RAIS DK MAGUFULI AMTEUA SIMON SIRRO KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI NCHINI

May 28, 2017


Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli leo tarehe Mei 28, 2017 amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Habari, Ikulu jijini Dar es Salaam, Gerson Msigwa  imesema, Sirro anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyi atapangiwa kazi nyingine.

Katika taarifa hiyo ambayo Kururugenzi ya Mawasilino ya Rais Ikulu, ameipokea  kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu Mei 29, 2017 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WA KITETO WAENDELEA KUJIUNGA NA MFUKO WA PPF

May 28, 2017



Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera (wa pili kulia) akikabidhiwa vifaa tiba na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele (wa pili kushoto) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kiteto katika hafla iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita. PICHA NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG- KITETO.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akitoa maelezo mafupi kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa PPF katika hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba toka Mfuko wa PPF kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Manyara.

Mkuu wa wilaya Kiteto, Manyara, Bw. Tumaini Magesa akitoa shukrani zake za pekee kwa Mfuko wa PPF jinsi ilivyoweza kuwakomboa wananchi wa wilaya yake kwa kuwapatia vifaa tiba.

Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw. Jacob Sulle akiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya ya Kiteto, Manyara ili waendelee kujiunga na Mfuko wa PPF.

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele akitoa maelezo mafupi wakati wa ugawaji wa vifaa tiba vilivyotolewa na PPF katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

NHIF YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA KWA KUTOA ELIMU YA MFUKO NA KUPIMA AFYA

May 28, 2017
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kulia akiteta jambo na  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia wakati alpolitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye  viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Wananchi wakipima presha kwenye banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo

Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia kushoto akisubiri kujeza fomu za wananchi ambao wanakwenda kupima uzito na afya kwenye Banda lao ambapo wanatoa elimu namna ya kujiunga na mfuko huo,kupima afya

MWANZA WATAKA VIWANDA VYA PEDI ZA KISASA

May 28, 2017
Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2017, kimkoa Mwanza yakifanyika uwanja wa Nyamagana hii leo Mei 28,2017.

#BMGHabari
Wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali Jijini Mwanza wameiomba serikali kusaidia ujenzi wa viwanda vya pedi za kisasa vitakavyosaidia pedi hizo kuuzwa kwa beo nafuu.

Hayo yamesemwa kwenye risala yao iliyosomwa na mwanafunzi Edna Ignas kutoka shule ya msingi Malulu, kwenye maadhimisho ya Siku ya hedhi duniani yaliyofanyika jana katika uwanja wa mpira Nyamagana.

Aidha wameomba ujenzi wa viwanda hivyo vya pedi uendani na kupunguza ama kuondoa kabisa kodi kwenye mauzo ya kodi hizo, hatua ambayo itasaidia kuuzwa kwa bei nafuu na hivyo kuwafikia wasichana wote hususani wanaotoka kwenye kaya zenye uwezo mdogo wa kiuchumi.

Mkurugenzi wa Shirika la Tanzania Youth With New Hope in Life Organization (TAYONEHO) la Jijini Mwanza, Dkt.Iman Tinda, amesema suala la hedhi limekuwa na changamoto kubwa ikiwemo baadhi ya mabinti wanafunzi kukosa masomo wakati wa hedhi.

Amesema mabinti hupoteza vipindi darasani kati ya siku mbili hadi saba kwa mwezi, siku 86 kwa mwaka na hivyo kuwa kikwazo kwao kimasomo ambapo ni vyema wadau wa elimu wakaungana pamoja ili kuvunja ukimya juu ya suala la hedhi na hivyo kuwasaidia mabinti kuondokana na changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi hicho.

Naye Mratibu wa Shirika la Plan International mkoani Mwanza, Emmanuel Asaph, amebainisha kwamba elimu ya hedhi tayari imewafikia wanafunzi 250 kutoka shule 10 za msingi Jijini Mwanza pamoja na waalimu wa kike na kiume 20 ambao wamefunzwa namna bora ya kuwa msaada wa kwanza kwa mabinti watakaokumbana na changamoto za hedhi wawapo shuleni.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan, amesema halmashauri zote mkoani Mwanza kwa kushiriakana na kamati za shule zinafanya juhudi za kuhakikisha mazingira yanakuwa salama ikiwemo upatikanaji wa maji safi ili kuwasaidia mabinti kujiweka nadhifu pindi wawapo kwenye hedhi.

Maadhimisho hayo mkoani Mwanza yameratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la TAYONEHO la Jijini Mwanza kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la Plan International pamoja na lile la SVC Mwanza.

Lengo ni uvunja ukimya juu ya masuala ya hedhi ikiwemo kuondokana na dhana potofu kwamba hedhi ni ugonjwa pamoja na namna bora ya kuhakikisha mtoto wa kike anajiweka katika hali ya usafi ili abaki shuleni badala ya kukosa masoko kila apatapo hedhi.

Siku ya hedhi duniani ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014 baada ya kuidhinishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo ni mara ya kwanza kuadhimishwa mwaka huu 2017 nchini Tanzania ikiwa na kauli mbiu isemayo "Elimu juu ya hedhi hubadili kila kitu".
Mkurugenzi wa Shirika la TAYONEHO, Dkt.Iman Tinda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwanafunzi Edna Ignas kutoka shule ya Msingi Malulu Jijini Mwanza, akisoma Risala kwa niaba ya wnafunzi wenzake kwenye maadhimisho hayo
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Tazama Video hapo chini

Utamaduni wa Tanzania Saudi Arabia

May 28, 2017
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.

Tanzania yatumia Siku ya Afrika Saudi Arabia kutangaza utamaduni wake

Na Mwandishi Wetu, Riyadh
Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.


Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.

Wanafunzi wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.

TADB YAASWA KUWAFIKIA WAKULIMA WADOGO NCHI NZIMA

May 28, 2017

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akikaribishwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) mara baada ya kufungua Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Mei had Juni 01.

Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Mhe. Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.

“Nawaomba mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole Nasha alisema.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.

“Naomba muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi  Bilioni 200 ili kuwaongezea tija katika shughuli zao,” aliongeza.

Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.

Mpango kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.

TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto) akizungumza wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) alipotembelea Banda la TADB.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akizungumza na maafisa wa TADB (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Benki hiyo kuwafikia wakulima wote nchini.
Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (wapili kulia) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) wakati alipotembelea Banda la TADB.
Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) akifafanua hoja mbali mbali kuhusiana na mikopo inayotolewa na Benki hiyo.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) mpango wa TADB kuwafikia wakulima nchi nzima.
WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

May 28, 2017
bumb1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar Es Salaam leo,  akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Tarehe 5 Juni, ambapo Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoani Mara kijijini Butiama kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Pamoja na Mambo Mengine pia alikuwa Mwanaharakati wa Mazingira. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Mwandisi Ngosi Mwihava.
bumb2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari ( Hawapo Pichani) katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar Es Salaam leo,  akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Tarehe 5 Juni, ambapo Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoani Mara kijijini Butiama kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Pamoja na Mambo Mengine pia alikuwa Mwanahakati wa Mazingira. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Professor Faustin Kamuzora na kulia ni Naibu katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mwandisi Ngosi Mwihava. ( Picha na Evelyn Mkokoi OMR)
RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

May 28, 2017
MUL1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
MUL2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu
MUL3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei.
MUL4 MUL5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimtakia heri mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mama yake Mwanahabibi Mohamed Mtei.
MUL6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
MUL7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
MUL8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya
MUL9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini