katika kiumbe hai kingine ili kupata sifa lengwa na kutengeneza bidhaa kwa matumizi mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu usalama wa matumizi ya Bioteknolojia hapa nchini alisema ni vema kuanza mchakato wa kuendeleza mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki (GMO) ambayo yameleta mafanikio makubwa katika nchi nyingine kwa mfano mahindi yanayostahimili ukame na bungua muhogo unaostahimili ugonjwa wa batobato na michirizi kahawia, migomba yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa mnyauko na pamba yenye ukinzani kwa wadudu waharibifu.

Dk. Nyange alisema Changamoto kubwa iliyopo katika matumizi ya teknolojia hiyo ni kuongezeka kwa upotoshaji kutoka kwa wanaharakati na wapinzani kutokana na 
ufahamu na uelewa wa watafiti, viongozi, wanasiasa na umma kwa jumla kuhusu masuala ya taaluma hiyo kuwa  bado ni mdogo ukiwemo uwekezaji mdogo katika utafiti na maendeleo.



WATUMISHI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KULIMA MAZAO YANAYOTUMIA MAJI KWA UFANISI

WATUMISHI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KULIMA MAZAO YANAYOTUMIA MAJI KWA UFANISI

January 21, 2017
IKUMkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akionyesha mbegu bora ya muhogo aina ya Momba inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na anayefuata ni Afisa Kilimo halmashauri ya Singida  Abel Mungale.
IKU 1
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akiandaa mashimo ya kupanda mbegu bora ya mbaazi inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida.
IKU 2
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipamba mbegu bora ya mbaazi inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida, anayefuata ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida Eliya Digha.
IKU 3
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akiwaonyesha watumishi wa  halmashauri namna ya kupanda mbegu bora ya mbaazi katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida.
IKU 4
 Watumishi wa halmashauri ya Singida wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi (hayupo pichani).
IKU 5
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda mti wa mwembe katika eneo la sekondari ya Ilongero Wilayani Iramba.
IKU 6 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe na mihogo katika shamba la mkulima bora wa eneo la Old Kiomboi Wilayani Iramba.
……………….
Watumishi wa halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida wameagizwa kulima nusu ekari ya mazao yanayotumia maji kwa ufanisi hasa zao la muhogo, viazi au mtama ili kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha msimu ujao huku shule zote zikiagizwa kulima ekari moja ya mihogo au mtama ili wanafunzi wapate chakula shuleni.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimi ametoa agizo hilo alipotembelea na kuzindua shamba la mbegu bora ya mihogo la ekari kumi lililopo kijiji cha Mpambaa, Halmashauri ya Singida ambalo litazalisha mbegu kwa ajili ya wakulima wa Mkoa wa Singida.
Dokta Nchimbi ametumia kauli mbiu ya kuongoza ni kuonyesha njia kwa kulima mihogo shamba lake mwenyewe lenye ukubwa wa ekari tatuna hivyo kuwaagiza watumishi na viongozi wote kuonyesha mfano kwa kulima mazao hayo kwa msimu huu.
Pamoja na upandaji wa mbegu za Muhogo, Dokta Nchimbi pia amezindua shamba la mbegu bora za mbaazi kwa kupanda mbegu hizo pamoja na kupalilia shamba la mbegu bora za mtama ambapo aina 25 za mtama zinafanyiwa majaribio ili kupata mbegu itakayofaa kwa mkoa wa Singida.
Aidha ametembelea mashamba ya wakulima wa mtama wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi pamoja na kushiriki upandaji wa mtama wa shamba la shule ya Msingi Mampanta wilayani Iramba na kupanda viazi na mihogo katika shamba la Mkulima wa Old Kiomboi wilayani Iramba.
Amesema wakulima wakielimishwa juu ya mazao yanayotumia maji kwa ufanisi watapanda mazao hayo ambayo ni mtama, viazi, muhogo na mbaazi ambapo wakulima watakuwa na uhakika wa chakula pamoja na kujipatia fedha kwa kuuza mazao hayo.
Dokta Nchimbi ametoa hamasa kwa wakulima wote kulima mazao hayo yanayotumia maji kwa ufanisi na wajitume kwa bidii kuliko kulalamikia serikali bila kufanya kazi kwakuwa awamu ya sasa ya uongozi ni ya kuchapa kazi kwa bidii.
Wakati huo huo Dokta Nchimbi amefanya vikao na watumishi wa halmashauri za Singida, Ikungi na Iramba mara baada ya kutembelea mashamba ya wakulima na kushiriki nao katika kupanda mtama, kupalilia baadhi ya mashamba, kupandqa mihogo na viazi.
Dokta Nchimbi amewaasa watumishi wote Mkoani Singida kuwa waadilifu, wachape kazi na hasa kulima mazao yanayotumia maji kwa ufanisi pamoja na kufanya shughuli nyingine za kuwaingizia kipato kama vile kufuga kuku na kuwa na mizinga ya nyuki ili wawe na kipato kingine nje ya mshahara.
Amesema watumishi wengine hujiingiza kwenye wizi kutokana na tamaa tu ila endapo watakuwa na vyanzo vingine vya fedha nje ya mshahara itapunguza kutokuwa waaminifu pamoja na kutokulalamika mara kwa mara.
Baadhi ya watumishi waliohudhuria vikao hivyo wamempongeza Mkuu wa Mkoa Dokta Nchimbi kwa nasaha alizowapa huku wakiahidi kuchapa kazi kwa bidii na uadilifu pamoja wakijishughulisha na kilimo ili wawe na kipato cha ziada.
NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

January 21, 2017
SAUTO
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo.
SAUTO 1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu   kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
SAUTO 2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari  lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele  ni   Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia)  na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
SAUTO 3
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula.
SAUTO 4
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-MAJALIWA

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-MAJALIWA

January 21, 2017
NJO 1
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga sh. bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 kwa kiwango cha lami.
Ametoa kauli hiyo jana  (Ijumaa, Januari 20, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete alipowasili katika kata ya Mtamba wilayani hapa akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.
Waziri Mkuu amesema usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makete kwa ujenzi wa kiwango cha lami umekamilika hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na subira.
Amesema barabara nyingine inayotarajiwa kujengwa ni ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Isyonji yenye urefu wa kilomita 96 ambayo imetengewa sh. milioni 50 kwa ajili ya kufanyiwa usanifu.
Waziri Mkuu amesema wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwani imedhamiria kuwatumikia kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wahandisi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawasimamia vizuri wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali katika halmashauri zao kuhakikisha kama viwango vinalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa Idara katika halmashauri kupambana na vitendo vya rushwa na wahakikishe watumishi hawatowi huduma kwa kuomba rushwa.
“Kwanza watumishi watambue kwamba rushwa ni dhambi. Pia kiutumishi ni makosa makubwa hivyo wajiepushe na vitemdo hivyo,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Veronica Kessy amesema kujengwa kwa barabara hizo kwa kiwango cha lami kutaimarisha ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo na Mkoa wa Njombe kiujumla hivyo wananchi kupata tija.
“Mfano barabara ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Bulongwa, Iniho, Kikondo na Isyonje itasaidia wilaya kufunguka hivyo kurahisisha usafirishaji wa mazao ya misitu kama mbao,” amesema.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema barabara hii pia itaunganisha Wilaya hiyo na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Songwe hivyo watapata fursa ya kuanzisha kilimo cha maua. Awali walishindwa kulima maua kwa sababu hakukuwa na usafiri wa uhakika.
Awali Waziri Mkuu alitembelea shamba la mifugo la Kitulo linalomilikiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lenye jumla ya Ng’ombe 750 wakiwemo ndama 61, majike 212, mitamba 273, madume 21, na madume wadogo 183.
Shamba hilo linazalisha wastani wa lita 450,000 za maziwa kwa mwaka kutokana na ng’ombe 123 wanaokamuliwa. 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 21, 2017.

SERIKALI KUANGALIA UPYA KANUNI ZA TAFITI ILI ZIWEZE KUFANYA KAZI KWA WAKATI

January 21, 2017


 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Waziri Tizeba.
 Mkutano ukiendelea.
 Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kuhusu, Bioteknolojia ya kisasa katika sekta 
ya kilimo nchini.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa mada kuhusu utafiti wa mahindi yanayohimili ukame.
 Taarifa ikitolewa mbele ya Waziri Tizeba (kushoto)
 Safari ya kuelekea shamba la jaribio la mbegu za mahindi ikiendelea. Katikati ni Waziri Tizeba.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi kuhusu shamba hilo la jaribio hilo.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
 Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba  (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.

Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.

"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.

Alisema ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.

Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.

"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais  Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.

Alisema kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.

Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.

Akizugumzia kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya wananchi kuhusu matumizi ya  vyakula vya GMO alisema mitazamo hiyo inachochewa na wanaharakati kwa faida zao binafsi na kama wanaushahidi wa jambo hilo ni vizuri wakatoa ushahidi huo hadharani badala ya kupotosha umma.

"Kama mtu anaushahidi huo namuomba aniletee badala ya kuzungumza mitaani kwani wenzetu wa nchi zingine wanatumia vyakula hivyo na kama vingekuwa si sahihi wangewezaji kuvitumia" alihoji Tizeba.



Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk.Hassan Mshinda alisema kazi kubwa ya Costech ni kufadhili tafiti mbalimbali na kuhakikisha zinawafikia walengwa na akaishukuru serikali kwa hatua iliyofikia ya kuona taratibu na kanuni zilizopo jinsi zinavyorudisha nyuma maendeleo ya tafiti hizo za uzalishaji wa mbegu ambazo zikipatikana kwa wingi bei yake itakuwa ndogo tofauti na sasa na kumkomboa mkulima.