RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMMED SHEIN AMETOA NISHANI KWA WATUMISHI MBALIMBALI WA SERIKALI YA ZANZIBAR

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMMED SHEIN AMETOA NISHANI KWA WATUMISHI MBALIMBALI WA SERIKALI YA ZANZIBAR

January 11, 2018
DSC_1337
Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya Utoaji wa Nishani mbalimbali ikiwemo nishani ya Mapinduzi na Utumishi wa Serikali uliotukuka Ikulu Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni miongoni mwa Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_1339
Baadhi ya Wageni waalikwa  waliohudhuria katika hafla ya Utoaji wa Nishani mbalimbali ikiwemo nishani ya Mapinduzi na Utumishi wa Serikali uliotukuka Ikulu Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni miongoni mwa Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_1387
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akimvisha nishani ya Mapinduzi Jaji Mstaafu wa Mahakama  ya Rufaa ya Tanzania Jaji Damian Lubuva katika hafla ya Utoaji wa Nishani mbalimbali. Ikulu Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni miongoni mwa Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_1402
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akimvisha nishani ya Utumishi wa Serikali uliotukuka Bibi Mwanacha Hassan katika hafla ya Utoaji wa Nishani mbalimbali. Ikulu Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni miongoni mwa Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_1430
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na  Waliopewa nishani  katika hafla ya Utoaji wa Nishani mbalimbali ikiwemo nishani ya Mapinduzi na Utumishi wa Serikali uliotukuka Ikulu Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni miongoni mwa Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

CAF YAMTEUA RAIS KARIA KUSIMAMIA CHAN

January 11, 2018

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN kati ya Morocco na Mauritania itakayochezwa Januari 13, 2018.
 
Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia akiwa Kamishna utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V huko Casablanca.
Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni Janny Sikazwe kutoka Zambia atakuwa muamuzi wa katikati akisaidiwa na muamuzi msaidizi namba moja kutoka Kenya Marwa Aden Range na muamuzi msaidizi namba mbili akitokea Msumbiji Arsenio Chandreque Maringula wakati muamuzi wa mezani Louis Hakizimana akitokea Rwanda.
Mchezo huo unaohusisha timu mwenyeji unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi.
Rais Karia hivi karibuni pia aliteuliwa na CAF kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya CHAN itakayoanza Januari 13 mpaka Februari 4, 2018.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tano(5) bingwa mtetezi akiwa DR Congo.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATANGAZA RASMI VIWANGO VIPYA VYA ADA KWA MAWAKALA WA KUSAFIRISHA WATALII NCHINI

January 11, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto).

Na Hamza Temba-WMU-Dar es Salaam
.......................................................................

Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza rasmi viwango vipya vya malipo ya ada kwa Mawakala wa kusafirisha watalii nchini baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni ya ada na tozo za biashara ya utalii yaliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana, 2017.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, imeeleza kuwa baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ya kanuni, Tangazo la Serikali namba 506 la tarehe 29 Desemba, 2017, limeweka viwango vipya vya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters).

Taarifa hiyo imeeleza viwango hivyo kuwa ni shilingi sawa na dola za Kimarekani 500 kwa kampuni za wazawa zenye umiliki mkubwa wa raia wa Tanzania na zinazomiliki gari 1 hadi 3.

"Shilingi sawa na dola za Kimarekani 2,000 kwa kampuni zenye gari 4 hadi 10, shilingi sawa na dola za Kimarekani 3,000 kwa kampuni zenye gari 11 hadi 50 na shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000 kwa kampuni zenye kumiliki gari 51 na kuendelea", imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa kampuni za kigeni zenye umiliki mkubwa wa raia wa kigeni na zinazomiliki gari 10 hadi 30 zitalipa ada ya shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000, kampuni zenye gari 31 hadi 50 zitalipa shilingi sawa na dola za kimarekani 7,500 na na kampuni zenye gari 51 na kuendelea zitalipa shilingi sawa na dola  za Kimarekani 10,000.

Kufuatia marekebisho hayo, muda wa kutumika kwa leseni za mwaka 2017 za Wakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters) umesogezwa mbele hadi tarehe 31 Januari, 2018 ili kuwezesha maandalizi ya kuingia kwenye mabadiliko ya viwango hivyo vipya.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa  maombi ya usajili na leseni za biashara ya utalii na leseni za waongoza watalii kwa mwaka 2018  kwa wafanyabiashara wapya na wanaoendelea na biashara yanaendelea kupokelewa.

Waombaji wote wametakiwa kufuata masharti ya uombaji wa leseni hizo ikiwemo kuwasilisha nakala za hati za usajili wa magari zilizothibitishwa kisheria kwa Wakala wa kusafirisha watalii (wapya na wanaoendelea na biashara) na kivuli cha leseni ya mwaka 2017 kwa wafanyabiasbara wote. 

"Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Desemba 10 na 11 mwaka 2017, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alikutana na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha kwa lengo la kuwashirikisha katika mapendekezo ya viwango vipya vya ada kwa Wakala wa kusafirisha watalii ambavyo vilivyotolewa na Wizara yake.  Mapendekezo ya viwango hivyo yalilenga kuongeza mapato na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wenye gari kuanzia moja kuingia katika biashara hiyo.

TANESCO YATOA SIKU NNE (4) KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME WAWE WAMELIPA, VINGINEVYO HUDUMA ZINASITISHWA

January 11, 2018
 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

JANUARI 11, 2018
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com
TAASISI YA TULIA (TULIA TRUST FUND) YAKABIDHI TV 6 KWA JKCI AMBAZO ZITAFUNGWA KATIKA WODI NA KLINIKI ZA WATOTO

TAASISI YA TULIA (TULIA TRUST FUND) YAKABIDHI TV 6 KWA JKCI AMBAZO ZITAFUNGWA KATIKA WODI NA KLINIKI ZA WATOTO

January 11, 2018

Picha no. 1a

Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo akimweleza  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson maendeleo ya afya za pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.

Picha no. 2

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson akiwajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.

Picha no. 3 Picha no. 4

Naibu Spika wa Bunge Mhe.  Dkt.  Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.

Picha no. 5 Picha no. 6

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu.  Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.

Picha na JKCI

TATU MZUKA YAKABIDHI MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA KITUO CHA POLISI MBANDE

January 11, 2018
Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka  kupitia mshindi wa wiki iliyo pita kutoka Temeke Erinisha Kilango aliyeshinda milioni 50,wamezawadia Wilaya ya Temeke mabati ya thamani ya milioni 5 kusaidia kujenga kituo cha polisi cha Mbande.

 Tatu Mzuka inasemaga kuwa "ukishinda na Tanzania inashinda. Kwenye wilaya ambayo mshindi anatoka, Tatu Mzuka wanazawadia wilaya milioni 5  kusaidia maendeleo ya wilaya hiyo. 

Ukicheza Tatu Mzuka , unaweza kushinda hadi milioni 6 kila lisaa, milioni 10 kila siks na jumapili hii kuna jackpot ya milioni 70 ya kuzawadia. 
  Afisa wa Mawasiliano Bi. Kemi Mutahaba akikabithi mabati ya thamani ya millioni 5 kwa Katibu Tawala wa Temeke Mh.  Hamisi Komba kusaidia kujenga kituo cha Polisi Mbande, wilaya ya Temeke.
 Mafundi wa ujenzi  wakiwa wana kabidhiwa mabati yenye thamani ya milioni 5 na Afisa ya Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Kemi Mutahaba.
Mhe Hamisi Komba, Katibu Tawala wa wilaya ya Temeke akikabidhiwa fedha tasilimu milioni 5 na Bi . Kemi Mutahaba  wa Tatu Mzuka kwa ajili ya kununua  mabati yatakayo tumika kujenga kituo cha Polisi Mbande, Temeke.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

SERENGETI LITE MDHAMINI RASMI LIGI YA SOKA LA WANAWAKE

January 11, 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne  na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.   
Ofisa mkuu wa michezo wa wizara ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama) akishuhudia tukio la kusaini Mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya  Wanawake kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL (Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu .

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne  na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.   

 Dar es Salaam, Januari 10 2018: Bia pendwa ya Serengeti Premium Lite, ambayo inazalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), leo imetangaza kuwa mdhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake (Women Premier League). Katika Mkataba uliosainiwa kati ya SBL na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne  na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.   
Kama mdhamini rasmi wa ligi hiyo, Serengeti Premium Lite itatoa msukumo kwa timu zote nane za wanawake kwenye ligi ambapo mshindi atakuwa mwakilishi wa taifa katika mashindano ya kikanda na ya kimataifa.  Kupitia udhamini huo, SBL ina matumaini makubwa kwamba itaweza kuwazindua wananchi na hasa mashabiki wa soka na kuwaunganisha pamoja ili kuongeza hamasa katika ligi ya taifa ya wanawake kupitia bia hiyo kipenzi cha watanzania ya Serengeti Premium Lite.  
“Tunayo furaha kubwa kuwa wadhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake kupitia bia yetu maarufu ya Serengeti Lite. Siku zote tumekuwa tukiamini katika kuendeleza vipaji katika sehemu mbali mbali za nchi na haswa inapokuja katika michezo inayotuleta pamoja. Tunaamini udhamini wetu utawavutia mashabiki wa rika mbali mbali kuiunga mkono ligi ya wanawake na kufikia mafanikio makubwa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, SBL inaamini katika nguvu ya mpiga wa miguu ambayo inawaunganisha watu.
Udhamini wa Twiga Stars unafuatia historia ndefu ya udhamini wa timu ya soko ya wanaume, Taifa Stars ambayo mpaka hivi sasa inaendelea kupata udhamini wa SBL kupitia bia yake mama ya Serengeti Premium Lager. SBL ni sehemu ya kampuni ya Diageo ambayo inauhusiano mkubwa na masuala ya soka duniani ikiwa ni pamoja na udhamini wa Ligi Kuu ya Uingereza kupitia bia ya Guinness
Kwa upande wake Makamu wa  Rais wa TFF Michael Wambura alisema; “Leo kwa mara nyingine tunashuhudia ushikiano muhimu kati yetu na SBL, kampuni maarufu ya bia na ambayo imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia maendeleo ya michezo nchini. Ushirikiano huu utasaidia sana katika kuendeleza soka letu la wanawake pamoja na mashindano tutakayokuwa tunaandaa. Tunafurahia udhamini huu kupitia bia ya Serengeti Lite na tunaamini utakuwa wa mafanikio makubwa,”
Utiaji saini kati ya pande hizo mbili ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Bw, Yusuph Singo ambaye aliipongeza SBL kwa kujitolea kwake katika kuunga mkono sekta ya michezo nchini na pia kuwataka Watanzania wenye mapenzi mema pamoja na makampuni mengine kuiga mfano mzuri wa kampuni ya SBL.
MWISHO………

TANESCO YATOA SIKU NNE (4) KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME WAWE WAMELIPA, VINGINEVYO HUDUMA ZINASITISHWA

January 11, 2018
 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

JANUARI 11, 2018
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com