Mh. Lowassa ashiriki sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa

July 02, 2014

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi  wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
MUFTI ATEGUA KITENDAWILI CHA UONGOZI ARUSHA

MUFTI ATEGUA KITENDAWILI CHA UONGOZI ARUSHA

July 02, 2014


MUFTI
Na  Mahmoud Ahmad, Arusha
MUFTI  Shekh  Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba, jana ameondoa sitofahamu ya muda mrefu kuhusu uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, uliopo Bondeni Manispaa ya Arusha na Masjid Quba, kwa kuwataja viongozi wanaostahili kuwepo madarakani.
Kabla ya kuwataja viongozi hao, alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na uongozi wa bakwata katika ngazi za juu za Mkoa, ambao umesababishwa na ukaidi wa makusudi wa baadhi ya watu kukiuka utaratibu wa katiba ya BAKWATA  juu ya upatikanaji uongozi katika ngazi hizo.
Alisema hali hiyo imesababisha kuw ana makundi mawili ya uongozi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya ya Arusha, Msikiti Mkuu wa Ijumaa Arusha Mjini na Masjid Quba, jambo linalokwamisha maendeleo ya Uislamu Mkoani Arusha.