KONCEPT Yawajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti

April 25, 2018



Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii

Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
Wanafunzi wa kidato cha sita wapatao 451 wa shule ya wavulana Kibiti Boys iliyopo wilaya ya kibiti Mkoani wakisikiliza kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele alipotembelea shule hii mapema wiki katika kuwajengea uwezo katika maandalizi yao ya mitihani ya mwisho na pia kuwapa dondoo za mafanikio katika maisha kwa ujumla.
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti wakionesha kuwa wamehamasika na nasaha zilizotolewa na Mkurungezi mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Mkuu wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys Dismas Njawa akifafanua jambo kabla ya kufunga kongamano hilo lililoendeshwa na Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele . Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT akifurahi jambo na Mkuu wa shule ya wavulana Kibiti Boys Dismas Njawa mara baada ya kumaliza kongamano.Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.






Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katikaa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys mara baada ya Kongamano.Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Tigo na Tecno Waungana Kuwapa Wateja Huduma Bora Zaidi za Kidigitali Wazindua simu janja ya 4G aina ya TECNO Camon X yenye ofa ya GB3 bure kila mwezi kwa miezi sita

April 25, 2018
Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (kulia) akionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu hiyo mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). 

Meneja wa Kitengo cha Ushirikiano wa Biashara wa TECNO Tanzania, Anuj Khosla (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto), Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati), Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (wa pili kulia) pamoja na Meneja Msaidizi wa Masoko wa TECNO Tanzania, William Motta wakionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. .

Mwandishi wa Habari, John Dande (wa pili kulia) akipokea kutoka kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto)  zawadi ya simu janja mpya aina ya TECNO Camon X aliyoshinda katika droo maalum iliyofanyika wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu janja za TECNO Camon X zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na kushoto ni  Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya.


Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania inaungana na kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kupanua wigo wa matumizi ya simu janja (smartphone) nchini pamoja na kuwapa wateja huduma bora zaidi za kidigitali, huku wakizundua simu mpya yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X.

TECNO Camon X imejazwa of ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata fursa ya kufurahia  huduma za kipekee za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G.

‘Tigo ipo katika kilele cha mageuzi ya kidigitali na ndio mtandao wa kwanza na pekee wa simu za mkononi nchini ambapo wateja wataweza kujipatia simu janja, za kisasa zaidi, zenye uwezo wa 4G za TECNO Camon X kupitia maduka yetu yote ya Tigo. Pia wateja wetu wana fursa ya kununua simu hizi janja za TECNO Camon X kwa njia ya kulipia kwa awamu kutoka kwa duka la simu la Tigo kwa kupiga *147*00#,’ Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alibainisha.

Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania Eric Mkomoya alisema ‘Tunafurahia ushirikiano huu utakaowezesha upatikanaji wa bidhaa murwa na ofa kabambe kwa Watanzania kupitia mtandao mkubwa, wa uhakika na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hii ni hatua kubwa ya ukuaji wa soko la simu nchini itakayowezesha wateja kupata simu janja ya kisasa zaidi ya TECNO Camon X kwa wakati ule ule ambapo simu hiyo inazinduliwa kote duniani”.

Umoh aliongeza kuwa, ‘Tigo inalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya zimu janja za kisasa nchini, huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma bora zaidi za intaneti kupitia mtandao wetu mpana na uhakika zaidi nchini wa Tigo 4G. Ndio maana Tigo inatoa ofa ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kwa wateja wote watakaonunua simu janja ya TECNO Camon X.’

Simu inayotumia kadi mbili ya TECNO Camon X ina kioo cha kikubwa cha inchi 6, uwezo wa 3GB RAM, memori ya 16GB, camera ya mbele yenye uwezo wa  20MegaPixel (MP) na camera ya nyuma yenye uwezo wa 16 MP pamoja na uwezo wa kutambua sura. Simu hiyo pia inakuja na garantii ya miezi 13. Vyote hivi vinaifanya simu hii kuwa bora kwa mtumiaji anayehitaji simu bora. Simu janja ya TECNO Camon X itapatikana kwa bei ya TSH 449,999/- na inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini, katika duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00# na kwenye duka la mtandao la www.jumia.co.tz/tigo-shop.

KITENGO CHA MAGONJWA YA DHARURA MUHAS WAZINDUA KITABU KWA AJILI YA KUFUNDISHIA

April 25, 2018


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura akipongezwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe mara baada ya kumaliza uzinduzi.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe na Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura wakimpatia zawadi ya kitabu mmoja ya kiongozi wa wanafunzi hao.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura akitoa shukrani zake wa wanafunzi wake ambao wamekuwa msitari wa mbele kumtia moyo wakati akiandika kitabu chake. Kitabu hicho ni mahususi kwa wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura.

Wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.

Mshehereshaji wa shughuli akitoa machache.

Picha ya pamoja.


Na Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG.

Jamii imetakiwa kushirikiana vyema na kitengo cha magonjwa ya dharura ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ili waweze kupatiwa huduma iliyo bora. Kauli hiyo ameitoa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe wakati akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa kitengo cha Dharula hafla iliyofanyika ukumbi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Kitengo cha Dharula jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa kitengo cha dharula kwa nchini Tanzania ni kipya sana na kilianza 2010 hivyo kinahitaji maboresho ya mara kwa mara ili kiwahudumie wananchi vyema.

"Tunaomba wananchi wawe bega kwa bega na kitengo cha dharula ili kuweza kutoa maoni yao pale wanapoona hawapewi huduma bora, tunahitaji kila mtu awajibike kwa upande wake tusikae kimya kuongelea uchochoroni," alisema Pembe. Aliongeza kuwa kitabu kilichozinduliwa kitaweza kumjenga mwanafunzi awe imara kwa kujua mengi katika utoaji wake wa huduma.

"Kitabu hiki kimeandikwa na Mtanzania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe na pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura hivyo aliyoyaandika yote ni yale ambayo amekuwa akiyafanya mpaka yakampa cheo hicho kikubwa, naamini hata wanafunzi watakao kisoma vile vile watafuata nyayo zake," alisema.

Nae mtunzi mkuu wa kitabu hicho, Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura alisema kuwa wameamua kuandika kitabu hicho ili kuweza kuwasaidia wanafunzi waweze kupata elimu halisi inayoendana na mazingira yetu ya kiafrika.


"Katika masomo ya udaktari kuna vitabu vingi kutoka nje ya nchi ambavyo havimsaidii mwanafunzi kwa vile vimeandikwa ili vitumike kwa nchi zilizoendela hivyo vinapofika nchini Tanzania havikidhi kiu ya wanafunzi maana mambo anayokuwa anasoma kama hadithi za kufikirika," alisema.


Alisema kuwa iko haja ya watunzi wa vitabu wakajikita kuangalia uandishi bora utakaoweza kumsaidia mwanafunzi aweze kujikwamua na si kusoma mambo yakufikirika tu. Kwa upande wake Bingwa wa Magonjwa ya Dharura, Prof. Victor Mwafongo ambaye ni mwalimu wa Dk. Hendry alitoa pongezi kwa kijana wake ambaye anasema nyota yake ameendelea kuwaka kila kukicha kwa kubuni njia mbali mbali za kuwasaidia wanafunzi.

"Dk. Hendry ni kijana ambaye walikuwa wanafunzi wangu wa kwanza na leo naona matunda yake kwa kuendelea kung'aa, na kitabu alichokiandikakitawasaidia sana wanafunzi wanaosoma masomo ya dharura," alisema.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KATIKA UKUMBI WA MSEKWA MJINI DODOMA

April 25, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma Aprili 24, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngoga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Job Ndugai baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa EAC Liberat Mfumukeko katika viwanja vya Bunge kabla ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa EALA Kenneth Mdete katika viwanja vya Bunge kabla ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngoga katika viwanja vya Bunge tayari kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge La jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati wa wimbo wa Taifa uliokuwa ukipigwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa Msekwa ambapo alihutubia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mkoni Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na viongozi wengine wakati wa wimbo wa Taifa uliokuwa ukipigwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa Msekwa ambapo alihutubia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mkoni Dodoma.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa tayari kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.

Wabunge wa EALA wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge hilo mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngoga katika viwanja vya Bunge baada ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuhutubia Bunge la EALA mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga baada ya kuhutubia Bunge la EALA mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga wa nne kutoka kulia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuwahutubia mjini Dodoma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa EAC Liberat Mfumukeko katika viwanja vya Bunge baada ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mbunge wa EALA wa Tanzania Mhe. Fancy Nkuhi baada ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma. Picha na IKULU
SERENGETI BOYS YATINGA FAINALI CECAFA U17 NCHINI BURUNDI

SERENGETI BOYS YATINGA FAINALI CECAFA U17 NCHINI BURUNDI

April 25, 2018
Serengeti Boys
TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U17 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Kenya leo Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa Serengeti Boys inayonolewa na Oscar Milambo chini ya Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen, kwani ililazimika kutoka nyuma kwa 1-0 ili kuwalaza Wakenya 2-1 baada ya dakika 90.
Mabao ya Serengeti Boys leo yamefungwa na Jaffar Juma dakika ya 21 na Kelvin Paul dakika ya 62 na sasa vijana wa Tanzania watakutana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine baina ya Uganda na Somalia.

RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AKUNWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI

April 25, 2018


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (katikati) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakiingia kwenye jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya Rais huyo kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mjini Dodoma

Sehemu ya ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukiwa katika chumba cha wageni Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (hayupo pichani) aliyewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) akisisitiza jambo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakigonga "tano" wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, DKT. AKINUMWI ADESINA, ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili ijayo,

Dkt. Adesina ameyasema hayo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

"Tunajivunia uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza miongoni mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.6" alisema Dkt. Adesina

Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

"Katika miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha usafirishaji wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji wa uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Adesina.

Dkt. Adesina ameutaja mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400 wenye njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda wa Kusini na Kusini Magharibi mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.

"Miradi hii pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji inayotarajiwa kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi wake mahili, wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu" aliongeza Dkt. Adesina.

Alisema Tanzania imepiga hatua katika viwango vya wananchi kupata huduma ya umeme ambapo awali ilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa kiwango hicho kimepanda hadi kufikia asilimia 38 na kwamba lengo la benki hiyo ni kutaka kiwango hicho kifikie asilimia 82 katika miaka michache ijayo.

Alisema ili kufikia hatua hiyo Benki yake ina mpango wa kuboresha Shirika la Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO ili liongeze uzalishaji wa umeme wenye gharama nafuu, kuongeza ufanisi na kutengeneza faida ili kuchochea maendeleo ya viwanda.

Aidha, Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, ameeleza kuwa benki yake inasiadia kuendeleza kilimo nchini kupitia Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, kwa kukuza masoko na uongezaji thamani ya mazao ya wakulima yanayozalishwa kupitia mradi huo.

Akizungumzia miradi ya kikanda, Dkt. Adesina alisema kuwa benki yake imewekeza katika miradi ya nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ili kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Kenya ili kurahisisha biashara na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika nchi hizo.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nyanja mbalimbali.

Alisema kuwa AfDB, licha ya kusaidia kwa kiasi kikubwa kufadhili miradi ya ujenzi wa barabara, nishati na mingine mingi na mfuko mkuu wa Serikali, mwaja jana ilitoa pia mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kukuza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, zinazotumika kukopesha wakulima. Dkt. Mpango amesema kuwa Rais huyo akiwa hapa nchini atatembelea mradi wa kituo cha kupooza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma na ataungana na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua barabara ya Dodoma-Babati hadi Arusha, iliyofadhiliwa na Benki hiyo na washirika wake.