SERIKALI KUCHUKUA RANCHI ZISIZOENDELEZWA.

October 26, 2017
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akilakiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe 
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mkinga (OCD) kushoto ni Katibu Tawala wa Mkinga,Joseph Sura
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili wilayani Mkinga
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega kulia akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kushoto wakati akisoma taarifa ya wilaya hiyo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali wilayani humo

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akiagana na na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kulia mara baada ya kusaini kitabu cha wageni na kupata taarifa ya wilaya hiyo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akilakiwa na Diwani wa Kata ya Mwakijembe.
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe kulia ni Diwani wa Kata ya Mwakijembe
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akizungumza na Jamii wa Wafugaji wa Kimasai na wakulima katika Kijiji cha Perani ambapo aliwataka kuishi kwa amani kwa kufuata taratibu ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema serikali itazirejesha ranchi zote zilizobinafsishwa na kushindwa kuziendeleza.
Amesema ranchi hizo zitagawiwa kwa wafugaji ili kufunguza tatizo la malisho nchini jambo.

Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa wilayani hapa wakati wa ziara yake ya siku moja ambapo alisema kwamba lengo la kuchukua ranchi hizo ni kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambao kwa mara kadhaa wamekuwa wakigombania maeneo ya ardhi kwa ajili ya malisho na kilimo.

Alisema kwamba serikali imeamua kuchukua uamuzi huo ili kuepusha wafugaji waishio mipakani wasipeleke mifugo yao katika nchi jirani ambako kuna malisho.

IDHAA YA KISWAHILI YA DW YAANDAA MDAHALO MKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM IJUMAA HII

October 26, 2017

Tigo Kukabidhi Nyenzo za Kidigitali shule ya sekondari wasichana Machame

October 26, 2017



Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa akikata utepe kuzindua rasmi maabara yenye nyenzo za elimu ya kidigitali ya Tigo eSchools kwa shule ya sekondari  wasichana Machame jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo.


Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa (aliyekaa kulia)akipata maelezo ya matumizi ya kujisomea vitabu kwa njia ya mtandao kupitia Tigo eSchools toka kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari wasichana Machame, Delynes Laurian mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhi huduma hiyo shuleni hapo jana.
Mtaalam wa tovuti toka Shule Direct, Emmanuel George akielezea jambo kwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gelacius Byakanwa wakati wa uzinduzi wa Tigo eSchools shule ya wasichana Machame leo. Wengine nyuma kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini, Henry Kinabo, mwalimu mkuu wa shule ya Machame, Asteria Massawe
Umati wa wanafunzi wa  shule ya wasichana Machame Machame wakiwa wanashuhudia uzinduzi wa Tigo eSchoolsl mapema jana.

WAGOMBEA UDIWANI WA CCM WAREJESHA FOMU DAR, LEO

October 26, 2017
 Wagombea Udiwani wa CCM katika Uchaguzi wa marudio katika Kata ya Saranga Wilayani Ubungo na Kata ya Kijichi wilayani Temeke leo wamerudisha fomu zao kwa wasimamizi wa uchaguzi katika kata hizo kwa kishondo huku wakisindikizwa na viongozi kadhaa ya wa CCM wakiongozwa ana Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe. Pichani, Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akimkabidhi fomu yake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja.
 Waendesha bodaboda wakiwa kwenye msafara kumsindikiza mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga, leo
 Mashabiki wa CCM wakiwa kwenye bajaji kwenye msafara kumsindikiza mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga, leo
 Masafara wa baadhi ya viongozi wa CCM wakipeleka mgombea wa CCM kurejesha fomu kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Saranga  
 Mwananchi aliyekuwa katika shughuli zake akishangilia msafaya wa mgombea huyo wa CCM wa Udiwani Kata ya Saranga
 Shamrashamra za wana CCM zikihanikiza baada ya msafara wa mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Saranga kufika kwenye Ofisi za Afisa Mtendaji wa wakata hiyo
 Mgombea Udiwani wa CCM katika uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga Haroun Mdoe (mwenye fulana yenye jina kubwa la Samia) akishangiliwa wakati akiwasili kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya saranga kurejesha fomu yake.
 Wanachi na wana CCM wakimsindikiza kuingia kwenye Ofisi mgombea huyo
 Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akikabidhiwa fomu za kiapo na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo, kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo, huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe (kulia) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja (kushoto) wakishuhudia.
 Msimamizi huyo msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Saranga akitazama kama Mgombea huyo wa CCM anajaza fomu yake kwa usahihi. Kulia ni Kusilawe. 
 Mgombea wa CCM akiijaza fomu yake ya kiapo
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akimwelekeza mgombea wa CCM ili asikosee wakati wa kujaza fomu yake ya kiapo 
 Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akimkabidhi fomu yake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja.
 Mgombea huyo wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Saranga (wapili kushoto) na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kukabidhi fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea
 Baadaye mgombea huyo akapiga picha ya pamoja na viongozi wa CCM waliosindikiza na baadhi ya wana CCM waliofika kwenye Ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Saranga kushuhudia akirejesha fomu. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam saad Kusilawe akimpongeza Mgombea Udiwani wa CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga Haroun Mdoe baada ya urejeshaji fomu kukamilika. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ubungo Lucas Mgonja na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalli.
 ---------------------

TBL EXPERIENCES PHENOMENAL GROWTH

October 26, 2017
The TBL Managing Director who is also AB-inBev’s President of the East African Business Unit,Roberto Jarrin ,at the Second Ministerial Dialogue with the Private Sector whose theme was “ The Sate of Doing Business in Tanzania”. --- We have experienced phenomenal growth from the second quarter of this year and will soon be looking to increase our production capacities, says the TBL Managing Director, Roberto Jarrrin. Jarrin was speaking at the Second Ministerial Dialogue with the Private Sector whose theme was “ The Sate of Doing Business in Tanzania”. The dialogue was hosted by the Minister of Finance and Planning - Honourable Philip Mpango and the Minister for Industry, Trade and Investment - Honourable Charles Mwijage in Dar es Salaam this week. This was a follow up to a similar meeting that was held in Dodoma early this year. The TBL Managing Director who is also AB-inBev’s President of the East African Business Unit, said that existing market conditions – the company had previously been growing at the rate of negative 0.3% - had forced the company to re-think its operating model and realign it to the realities of the market . This had in turn led to TBL growing its business by 20% since June this year. Adding that, “We are optimistic that this growth will continue and are looking to invest in increased production capacity to cater for this because our plants are currently operating at maximum capacity.” On what was driving the growth, Jarrin said it is mainly driven by the affordable brands and packs segment which are primarily sorghum based. “The affordable segment of our market which essentially sources its growth from the informal sector, is price sensitive and for us to invest in a new brewery we would like to work with the Government of Tanzania to create a stable and predictable excise regime. Increased production volumes will in turn translate into increased revenue collection,” he said. Insofar as supporting the government’s industrialisation drive is concerned, the Managing Director had this to say, “ We at TBL Group consider ourselves an agro-processing industry because agricultural produce – barley, sorghum, maize and sugar - are the key ingredients in our products. Increased production levels thus require increased purchases of the cereals that we use in our breweries. Our continued growth as a business has a direct impact on many sectors of which agriculture is the main one.” TBL Group has been a consistent top performer since its privatization in 1993. The business has also doubled in size over the past five years due to the on-going investments in our operations. “We plough back between TShs. 90 -150 billion in the upgrading of our breweries and distilleries to world-class standards around the country every year, “ says Jarrin.
NMB yaahidi kuzingatia uwiano wa kijinsia kuchochea maendeleo

NMB yaahidi kuzingatia uwiano wa kijinsia kuchochea maendeleo

October 26, 2017
Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias katika mdahalo kuhusu uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias (wa pili kulia) akizungumza katika mdahalo kuhusu uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni washiriki katika mdahalo huo.  

 BENKI ya NMB Tanzania imesema licha ya kutoa huduma bora kwa wateja wake itaendelea kuhakikisha inazingatia uwiano wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume ili kuwapa nafasi wote kushiriki katika shughuli za maendeleo. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias katika mdahalo kuhusu uwaniano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking ambao unalengo la kuangalia namna bora ya kuwafikia wanawake katika maeneo mbalimbali duniani ili wapate huduma za kifedha. Gladness alisema benki hiyo inatambua umuhimu wa kuwa na uwiano wa kijinsia kuanzia kwa wafanyakazi wake mpaka aina ya huduma ambazo wanazitoa kwa wateja wake. Alisema NMB imekuwa na sera bora ambazo zinawapa nafasi sawa wanawake na wanaume katika vyeo mbalimbali vya ofisi, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo namna wanaweza kufanya ili kufanikiwa na kwa wajasiliamali kutoa mafunzo kuhusu njia bora ambayo wanaweza kuitumia kuendeleza biashara zao. “Uwiano wa kijinsia katika mashirika ni muhimu ili kuwapa nafasi wanawake washiriki katika shughuli za maendeleo, kwetu NMB wanawake wanapewa nafasi na hii inatokana na benki yetu kuwa na sera bora ambazo zinazingatia uwiano uliopo kwa wafanyakazi wake kuanzia wafanyakazi wetu wa kawaida hadi viongozi lakini pia tuna Jukwaa la Wanawake ambalo linatumika kutuunganisha wanawake," “Tumekuwa tukitoa mafunzo katika chuo cha IFM, CBE na UDSM, tunakutana na wanawake na tunawapa historia zetu jinsi tulivyoweza kufanya na kufanikiwa na wapo ambao wanatamani kufanya kazi benki tunawapa mbinu ambazo wanaweza tumia kupata nafasi benki kama unavyojua wanawake wengi wana aibu na hawajiamini hivyo tunawambia nini wanatakiwa kufanya,” alisema Gladness na kuongeza. “Jukwaa letu la wanawake linafanya kazi kwa karibu na kitengo chetu cha Business Bank ambao wao wanatoa mafunzo kwa Klabu za Biashara (Business Club), wao tumekuwa tukiwaomba watoe limu kwa wajasiliamali wanawake huko mikoani kama unavyojua ukiweza kumkomboa mwanakme kiuchumi umekomboa jamii nzima.” Gladness alisema changamoto kubwa ambayo inawapata wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na elimu ya namna wanaweza kutunza taarifa zao za kuuza na kununua bidhaa ili wanapokwenda benki waweze kupatiwa mikopo kwa urahisi jambo ambalo Business Club imekuwa ikilitolea mafunzo kwa wajasiriamali. Aidha Gladness alisema kwa wajasiriamali wanawake benki ya NMB ina akaunti ambayo inatwa Pamoja (Pamoja Account) ambayo inatumiwa na vikundi na hivyo kuwataka wanawake kuitumia akaunti hiyo kwani ina huduma za kisasa ambazo zinaweza kuwasaida kukuza biashara zao na kuinuka kiuchumi. “Akaunti ya Pamoja ina huduma ambazo hazipo katika akaunti za kawaida, wataweza kuona mahesabu yao vizuri, wanaweza kupata huduma kwenye simu inakuwa sio kama zamani ambapo ilikuwa ukitaka kuchukua mkopo mpaka mweka hazina awepo lakini kwasasa wanaweza kutumia NMB Mobile Banking,” alisema Gladness.   
Mdahalo kuhusiana na uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam ukiendelea.

Dkt. Kigwangalla atua Loliondo, afanya kikao kizito na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngorongoro

October 26, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewasili Makao makuu ya Wilaya ya Ngorongoro na kisha kufanya mkutano maalum na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ambapo kisha atazungukia kwenye maeneo yenye migogoro.
Waziri Dkt.Kigwangalla ametua uwanja mdogo wa Wasso uliopo eneo la Loliondo na kisha kukutana na viongozi hao wa Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka.
Dk Kigwangalla baada ya kumaliza kikao hicho maalum na wakuu hao, anatarajia kutembelea maeneo yenye migogoro ili kubaini kiini cha mgogoro wa eneo hilo la pori tengefu la Loliondo.
Aidha, pia anatarajia kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo pamoja na kufanya mkutano wa wazi ikiwemo kusikiliza kero kutoka kwa wananchi hao.
Waziri Dkt.Kigwangalla yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)mjini Arusha, na baadae Mamlaa ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa namna ya kitatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea Loliondo.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongozana na na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro  kwenye uwanja wa ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea wilayani humo.
  
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka akimwakilisha Waziri Dk.Kigwangalla katika mkutano huo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama

Tigo yazindua mbio za Kili Half Marathon 2018, kufanyika March 4.

October 26, 2017

Kaimu mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo    akijitambulisha wakati wa kuzindua mbio za Kili Half Marathon kwa mwaka 2018, mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo itadhamini mbio za kilomita 21 kwa jina la Tigo Kili Half Marathon.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni  Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo ambao wamedhamini mbio za kilomita 21 ziitwazo Tigo Kili Half Marathon

KUKATIKA KWA UMEME NCHI NZIMA: DKT. KALEMANI AWAOMBA RADHI WANANCHI.

October 26, 2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (pichani juu), amewaomba radhi wananchi kufuatia kukatika kwa umeme nchi nzima Oktoba 25 na 26, 2017 kulikosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.
Dkt. Kalemani amabye alikuwa mjini Dodoma akishiriki vikao vya kamati za bunge, alilazimika kusafiri mapema leo asubuhi Oktoba 26, 2017 kuja jijini Dar es Salaam ili kufuatilia juhudi za kurekebisha tatizo hilo.
"Ndugu wananchi hali ilivyotokea sisi kama Shirika la TANESCO na Serikali tunawataka radhi wananchi kwa matatizo yaliyotokea lakini niseme tu kwamba kuna hatua madhubuti zinazochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali hiyo ili wananchi muendelee kupata umeme wa uhakika." Alisema Dkt. Kalemani katika taarifa yake kwa wananchi aliyoitoa makao makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam baada ya ziara yake ya kutembelea kituo cha udhibiti cha Gridi ya Taifa, (GCC), kilichoko Ubungo na kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi1 jijini  Dar es Salaam.

Taarifa za awali zilieleza kuwa kukatika kwa umeme kulisababishwa na "Gridi kuchomoka" Oktoba 25, 2017 majira ya saa 10;08 alfajiri na kurejea saa 12:09 asubuhi ambapo umeme ulirejea mikoa yote isipokuwa Zanzibar, ingawa juhudi za mafundi wa TANESCO ziliwezesha umeme kurejea Zanzibar majira ya saa 1 asubuhi.
Hata hivyo tatizo hilo lilirejea tena majira ya saa 12:30 jioni siku hiyo hiyo ya Oktoba 25, 2017, ambapo takriban mikoa yote iliathirika. Umeme ulirejea tena majira ya saa 3 usiku lakiji ilipofika Oktoba 26, 2017 majira ya saa 12:03 tatizo hilo likajirudia tena na kuathiri takriban mikoa yote ikwiemo Zanzibvar.

"Nimekuja kutoka Dodoma ili kuona nini kimetokea, nini kimesababisha na hatua gani za haraka zichukuliwe ili kuondoa tatizo hilo hii ndio hasa dhamira ya safari yangu." Alisema Dkt. Kalemani baada ya kufika kwenye kituo cha udhibiti Gridi ya Taifa, Ubunmgo.
Lakini niwapongeze TANESCO kwa kutoa taarifa mapema kwa wananchi kuwajulisha kuhusu tatizo hilo, alisema.
Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema, chanzo cha tatizo ni pamoja na mfumo wenyewe (GCC) na bado unafanywiwa marekebisho na taratibu zinaendelea, na kule Kinyerezi kuna mashine moja haifanyi kazi nayo inafanyiwa marekebishiom ikiwa ni pamoja na valvu moja iliyoharibika nayo pia inafabnyiwa kazi.
"Gridi ya taifa imerejea tangu jana usiku (Oktoba 25), na umeme unapatikana nchi nzima lakini hata hivyo yapo maeneo machache ambayo hayapati umeme wa kutosha kwa sababu mtambo mmoja wa Ubungo namba mbili wenye jumla ya megawati 129 haujaanza kufanya kazi na nimeelekeza wataalamu wafanye kazi usiku na mchana na wamenihakikishia kufikia saa 5 asubuhi kesho  (Oktoka 27), mtambo huo utaanza kufanya kazi na umeme utarejea katika hali yake ya kawaida." Alibainisha.

Dkt. Kalemani akiwa kwenye kituo cha udhibiti wa Gridi ya Taifa (GCC), Ubungo jijini Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji (Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Dkt. Kalemani alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi 1 jijini Oktoba 26, 2017. Wakzanza kulia ni NJaibu Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Juliana Palagyo
Meneja Mwandamizi wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Costa Rubagumya akifafanua jambo.
Meneja wa udhibiti  ifumo ya Gridi ya Taifa (Protection), Mhandisi Izahaki Mosha, akimfafanulia Waziri Dkt. Kalemani (kushoto).
Dkt. Kalemani (kushoto), akiwa kwenye chumba cha udhibiti cha Kinyerezi 1 akifafanua jambo.