Tizama:MAJAMBAZI YALIVYO MIMINA RISASI NA KUSABABISHA VIFO VYA ASKARI POLISI WAWILI.

April 30, 2014


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG
Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja  aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN
Mwili wa askari namba F.5179 PC JUMANNE ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete,askari huyo alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na majambazi matatu huko Ussoke wakati askari huyo akiwa anajipanga na mwenzake kukabiliana na majambazi hayo yaliyovamia nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja Ibrahimu Mohammed.

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI

April 30, 2014

 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe kama ishara ya kuzindua Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Naibu Kati u Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi huo wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam. 
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
*********************************************
Na Benedict Liwenga - MAELEZO
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang)  ambayo imechezwa na China na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.

Sherehe hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.
Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.

Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo zote zimepata umaarufu.

WAHARIRI NA WAANDISHI WA NEW HABARI WAPINGA VITENDO VYA UBAGUZI WA WACHEZAJI WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA LA KULIPWA ULAYA

April 30, 2014


 NI MCHEZAJI WA BARCELONA ALIYERUSHIWA NDIZI NA KISHA AKAIOKOTA NA KUIMENYA NA KISHA KUILA.  
Baadhi ya wahariri na waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, Mwani Nyangasa na wenzake wakila Ndizi kwa pamoja kama ishara ya kumuunga mkono mchezaji wa Barcelona Daniwl Alves, ambaye ni Mwafrika aliyeonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi hivi juzi wakati akiwa mchezoni na timu yake ilipokuwa ikicheza na Villarreal ya Hispania, ambao mashabiki walimrushia ndizi mbivu uwanjani wakimaanisha kumfananisha na Nyani na yeye kwa kuwaonyesha kuwa hajali kitendo hicho aliiokota na kuimenya na kisha kuanza kuila, jambo ambalo liliungwa mkono na wengi na kumpongeza kwa kitendo chake cha ujasiri, na kuendelea na mchezo.
Baloteli pia ni mmoja kati ya wachezaji Waafrika aliyeunga mkono kitendo cha mwafrika mwenzake kuwakebehi na kuwadharau mashabiki hao wa ubaguzi. Na pia Baloteli ni mmoja kati ya wachezaji wanaokumbana na vitendo hivyo vya unyanyasaji uwanjani mara kwa mara.