Green Sports Africa Academy kufanya ziara Azam FC

Green Sports Africa Academy kufanya ziara Azam FC

December 01, 2016


KITUO cha kukuza vipaji cha Green Sports Academy kutoka jijini Nairobi, Kenya kinatarajia kufanya ziara maalumu kwenye makao makuu ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.
Ziara hiyo ya siku sita itakayoambatana na mechi za kirafiki, itaaanza rasmi Desemba 20 jioni watakapowasili nchini hadi Desemba 25 mwaka huu watakaporejea nchini kwao.
Green Sports itakuja nchini ikiwa na timu zake nne za umri tofauti chini ya miaka 13, 15, 18 na 21, ambapo itacheza mechi tatu za kirafiki kuanzia Desemba 22, 23 na 24 dhidi ya timu za vijana za Azam FC.
Uongozi wa kituo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Stephen Ochiel Otieno, umetoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Azam FC kwa kuwakubalia ziara hiyo ya kuja hapa nchini.
Otieno amesema kuwa hiyo itawahamasisha sana vijana wadogo wenye vipaji kuelekea kuwa nyota wa kimataifa katika siku za usoni, huku pia kwa upande wao wakiangalia mbele kuendeleza ushirikiano wa kudumu na Azam FC, ambayo kwa sasa ndio klabu bora iliyowekeza kwa vijana katika ukanda huu.
Huu ni ugeni mkubwa wa pili kwa mwaka huu kwa Azam FC ikihusisha kituo cha kukuza vipaji, wa mara ya kwanza ulikuwa ni mwezi Juni ilipozialika timu mbili za Afrika Mashariki, Football For Good Academy ya Uganda na Ligi Ndogo Academy ya Kenya kwenye michuano ya Azam Youth Cup 2016, ambayo pia iliishirikisha Future Stars Academy ya Arusha na kushuhudiwa wenyeji Azam FC Academy ikitwaa ubingwa wa michuano hiyo.

RC MAKALLA AISHUKURU UN KWA MISAADA NA USHIRIKIANO KWA SERIKALI YA TANZANIA

December 01, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akielezea mipango aliyonayo ya kuinua uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia) nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: 'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI JIJINI ARUSHA TAYARI KUANZA ZIARA YAKE YA KIKAZI

December 01, 2016

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo baada ya kuwasili jijini Arusha kuanza ziara ya kazi mkoani humo Desemba 1, 2016.Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Iddi Kimanta baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige  baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.

TTCL yawakumbuka wanafunzi wa vyuo huduma za intaneti

December 01, 2016


Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS). 
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
Semina ikiendelea kwa wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela. 
Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack. 

VIWANDA VYA UZALISHAJI VYATENGENEZA AJIRA 16000

December 01, 2016
                       Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
JUMLA ya ajira 16,671 zimetengenezwa na viwanda vya uzalishaji nchini ambapo viwanda vya wawekezaji kutoka nje ya nchi vikiongoza kwa utoaji wa ajira hizo.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu ongezeko la wawekezaji nchini kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Waziri Mwijage amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanya juhudi za kuwahamasisha wawekezaji ili waweze kushiriki katika kuchochea mageuzi ya kiuchumi hivyo imeanza kupunguza uuzaji wa malighafi nje ya nchi ikiwa ni njia mojawapo ya kuwavutia wawekezaji kuwekeza nchini.

”Katika kujenga uchumi wa viwanda, tunalenga kujenga uchumi shirikishi na ulio endelevu ambao utahusisha watu wengi hivyo utaratibu wa aina hiyo utawasaidia kuwainua wananchi kiuchumi pamoja na kukuza pato la taifa,” alisema Mwijage.

Kwa mujibu wa Mwijage ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, takwimu zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la uwekezaji katika sekta za ujenzi wa majengo, maliasili, rasilimali watu, viwanda vya uchakataji bidhaa, sekta ya nishati, kilimo, huduma, usafiri pamoja na mawasiliano.

Aidha, amezitaja sekta zingine za uwekezaji ambazo zinaongoza kwa uzalishaji wa ajira kwa wingi kuwa ni majengo ya biashara ambayo yanazalisha ajira 5537, sekta ya utalii ajira 2011 pamoja na sekta ya huduma inayozalisha jumla ya ajira 680.

Akizungumzia kuhusu ubora wa makaa ya mawe, Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, John Shija amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na makaa ya mawe ya kutosha ya kuweza kuchimbwa na kutumiwa kwa zaidi ya miaka 200.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, Mhandisi Lugano Wilson amesisitiza kuwa kati ya nchi zinazozalisha makaa ya mawe zikiwemo za India, China na Afrika ya Kusini, nchi ya Tanzania ndiyo inayoongoza kwa kuwa na makaa ya mawe yenye ubora unaokubalika.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage  akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ongezeko la wawekezaji nchini katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA

December 01, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
 

Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. 
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).  
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.

Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
  
Na Mathias Canal

Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.

Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.    

SERIKALI YASHAURI MAJINA YA WAHASIBU WEZI YAWEKWE HADHARANI

December 01, 2016
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

 Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
 Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
 Katika hafla ya kufungua kituo hicho nyama choma zilikuwepo ingawa mimi sikubahatika kupata walau finyango moja.
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na 
wageni waalikwa.
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wengine akitoka kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
 Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
 Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani 
kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
 Mkutano ukiendelea.
 Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa bodi ya NBAA na Mfuko wa GEPF
Picha ya pamoja.


Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na  Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.

"Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.

Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.

"Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.

Aliwataka wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.

Mpango alisema kuwa serikali itaendelea kuwatumbua watumishi wasio waaminifu na wahasibu bila ya kumuonea muhusika huruma na kuwa atakayebainika atapelekwa mahakama ya mafisadi iliyofunguliwa.

 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA Pius Maneno alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia sh. biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia kumbi hivyo ujenzi wa kituo hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa kitakuwa ni chanzo cha mapato.

Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.

Alisema awali walikadiria ujenzi huo ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14 lakini kutokana na sababu mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh. bilioni 33 zaidi ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.

Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi aliishukuru serikali kwa ushirikiano na mifuko ya jamii na NBAA  hasa katika suala zima la kusukuma maendeleo ya nchi ikiwa na kuzitaka taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho cha kimataifa ili kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.


NAIBU INSPEKTA JENERALI WA POLISI ABDULRAHMANI KANIKI AFUNGA MAFUNZO YA KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA POLISI KIDATU.

December 01, 2016
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akimkabidhi cheti cha Upelelezi Polisi Konstebo Jonathani Tossi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akifafanua (katikati) jambo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro. Kulia ni Kamishina wa Polisi operesheni na mafunzo, Nsato Marijani 
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ( CP) Nsato Marijani akimsikiliza mwakilishi wa Taasisi ya Hans Sidel Bi Juliana wakati wakimsubili Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi kuwasili katika chuo cha maafisa wa Polisi Kidatu kwa ajili ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari Polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni. ( picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akisalimiana na Kamishina wa Polisi operesheni na mafunzo, Nsato Marijani alipofika kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akisamilimiana na Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni Mark Njera alipofika kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro

KAMISHNA WA TRA AHITIMISHA MAFUNZO YA ‘SCANNER’ MPYA BANDARINI

December 01, 2016

Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa mashine za ukaguzi wa mizigo ‘scanner’ kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na TRA. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Abdulrahman Mbamba pamoja na Wakufunzi kutoka Kampuni iliyofunga mashine hizo.


Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akikabidhi vyeti kwa wahitimu mbalimbali kutoka TPA na TRA.



Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu na Wakufunzi