MKAPA AKARIBISHWA MONDULI

April 14, 2014
Rais mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa leo (jumatatu) amefanya ziara kutembelea shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African Wildlife Foundation  Wilayani Monduli. Mzee Mkapa ni Makamu Mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini Washington Marekani. picha mbalimbali zinamuonesha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza Mzee Mkapa
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiagana na  Mzee Mkapa
 MISS ILALA 2013 DORIS MOLLEL AKABIDHI VITABU 50 SHULE YA MSINGI PUGU DAR

MISS ILALA 2013 DORIS MOLLEL AKABIDHI VITABU 50 SHULE YA MSINGI PUGU DAR

April 14, 2014

Img_4285
Miss Ilala 2013, Doris Mollel ijumaa ya wiki iliyopita alitembelea shule ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam na kukabidhi vitabu 50 za hadithi kwa wanafunzi wa shule hiyo katika harakati zake binafsi za kuwajengea wanafunzi na watoto utamaduni na tabia ya kujisomea kwenye umri mdogo.
Miss Ilala huyo wa mwaka 2013 alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi kujisomea kama ufunguo wa maisha yao ya baadaye.
Img_4273
Miss Ilala 2013, Doris Mollel akimkabidhi vitabu Mwalimu Josephine Matiku kwenye hafla rasmi ya makabidhiano shule hapo ijumaa iliyopita jijini Dar.
Img_4236
Miss Ilala 2013, Doris Mollel akipozi na walimu wa shule hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu.
Img_4265
Miss Ilala 2013, Doris Mollel katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Pugu.
Img_4294
YALIYOJIRI DODOMA.......ASILIMIA KUBWA YA WAJUMBE WAUNGA MKONO SERIKALI MBILI

YALIYOJIRI DODOMA.......ASILIMIA KUBWA YA WAJUMBE WAUNGA MKONO SERIKALI MBILI

April 14, 2014


1k
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Msemaji wa walio wachache wa Kamati namba saba Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa maoni ya walio wachache leo mjini Dodoma. 
2d
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Msemaji wa walio wachache wa Kamati namba sita Ismail Jussa akitoa ufafanuzi wa maoni ya walio wachache leo mjini Dodoma. 
3
Mwenyekiti wa Kamati namba saba ya Bunge Maalum la Katiba Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi akiwasilisha maoni ya kamati yake leo mjini Dodoma kuhusu sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.
4
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mohamed Abood(kushoto) na Stephen Wassira wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
5a
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sophia Simba (kushoto) na James  Lembeli (katikati) na Job Ndugai (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
 6a
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Philemon Ndessamburo (kushoto) na James Mbatia (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
mwenyekiti
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(wa pili kulia) akiongoza na wajumbe wengine wa Bunge hilo kuelekea katika mapumziko mafupi mara baada ya kikao kuharishwa leo mchana mjini Dodoma.
raza
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Mbatia (kushoto), Mohamed Raza( wa pili kushoto) , Profesa Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Freeman Mbowe(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.(Picha na Bunge Maalum la Katiba -Dodoma).

TAZAMA YANGA ILIVYOWASILI MOSHI KUKABILIANA NA TIMU YA PANONE FC...,

April 14, 2014

Leo majira ya saa nne na nusu Asubuhi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro mashabiki mbalimbali wa Mpira wa miguu hususani Mashabiki na wanazi wa Timu kongwe ya mpira wa Miguu Daresalaam Yanga African Walikua katika barabara kuu ya Moshi Arusha kuipokea Timu ya Yanga.
Basi la Yanga likiwa nje ya kituo cha Mafuta cha Panone kilichopo weruweru nje kidogo ya Mji wa Moshi.

Timu ya Yanga ambayo inatarajia kushuka dimbani hapo kesho katika Mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Panone Fc ambayo ni  Mabingwa wa Ligi Daraja la Tatu mkoa Kilimanjaro. Mchezo huo uliodhaminiwa na Panone and Co. Ltd na Ngiloi ulomi enterprises huku wakishirikiana na wadau mbalimbali wa mpira wa Miguu mkoani Kilimanjaro ambao ni Ngorika bus Service, Kili Fm Radio, Kifaru oil, Malindi Night Club, Ibra Line, Marenga Investment co. Ltd na  Moshi fm Radio. Katika kufanikisha hilo Panone wamejiandaa kuhakikisha Historia ya Kimichezo inavunjwa kwani Yanga imewahi kucheza ndani ya Kilimanjaro Miaka 23 iliyopita.
Mchezaji wa Yanga Didie Kavumbagu akifurahia Mandhari ya Mji wa Moshi.

Tukizungumza na Kocha mkuu wa yanga  Hans Plujim kuhusiana na mchezo huo baada ya kuwasili Moshi mkoani Kilimanjaro. Amesema anategemea kutumia Mchezo huo wa Kirafiki na Timu ya Panone Fc kama mchezo wa Maandalizi wa mechi yao ya mwisho dhidi ya timu ya Simba Sport Club. Akizungumzia kikosi atakachokichezesha amesema anategemea kuchezesha wachezaji ambao watacheza na yanga ndio maana amebeba wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo huu.

Meneja wa Panone and Co. Ltd Gido Marandu akiwa na Kocha Mkuu wa Yanga Hans Plujim na Kocha Msaidizi ndugu Mkwasa Baada ya Kuwapokea Katika Kituo cha Mafuta Cha Panone Kilichopo Weruweru leo Asubuhi.
Akizungumza nasi Meneja wa Panone and Co. Ltd kwa kanda ya Kaskazini ndugu Gido marandu amesema Kampuni imejiandaa vizuri kuweza kuhakikisha kilakitu kinakwenda sawa na Timu ya Yanga imeshawasili. Hata hivyo alitaja Viingilio nitakua shilingi 10000 kwa viti maalumu na 7000 kwa viti maalumu B na shilingi 5000 kwa Mzunguko. Kuhusu suala la Ulinzi alisema ulinzi uko wa Kutosha kutoka kwa Jeshi la Polisi na Kampuni ya ulinzi wenye Dhamana ya kuhakikisha ulinzi unakua hapo.

Alimaliza kwa kusema “Huu ni wasaa wa washabiki na wapenzi wa timu ya Yanga ndani ya mkoa wa kilimanjaro baada ya miaka mingi kukosa mchezo mkubwa ndani ya mkoa wetu na huu ndio mwanzo tu”

Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa Akiwa ametulia katika Gari baada ya Kuwasili Moshi.

KATIBU MKUU WA FIFA KUFUNGUA SEMINA YA MAWASILIANO JIJINI DAR

April 14, 2014


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke atawasili nchini Mei 1 mwaka huu ambapo atafungua semina ya mawasiliano itakayoshirikisha viongozi wa vyama wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza Dar es Salaam leo (Aprili 14 mwaka huu), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema Valcke ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania atafuatana na maofisa wengine wa saba wa FIFA.
Amesema semina hiyo iliyoandaliwa na FIFA itafanyika kwa siku mbili (Mei 1 na 2 mwaka huu) ambapo vilevile Valcke atapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa.
Rais Malinzi amesema washiriki wa semina hiyo ni marais, makatibu wakuu na wakuu wa mawasiliano wa wanachama 12 wa CECAFA ambao ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somali, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Naye Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wake Nicholas Musonye amemshukuru Rais wa TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji wa semina hiyo kwani itasaidia katika maendeleo ya mpira wa miguu katika ukanda huu.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA JOSEPHAT MAGAZI

April 14, 2014


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu (FRAT) Mkoa wa Singida, Josephat Magazi kilichotokea jana mkoani Kilimanjaro.
Magazi ambaye pia aliwahi kuwa mwamuzi na kamishna wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) alikuwa amelazwa katika Hospitali ya KCMC. Mazishi yatafanyika kesho (Aprili 15 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwao Ushirombo mkoani Shinyanga.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Magazi alishirikiana na TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu katika masuala ya uamuzi na uongozi, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Magazi, FRAT na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SHIREFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

*WATUMISHI WA SERIKALI NA MASHIRIKA YA UMMA WAFANYA TAMASHA LA MICHEZO KUADHIMISHA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

April 14, 2014

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo na Burudani kuelekea maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bw. Leonard Thadeo wakwanza kulia akiongoza tamasha la mazoezi ya viungo kwa Watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma mapema wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Tamasha hilo ni muendelezo wa program mbalimbali za kuadhimisha Muungano kwa njia ya Mchezo na Burudani.
 Baadhi ya watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma wakiwa katika tamasha la michezo katika kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara ya Habara, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Barnabas Ndunguru(kushoto) na Afisa Tawala wa Wizara hiyo Bw. Mussa Varisanga wakifanya mazoezi wakatio wqa Tamasha la mchezo kwa ajili ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika mapema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mtumishi kutoka Wizara ya Ulinzi Bw. Abdul Nyumba akiwaongoza watumishi wenzake katika mazoezi ya viungo mapema mwishoni mwa wiki wakati wa Tamasha la Michezo kwa ajili ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo na Burudani kuelekea maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bw. Leonard Thadeo akizungumza na watumishi kutoka wizara mbalimbali na mashirika ya Umma walioshiki tamasha la michezo kwa ajili ya kuadhimisha Muungano mapema wikiendi hii. Picha na Frank Shija.
*CHEKI JINSI SIMBA ALIVYOMUUA MAMA WA NYANI NA KUMLEA MTOTO WA NYANI, NYANI MTOTO AJARIBU 'KUESKEP' LAKINI...!!!!!!!!!!!

*CHEKI JINSI SIMBA ALIVYOMUUA MAMA WA NYANI NA KUMLEA MTOTO WA NYANI, NYANI MTOTO AJARIBU 'KUESKEP' LAKINI...!!!!!!!!!!!

April 14, 2014


Simba akiwa amembeba nyani baada ya kumuua, huku mtoto wa nyani akiwa amemkumbatia mama yake bado.
**********************************************************
Mpiga picha Evan Schiller na Lisa Holzwarth wametumia muda wao wa kutosha tu kuchukua picha za tukio la kusisimua na kusikitisha huko Botswana baada ya kushuhudia nyani mwenye mtoto akikumbana na hasira za simba jike mwenye njaa ambaye alimfukuza na hatimaye kumkamata na kumuua.

Nyani huyo aliuawa huku mtoto wake mchanga akiwa amemkumbatia pasipokujua kuwa mama yake tayari alikuwa ameshakufa. baada ya simba kuua nyani huyo sasa kibao alikigeuzia kwa mtoto ambapo aliaanza kumtisha pamoja na mtoto huyo wa nyani kutaka kukimbia simba alimkamata tena. chanzo tabianchi

Baadae mtoto wa nyani alianza kucheza na simba na kumfanya kama mamayake. Tazama picha uone tukio kamili hatua kwa hatua.

Muda mfupi, mtoto wa nyani alitaka kutoroka lakini alishindwa kupanda mti, sasa simba akamfuata kuona nini kinaendelea.
Lakini cha ajabu badala ya simba kumuua mtoto huyo wa nyani alianza kucheza naye na kukafanya kanyani kasahau machungu.
Hapa sijui nyani mtoto anawaza nini, weee usicheze na simba jamani.
Wacha weee, sasa hapa simba sijui ndo kamsamehe kweli huyu nyani au ndo amemuweka kiporo njaa ikiuma amtafune, lakini mtoto wa nyani anaonekana kuenjoy tu.
Nyani mtoto kashapagawa na joto la simba, anaanza kutafuta kunyonya kifuani kwa simba, ana hatari huyu mtoto.
Raha iliyochanganyikana na hofu, hatari tupu....
Wasije simba wengine! simba jike akaanza kuwatimua sasa sijui alikuwa anakalinda katoto ka nyani kasiliwe au aliona wenzake watammalizie msosi wake wa baadae.
Stori hii ni ya kufurahisha, huzunisha na kushangaza na inaonyesha ni kwa kiasi gani kila jambo limepangwa kwa maksudi yake na kwamba hata tukiwa katika magumu ya hali gani ukombozi unaweza kupatikana kikubwa tu ni kujiamini kama mtoto wa nyani alivyofanya.
Haa! kumbe baba nyani alikuwa kando akifuatilia issue yote na wakati simba wanazinguana akapata upenyo wa kumuokoa mwanaye na kupanda nae kwenye mti, uuuh kweli kama siku yako haijafika unaweza hata kumkamua maziwa simba na akabaki kukuchekea tu. Habari Picha kwa hisani ya tabianchi blog

MASAA 14 YA SAFARI YA KINANA ZIWA TANGANYIKA

April 14, 2014


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka mkoa wa Kigoma kuelekea Karema mkoani Katavi kwa siku nne.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Sigunga wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipowasili kijijini hapo kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiondoka kijijini Sigunga baada ya  kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi anayepiga kasia na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembea kwenye mitaa ya kijiji cha Mgombo  Kata ya Buhingu wakati aliposimama kuwasalimia wanakijiji hao,Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kijiji cha Buhingu.
 Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwapungia mkono wakazi wa Karema mara baada ya kuwasili katika bandari ya Karema mkoani Katavi.
Umati wa watu uliofika kumlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake walipowasili Karema mkoani Katavi

KWA MARA YA KWANZA AZAM FC MABINGWA WAPYA LIGI KUU BARA 2014 TANGU 1965

April 14, 2014


 Wachezaji wa Azam Fc, wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya city katika mchezo wao wa Ligi Kuu uliochezwa jana Jijini Mbeya na kutangaza ubingwa rasmi kwa kufikisha jumla ya Pointi 59 wakiwaacha Yanga ambao nao pia waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Orjolo walicheza jana jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi 55 huku wakiwa wamesalia na mchezo mmoja dhidi yao na Simba utakaochezwa Aprili 19, ambao hata wakishinda hawataweza kufikia pointi za wapinzani wao katika mbio hizo Azam, ambao nao pia wamesalia na mchezo mmoja ambao hata wakishinda au kushinda hauna faida wala hasara kwao.
BAADA ya Azam kufanikiwa kutwaa taji la ubingwa jana jijini Mbeya kwa kuwalaza wenyeji wao Mbeya City, imeweka rekodi ya kuwa klabu ya tisa kunyakua taji hilo nchini tangu mwaka 1965.

Azam imetwaa ubingwa huo ikiwa na jumla ya Pointi 59 ikiwa imecheza michezo 25, huku wapinzani wao katika mbio hizo, Yanga wakibaki nafasi ya pili baada kuwabamiza Oljoro JKT mabao 2-1 katika mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh AMri Abeid jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi 55.

Azam waliweza kushika nafasi ya pili misimu miwili mfululizo nyuma ya Simba na Yanga, ambapo msimu huu wameonyesha uchu wa kuitamani na kumudu kuiwania vyema nafasi ya kwanza na hatimaye kufanikiwa.

Ukiondoa Yanga na Simba walionyakua mataji mara nyingi, Azam itaingia kwenye orodha ya walionyakua ubingwa huo ikifuata nyayo za Cosmopolitan iliyofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1967.

Baada ya Cosmo waliofuata walikuwa ni Mseto ya Morogoro waliofanya hivyo mwaka 1975, kisha Pan Africans iliyoweka rekodi mwaka 1982, ikafuatiwa na Tukuyu Stars iliyonyakua mwaka 1986 na kufuatiwa na Wagosi wa Kaya, Coastal Union mwaka 1988.

Klabu ya Mtibwa Sugar ilikuja kuweka rekodi ya kunyakua taji hilo la Ligi Kuu misimu miwili mfululizo mwaka 1999 na 2000 kabla ya Simba na Yanga kupokezana taji hilo tangu hapo hadi msimu huu ambapo inaelekea wazi Azam wanaingia kwenye orodha hiyo.


 Azam imeweka rekodi hiyo ya kuwa timu ya tisa kunyakua taji hilo na kuisimamisha Yanga iliyoshikilia taji hilo la 24, ikiongoza orodha ya klabu zilizonyakua mara nyingi ikifuatiwa na Simba iliyotwaa mara 18.

ORODHA KAMILI YA MABINGWA WA LIGI KUU TANGU 1965-
    1965 Sunderland (Simba)
    1966 Sunderland
    1967 Cosmopolitan
    1968 Yanga
    1969 Yanga
    1970 Yanga
    1971 Yanga
    1972 Yanga
    1973 Simba 
    1974 Yanga
    1975 Mseto 
    1976 Simba 
    1977 Simba 
    1978 Simba 
    1979 Simba 
    1980 Simba 
    1981 Yanga
    1982 Pan Africans
    1983 Yanga
    1984 Simba 
    1985 Yanga
    1986 Tukuyu Stars
    1987 Yanga
    1988 Coastal Union
    1989 Yanga
    1990 Simba 
    1991 Yanga
    1992 Yanga
    1993 Yanga
    1994 Simba 
    1995 Simba 
    1996 Yanga
    1997 Yanga
    1998 Yanga
    1999 Mtibwa Sugar
    2000 Mtibwa Sugar
    2001 Simba 
    2002 Yanga
    2003 Simba 
    2004 Simba 
    2005 Yanga
    2006 Yanga
    2007 Simba 
    2007/08 Yanga
    2000-09 Yanga
    2009-10 Simba SC
    2010-11 Yanga
    2011-12 Simba SC
    2012-13 Yanga 
    2013-14 Azam Fc

DC GAMBO AHIMIZA UJENZI WA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA KATA KWA WANANCHI.

April 14, 2014
Na Mashaka Mhando,Korogwe
MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo amehimiza wananchi wilayani humo, kuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za kata unaoendelea wilayani humo ili kuwawezesha watoto waweze kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo na kupata elimu sahihi.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Makuyuni wakati alipotembelea ujenzi wa smaabara ya shule ya sekondari Madago iliyopo katika kata hiyo, Gambo alisisitiza kwamba katika mpango huo wa ujenzi wa maabara wananchi wote wanawajibu wa kushiriki kikamilifu kwa kutoa michango ili kufanikisha ujenzi katika kipindi kilichopangwa.

Alisema mpango huo wa ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari ni agizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye leo atakuwa wilayani hapa, hivyo wananchi wanatakiwa kulitekeleza ili kusaidia kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu na kuwawezesha watoto wanasoma na kupenda masomo ya sayansi.

“Ndugu zangu wananchi napenda mwelewe kwamba hili ni agizo la Rais na hizi maabara sitosoma mimi wala kiongozi yeyote hapa ila watoto wetu ndiyo watakaonufaika nazo, hivyo ni vyema mkashiriki kikamilifu katika ujenzi huu,” alisema Gambo.

Hata hivyo, Gambo aliwapongeza wananchi wa kata hiyo pamoja na Mtendaji wa Kata Bonifasi Siruri kwa jitihada walizozifanya kuhakikisha maabara ya shule yao ya Madago imefikia katika hatua nzuri ya kuezekwa bati tofauti na maeneo mengine katika wilaya hiyo.

Awali Mtendaji huyo akimsomea taarifa hiyo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa hadi kufikia hatua hiyo wananchi tayari wametumia kiasi cha sh. 60,670,000 ambapo wamejenga kwa nguvu zao na kufikia hatua ya kumalizia chumba kimoja kati ya vitatu vilivyopo kupiga bati.

Siruri ambaye ni kati ya watendaji wachache wilayani humo wanaojituma kusimamia na kumaliza miradi kwa wakati, alisema maabara hiyo hadi itakapomalizika itatumia kiasi cha sh. 133,070,960 ambapo hata hivyo, sasa aliiomba serikali iisaidie maabara hiyo.
MWISHO

DC DENDEGO ASIKITISHWA NA BAADHI YA WAZAZI KUWAOZA MABINTI ZAO WALIOPO MASHULENI.

April 14, 2014
(mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego wa kwanza kushoto akisikiliza maelekezo toka kwa mwanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari st.Christina wakati alipotembelea chumba cha maabara ya sayansi shuleni hapo kwenye mahafali
Salim Mohammed,TANGA
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego amesikitishwa na baadhi ya wazazi kuwaoza mabinti zao wakati wako katika masomo na kutoa ovyo kuwa mtu yoyote atakaebainika kumuachisha masomo mtoto wake atapambana na sheria.



Ameyasema hayo  wakati wa mahafali ya 12 shule ya sekondari ya St Christina iliyoko Kange Maziwa mjini hapa na kusema kuwa tabia ya wazazi kuwapa waume mabinti zao wakati wakiwa shuleni inasikitisha na hivyo ofisi yake kuadhimia kuikomesha.



Alisema kitendo hicho kinawanyima mabinti hao haki ya kupata elimu na kuweza kumkomboa mwanamke katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii hasa kwa wakati uliopo  sasa wa sayansi na teknolojia ulimwenguni.


“Kupitia mahafali haya ya 12 ya shule hii ya St Christina  tukiwa na  mama na wababa wetu natoa wito kukomeshwa watoto wetu wa kike kupewa waume wakati wanasoma----hili binafsi nitalivalia njuga kuhakikisha halitendeki” aliongeza na kusema


“Nadhani hao wazazi wenye tabia hii kwa kweli  wako na jambo kama sio maslahi ni shida za papo kwa papo---sera ya mwanamke kuongoza na kuweza bila kuwezeshwa haijawafika baadhi ya wazazi na hivyo nawataka kuelimika” alisema Dendego


Alisema ofisi yake haitomvumilia mzazi wala mlezi yoyote atakaebainika kumuoza binti yake wakati yuko katika masomo na hivyo atahakikisha tabia hiyo inakomeshwa ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuweza kuleta mapinduzi ya ukombozi wa wanawake katika kujiletea maendeleo.


Akizungumzia wazazi kuwabidiisha watoto wao katika elimu, Dendego aliwataka kuwa na ada ya kuwafuatilia maendeleo yao shuleni na kuacha kuwaruhusu kushiriki katika shughuli ambazo zinaweza kumtoa kimawazo katika masomo yake.


Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumia vibaya watoto vipindi vya likizo kwa kuwapa kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao pamoja na kuwashirikisha katika biashara na kusahau kuwa vipindi hivyo ni vya maandalizi ya kujiandaa na masomo yalioko mbeleni kwao.


“Ni jambo la kushangaza kuona vipindi vya likizo kwa wanafunzi wazazi wanafurahia kama wamepata kitu kizuri---kumbe furaha yao ni kuwatumikisha katika kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao na kusahau kuwa nihatari” alisema Dendego


Alisema ili kuwawezesha watoto kufanya vizuri vipindi vyote vya masomo yao ni jukumu la wazazi kuwabidiisha katika masomo vipindi vya likizo ili karo wanazolipa faida yake iweze kuonekana na kuacha kuzilaumu shule kuwa hazisomeshi.

                                            
   Mwisho