JK AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA YENYE UREFU WA KILOMETA 60 MKOANI LINDI

August 07, 2015

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.
 Rais Kikwete akimshukuru  Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma  Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na   Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na  Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho  Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.
 Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akiwa sambama na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh.Mwantumu Mahiza.
Wananchi kutoka kijiji cha Marendego na vijiji vyake wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu –Somanga yenye urefu wa kilometa 6,inayojengwa na Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa mfuk wa Kuwait pamoja na Opec.Katika unziduzi huo viongozi mbalimbali wa chama na serikal,viongozi wa dini pamoja na watu wengine walishiriki kushuhudia tukio hilo adhimu hapa nchini.
 Wananchi wakifuatilia tukio hilo
 Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ya Ndundu -Somanga yenye urefu wa kilometa 60
 Wananchi wakifurahia ufunguzi wa barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi
  Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.
 Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
 Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.

Wataalamu wa Magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Apollo India Watembelea Tanzania

August 07, 2015




Na Mwandishi Wetu, Dar 
Kwa miaka mingi upatikanaji wa wataalamu wa Afya na matibabu ya uhakika unakabiliwa na changamoto kuu mbili inayowakumba wagonjwa wengi Tanzania.Watanzaniawamekuwa wakisafiri nje ya nchi kupata matibabu ya Figo na magonjwa yanayohusiana na kibofu. Hivyo wataalamu wawili waliobobea katika magojwa ya Figo na Kibofu kutoka Hospitali za Apollo walitembelea nchini Tanzania wakishirikiana na madaktari kutoka Hospital ya Hindu Mandal ili kuwafanyia uchunguzi, kutoa tiba na kutoa ushauri kwa wagonjwa mbalimbali Tanzania. Dkt V. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya njia ya mkojo na mfumo wa uzazi wa kiume na amekuwa mshauri mwandamizi wa magonjwa ya kibofu katika Hospitali za Apollo huko Hyderabad India tangu mwaka 1994. Dkt. Sanjay Maaitra ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya Figo kwa kutoa huduma za matibabu ya figo na magonjwa yanayoambatana na Figo ikiwa lengo kuu la ujio wao ni kuhakikisha wagonjwa wanapata uchunguzi sahihi bila kuingia gharama kubwa za kwenda nje ya nchi.
Wagonjwa wanaosubuliwa na magonjwa yanayohusiana na figo pamoja na mkojo walihudhuria na kushiriki katika tukio hili.  Madaktari hao waliwafanyia wagonjwa uchunguzi kwa kupitia taarifa zao nyuma na kuzipitia upya, kutoa historia ya matibabu na kutoa ushauri wa matibabu na tiba kwa wagonjwa wapya waliojitokeza.
Kama ilivyoelezwa hapo juu lengo la ujio wa madaktari hawa ni kupata taarifa za wagonjwa wote ambao walipata huduma za matibabu kutoka kwao iwe ndani ya nchi au katika Hospital za Apollo huko Hyderabad. Lengo la Dkt. Rajagopal na Sanjay Maitra ilikuwa ni kuangalia jinsi gani wagonjwa wao wamepata nafuu na kama wanahitaji vipimo zaidi na marekebisho ya tiba. Kwa mfano mgonjwa ambaye amepandikishwa figo anahitaji muda mrefu wa ushauri na uchunguzi wa mara  kwa mara. Ujio wa madokta hawa hapa nchini umekuwa jambo jema kwa kuwa umewarahisishia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi na uchunguzi wa muda mfupi. Endapo kama afya za wagonjwa zilitambulika kuzorota hivyo madaktari walipendekeza wapate vipimo zaidi katika Hospitali za Apollo, Hyderabad au Hospitali zozote zile.
Taasisi ya Upandikizaji ya Apollo (ATI), ni sehemu ya Hospitali za Apollo ambayo niTaasisi kubwa na imara katika mpango wa upandikizaji figo duniani. Wanatoa huduma za uchunguzi wa figo, Ini, Upandikizaji figo,   upandikizaji wa ‘Corneal’ ‘GI’,  matibabu ya tumbo na huduma nyinginekwa watoto. Taasisi hii inatoa ushari mbalimbali, vipimo na tiba.
Wakati wa ujio wa madaktari, tulipata fursa ya maohijiano na Dkt. V. Rajagopal pamoja na Dkt. Sanjay Maitra, tuliwauliza kama wameona mabadiliko yoyoteya afya Tanzania tangu walipokuja safari yao ya mwisho. Pia madaktari hawa walitaja idadi ya wagonjwa ambao waliofika katika kliniki na kuona idadi kubwa kuongezeka kutokana na watu kutambua upatikanaji wa huduma hizo na mafanikio ya watu waliowahi kutibiwa na  kushauriwa na madaktari hao wa kimataifa wenye ujuzi mkubwa.  Hata hivyo Watanzania bado wanakosa njia za kupambana na magonjwa haya tangu mwanzo. Madokta walikuwa na maoni kwamba, mwamko utaongezeka kama watu wanatapata elimu ya kutosha kutoka kwa  madaktari juu ya uzuiaji wa magonjwa haya kwa kutambua dalili za mwanzo.
Daktari. V. Rajagopal na SanjayMaitra walisisitiza umuhimu kuzuia magonjwa haya na pia kufanya vipimo mara kwa mara.  Waliendelea kusema kwamba magonjwa haya huwapata hasa watu wenye umri mkubwa lakini pia huweza kuzuilika. Watanzania wanatakiwa kuwa makini kutokana magonjwa mengi yanayotokana na figo hasa kwa watu wazima ni kutokana na Shinikizo la Damu, Kisukari, wingi wa Lehemu, kutofanya mazoezi, Ulaji mbaya pia utumiaji usio sahihi wa dawa hasa za kutuliza maumivu. Hivyo  husababisha  ulemavu wa figo.
Pia Dkt. Sanjay Maitra alitoa ushauri  ni vyema kuzingatia vipimo mara kwa mara kwani inasaidia watu kujua afya  zao.Alitoa mfano wa mtu mmoja,  ambaye  ni dereva mwenye ujuzi wa miaka hamsini na kipindi chote alikuwa anaumwa miguu na mwishowe aligundulika kuwa na kisukari kwa miaka kumi na tano. Pia mgonjwa huyo hakujua kuhusu shinikizo la damu wala hakuwa na walipompima walimgundua hana uwezo wa kuona vizuri. Dkt. Sanjay Maitra aligundua kuwa ana ugonjwa wa kisukari. Pia kwa bahati mbaya pia watanzania wengi wanashabihiana na mfano huo kwa kuwa hawajui dalili mwanzo za magonjwa haya. Aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu kwa wao kutembelea kwani wameleta mwamko mkubwa.Pia Madokta hawa wametoa wito kwa Watanzania kupata taarifa zaidi juu ya kupambana na magonjwa haya ili kuishi kwa afya njema na maisha marefu.
Tukio hili la madaktari kutembelea taasisi za afya hapa nchini  lengo ni kuleta ushirikiano katika huduma za afya na mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini. 
Dkt. Sanjay Maitraamesema ni jambo gumu na linahitaji hela nyingi  kwa wagonjwa kusafiri nje ya nchi, hivyo yeye ameona ni vyema kuweka muda ili kuja kutoa huduma  kwa ukaribu zaidi.  Anatumaini kwamba wagonjwa watatibiwa kwa urahisi hata wakiwa nje ya nchi.

Lengo la ujio wao si kwamba kuwachukua wagonjwa na kuwatibia katika Hospitali za Apollo bali ni kuwapa ushauri sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya matibabu. Mbali na suala la wagonjwa lakini tumeona pia wachache kati yao wataweza kwenda Apollo kama watahitaji matibabu.
Alipoulizwa kuhusu watanzania watakachopata wakienda Hospitali za Apollo, Dkt. V Rajagopal alisema kwamba mpango wa Kimataifa wa Apollo ni kusaidia wagonjwa na washirika wao ili kurahisisha huduma za afya. Pia wanatoa ratiba ya uteuzi, usafirishaji, na huduma za ukalimani kwani Hospitali za Apollo pia zinatoa huduma ya ukalimani kwa lugha ya Kiswahili ili kuwahudumia wagonjwa wanaotoka Kenya, Uganda na Tanzania kwa urahisi.  Hospitali za Apollo zinajulikana kwa kwenda mbali zaidi kuwafanya wagonjwa kuhisi unafuu.

Mwaka 2014, Mji wa Apollo (Apollo Health City) Hderabad, ulipata tuzo ya heshima ya KIMATAIFA YA MATIBABU NA UTALII kutoka Jarida la  Kimataifa la Matibabu na Usafiri  kutokana na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Hospitali za Apollo zinamfanya mgonjwa ajisikie kama yupo nyumbani kwani huwaandalia wagonjwavyakula vikuu kama ugali, ndizi mtori, ingawa wagonjwa wengi wa kiafrika wanapenda kujaribu vyakula vya kihindi. Pia mapishi yanaenda mbali zaidi kwa kuandaa chakula cha watoto na watu wazima. Chakula ni muhimu sana kwa wagonjwa ili kuwa na afya. Hospitali za Apollo zinaamini kwamba “kama tunafahamu chakula basi pia tunafahamu tamaduni husika”.

Kuhusu Apollo:
Mnamo mwaka 1993, Dkt. Prathap C. Reddy, mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika nchini India, Hospitali za Apollo Chenai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo zimeweza kukua kufikia moja ya shirirka kubwa la afya barani Asia likiwa na uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya dawa na zaidi ya kliniki za uchunguzi 100.  Pia hospitali za Apollohutoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa kibiashara, huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile. Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezekaa katika utoaji huduma za hali ya juu, Hospitali za Apollo zina jumlaa ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospital za Apollo kupata tuzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa ( Hospitali saba za Apollo zinatambuliwa na kutunikiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika hesima nadra, serikali ya india ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa Hospitali za Apollo Dkt. Prathap C Reddy,  alitunukiwa tuzo ya heshima ya Padma Vbhushan’ mnamo mwaka 2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kimataifa na maendeleo ya kiteknolojia. Hospitali zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimatifa katika huduma za kitabibu pamoja na utafiti.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene atembeleakiwanda cha kutengeneza vigae mkoani mbeya

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene atembeleakiwanda cha kutengeneza vigae mkoani mbeya

August 07, 2015

unnamed (40)
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akizungumza, mmoja wa viongozi wa kampuni ya Marmo and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani mbeya hivi karibuni.
unnamed (41) unnamed (42)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Janet Mbene,akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
unnamed (43)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janet Mbene, akitembelea sehemu ya kiwanda cha Marmo anda Granito Mines
KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC ZANZIBAR

KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC ZANZIBAR

August 07, 2015

x1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) mara walipoingia katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto)
Picha zote na Ikulu.
x2
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akitoa taarifa ya kikao kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo kbla ya kukifungua kikao hicho,
x3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikifungua  kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto)
x4
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar wakifuatuilia kwa makini ratiba ya kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,
x5
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar wakifuatuilia kwa makini ratiba ya kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,

ADC YAFANYA MKUTANO WA HADHARA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA WA URAIS KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

August 07, 2015

 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli Dar es Salaam jana. 
 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
 Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
  Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli jana.
Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu. 
OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA NA URATIBU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NDANI YA MAONESHO YA NANE NANE – LINDI

OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA NA URATIBU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NDANI YA MAONESHO YA NANE NANE – LINDI

August 07, 2015


xxx1
Mratibu  wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Edgar Senga akieleza uratibu wa shughuli za maafa kwa  wananchi waliotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti , 2015.
xxx3
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ndada wakipata maelezo juu ya sera baina ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka kwa Mchumi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji , Vedastus Manumbu walipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti , 2015

BENKI YA NIC YATOA MADAWATI 25 SHULE YA MSINGI CHAMANZI

August 07, 2015

 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ancent Shayo akiwa na wafanyakazi wa shule ya msingi chamanzi wakizungumza na wafanyakazi wa NIC hawapo pichani katika ofisi ya mkuu wa shule ya msingi chamanzi jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 BENKI ya NIC imetoa msaada wa madawati 25 katika shule ya msingi Chamanzi yenye thamani ya Sh.Milioni tatu kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya madawati.

Akizungumza baada ya kukabidhi  madawati  hiyo, Mkuu wa Biashara za Kibenki,Rahim Kanjii amesema kuwa shule hiyo waliona ina umhimu wa kusaidiwa sehemu ya madawati katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini ardhi wakiwa darasani.

Amesema shule hiyo inatakiwa kusaidiwa kwa kila hali kwani watoto wanaoandaliwa hao ni taifa la leo hivyo wanatakiwa kuandaliwa mazingira bora ya kupata elimu.

Kanji amesema kuwa ameguswa sana na benki itaendelea kadri ya uwezo wake kusaidia shule katika kuweza kuondokana na chagamoto ya madwawati  katika kujenga mazingira bora ya kusomea watoto kwani wanaandaliwa kuja kuwa wanataaluma mbalimbali.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Ancent Shayo amesema kuwa shule ina wanafunzi 3200 lakini vyumba vya madarasa 11 na kufanya kila darasa kukaa wanafunzi 150.

Amesema madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne kutokana na upungufu wa madwati 175 ambapo NIC imepunguza imetoa madawati 25 hivyo kwa darasa hilo linahitaji madawati 150 ili waweze kukaa katika siku ya mtihani wa taifa.

Shayo amesesema hitaji katika shule licha ya madawati wanaupungufu wa vyumba vya madarasa  kutokana na idadi ya wanafunzi hao.
 Wanafunzai wa shule ya msingi Chamanzi wakiwa darasani wakiwa wamekaa chini kwa kutokuwa na madawati ya kutosha katika chumba cha darasa la tatu walipotembelewa na wafanyakazi wa Benki ya NIC leo jijini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo akizwa na wafanyakazi wa Benki ya NIC walipowatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamanzi jijini Dar es Salaam walipotembelea chumba cha darasa la kwanza katika shule hiyo. 
Wafanyakazi wa Benki ya NIC akifungua meza na viti walivyotoa msaada katika shule ya Msingi Chamanzi ikiwa meza 25 na viti 25.
 Wafanyakazi wa Benki ya NIC waliosimama wakiwa wanafunzi wa shule ya msingi Chamanzi waliokaa baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Picha ya pamoja ya wanafunzi wa shule ya msingi Chamanzi na wafanyakazi wa Benki ya NIC baada ya kutoa msaada wa meza 25 na viti 25 vya plastiki katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Biashara za Kibenki, Rahim Kanjii akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo  mara baada ya kutoa msaada wa meza 25 na  viti 25.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chamanzi wakiwa wamekaa kwenye viti na meza walivyopewa msaada na Beni ya NIC jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.