TAARIFA: POLISI WAKAMATA BUNDUKI AINA YA SMG NA JUMLA YA RISASI 59 PAMOJA NA WATUHUMIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI JIJINI DAR

June 06, 2015

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.

Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS  maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa  HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31, Mfanyabiashara, Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10. Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa, wanajihusisha na unalifu wa kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichan) Bunduki aina ya (SMG) iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10.
Katika tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko maeneo ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya kuwakurupua vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.

Hii ni kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa taslim TSHS. 300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Kawe na ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha risasi zilizokamatwa katika oparesheni hiyo.
Wakati polisi wakijiandaa kuwakamata walikurupuka na kukimbia ndipo polisi walifanya upekuzi wa eneo hili na kufanikiwa kupata risasi hizo zikiwa katika mfuko wa plastiki maarufu kama “mfuko wa Rambo”. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na
1. RAMADHANI S/O NUHU, Miaka 20,  Mkazi wa Kiwangwa.
2. ABED S/O SALUM, Miaka 18, MKAZi wa Kibaoni.
3. HANIF S/O HAMIS, Miaka 19, MKAzi wa Tegeta.

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro Sirro akiwaonesha baahdhi ya waandishi wa habali hawapo pichan Bembe za Ndovu zilizo kamatwa maeneo ya Kimara Suka katika oparesheni ukaguzi wa magari.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
KUKAMATWA KWA ROLA 15 ZA NYAYA ZA UMEME PAMOJA NA WATUHUMIWA SABA.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata kontena lenye namba 00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya (zenye thamani ya shilingi 150,000,000/= milioni mia moja na hamsini) zilizoibwa tarehe 26/02/2015 zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA). Baada ya wizi wa kontena hilo kesi ilifunguliwa kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa watano walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Wakati upelelezi ukiendelea ndipo tarehe 25/05/2015 Polisi Buguruni walipokea taarifa toka kwa msiri kwamba huko maeneo ya Kibamba mtaa wa Kibwegele wilaya ya Kimara Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuna kontena limefichwa katika kiwanda cha kutengeneza matofali.

Askari wa kikosi kazi walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo lenye namba 00LU2876031 na walimhoji mlinzi wa eneo ili kupata mmiliki wa eneo na kontena hilo. Ilipofika saa 23:55hrs mmiliki wa eneo hilo aitwaye DONESIA D/O AIDAN @ KIFYOGA, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Makabe ambaye ni mtuhumiwa wa sita.
Taratibu zilipokamilika kontena hilo lilifunguliwa ndipo zilipokutwa rolla za nyaya zipatazo 15 kati ya 17 zilizokuwepo katika kontena hilo siku lilipokuwa linasafirishwa. Tarehe 27/05/2015 majira ya saa 00:30hrs maeneo ya Kimara mwisho alikamatwa mtuhumiwa mwingine wa saba PROSPER S/O MTEI, Miaka 43, Mfanyabiashara  na upelelezi unaendelea ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi.

KUKAMATWA KWA BASTOLA MOJA NA MAGANDA YA RISASI
Mnamo tarehe 28/05/2015 majira ya saa 23:00hrs maeneo ya Kiwalani Minazi Mirefu Kata ya Ilala WIlaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Polisi walifanikiwa kukamata silaha Bastola yenye nambari 05532 pamoja na maganda mawili ya risasi aina ya SMG katika eneo la tukio baada ya majambazi kuitelekeza mara walipozingirwa na wananchi waliotaka kuwakamata.
Majambazi hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya vingunguti wakitumia pikipiki mbili ambapo moja ina namba za usajili MC610 ABU aina ya Boxer rangi nyekundu ambayo pia waliipora kwa mtoa taarifa. Aidha katika tukio hilo pia majambazi hao walimpiga mtoa taarifa na kitako cha bunduki waliyokuwa nayo kisha kumpora pikipiki hiyo na pesa taslim shilingi 300,000/= Hata hivyo majambazi hao walifanikiwa kutoroka. Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliweza kuikamata pikipiki hiyo.

KUKAMATWA KWA VIPANDE 20 VYA PEMBE ZA NDOVU.
Katika oparesheni iliyoendeshwa tarehe 25/05/2015 na idara ya INTERPOL jijini Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine. Ilipofika majira ya saa 18:00hrs maeneo ya Kimara Suka ambapo kutokana na foleni ya magari iliyosababishwa na ukaguzi wa magari katika zoezi hilo alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39- 45 kwa dhumuni la kukodi pikipiki.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya kuwaona askari wa unifomu kijana huyo alitupa kifurushi alichokuwa nacho na kukimbia. Askari walilichukua hilo furushi na kulipekuwa na kukuta kuna meno ya tembo vipande ishirini pamoja na nguo kuku. Kielelezo kilipelekwa kituo cha Polisi Mbezi na kufunguliwa jalada la uchunguzi KMR/PE/67/2015.

KUKAMATWA KWA MLIPUKO, VIFAA VYA KUVUNJIA, DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA MTUHUMIWA.
Tarehe 04/06/2015 majira ya saa 10:00hrs maeneo ya Chamazi ulifanyika msako mkali wa kupambana na uhalifu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa MICHAEL S/O KASAMBALE, Miaka 28, Mkazi wa Chamazi akiwa na mlipuko mmoja na vifaa vya kuvunjia. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika. Aidha mtuhumiwa huyo amekamatwa na kete kadhaa za madawa ya kulevya.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA AKIWA NA BASTOLA BANDIA
Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa JACOB S/O NATHANIEL MWETA, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kimara ambaye alikuwa anaitumia kutishia watu kisha kupora. Mtuhumiwa ame kiri kuhusika katika matukio kadhaa ya unyang’anyi hasa katika maeneo ya Tegeta na Kunduchi jijini Dar es Salaam.

MAFANIKIO MENGINE YA OPARESHENI INAYOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparesheni ya kupambana na uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata vitu vifuatavyo:
1. Mitambo mitano (5) ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo)
2. JUmla ya lita mia mbili (200) za pombe ya Moshi (Gongo)
3. Gunia mbili za banghi.
4. Kupatikana na Mirungi box moja (1).
5. Kete kadhaa za madawa ya kulevya.


SIMON SIRRO – DCP
KNY. KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
MWIGULU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

MWIGULU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

June 06, 2015

Mh.Mwigulu akiwasili makao makuu ya CHAMA CHA MAPINDUZI mjini Dodoma kwaajili ya Kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.
Mh:Mwigulu akisaini kitabu cha Wagombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi.
Mh:Mwigulu Nchemba na Mke wake Bi.Neema Mwigulu wakifurahia kukabidhiwa nyaraka mbalimbali za kufanikisha mchakato wa Kutafuta Wadhamini Nchi Nzima kuelekea hatua ya pili ya Mchujo wa Wagombea Urais ndani ya CCM.
Mwigulu Nchemba akimtambulisha Mke wake Bi.Neema Ngure kwa Umma wa Watanzania kuwa ndiye FIRST LADY ajaye wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa anateta na mtu mwenye Ulemavu mara baada ya kupokea Nyaraka za Kuanza safari ya Kuwania Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Nje ya Ukumbi wa NEC hapa Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi,Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Mkewe Bi.Neema Mwigulu wakilakiwa na mamia ya Wananchi waliojitokeza kuwasapoti hii leo wakati wa uchukuaji wa fomu ya Kuwania Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM.
Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kumsapoti Mh:MWigulu Nchemba wakati wa uchukuaji wa fomu ya Kuwania Urais wa JMT.
Mh:Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi waliofika kumsapoti wakati wa Uchukuaji wa Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.
 
Picha na Maelezo na Festo Sanga

CHADEMA YATIKISA ARUSHA

June 06, 2015

 Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"
 Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura" Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha  AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
 umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha
Mjumbe wa Kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum Mh Grace Kiwelu amewataka Wanawake kuwa Chachu ya mabadiliko kwa Taifa letu."MUDA WA KUDANGANYWA KWA KANGA UMEPITA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI OCTOBER TUPATE UHURU WA UHAKIKA,WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZA"
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na Chadema Kanda Ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za Hamasa ya kujiandikisha kanda ya kaskazini amewaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndio imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili October tufanye maamuzi sahihi

Mbunge wa Rombo Joseph Selasini" WATANZANIA WENZANGU HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OCTOBER TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIO SAFARI YA MATUMAINI"
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mh Pauline Gekul awatakwa Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi wetu kwa kutumia simu mitandao ya kijamii vikao vya kijamii ili ifikapo October tuiondoe CCM madarakani.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI. 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Rebecca Mgodo amewataka wananchi kusoma nyakati"NDUGU ZANGU MIAKA YA MATESO KWA WATANZANIA SASAS IMEFIKA MWISHO, TWENDENI KWA UMOJA WETU TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURATUITOE CCM MADARAKANI"-Mgodo
Mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Kaskazini Mh Israel Natse akiwaongoza viongozi na Wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuingia uwanjani huku wakiwapungia wanachama na wapenzi wa Chadema waliofika uwanjani vya kilombero (PICHA NA WOINDE SHIZZA)

Balozi Seif Iddi afungua Semina ya usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar

June 06, 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua Semina ya siku moja ya Usafiri Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika kwenye ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Juma Duni Haji akitoa maelezo kwenye Semina ya Usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kabla ya ufunguzi wa Senmina hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wadau wa usafiri walioshioriki semina ya usafiri wa bara barani wakifuatilia Horuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupa Pichani.
Mkurugenzi wa Idara ya Usafiri na Leseni Nd. Suleiman Kirobo akitoa Mada kwenye Semina ya Usafiri wa Barabarani iliyoshirikisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wadau wa sekta ya usafiri.
Mkuu wa Kikosi cha UsalamaBara barani Kamishna Msaidizi wa Polisi { ACP } Nassor Ali Moh’d akitoa ufafanuzi wa ajali za barabarani zinazoonekana kuongezeka kutokana na matumizi mabovu ya bara bara kwenye semina ya usafiri wa bara barani. Picha na – OMPR – ZNZ.

Viongozi wenye fursa za maamuzi pamoja na nyadhifa katika Taasisi za Umma Nchini wameombwa kuwaelimisha Vijana wao wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani badala ya kuwasubiri kuwaombea wanapokamatwa na askari wa usalama bara barani kwa kufanya makosa tofauti ambayo mengi kati yao ni yale ya  makusudi.

Akiifunguwa Semina ya usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hapo kwenye ukumbi wa Baraza hilo Mbweni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya viongozi kuwaombea Vijana wao kuwachiliwa kwa makosa yao ya makusudi ni kuwavunja moyo Polisi na kupelekea kuonekana hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.

Balozi Seif alisema imekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa kwa baadhi ya Viongozi   kuwaombea vijana wao wasifikishwe Mahakamani  wakati wanapofanya  makosa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaondosha heshima yao ndani ya jamii.

Alisema uvunjwaji wa sheria za usafiri wa barabarani unaofanywa na watumiaji wa barabara hizo kama waendesha vyombo vya moto, gari zinazobururwa na wanyama, baskeli na ha waendao kwa miguu husababisha  ajali zinazoleta  madhara kwa Taifa.

Alisema jamii imekuwa shahidi iliwaona Vijana wanaoendesha Vyombo vya ringi mbili Vespa na Pili pili wakipakizana watu zaidi ya wawili katika chombo huku wakifukuzana kwa mwendo wa kasi wakiwa wamekaa katika mkao wao maarufu   { T. ONE } huku vyombo hivyo vikichomolewa breki kwa makusudi.

Alisema chakusikitisha zaidi baadhi ya vijana hao huendesha vyombo hivyo kwa ringi moja tuu vikiwa kwenye mwendo mkali bila ya hata kuvaa kofia ngumu lakini jambo  la ajabu zaidi baadhi yao ni viongozi katika Jamii hii.

Mapema Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mh. Juma Duni Haji  alisisitiza umuhimu wa mashirikiano ya pamoja kwa Taasisi zote zinazosimamia  shughuli na harakati za Bara bara ndio njia pekee itakayosaidia kupunguza au kuondosha kabisa changamoto ya usafiri wa Barabarani.

Wakitoa mada kwenye semina hiyo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu usafiri na usalama Barabarani Mkurugenzi wa Idara ya usafiri na Leseni Nd. Suleiman Kirobo, Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Msaidizi Kamishna wa Polisi ACP Nassor Ali Moh’d pamoja na Mdau wa Sekta ya Usafiri Bwana Waziri Hashim  walisema zipo sheria zilizopitwa na wakati mabazo kutofanyiwa marekebisho ya haraka zitaendelea kuchangia matatizo yanayopatikana katika matumizi ya usafiri wa Bara barani.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/6/2015.
 MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA YA GBP MKOANI TANGA

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA YA GBP MKOANI TANGA

June 06, 2015
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Jeti ya kupokelea mafuta na Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana Juni 5, 2015.
Picha zote na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kukagua kituo hicho cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoizana na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya GBP, wakati akielekea kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, (wa pili kulia) wakati alipotembelea Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo, akiongozana na Mkurugenzi wa ya GBP, Badar Seif Sood (kushoto), Waziri wa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge na baadhi ya viongozi, baada ya ukaguzi wa Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, jana mkoani Tanga.

LOWASSA ASHIRIKI JUBILEE YA MIAKA 50 YA SEMINARI YA MTAKATIFU KALOLI LWAHANGA, HUKO NGARA

June 06, 2015


Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,
(wapili kushoto), akiwa na Askofu  wa
Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemuguzi baada ya
kuzindua jiwe la msingi kuashiria maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50, Seminari
ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Jumamosi
Juni 6, 2015
Waziri  Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa, akisalimiana na
Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge
Ngara, Severine Niwemuguzi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Biharamulo
Mkoani Kagera kwa ajili ya kusherekea Miaka 50 ya Seminari ya Katote

Lowassa,
akiwasha kompyuta baada y kuzindua chumba cha mafunzo ya Kompyuta
katikaKuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 Seminari ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga
Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara mkoani KageraJumamosi Juni 6, 2015.
Kushoto ni  Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Severine
Niwemuguzi