Taarifa kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa Magari kutoka Tanzania kuingia mbugani, viwanja vya ndege

Taarifa kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa Magari kutoka Tanzania kuingia mbugani, viwanja vya ndege

February 06, 2015

safari2-2
Mvutano katika ishu ya utalii  imeendelea kuingia kwenye headlines kubwa leo, vyombo vya habari Kenya vimeripoti ishu ya Serikali ya Kenya kupiga marufuku magari ya kitalii kutoka Tanzania kuingiza watalii katika mbuga za wanyama na viwanja vya ndege vya nchi hiyo.
Waziri wa Masuala ya Jumuia ya Afrika na Utalii nchini humo, Phyllis Kandie ametangaza kutekelezwa kwa hatua hiyo mara moja  hadi pale mzozo uliyopo kati ya nchi hizi mbili juu ya masuala ya utalii utakapomalizika.
.
Phyllis Kandie
Waziri huyo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mataifa haya mawili kushindwa kufanya kikao maalum kama ilivyotegemewa baada ya muda wa wiki tatu uliokuwa umepangwa kuisha.
024-lioness 
Kwa sasa magari ya watalii nchini Tanzania yataruhusiwa kuingia nchin i humo lakini yanatakiwa yawe na leseni, ingawa Kenya imeruhusu magari ya watalii kuingia maeneo yote nchini humo, kwa upande wa Tanzania imeruhusu magari ya kitalii kutoka Kenya kuingia katika mikoa ya Tanga, Moshi, Arusha na Musoma.
Sikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K 24 kutoka Kenya.

MAJAJI BONGO KUPIGWA RISASI, RIPOTI KAMILI HII HAPA!

February 06, 2015

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam. ENDAPO ulinzi binafsi na wa kazini hautaimarishwa kwa majaji, uwezekano ni mkubwa wa watu wabaya kuwavamia ofisini na kuwapiga risasi kwa sababu ya hukumu zao za kunyonga au kufunga watu jela maisha, Risasi Jumamosi limebaini.
Hilo limekuja kufuatia chanzo kimoja toka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kupiga simu kwenye Ofisi za Magazeti Pendwa ya Global Publishers na kusema anasikitika kuona majaji, licha ya kutoa hukumu nzito zinazowaumiza watu lakini hawana ulinzi wa maisha yao.




Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu Tanzania. MSIKIE HUYU
“Jamani naamini hapo ndo Global?”
Risasi Jumamosi: “Ni sahihi kabisa, tunaweza kukusaidia?”
Chanzo: “Jamani ni hivi, mnawajua majaji wetu hapa mahakama kuu. Wanahukumu watu kunyongwa, wanafunga watu maisha, lakini pamoja na mambo yote hayo makubwa hawana ulinzi.”



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Mhe Winfrida Beatrice Korosss kuwa Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania katika sherehe zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aqgosti 15, 2014 KUMFIKIA JAJI RAHISI TU
“Utakuta jaji yupo ndani ya ofisi yake lakini hana ulinzi wowote. Mtu mbaya anaweza kuingia kuanzia chini mpaka ofisini akamfanya lolote.
“Nadhani serikali ingetafuta njia ya kuwalinda hawa watu. Kazi yao ni ya hatari sana na inagusa jamii moja kwa moja.”

WASIWASI ULIOPO
“Unajua, kumfunga mtu maisha jela au kumhukumu kunyongwa ni hatari sana. Utakuta mtu ana familia inamtegemea, sasa unadhani familia anayoiacha itafurahi kumwona jaji aliyeharibu maisha yao? Wasiwasi wangu ipo siku tutasikia jambo kubwa sana.”
Risasi Jumamosi: “Tumekusikia, hilo tutalifanyia kazi ndani ya siku moja tu. Tutaona kama madai yako ni ya kweli au la!”
Chanzo: “Nyiye chunguzeni tu mtajua ni kweli.”

OFM YAINGIA KAZINI
Baada ya kupewa taarifa hizo, Makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ wa Global walijipanga kwenda mahakama kuu wakiwa na bastola mfukoni ili kuona kama kweli raia yeyote anaweza kupita kuanzia lango kuu hadi kupanda ghorofa ya kwanza ambako majaji wana ofisi bila kukutana na ulinzi wa upekuzi!

Kamanda mkuu wa OFM akiwa na wasaidizi wake, wiki iliyopita walifika mahakamani hapo akiwa na bastola hiyo na kuzama ndani bila kukutana na kizuizi chochote kinachoweza kubaini (detector) kuwa mtu anayeingia ana silaha.

OFM MLANGONI KWA JAJI
Kama vile haitoshi, kamanda wa OFM bado akiwa na bastola kwenye mfuko wa suruali alipandisha ngazi hadi ghorofa ya kwanza na kutembea kwa kujidai kwenye korido yenye milango ya vyumba vya majaji.Kuna wakati, kamanda huyo alisimama kwa muda kwenye mlango wa jaji mmoja (jina tunalo) na kuchomoa bastola kisha akairudisha tena mfukoni, hakuna mlinzi aliyejitokeza wala mtu wa kuuliza kamanda alikuwa akifanya nini katika eneo hilo! Ni hatari sana!

DAKIKA KUMI
Mpaka dakika kumi zinakatika, kamanda wa OFM huku akipigwa picha mbalimbali na fotografa wake, hakuna mtu aliyeonekana kuhusika na masuala ya ulinzi.

TAFSIRI RAHISI
Kwa maana hiyo, kama kamanda angekuwa ndiye adui wa mmoja wa majaji, angeweza kusukuma mlango na kuzama ndani kisha kufanya lolote akiwa na silaha yake hiyo. Majaji wafikiriwe upya!

MSEMAJI WA MAHAKAMA AONGEA
Baada ya kamanda wa OFM kuondoka eneo la mahakama, siku iliyofuata, Risasi Jumamosi, lilimtafuta Kaimu Msemaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Mary Gwela ambapo alisema:
“Kwanza ni kweli majaji wanastahili kuwa na ulinzi wa kutoka ofisini hadi nyumbani na nyumbani hadi ofisini.

“Lakini hali hii imetokana na ukweli kwamba, askari ni wachache. Hata Kova (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam) alisema askari ni wachache.
“Hata hivyo, majaji wanapokwenda kikazi mikoani ndiyo wanaondoka na ulinzi wa askari. Majaji ni uteuzi wa rais, kwa hiyo kisheria walitakiwa wawe na ulinzi.

“Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, majaji waliopo mikoani wote wana ulinzi kwa hiyo wako salama.”
Baada ya maelezo hayo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-rose Mtengeti Migiro ambapo hakuwa hewani.

Kwa upande wake, Kamanda Kova ambaye ilidaiwa aliwahi kutamka kuwa askari ni wachache, hakuwa hewani ambapo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

MEZANI KWA MHARIRI
Ni vizuri serikali ikaliangalia hilo ili kuweza kuwapa ulinzi majaji wetu kwani kazi wanayoifanya ni ya hatari. Kumfunga maisha au kumhukumu kunyongwa mtu aliyekutwa na hatia si jambo dogo katika jamii.
CHANZO:BLOG YA WANANCHI

ZIMAMOTO WA JIJI LA LINZ, AUSTRIA WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

February 06, 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi akiongoza kikao wakati Viongozi wa Kikosi cha Zimamoto toka Jiji la Linz, Austria walipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji la Linz, Austria Christian Puchner, akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi mojawapo ya kofia za zimamoto zilizotolewa kama msaada kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Tanzania. Kushoto ni Diwani wa Jiji la Linz Bwana Deltef Wimmer.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi akijaribisha mojawapo ya kofia za zimamoto zilizotolewa na Jeshi la Zimamoto la Jiji la Linz, Austria kama msaada kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kikosi cha Zimamoto toka Linz, Austria waliotembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi akiagana na Diwani wa Jiji la Linz, Austria, Deltef Wimmer, baada ya ujumbe wa Kikosi cha Zimamoto cha Jiji la Linz kumaliza ziara yao katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Bwana Wimmer alikuwa kiongozi wa ujumbe huo.
Ujumbe wa Kikosi cha Zimamoto toka Jiji la Linz, Austria, wakifurahia mazingira ya Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kumaliza ziara yao wizarani hapo.

DKT JOHN POMBE MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI SINGIDA

February 06, 2015

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya  km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Mradi huu utakapokamilika na kupokelewa na Serikali Mkandarasi atakaa site miaka mitatu kwa ajili ya uangalizi na kufanya marekebisho yoyote yatakayojitokeza kwa gharama zake mwenyewe.
 . Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya  km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii imekamilika kujengwa kwa asilimia 97.
 Sehemu unapojengwa mzani utakaotumika kupimia magari makubwa yatakayopita kwenye barabara hiyo.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itigi waliofika kumpokea kabla ya kuwahutubia wananchi kuhusu maendeleo ya mradi huo wa barabara.
 Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya (km 89.3) katika eneo la Itigi kama unavyoonekana.
 Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Patrick Mfugale akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara Manyoni-Itigi-Chaya (km 89.3) inayotarajia kukamilika hivi karibuni.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo
 Waziri wa Ujenzi akiagana na baadhi ya  Wanafunzi wa shule ya Sekondari Itigi mara baada ya kuhutubia mkutano huo uliofanyika Itigi mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kushoto  akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Patrick Mfugale katikati kuhusu mradi wa ujenzi huo wa barabara
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoa maelezo kwa watendaji wa Wizara ya Ujenzi pamoja na TANROADS kabla ya kuanza kukagua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya  kilometa 89.3.
BALOZI WA RWANDA AONANA NA DR.K SHEIN ZANZIBAR

BALOZI WA RWANDA AONANA NA DR.K SHEIN ZANZIBAR

February 06, 2015
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Eugene S.Kayihura alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo Picha na Ikulu.] BALO2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akibadilishana mawazo na  Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Eugene S.Kayihura (katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar (kushoto) Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi wa Mohamed Ramia Abdiwawa.  Picha na Ikulu.]
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

February 06, 2015

“BELLE 9, PHD, IZZO B KUTUMBUIZA TANGA USIKU WA WAPENDANAO”

February 06, 2015
WASANII nguli wa mziki wa Bongo Fleva hapa nchini Belle 9,Hemed Phd na Izzo Business wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la Red &White Party kwa wapendanao .
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika February 14 mwaka huu kwenye ukumbi wa Club Lacasa Chika kuanzia saa saa tatu usiku mpaka majogoo ambapo wasanii hao watasindikiwa na wasanii wengine kutoka mkoani hapa.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG, Mratibu wa Onyesho hilo,Mbwana Imamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni  ya Arbarb Intertainment alisema kuwa maandalizi yake yamekamilika kwa asilimia kubwa na wasanii watakaotumbwiza watawasili mkoani hapa siku moja kabla.

 

 Mbwana alisema kuwa lengo kubwa la onyesho hilo ni kuwapa burudani wakazi wa Tanga hasa kwenye siku hiyo maalumu ya wapendanao ambayo huazimishwa kila mwaka hapa nchini.
   “Napenda kuwataka wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi
kwenye onyesho hilo maana litakuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayofanyika “Alisema Mratibu huyo.

 
 Aidha aliwataja wasanii wa mkoani Tanga watakaosindikiza onyesho hilo kuwa ni Man Sasha, Kidani, Meratha, Voicer na Fat Zinga ambao watauwasha moto kwenye ukumbi huo siku hiyo.

KAMATI YA NIDHAMU YAWAADHIBU NYOSO, MORRIS

February 06, 2015


 

  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanyawakiwa uwanjani.

Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

 Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhimchezaji Maguri kwa kitendo hicho.

 Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wamtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.

 
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea mgongano huo.

Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.

 
Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na kumpa onyo kali.

 Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000 Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

 Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.
 
Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza upande wa walalamikaji pekee.

 Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa kumchezea ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya mlalamikiwa kupata udhuru uliosababisha asiwepo.

 Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa, kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.

Airtel yashirikiana na Kitengo cha damu salama cha taifa kuokoa maisha

February 06, 2015

Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Daudi Mkawa akimtoa damu Mfanyakazi wa Airtel Tanzania, Amitin Mbamba wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Adam Suleiman na Frank Munale wakitolewa damu kwa ajili ya kuchangia katika Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Judith Goshashy akimpima shinikizo la damu Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Mnasihi wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Julius Nkomwa akimtoa damu Mkurugenzi wa Fedha wa Airtel Tanzania, Ketan Mehta wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.

Airtel Tanzania imeshirikiana na Kitengo cha damu salama cha taifa (National Blood Transfusion Services) katika zoezi la kuchagia damu ili kupunguza upungufu mkubwa nchini ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwaajilii ya dharura za kitabibu kila mwaka.

Zoezi hilo la kuchangia damu limewashirikisha wafanyakazi wa Airtel kutoka katika vitengo mbalimbali kujitolea na kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia jamii.

Akiongea kwa niaba ya Airtel , Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema “ Airtel tunaamini katika kugusa maisha ya watanzania kwa njia mbali mbali huku tukishirikiana na wafanyakazi na wadau mbali mbali katika kufanikisha hilo. Tumekuwa tukishirikiana na Kitengo cha kuchagia damu kila mwaka kwa kuhusisha wafanyakazi na wadau mbali mbali kuchangia ili kuongeza damu katika benki ya damu ya taifa kwa ajili ya mahitaji ya dharura. Mwaka huu tunaendeleza utamaduni huu ili kuwawezesha matibabu hususani kwa wanawake na watoto wanaohitaji msaada wa damu kupata huduma hii kwa urahisi.

Tunawashukuru wafanyakazi na wadau wetu mbalimbali kwa kujitolea na kushiriki katika kuchangia kila mwaka na pia tunaahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii na wafanyakazi wetu juu ya umuhumi wa kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo tunaweza kuokoa maisha ya wengi wanaohitaji huduma hii kuipata kwa haraka na urahisi.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka kitengo cha damu salam Judith Charles alisema” Tunawashukuru wafanyakazi wa Airtel kwa kuonyesha mfano kwa kujitokeza kuchangia damu leo, Natoa wito kwa watanzania kujenga tabia ya kujitolea kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo kutatuwezesha kuwa na units za kutosha kuhudumia wale wanaohitaji wakati wa dharura. Maisha hayana uhakika inawezekana siku moja wewe ukawa ni mmoja kati ya wale wanaohitaji, hivyo tunahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia damu.

Mpaka sasa kitengo chetu kina tatizo la uhaba mkubwa wa damu hivyo natoa wito kwa watanzania mmoja mmoja au kwa makundi kujitokeza kuchangia ili tuwe na kiwango cha damu kinachokidhi mahitaji yanayokua kwa kasi kila siku.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMFARIJI JAJI MSTAAFU AGOSTINO RAMADHANI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMFARIJI JAJI MSTAAFU AGOSTINO RAMADHANI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

February 06, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Jaji Mkuu mstaafu Agostino  leo alipomtembelea nyumbani kwake kimara leo Februar 06, 2015 kwa ajili ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi. ja2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha kumbukukmbu kufuatia kifo cha mama mzazi wa Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015 alipofika kwa ajili ya kumfariji. ja3 
Maka wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwafariji wana familia ya Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015,  kutokana na kufiwa na mama yake mzazi. ja4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani Baada ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015. (Picha na OMR)