MAMA SALMA KIKWETE AMPOKEA MKE WA RAIS WA JAMHURI YA UJERUMANI MAMA DANIELLA SCHADT

MAMA SALMA KIKWETE AMPOKEA MKE WA RAIS WA JAMHURI YA UJERUMANI MAMA DANIELLA SCHADT

February 03, 2015

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha Ikulu Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam tarehe 3.2.2015.
2
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova kwenye viwanja vya Ikulu
3
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea salamu ya heshima mara baada ya mgeni huyo kuwasili Ikulu akiwa kwenye ziara ya kiserikali hapa nchini.
4 5
Rais Jakaya Kikwete na Mke wake Mama Salma wakiandamana na wageni wao Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Mke wake Schadt wakingia Ikulu huku mamia ya wananchi wakishangilia kwa furaha huku wakipeperusha bendera za hizo nchi mbili.
7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt   Ikulu.
8
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, wakati mgeni huyo alipowasili kwenye ofisi hizo akiambatana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
9
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Daniella Schadt wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya WAMA, Mama Hulda Kibacha (kushoto ni Blandina Nyoni (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea ofisi hiyo
10
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akiweka saini yake kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za WAMA akiambatana na mwenyeji wake Mama Salma Kikwete.
11
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi Jarida la WAMA kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt wakati alipotembelea ofisi za WAMA.
13
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Schadt zawadi ya kanga.
14
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt kwenye ofisi za WAMA tarehe
15
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt akiagana na wajumbe wa bodi ya WAMA pamoja na wafanyakazi mara baada ya kutembelea ofisi hizo
16
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Scahdt wakimwangalia mgonjwa Kundi Girogui aliyetoka wilaya ya Serengeti ambaye aliyefanyiwa upasuaji wa mdomo kwenye hospitali ya CCBRT huko Msasani.
18
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na mgeni wake Mama Daniella Schadt, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani mara baada ya viongozi hao kutembelea hospitali ya CCBRT huko Msasani

CCM TABORA YAWATUNUKU VYETI MAKADA WAKE WALIOKISAIDIA CHAMA HICHO KUPATA USHINDI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

February 03, 2015

Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akimkabidhi cheti mmoja kati ya makada wa chama hicho Bw.Emmanuel Mwakasaka waliokisaidia kupata ushindi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wilaya ya Tabora mjini ambapo CCM ilipata ushundi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akizungumza katika maadhimisho ya 38 ya kuzaliwa kwa CCM ambapo aliwataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwakuwa kimewaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu wa Taifa.
Makada mahili wa CCM mkoa wa Tabora ambao wametambulika michango yao katika kukisaidia chama kwa hali na mali na kuhakikisha chama kinaendelea kujenga heshima yake katika kuwaongoza wananchi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye ni kada wa chama hicho  Bw.Emmanuel  Mwakasaka akionesha heshima ya utii mbele ya viongozi baada ya kupokea cheti cha kumpongeza na kutambua mchango wake katika kukisaidia chama kupata ushindi uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wa mwaka 2014 ambapo CCM iliibuka mshindi dhidi ya vyama vya upinzani.
HABARI ZA MPENZI WA SUPER STAR DIAMOND PLATZNUMZ SASA NDIO HOMA YA JIJI LEO NI KUHUSU LE MBEBEZZ KUWA MJAMZITO NA UNFILTERED COMMENTS LIVE!!

HABARI ZA MPENZI WA SUPER STAR DIAMOND PLATZNUMZ SASA NDIO HOMA YA JIJI LEO NI KUHUSU LE MBEBEZZ KUWA MJAMZITO NA UNFILTERED COMMENTS LIVE!!

February 03, 2015
Mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu athibitisha kuwa ZARI ni mjamzito
Mwanamuziki maarufu nchini na sehemu nyingi za dunia – Diamond Platnumz ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mwanadada Wema Sepetu ameendelea kuuhakikishia ulimwengu kuwa,  mpenzi wake wa sasa ZARI al-maarufu kama “The boss lady”, ni mama mtarajiwa aliyebeba ujauzito wa msanii huyo nguli nchini na kwamba hii sio project nyingine.

Huku akitumia mafumbo kwenye maneno yake ambayo wataalamu wetu wa Kiswahili ndio wametufafanulia kisanifu zaidi, Diamond aliandika
 “Kileeeeeeee kinaanza kumuharibia mtu Mavazi..”
huku akiweka picha yake na mpenzi wake huyo wakitoka kwenye show ya miaka 38 ya CCM huko songea. Baada ya kukaa chini vizuri na wataalamu wetu hawa wa fasihi , walituhakikishia kuwa “Kileeeee” katika sentensi hiyo sio kitu kingine bali ni ujauzito alionao mrembo huyo na mara nyingi ukichunguza ndio kitu kinachomuharibia mwanadada au yoyote mavazi kirahisi hasa “kinapoanza” kuwa kikubwa.
Kweli tumeamini  lazima ujue tofauti ya msalaba na kujumlisha.

TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZENYE THAMANI YA SH MIL.5, SIKONGE MKOANI TABORA

February 03, 2015


Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa na Maofisa wakaguzi wa TFDA wilayani Sikonge.
Maofisa wakaguzi wa TFDA kanda ya kati wakijiandaa kuteketeza bidhaa zilizoisha mda wake ikiwemo vinywaji wilayani Sikonge (picha na Allan Ntana).

Na Allan Ntana, Sikonge

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa mbalimbali za chakula, vinywaji, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba vilivyoisha muda wake na vingine feki vyenye thamani ya zaidi ya sh mil.5 katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Akisoma taarifa ya ukaguzi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hapo juzi Afisa Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kati Sifa Chamgenzi alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia ubora na usalama wa dawa za binadamu na mifugo, uwepo wa vipodozi vilivyopigwa marufuku na bidhaa zingine zilizoisha muda wake wa matumizi. 

Alisema lengo la TFDA ni kufuatilia utekelezaji wa sheria na.1 ya mwaka 2003 ya chakula, dawa na vipodozi kwa wauzaji na wasindikaji wa vyakula na dawa na kuongeza kuwa zoezi hili lililenga kutekeleza mpango kazi wa Mamlaka hiyo wa kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa hizo kwa mtumiaji.

Ukaguzi huo uliofanyika tarehe 20-29 Januari 2015 uliongozwa na Maafisa wakaguzi wawili kutoka TFDA Kanda ya Kati Fredrick Luyangi na Sifa Chamgenzi ambao waliungana na wakaguzi wenyeji wawili toka Ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Afya na askari polisi wanne wilayani Sikonge na jumla ya majengo 118 yanayojihusisha na biashara ya chakula, vinywaji, dawa, vipodozi na vifaatiba yalikaguliwa.

Katika ukaguzi huo baadhi ya maduka yalikamatwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku vikiwa na uzito wa kilo 164.4 na thamani ya sh 1,856,000/- na katika maduka ya vyakula walikamata vyakula vilivyoisha muda wake vyenye uzito wa kilo 825.5 vikiwa na thamani ya sh 2,720,000/-

Na katika maduka ya dawa za binadamu na mifugo walikamata jumla ya kilo 37 za dawa zilizoisha mda wake na feki zenye thamani ya sh 1,200,000/-.

Aidha katika ukaguzi huo kiasi cha sh 1,580,000 kilipatikana kutokana na ada za usajili wa maduka ya biashara ya chakula ambapo 40%  ya kiasi hicho sawa na sh 632,000 inabakia katika halmashauri kwa ajili ya kufanya kazi za TFDA.

Akizungumzia mambo waliyoyabaini wakati wa ukaguzi huo, Chamgenzi alisema ukaidi na uelewa mdogo wa sheria na.1 ya mwaka 2003 wa kulipa ada na tozo husika kwa baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya chakula, dawa na vipodozi bado ni tatizo sambamba na kutotoa ushirikiano kwa Afisa wakaguzi.

Aidha uwepo wa dawa bandia (feki) zilizoondolewa sokoni, dawa na vyakula vilivyoisha muda wake, kukosekana feni za kutunzia dawa katika stoo ya kituo cha afya Kitunda, maduka ya dawa za kilimo kuuza dawa za mifugo kinyume cha sheria, utunzaji mbovu na mlundikano wa dawa zilizoisha muda wake, viwanda na mashine za unga kuwa katika makazi ya watu ni miongoni mwa yaliyobainika.

Wakaguzi hao pia hawakuridhishwa na hali ya machinjio ya halmashauri hiyo kukosa uzio, kutokuwa na chanzo cha maji cha kuaminika na sakafu kuwa na mashimomashimo hali iliyosababisha kutuama kwa maji na damu na hivyo kuhatarisha afya za walaji, hivyo wakamwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shadrack Mhagama kufanyia kazi mapungufu hayo kwani yanarekebika, jambo ambalo aliliafiki na kuahidi kutekeleza mara moja.
 RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AKARIBISHWA IKULU NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AKARIBISHWA IKULU NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

February 03, 2015

1
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake Ikulu Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck ambaye ameongozana na mke wake Bibi schadt leo tarehe.03.02.2015.
2
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimtambusha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa waliojitokeza kumpekea leo tarehe.03.02.2015 katika viwanja vya Ikulu.
3
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakipata mapokezi kwa kuimbwa kwa nyimbo za taifa za mataifa hayo mawili.
4
Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ajili yake leo katika viwanja vya Ikulu
5
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na ujembe kutoka ujerumani uliondamana na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakati Rais huyo alipowasili Ikulu.
6 8 10
Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akipokelewa na wanafanyakazi wa Ikulu,wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoawa wa Dar es salaam waliojitokeza viwanja vya Ikulu leo tarehe.03.02.2015 kumpokea.
11
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck Ikulu na kufanyanaye mazungumzo.
12
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck pamoja na ujumbe wake .
(PICHA ZOTE NA FREDDY MARO)

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AVUTIWA NA SHAMBA LA KAHAWA LA AVIV LILILOKO KWENYE KIJIJI CHA LIPOKELA, WILAYA YA SONGEA

February 03, 2015


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema amevutiwa sana na kazi iliyofanywa katika muda mfupi kwenye shamba la kahawa la Aviv lililoko kwenye kijiji cha Lipokela, wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma. Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, eneo kubwa la shamba limepandwa miche ya kahawa na mingine imezaa na imeshavunwa ikilinganishwa na wakati alipofika shambani hapo Julai 2013 na kutembelea tu kitalu cha miche ya zao hilo. Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 2, 2015) wakati akizungumza na wafanyakazi na menejimenti ya shamba la Aviv baada ya kulitembelea na kukagua miundombuinu ya umwagiliaji wa matone ya maji kwenye shamba hilo. “Mkuu wa shamba hili, Bw. Medu amenieleza kwamba mpaka sasa, wameshavuna kahawa mara moja na wanatarajia kuvuna tena hivi karibuni; lakini ili waweze kuanza kupata faida ni lazima wavune mara nne.” “Kilimo kinataka uvumilivu na kinataka uwekezaji mkubwa… ni lazima kiwepo; hata kwa wakulima wadogo ni lazima kiwepo licha ya ugumu wake. Sasa ukisema kilimo ni kigumu na ukaacha kulima wakati una mke na watoto, je hao watakula wapi?”, alihoji. Aliwasifu wamiliki wa shamba hilo kwa kuchagua kulima zao la kahawa kwani lina walaji kila mahali ulimwenguni kote. “Wameamua kulima kahawa aina ya Arabica ambayo inakubalika duniani. Uhitaji wa kahawa hii upo kila mahali kwa sababu wanywaji wapo,” alisema. Waziri Mkuu alisema pamoja na mafanikio hayo, shamba la Aviv linakabiliwa na changamoto ya nishati kwani linahitaji megawati 2.5 ili liweze kuendesha mitambo yake ambayo kwa sasa inatumia mafuta yanayoligharimu fedha nyingi. Aliwataka wamiliki wa shamba hilo waendelee kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. Mapema, akisoma risala ya kampuni ya Aviv, Mkuu wa shamba hilo ambaye pia anasimamia uzalishaji wa zao la kahawa Afrika Mashariki, Bw. Medu Medappa alisema hadi sasa wamekwishalima hekta 1,060 na zote zimekwishawekewa miundombinu ya umwagiliaji wa matone na kati ya hizo, hekta 810 zimekwishapandwa miche ya kahawa. “Shamba letu lina ukubwa wa hekta 2,000 na hadi sasa tumeshalima hekta 1,060 na zilizobakia ni kwa ajili ya kutunza mazingira na uoto wa asili kwenye vilima vinavyotuzunguka,” alisema. Alisema hadi sasa wamekwishaajiri wafanyakazi 1,500 kwenye shamba hilo na kutoa mafunzo kwa wakulima wanaoishi vijiji vya jirani. “Pia tumewapatia miche ya bure kaya 673 na kutokana na mafunzo tunayowapa, wanavijiji wameweza kulima kahawa inayoendana na viwango vya kimataifa vya uzalishaji kahawa ambavyo ni miezi 22,” alisema. Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu akijibu moja ya hoja kwenye risala ya Bw. Medappa iliyohusu eneo la hekta tisa kuchukuliwa na Wakala wa Ujenzi wa Barabara (TANROADS), alisema eneo hilo ni muhimu kwa ujenzi wa barabara za mkoa huo kama ambavyo shamba hilo ni muhimu kwa mkoa huo. “Lile eneo limetengwa na TANROADS kwa ajili ya kutengeneza kokoto za ujenzi wa barabara. Barabara za lami tunazitaka. Tunahitaji kazi hii iendelee la sivyo barabara zetu zitakufa,” alisema. Alisema watu wa TANROADS wakimaliza kazi yao, lile eneo litabaki tupu na mwekezaji huyo anaweza kulitumia kadri atakavyoona inafaa kwa sababu liko ndani ya eneo lake.
……………………………..
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 FEBRUARI 3, 2015.
RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI USIKU HUU.

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI USIKU HUU.

February 03, 2015

Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam. unnamed1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. unnamed2 unnamed3 
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa na mkewe Bibi Schadt  na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam. unnamed4 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
……………………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na msafara wake amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa 2.40.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt  amelakiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali pia mapokezi ya burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea.
Rais huyo  ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia  mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete atapata mapokezi rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.
Akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.
Pia Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.
RAIA WATATU WA KUTOKA NORWAY WAMEJIKUTA MIKONONI MWA BODI YA FILAMU WAKITENGENEZA FILAMU ZA BILA KIBALI

RAIA WATATU WA KUTOKA NORWAY WAMEJIKUTA MIKONONI MWA BODI YA FILAMU WAKITENGENEZA FILAMU ZA BILA KIBALI

February 03, 2015

 2
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo( wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu filamu hiyo iliyokuwa ikirekodiwa na raia wa Norway katika Ofisi ya Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam
.3
Raia wa Norway  waliokamatwa wakiwa katika kikao kuhusu filamu waliyokuwa wakirekodi kwenye Ofisi ya Bodi ya Filamu.4
Torshin Nodland raia wa Norway  (watatu kulia) akijitetea kuhusu filamu hiyo waliyokuwa wakirekodi.
1
Baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia raia hao wa Norway katika kurekodi filamu hiyo vikiwa katika Ofisi ya Bodi ya Filamu.
………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Raia watatu wa Norway wamejikuta mikononi mwa Bodi ya Filamu nchini baada kuchukua picha kwa ajili ya kutengeneza makala ya filamu inayohusu kazi za kutafsiri filamu za nje zinazofanywa na Bwana Derick Mukandala maarufu kama Mzee Lufufu maeneo ya Vingunguti. Wageni hao hawakuwa na kibali cha kutengeneza filamu kinachotolewa na Bodi hiyo hii ni kutokana na kunywimwa kibali kwa makubaliono ya kubadili mswada wa filamu hiyo.Uongozi wa Bodi ya Filamu iliwabaini zoezi hilo katika operesheni zake za kawaida zilizofanyika mwishoni mwa wiki,. Miongoni mwa wageni hao waliobainika ni mwandishi wa Mwongozo/Mswada (Script) Bw.Bjorn_Eric Hansen, Mpiga Picha(Cameraman) Bw.Torshin Nodland na mnasa sauti,kutoka Kampuni ya Grunder Film ya nchini Norway. Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo alisema filamu hiyo iliyokuwa ikitengenezwa na wageni hao kwa kushirikiana na Kampuni ya Get Real Training ya hapa nchini ilikuwa inahusu kazi anazozifanya Mzee Lufufu zinazokinzana na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya 1976 na pia Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 ya nchi. Bibi Fisoo aliendelea kusema bodi ya Filamu haiwezi kuruhusu utengenezaji wa filamu hiyo inayoonyesha ukiukwaji wa Sheria kwani kuna kinzana na juhudi za serikali katika kupambana na uharamia wa kazi za filamu na kwamba kamati tayari ilikwisha waandikia wahusika barua ya kuzuia uandaajwi wa filamu hiyo. “Wajumbe wa kamati ya vibali walielekeza wahusika kubadili maudhui ya mswada wao wakati walipopitia maombi ya kibali jambo ambalo halikukamilishwa. Hii ni kwa sababu mswada wa kutengeneza filamu hiyo unaonyesha kwamba mhusika watakayemtumia ni mtu ambaye amekuwa akikiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999,pamoja na mikataba ya Kimataifa inayosimamia Hakimiliki na Hakishiriki kama vile Mkataba wa Berne ambao Tanzania imeridhia ”,alisema Bibi Fissoo. Kwa upande wa raia hao wa Norway walikiri kuvunja Sheria na kukiuka taratibu za uandaaji wa filamu katika nchi na kuomba kwenda kubadili mswada wa filamu hiyo kwa mara nyingine ili waweze kuwasilisha upya pamoja na kufuata taratibu za kuomba kibali cha kutengeneza filamu kwa mujibu wa Sheria za nchi na ithibati ya Hakimiliki kutoka COSOTA. “Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976, iwapo Bodi itadhihirisha ukiukwaji wa sheria hiyo itaamuru tozo la faini papo kwa papo isiyopungua shillingi milioni moja, kuamuru kusitisha utengenezaji wa picha jongevu husika au kuamuru mkosaji kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria”alisema Bibi Fissoo. Kwa niaba ya wenzake Bw.Hansen alisema wameipokea faini hiyo na wanaahidi kulipa faini mara moja na kuwasilisha risiti, aidha walioomba radhi kwa kosa hilo na kuahidi kutotumia picha hizo mahali yoyote. Katika kuthibitisha raia hao wa Norway hawataendelea na zoezi la uchukuaji wa filamu hiyo, Bodi ya Filamu iliwekaana makubaliano nao kwa maandishi kuwa kutoendelea kupiga picha hizo hadi pale watakapobadilishi muswada wao na kupewa kibali cha kutengeneza filamu.