Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu kulia ,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Rais Dr.
Jakaya Kikwete akipata taarifa ya mradi huo wa nyumba za gharama nafuu
kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Rais Dr.
Jakaya Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama
nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) na kupokelewa na Ndg.
David Shambwe Kaimu Mkurungenzi Mkuu NHC na Mkurugenzi wa Uendelezaji
Biashara wakati alipokagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Songea
mkoani Ruvuma akiwa katika ziara yake ya kikazi leo, Rais Dr. Jakaya
Kikwete anaendelea na ziara mkoani humo leo. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC)
Rais
jakaya Kikwete akipata maelezo ya kuhusu Mashine za kufyatulia matofali
ambazo zimegawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo mchana huu
Akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Vikundi vya nguma na burudani ikiburudisha katika tukio hilo mchana wa leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alipofungua leo hii nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika eneo la Mkuzo, Mkoani Ruvuma.
Kwa ujumla Mh. Rais alisema yafuatayo:-
Amerejea kauli yake
aliyoitoa Kasera , Mkinga Tanga kwa kulipongeza Shirika kwa kazi nzuri
linayofanya hususan ya uamuzi wake wa kizalendo wa kujenga nyumba za
watu wa kipato cha kati na chini katika Halmashauri za Miji na Wilaya
hapa nchini.
Alizitaka Halmashauri za
Miji na Wilaya kulipatia Shirika pamoja na mashirika na mifuko mingine
ya jamii kama NSSF, PPF, LAPF, GEPF na mengineyo ardhi yenye masharti
nafuu ili kuwezesha ujenzi wa nyumba na hatimaye kuweza kuipanga miji
ipasavyo.
Aliziagiza Halmashauri
hasa ya Songea kutumia fursa za mikopo kutoka benki washirika na NHC
kuweza kununua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa badala ya kuendelea
na mtindo wa kutaka kupanga nyumba hizo..
Alilipongeza Shirika kwa
kuwezesha vijana mashine za kufyatulia matofali jambo ambalo litatoa
ajira kwa vijana. Alifurahishwa na mpango huo na kuzitaka Halmashauri
nchini kuusaidia mpango huo ili uwe endelevu na wenye manufaa kwa
vijana.