WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA ILIYO ENDESHWA NA MJASIRIAMALI BI. MARY DAVID JIJINI DAR

April 08, 2015

 Mjasiriamali na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja wa wajasiliamali ambaye pia ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake wa jinsi alivyo nufaika na mafunzo kama haya na mpaka sasa anajitegemea na Kupata kipatochake na kuwasaidia wengine.
Wa kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada  ambaye amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi  wake umuhimu wa mikutano kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata elimu Bora ya Kilimo.
Bwana Daniel Ambaye ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake katika maswala ya kilimo.
Mwendeshaji msaidizi wa Semina Hiyo Bwana Saidi akitoa mafunzo ya juu ya kuanzisha kilimo kwa kutumia Green House pamoja na faida zake 
Bize akichukua yale ya Muhimu kabisa katika semina hiyo.
 Wanasemina wakiwa wanasikiliza kwa makina mada mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa
 Semina ikiwa inaendelea
Baadhi ya wanasemina wakiwa katika Picha ya pamoja

 Kilimo na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary David Kinong'o.

Katika Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.

Pia walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi, Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.

Mwisho Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.

Dk Shein Ajumuika na Wananchi Katika Kisomo cha Hitma kumsomea Mzee Karume Afisi Kuu ya CCM Zanzibar

April 08, 2015
Mama Fatma Karume akiwasili katika viwanja vya Afisdi
Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kuhudhguria Hitma na dua ya kumuombea
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Mjini Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akiwaili
katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria hitma ya Baba yake Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM na kupokelewa
kwa na Askari wa JWTZ , akihudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Afisi Kuu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili
katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Hitma na Dua
ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika leo.
Shekh Thabit Noman Jongo akitowa maelezo ya hafla ya kuaza kwa hitma na dua ya
kumuombea Mzee Karume iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.
 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi akisoma
dua kabla ya kuaza kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani
Karume.kilichofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi akisoma dua kabla ya kuaza kwa kisomo
cha hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.kilichofanyika leo
Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis na kushoto Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Mstaaf wa Zanzibar
Dk Amani Abeid Karume.
Viongozi wa Dini na Wananchi wakiwa katika ukumbi wa hafla
wakiitikia Dua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika kisomo cha hitma
kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kulia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kadhi Mkuu wa Zanzibar  Shekh. Khamis Haji Khamis, Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mhe, Pandu Ameir Kificho.
Viongozi wakisoma hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
wa kwanza Mufti Mkuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi, Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman
Makungu.
Wananchi wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM
wakimsomea kisomo cha Hitma Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Sh. Alhad Mussa akitowa mawaidha kwa Wananchi na
Viongozi waliohudhuria kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee
Karume kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar leo.   
Viongozi wa Serekali na Dini wakimsikiliza Shekh wa Mkoa waDar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa akitowa mawaidha baada ya kumaliza kusoma hitma na dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.wa kwanza Muftim Kuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalif Seif Sharif Hamad, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume 
Viongozi wa Serekali na Dini wakimsikiliza Shekh wa Mkoa wa
Dar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa akitowa mawaidha baada ya kumaliza kusoma
hitma na dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. 
Mhe Mark Mwandosa akiwa makini akimsikiliza Mhe Bernard
Membe wakiti wakihudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abaid Amani
Karume iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakihudhuria hafla hiyo ya kisomo cha
Hitma na Dua Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Mama Fatma Karume akiwa na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar  Dk Amani Karume na Mke wa Balozi Ali Karume,
wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM wakihudhuria hitma na Dua ya kumuombea
Mrehemu Mzee Abeid Amabni Karume ilofanyika leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema
Shein, akiwa na Wake wa Viongozi wakihudhuria hitma na dua ya kumuombea Mzee
Karume iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar
Walimu wa Madrasa wakihitimisha hitma kwa upande wa Wanawake waliohudhuria katika
kisoma hicho Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM wakimsomea kisomo cha Hitma Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume.
Wanafunzi wa Madrasa Zanzibar wakihudhuria katika hafla hiyo
ya kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar leo.
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

April 08, 2015

index 
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (She-Polopolo) kiingilio cha juu sh.5,000 kwa VIP na sh. 2,000 kwa majukwaa yaliobakia, mechi hiyo itachezwa ijumaa jioni saa 10 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Twiga Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage imeendelea kujifua katika hosteli za TFF zilizopo Karume, kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kuwnaia kufuzu kwa Michezo ya Afrika nchini Congo- Brazzavile mwezi Septemba mwaka huu.
Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki tatu zilizopita jijini Lusaka nchini Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Zambia, hivyo katika mchezo wa ijumaa kuhitaji ushindi wa aina yoyote tu ili kuweza kufuzu kwa fainali hizo.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi siku ya ijumaa jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuja kuwapa sapoti Twiga Stars watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Taifa.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (She-Polopolo) inatarajiwa kuwasili usiku wa saa 7.25 kuamkia alhmisi kwa shirika la Ndege la Ethiopia wakiwa na msafara wa wachezaji 18 na viongozi saba na watafikia katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani Kariakoo.
Msafara wa Zambia (She-Polopolo) unaongozwa na mkuu wa msafara Lenny Khuwa, kocha mkuu Albert Kachinga, kocha msaidizi Kape Saili, kocha wa magolikipa Yona Phiri, daktari wa timu James Nyimbili, mchua misuli Conerlia Chazura, na meneja wa timu ni Besa Chibwe
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili ni Rachel Nachula, Annie Kibanji, Chiko Nkhoma, Osala Kaleo, Joana Benai, Meya Banda (Nahodha), Misozi CR Chisamu, Jane Nshika Chalwe, Milika Limwanya, Mary Wilombe, Grace Chanda, Barbra Banda, Memory Mwaseba, Hazel Natasha Nali, Martha Tembo, Mary Mwakapila na Ireen Lungu
Kesho jioni She-Polopolo wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa, uwanja ambao ndio utakaotumika kw amchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Uganda wanatarajiwa kuwasili leo mchana ambao ni  Ms Anna Akoyi , Ms Nakkito Nkumbi , Ms Jane  Mutonyi, na Ms Nabikko Ssemambo, Kamishina wa mchezo  Ms Nomsa Jacobeth Mhalangu kutoka nchini Afrika Kusini anatarajiwa kuwasili leo jioni.
TFF YAMPONGEZA TENGA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe  waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na  kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.
NB: Kesho alhamisi saa 5 kamili asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TFF uliopo Karume, makocha wa Twiga Stars na She-Polopolo wataongelea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa siku ya ijumaa.