MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MV TANGA KUZINGATIA USALAMA WA ABIRIA.

MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MV TANGA KUZINGATIA USALAMA WA ABIRIA.

October 26, 2016
temi1
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa  Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko  Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David.
temi2
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto aliyesimama) akizungumza  na watumishi wa TEMESA Tanga wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia hali ya utendaji kazi, kulia ni Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko  Ngoroma.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Tanga
……………………………………………….
Na Theresia Mwami TEMESA TANGA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.
Amesema hayo alipotembelea na  kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama wa abiria na  kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko hicho.
Ndugu zangu hapa tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia” Alisisitiza Dkt Mgwatu.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko  Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine vilivyopo mkoani Tanga.
Aidha kwa upande wao watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
 Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.
 MUSWADA WA HABARI UTATOA FURSA KWA CHOMBO CHA HABARI KUOMBA RADHI PASIPO KUCHUKULIWA HATUA NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA

MUSWADA WA HABARI UTATOA FURSA KWA CHOMBO CHA HABARI KUOMBA RADHI PASIPO KUCHUKULIWA HATUA NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA

October 26, 2016
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Uhuru FM, Sheila Simba wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel Akilimali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi wa gazeti la Uhuru wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Ramdhani Mkoma na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara Habari( MAELEZO), Jonas Kamaleki.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru, Sophia Ashery wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa gazeti la uhuru, Njumai Ngota wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Ramadhani Mkoma akimpatia maelezo kuhusu uhifadhi wa magazeti ya zamani kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahariri wa Gazeti la Uhuru wakifuatilia kwa makini mkutano wa mazungumzo baina yao na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza wakati wa mkutano wake na bodi ya uhariri wa gazeti la uhuru wakati wa ziara yake ya kutembela ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mhariri wa Picha, Yassin Kayombo na Mhariri wa Habari Abdallah Kimweri.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akisalamiana na Mhariri msanifu kurasa wa gazeti la Uhuru, Jane Mihanji mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Uhariri ya gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.

………………………………………..

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

Dar es Salaam.

SERIKALI imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.

“Sifa moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.

Aidha Abbas alisema kuwa ipo misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

Aidha Abbas aliongeza kuwa muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa wanahabari kwani unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa habari ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari pekee.

Mkurugenzi Abbas alisema kila taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati kwa Tanzania napo kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki taaluma ya habari.
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

October 26, 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Japan nchini, Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi, na kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo la mazungumzo hayo ni kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi jirani ya Rwanda na Tanzania. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA

October 26, 2016


Na Daudi Manongi,MAELEZO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.

Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora. 
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shirika la Posta kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika jijini Dar es salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Dkt. Haruni Kondo akisoma taarifa ya uendeshaji wa Shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 
WAZ IRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

WAZ IRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

October 26, 2016
mbk1
Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
mbk2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira
mbk3
Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua
……………………………………………………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe January Makamba hii leo ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.
Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
  1. Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.
  2. Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
  3. Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu
  4. Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
  5. Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi
  6. Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji
  7. Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira
  8. ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma
  9. Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
  10. Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini
Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:
  1. Wananchi kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na Uchomaji wa misitu.
  2. kuwakumbusha wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu wachache
  3. Serikali inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998
  4. Kuundwa kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji
  5. Kuundwa kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho
  6. Kuondokana na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.
HAFLA MCHAPALO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YAFANA JIJINI DAR

HAFLA MCHAPALO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YAFANA JIJINI DAR

October 26, 2016
Ziafuatazo ni picha za hafla mchapalo (Cocktail Party) ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za serikali, binafsi pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakigonga 'cheers' ya kutakiana kheri na afya njema katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kugonga glass.
Shamra shamra za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zikiendelea jukwaa kuu.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakitazama 'documentary' fupi kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.
MC wa hafla mchapalo ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba kutoka ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiendesha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo Anthony Rutabanzibwa (kushoto) na Amon Manyama katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (katikati) kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Emslies Travel Ltd. Jaffer Hirji (kushoto) wakati wa hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wageni waalikwa na waheshimiwa mabalozi wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.






Nguse Nyerere akiwa na baadhi ya Maafisa wenzake wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa.
Edgar Kiliba (katikati) wa ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.

Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba na Beatrice Mkiramweni katika picha ya pamoja.

Baadhi ya madereva wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb) katika hafla ya kushehereka miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA