CCM TANGA YADHAMIRIA KUSHINDA VITI VYOTE VYA UDIWANI

CCM TANGA YADHAMIRIA KUSHINDA VITI VYOTE VYA UDIWANI

March 13, 2024

Ndugu Selemani Sankwa – Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga.

………………… 

Na: Mwandishi wetu, Tanga.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga kimedhamiria kushinda viti vyote vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 20 mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Selemani Sankwa alipokuwa akitoa mwelekeo wa kampeni kwenye kata nne ndani ya mkoa wa Tanga ambapo uchaguzi utafanyika.

“CCM Mkoa wa Tanga tuna uhakika wa kushinda kata zote nne ambazo ni Mkuzi wilayani Muheza, Boma, Mtimbwani na Mayomboni zilizopo Wilaya ya Mkinga. Ninaposema tuna uhakika wa ushindi si kwamba nabahatisha au najifariji bali ushindi wetu unatokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM uliofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kata hizo tumeshuhudia ujenzi wa miradi ya Elimu, Afya, Umeme, Maji, Barabara na mingineyo.” amesema Sankwa

Mtendaji huyo Mkuu wa Chama Mkoa wa Tanga aliendelea kusisitiza kuwa “Tunajivunia kazi kubwa iliyofanywa na Viongozi wa Chama Wilaya na Mkoa chini ya Ndugu Rajabu Abdallah (MNEC) ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ya kuisimamia Serikali katika Miradi ya Maendeleo ambayo ni chachu ya kuchaguliwa kwetu.”

Vilevile, Sankwa amesema CCM inaamini katika kuwatumika wananchi kikamilifu kama siri ya ushindi wake, na ndiyo maana viongozi wa chama na serikali wamejitahidi sana kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Hatua hatua nyingine, Sankwa amesema Chama kimefanikiwa kuendesha vyema uchaguzi wa kura za maoni ambapo wagombea wamepatikana huku umoja na mshikamano wa Wanachama ukibaki imara bila makundi ya aina yeyote. “Niwasihi Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi ili kutumia haki yao ya kuchagua Viongozi bora wanaotokana na CCM.” amesema Sankwa.

Februari 15, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata 23 za Tanzania Bara ambapo Uchaguzi utafanyika Machi 20. Kata nne ndani ya Mkoa wa Tanga zitafanya Uchaguzi mdogo huku CCM ikijinadi kushinda kata zote kwa ushindi wa kishindo.

RAIS SAMIA AFUTURISHA VIONGOZI PAMOJA NA MAKUNDI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

March 13, 2024

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kuftarisha viongozi pamoja na Makundi mbalimbali ya Kijamii tarehe 12 Machi, 2024.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko akiwa kwenye Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2024.



Viongozi mbalimbali waliohudhuria Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2024.



Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka wakati wa Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2024.
Baadhi ya Waandishi wa Habari Waandamizi pamoja na Wahariri wakiwa kwenye Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wauza madafu wakati akiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kuftarisha viongozi pamoja na Makundi mbalimbali tarehe 12 Machi, 2024.

CCM YAPANIA KUIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA UDIWANI KATA YA MSANGANI

March 13, 2024

 

NA VICTOR MASANGU KIBAHA

KATIBU wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Bernard Elias Ghati amewahimiza wana ccm pamoja na wananchi kwa pamoja kumchagua kwa kishindo mgombea wa udiwani kata ya Msangani Gunze Yohana ili aweze kuwaletea wananchi maendeleo.

Katibu huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa hadhara kwa ajili ya kuweza kumnadi mgombea wa udiwani uliofanyika katika mtaa Garagaza.

Katika mkutano huo wa kampeni ambao ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ngazi ya Wilaya pamoja na ngazi ya Mkoa sambamba na wananchi wengine kutoka Jimbo la Kibaha mjini.

Katibu huyo aliwaomba katika kuelekea katika uchaguzi huo wananchama wa ccm wanapaswa kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha kwamba wanashinda kwa kishindo kwa asilimia kubwa katika uchaguzi huo.

"Kikubwa tunakuja katika mikutano hii kwa ajili ya kuzungumza mambo mbali mbali ambayo chama cha mapinduzi mambo ambayo yamefanyika katika utekelezaji wa Ilani hivyo wananchi wa Msangani inabidi kumchagua mgombea wetu Gunze '"alisema katika huyo.

Aidha katibu huyo alisema kuwa wana ccm wanatakiwa kuungana kwa pamoja na wananchi wote wa kata ya Msangani kwa lengo la kuwaeleza mambo mbali mbali yaliyofanyika ya kimaendeleo.

"Inatakiwa wana msangani wote muelewe shughuli mbali mbali za kimaendeleo ambazo zimefanywa na hivyo ninawaomba wananchi kumchagua Gunze awe diwani wa kata ya Msangani,"alisema Katibu huyo.

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa endapo wananchi wa kata ya Msangani wakimchagua Gunze kuwa diwani wa Kata ya Msangani ataweza kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo maji,afya,elimu pamoja na maeneo mengine.

Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani amnayo ilikuwa wazi unatarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu.