MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

February 21, 2018
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani,  Mkuu  wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. 
 Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda,   akichangia hoja wakati wa wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto). 
Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara  ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakishiriki  kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAKANDARASI WASIO WAZALENDO WASIPEWE KAZI NDANI YA JIJI LA DAR - NAIBU WAZIRI AWESO

February 21, 2018

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miundo mbinu ya maji safi na maji taka iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemshukuru Naibu Waziri Aweso kwa msikamano ambao amekuwa akiufanya na wilaya yake ya kuwapa kipaumbele cha kuwatembelea mara kwa mara hali inayoamsha maendeleo zaidi.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASCO, Injinia Aron Joseph amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwa vile kwasasa wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati alipofanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya  maji kwa jiji la Dar es Salaam ambapo amejionea maendeleo mbali mbali ya ujenzi. Pichani akiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya alipoanzia ziara hiyo.
Akikagua mradi wa Maji Taka (DEWAT) - Mlalakuwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji eneo la Makongo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipewa maelezo machache na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati Waziri Awezo alipofanya ziara ya mradi wa maji eneo la Makongo juu ambapo ujenzi bado unaendelea.
Viongozi wa DAWASA, DAWASA pamoja na uomgozi wa serikali ya kijiji wakimsikiliza Naibu Waziri Aweso.
Wakitoka kukagua mradi wa ujenzi wa makongo juu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi akisalimiana na Meneja wa DAWASCO-Kimara, Peter Fumbuka. Ambapo aliweza kumshukuru na kumpongeza kwa utendaji kazi wake na kumuomba achape kazi kwa bidii.
Muonekani wa ujenzi tanki la maji Makongo juu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na mmoja ya wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KLINIKI YA METHADONE MWANZA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA

February 21, 2018
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amezindua Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA ENTEBE NCHINI UGANDA

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA ENTEBE NCHINI UGANDA

February 21, 2018

1.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda
9 11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
14 15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.
16
Kikundi cha ngoma za Asili cha Masters of ground kutoka Wilaya cha Kyotera, Masaka nchini Uganda wakitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda.
PICHA NA IKULU

USAJILI WA TIGO KILI HALF MARATHON 2018 WAANZA KUPITIA *149*20#

February 21, 2018
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanza kwa usajili wa mbio za km 21 za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi tarehe 4 Machi ya mwaka huu. Kulia ni Afisa wa Lipa kwa Tigo Pesa, David Chinguile. 

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanza kwa usajili wa mbio za km 21 za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi tarehe 4 Machi ya mwaka huu. Kulia ni Afisa wa Lipa kwa Tigo Pesa, David Chinguile. 


Usajili upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo
Tigo Kili Half Marathon kuhamasisha afya bora miongoni mwa Watanzania
21 Januari, 2018. Dar es Salaam.  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania leo imetangaza kuanza kwa usajili wa mbio ndefu za Tigo Tigo Kili Half Marathon kupitia namba *149*20#.

Kwa mwaka wa nne mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mbio za KM 21 za Tigo Kili Half Marathon ambazo zitafanyika tarehe 4 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Ushirika,  mjini Moshi. Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa shindano la Tigo Kili Half Marathon 2018  linaunga mkono juhudi za serikali za kuinua viwango vya michezo na kujenga afya bora za Watanzania kupitia ushiriki wao katika michezo.

“Usajili wa mbio za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Kujisajili, piga simu namba *149*20#, kisha fuata maelekezo rahisi ya kuchagua mbio unazotaka kukimbia na kulipia ada ya usajili kwa mbio husika. Baada ya kutuma ada ya ushiriki, utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakaokujulisha kuhusu kukamilika kwa muamala wako.  Utunze ujumbe huu mfupi wa maneno na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika kituo utakachojulishwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Moshi ili kuchukua namba yako  ya ushiriki,’ Woinde alieleza.

Tigo inatoa jumla ya TZS 11m kama zawadi kwa washindi kumi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanaume na wanawake. Pia kuna medali  na vyeti vya ushiriki kwa watu 4,500 wa kwanza watakaomaliza mbio hizo.

‘Tunachukua fursa hii kuwakaribisha washiriki wote, ikiwemo wanariadha wa kimataifa, wa kitaifa, wapenda michezo na wanafamilia wote kuja kushiriki katika mbio hizi za Tigo Kili Half Marathon, ili waweze kutunza afya zao pamoja na  kufurahia kumbukumbu za matukio yanayoendana na shamrashamra za mashindano,’ Woinde alisema.

Naye Afisa wa Lipa Kwa Tigo Pesa, David Chinguile alisema kuwa Tigo imepanua huduma ya Tigo 4G kufikia miji 22 nchini Tanzania, ikiwemo katika mji wa Moshi na kanda yote ya Kaskazini.  Uwekezaji huu mkubwa utahakikisha kuwa watakaohudhuria Tigo Kili Half Marathon 2018 watapata huduma bora na za uhakika za mtandao wa simu utakaowawezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa, na marafiki pamoja na kutuma picha na video za matukio na kumbukumbu nyingine muhimu kwa kasi ya juu kupitia mtandao wa Tigo 4G.
      
Tigo inajivunia kuwa sehemu ya mbio za Tigo Kili Half Marathon 2018 ambazo zinazidi kujizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni mwaka hadi mwaka.





DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI

February 21, 2018

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC)  imeamua kusitisha mpango wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa halmashauri hiyo itakapopatikana. 

Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika (Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu ya suala hilo. .

Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao juu ya wapi pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo.

Baadhi ya viongozi wanadai utaratibu  wa fedha  za manunuzi haukufuatwa katika kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la Kwehangala na kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya Sh. milioni 700.

 Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kikao kiliafiki  kisitishe zoezi hilo  mpaka maelewano yatakapopatikana.

" Wajumbe wameshauri suala la  kuhamisha makao makuu lisitishwe  hadi hapo utakapopatikana utangamano,kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao umeleta utengano kwa viongozi" Alisema Lugangika .

Mbunge wa jimbo hilo, January Makamba alikiri kuwepo kwa mvutano huo ambao alisema hauna tija katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bumbuli.

Makamba alisema ni vyema kama viongozi wakazungumzia suala la maendeleo mfano;maji,barabara,umeme,nyumba za watumishi badala ya kila siku kuzungumzia wapi kujengwe jengo la halmashauri.

Alishauri kuwa wananchi washirikishwe katika suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya kutosha juu ya hoja ya kuhamisha halmashauri kwa kuwa ndio wenye chombo chao badala ya viongozi kuamua wao pekee.


"Suala hilo nakubaliana na maoni wa kikao cha DCC tulisitishe kwani kwa sasa hatuna shida na majengo ya halmashauri kwa sababu majengo tunayo ambayo hatulipii kodi ya pango. Sasa hivi tuzungumzie maendeleo kwani wananchi mwaka 2020 hawatatudai majengo ya halmashauri bali watatudai maendeleo juu ya huduma muhimu za jamii alisema Makamba.


Hivi karibuni baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura ya kupitisha  azimio la kujenga jengo hilo la halmashauri  huku Madiwani nane wakigoma kupiga kura kwa madai kuwa hawawezi kupiga kura wakati kuna ukiukwaji wa kanuni na utaratibu ktk kitengo cha manunuzi.


Madiwani hao nane ambao waligoma kupiga kura kupitisha azimio hilo  mnamo January 18 mwaka huu walimuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuingilia kati mgogoro na kuzuia walichokiita  ukiukwaji wa utaratibu  wa manunuzi pamoja na maelekezo mbalimbali ya viongozi juu ya mpango huo.


Pia walimuomba aingilie kati na kuchukua hatua dhidi  ya ubadhirifu  wa fedha za umma na ukiukwaji wa utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri na kudharau kwa makusudi maelekezo yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa serikali kuu.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amir Shehiza  alisema kuwa baraza ni chombo chenye maamuzi sahihi  hivyo  alikitaka Kikao hicho cha DCC kuacha  kuingilia Kazi za baraza .