TIGO YAFUNGUA DUKA LA KISASA SAME

January 15, 2016
Katibu wa wilaya ya Same Mhe. Evagry Keiya (katikati)akikata utepe kufungua duka la Tigo Same, wanaoshuhudia ni Meneja wa huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola(kushoto) na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) mapema mwishoni wa wiki iliyopita

Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo  wakiwa katika tafrija ya ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema wa mwishoni  wa wiki iliyopita 

Mkurungezi wa Tigo kanda ya kaskazini Bw.George Lugata akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema mwishoni wa wiki iliyopita 

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye tafrija ya kufungua duka la Tigo same wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mh Evagry Keiya  mapema mwishoni wa wiki iliyopita 



Kampuni ya simu ya Tigo imefungua duka jipya la  same ambalo limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kaskazini Bw.George Lugata alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.

"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Same ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu za mkononi"Alisema Lugata

Aliongeza kuwa ufunguzi huo unaendana na kuboresha muonekano wa duka hili kuwa wa kisasa 

Lugata alisema kuwa duka hilo linalopatikana katika mtaa wa shule linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.

Kwa upande wa katibu wa mkuu wa wilaya ya same  Mhe. Evagry Keiya alipongeza hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya same .



photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

TASWIRA MBOVU YA BARABARA YA "MARKET STREET" JIJINI MWANZA.

January 15, 2016
Hii ni barabara inayotegemewa na daladala za Bwiru-Kisesa, Airtport- Kishiri pamoja na Ilemela-Kishiri hii ikiwa ni kwa upande wa daladala. Lakini pia ikitegemewa na watumiaji wengine wa vyombo vya moto vya binafsi.
Ni barabara iliyotumika pia na wakazi wengi wa Jiji la Mwanza wakiwa wanatoka katika mizunguko yako ikiwemo kutoka Soko Kuu la Jiji la Mwanza. Kama inavyoonekana katika picha inahitaji msaada maana wakati huu wa mvua imeharibika sana.

"Hii barabara inaharibika mara kwa mara kutokana na mitaro iliyopo hapa kuziba mara kwa mara kutokana na wafanyabiashara katika maeneo haya kuwa na tabia ya kutupa makopo mitaroni na hivyo kusababisha mitaro kuziba na hivyo mvua ikinyesha maji yanajaa katika barabara hii na hatimae kusababisha hali hii unayoiona". Binagi Media Group imeeleezwa na baadhi ya wafanyabiashara waliopo jirani na barabara hiyo.

Watumiaji wa barabara hiyo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kushughulikia ukarabati wa barabara hiyo pamoja na kusimamia suala la usafi ili kuzuia uchafu kutupwa katika mitaro iliyo katika barabara hiyo ili kuzuia kuziba na hatimae kusababisha uharibifu katika barabara hiyo.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHILISHWA.

January 15, 2016
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae kuahilishwa kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea kusikilizwa kuanzia majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na moja jioni.
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani) akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema)

KITUO CHA UTAFITI CHA RCRSDS KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUKUSANYA, KUHIFADHI NA KUWEKA ANGANI TAARIFA ZA KITAFITI ZA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA BINAFSI NA UMMA

January 15, 2016
Mkurugenzi Mtendaji wa  Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)















Celina Mathew

KITUO cha Utafiti wa shughuli za maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.

Mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo utapelekwa katika mikoa 30 Tanzania Bara pamoja na maeneo 100 yenye wananchi wenye uhitaji mkubwa.

Akizungunza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.

"Sisi kama RCSDS tunatambua uwepo wa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi zinazochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji na hata majanga yanapotokea ili kunusuru na kuboresha maisha ya watanzania wenzetu na kuthamini michango na misaada yao,"alisema.

Alisema mfumo huo unaoaznishwa una lengo la kutambua michango na misaada mbalimbali inayotolewa na wadau kwa jamii pia wadau nao wapate fursa ya kuweka malengo yao ya uwajibikaji kwa jamii kwa kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi kiuwajibikaji na eneo lipo nani amewekeza.

Shempemba alisema utafiti walioufanya na kuutolea taarifa msimu ulipita  kwa kushitikiana na taasisi ya ukaguzi ya Konsalt inayofanyika kila mwaka wapo waliosaidia jamii kwa sekta mbalimbali kama huduma za afya, maji, miundombinu, elimu, michezo, maafa na mambo mengine kwa asilimia tofauti.

Aliongeza kuwa tafiti hizo pia zimesaidia takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji jamii ulivyowekezwa, jamii ilivyonufaika na misaada hiyo na wadau walivyonufaika na uwekezaji wao kwa jamii hizo.

TIMU ZA PATH NA TANGA BEACH RESORT HAKUNA MBABE ZAFUNGANA BAO 1-1 UWANJA WA POPATLALY SEKONDARI JIONI HII

January 15, 2016





KIONGOZI WA ORGANISATION YA PATH TANZANIA ZAHRA MKOMWA AKIPASHA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO

MENEJA MKUU WA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT ,JOSEPH NGOYO AKIFUATILIA MECHI KATI YA PATH DHIDI YA TIMU YA HOTEL HIYO MCHEZO ULIOMALIZIKA KWA TIMU HIZO KUFUNGANA BAO 1-1





PROF. MUHONGO AITAKA KAMPUNI YA TANZU YA TANESCO (TGDC) KUHARAKISHA UZALISHAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI KUTOKA ZIWA NGOZI

PROF. MUHONGO AITAKA KAMPUNI YA TANZU YA TANESCO (TGDC) KUHARAKISHA UZALISHAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI KUTOKA ZIWA NGOZI

January 15, 2016

muhongo 
Na Asteria Muhozya
…………………………….
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameiaigiza  Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi  Tanzania (TGDC Ltd) kuwa ifikapo June 2016, iwe imeanza kuchoronga mashimo 3 katika eneo la Ziwa Ngozi ikiwa ni hatua ya mwisho inayohitajika kabla ya kuanza kujenga mitambo ya kuzalisha jotoardhi.
“Utafiti muhimu umekamilika. Joto la maji ni kubwa, 230-250C linalokidhi uzalishaji wa umeme. Hiki kitakuwa ni chanzo kipya muhimu cha umeme jadidifu” ,alisema Prof. Muhongo.
Ameongeza kuwa, jambo hilo haliwezi kuendelea kusubiri kutokana na mahitaji ya nishati hiyo nchini ikizingatiwa kuwa, Tanzania inapitiwa na  Bonde la Ufa kwa kiasi kikubwa.
“Tayari wenzetu Kenya na Ethiopia wamepiga hatua kubwa katika nishati hii lakni kwa upande wetu hatuna megawati hata moja kwa hili lazima tuchukue hatua tutoke hapa tulipo. Hakuna kusubiri anzeni na Ziwa Ngozi” amesema Muhongo.
Prof. Muhongo aliitaka Kampuni hiyo kuongeza nguvu katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la  Ziwa Ngozi kutokana na kuwepo maendeleo makubwa ya kitafiti ikilinganishwa na maeneo mengine yenye viashiria kama hivyo ikiwemo eneo la Mbaka lililopo Wilaya ya Rungwe.
“TGDC tunataka umeme wa jotoardhi, wananchi wanataka umeme, hawatakuwa kusikia maneno, ifikapo Mwezi juni na  mimi nitakwenda Ngozi kuangalia mmefikia wapi na kama hakuna maendeleo tutabadilisha timu ya wataalamu”, alisisitiza Prof. Muhongo.
Akizungumzia kuhusu fedha za miradi, Prof. Muhongo alieleza kuwa, nchi nyingi duniani hazitegemei fedha za Serikali kutekeleza  miradi mikubwa ya nishati na ndiyo sababu hata Tanzania inatafuta fedha katika taasisi mbalimbali ikiwemo kukaribisha wawekezaji  ili kutekeleza miradi hiyo.
“Serikali kwa upande wake itasaidia kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi na ninyi kazi yenu ni kuhakikisha umeme wa jotoardhi unaanza kutumika Tanzania kwa kuanza na Ziwa Ngozi”.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa amefarijika na maelekezo aliyoyatoa Prof. Muhongo na kuahidi kuweka nguvu kubwa katika kufuatilia suala hilo. ” Ujio wako umetupa ari mpya katika kusimamia miradi hii kwa sababu rasilimali zipo lakini zimekaa tu nakuahidi kasi ya ufuatiliaji itaongezwa”,alisema Kandoro
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rugwe ,Mwalimu Zainabu Mbusi alieleza kuwa maagizo ya Prof. Muhongo yamekuwa faraja na kuongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo itaongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa miongoni mwa nchi za uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Kwa pande wake  Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Fred Atupele alieleza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutachochea kasi ya uendelezaji wa viwanda vikubwa na vidogo na kueleza kuwa, kwa nafasi yake  watachukua jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa vyanzo hivyo.
Awali akieleza akieleza Mikakati ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi wa TGDC , Mhandisi Boniface Njombe alisema eneo la Mbaka ni miongoni mwa maeneo ya maji moto yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi.
Vilevile, alieleza hivi sasa wataalam kadhaa wamesambaa wakifanya tafiti za mwisho katika  eneo la Mbaka ili kuanisha mipasuko na maeneo ya kuchimba nishati hiyo na kuongeza kuwa, TGDC imelenga kwa  kuanza kuzalisha umeme wa jotoradhi  wa kiasi cha  megawati 200 huku lengo ikiwa ni kufikia megawati 5000.
Aidha, alieleza kuwa, mbali na kuzalisha umeme , maji moto yanaweza kutumika viwandani na majumbani katika kukausha mazao ikiwemo kuwa kivutio cha utalii kuoga kwa kuwa inaelezwa kuwa maji hayo yanatajwa kuwa tiba ya magonjwa ya ngozi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopitiwa na Bonde la Ufa eneo ambalo linatajwa kuwa na viashiria vya nishati ya jotoardhi.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

January 15, 2016

W6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
W7
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Rogatius Kipali, akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
W8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Injinia Pius Nyambacha na wa poli kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utalawa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lilian Mapfa.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Mhe. Kassim Majaliwa awataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan

Mhe. Kassim Majaliwa awataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan

January 15, 2016

k5
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, akizungumza na Wadau wa Sekta ya Ujenzi kuhusu Kuungana na Kushirikiana katika kuboresha Miundombinu hapa nchini katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
k6
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Joseph Nyamhanga akizungumza kuhusu fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Miundombinu hapa nchini katika Mkutano huo uliyohusisha sekta binafsi na Serikali kuhusu namna ya kuboresha sekta ya Miundombinu.
k7
Naibu Waziri wa Miundombinu wa Japan Koji Yonetani akizungumza katika Warsha hiyo na kusema nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuboresha Miundombinu hapa nchini.
k9
Watendaji na Wadau wa Sekta ya Ujenzi wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Serikali na Binafsi kuhusu Ubora wa Miundombinu nchini.
k8
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa (Wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Japan Koji Yonetani(Wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (Wa Pili kushoto).
…………………………………………………………………………….
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan katika kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi, usafirishaji na mawasiliano nchini. Akizungumza jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo kutoka nchini Japan na Tanzania, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ushirikiano huo utaleta tija kwa taifa kwani wadau wa Sekta hiyo wataweza kujifunza masuala mengi kutoka kwa wataalam hao. “China na Japan ni moja ya nchi zenye Wakandarasi wengi na wazoefu katika sekta ya ujenzi, kushirikiana nao kutaongeza ushindani na kupelekea kupata fursa ya uwekezaji ndani na nje ya nchi, amesema Waziri Mkuu. Waziri Mkuu Majaliwa ameyataka Makampuni yote yenye miradi ya ujenzi nchini kufanya kazi vizuri na kumaliza kwa wakati katika kipindi hiki ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Amesema fursa ipo kwa Kampuni kutoka Nje ya nchi kufanya kazi na Kampuni za ndani kwa lengo la kupata Zabuni ndani na nje ya nchi, mara zinapotangazwa. “Kutokana na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi, hatuna budi Makandarasi wetu kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzenu kutoka nje ili kupata maendeleo katika Sekta hii”, alisisitiza Waziri Mkuu. Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri, Prof. Makame Mbarawa amewaomba Wawekezaji, Wakandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia fursa hiyo, kuungana na kutengeneza kampuni za ubia baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. “Tumieni fursa hii kupata elimu na uzoefu na hata kuunganisha Makampuni kwani wenzetu wa Japan wana uzoefu mkubwa na maendeleo katika Sekta hii, ukilinganisha na sisi”, alisema Naibu Waziri. Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kupitia mkutano huo Wakandarasi nchini wataweza kujifunza njia za kisasa ambazo zitasaidia katika kuboresha Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan, Bwana Takatoshi Nishiwaki, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukubali kushirikiana katika kuendesha mkutano huo na wadau wa sekta ya ujenzi wenye lengo la kubadilishana ujuzi na teknolojia kuhusu Miundombinu bora. Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha Wawekezaji, Wakandarasi na na Wafanyabiashara kutoka nchini Japan na Tanzania walio katika Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano. IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA CHINA

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA CHINA

January 15, 2016

el1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akiongea na Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali ya Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
el2
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akiongea na na Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).
el4
Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa kwanza kulia kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM
el5
: Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto akimpa zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya mazungumzo ya uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)