Jitihada Za Serikali Na Wadau Zachangia Kuimarika Kwa Hali Ya Lishe Na Kupungua Kwa Viwango Vya Utapiamlo Nchini.

October 27, 2023

 NA. MWANDISHI WETU


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Masuala ya Lishe wa mwaka 2021-22-2025/26 umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na juhudi za pamoja za wadau wa lishe nchini na kupelekea kuimarika kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe na kupungua kwa viwango vya utapiamlo kwa baadhi ya viashiria.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe nchini unaofanyika Jijini Arusha katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Meru tarehe 25 Oktoba, 2023, Dkt. Yonazi amesema kupitia mkutano huo utaweza kujadili mafanikio hayo na kuona uwezekano wa mikoa mingine kutumia mbinu zilizotumika katika mikoa iliyopata mafanikio na dhairi kuwa kasi ya kupungua viwango vya udumavu kwa watoto nchini itaongezeka


Dkt. Yonazi amesema kiwango cha Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambacho ndiyo kiashiria kikuu cha Utapiamlo kimepungua kutoka asilimia 34 mwaka 2016 hadi asilimia 30 mwaka 2022 na tathmini imeonesha kuwa mikoa saba imefanikiwa kupunguza vinwango hivyo kwa watoto zaidi ya asilimia 10 katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2022.


“Mafanikio mengine yanajumuisha kupungua kwa kiwango cha ukondefu kutoka asilimia 3.8 mwaka 2016 hadi asilimia 3.5 mwaka 2022 pamoja na kupungua kwa tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa wanawake walio katika umri wa uzazi (miaka 15 hadi 49) kutoka asilimia 44.8 mwaka 2015 hadi asilimia 28.8 mwaka 2018.” alisema Dkt. Yonazi


Aidha, Dkt. Yonazi amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Masuala ya Lishe wa mwaka 2021-22-2025/26, amesema bado kuna changamoto ambazo zimeendelea kuongezeka ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watoto wenye udumavu ambapo takwimu zinaonesha kuongezeka kutoka 2,700,000 mwaka 2016 hadi kufikia 3,400,000 mwaka 2022.


“Ni wajibu wetu sote katika mkutano huu kuhakikisha mikakati na maazimio tutakayoyafikia yanalenga kupunguza changamoto zinazotukabili katika utekelezaji wa Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe, ikiwemo changamoto ya kuongezeka kwa idadi ya watoto wenye udumavu.” Alisema Dkt. Yonazi


Akitoa salamu za kwa niaba ya Wadau wa Lishe nchini, Mkuu wa Shughuli za Lishe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Patric Codjia, amesema wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha masuala ya lishe yanaendelea kuimarika na kuyafikia malengo yaliyopo.


“Tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu wa Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa matokeo Chanya katika kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele na kuwa na matokeo tayarijiwa na tumefarijika kuwa sehemu ya kongamano hili la wadau wa masuala ya Lishe,” alisema Patric.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha tarehe 25 Oktoba, 2023.Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni: “Kuimarisha Mifumo ya Chakula kwa Matokeo Bora ya Hali ya Lishe na Maendeleo ya Rasilimali Watu na Ukuaji wa Uchumi"
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu kushoto (kwake) pamoja na wajumbe wa meza kuu wakifuatilia Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula an Lishe Nchini (TFNC) Dkt. Ray Masumo (kushoto)pamoja na Mkurugenzi Idara ya Lishe, Sera na Mipango TFNC Dkt. Japhet Mtaturu wakifuatilia hoja wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia mimea ya protini alipotembeela banda la ECHO wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu




Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe wakifuatili mawasilisho wakati wa mkutano huo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto),Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe wakiwasili kushiriki mkutano wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa sektarienti ya maandalizi ya Mkutano Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)



RC TANGA AWATAKA WANANCHI KUACHA KUTUMIA MIFUMO YA KIZAMANI KUHIFADHI FEDHA ZAO

October 27, 2023

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungusha mfano wa kadi ya NMB leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata –Halipoi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungusha mfano wa kadi ya NMB leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata –Halipoi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungusha mfano wa kadi ya NMB leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata –Halipoi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungusha mfano wa kadi ya NMB leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata –Halipoi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungusha mfano wa kadi ya NMB leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata –Halipoi uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabara –Halipoi iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus,

Mkuu wa Idara ya Kadi ya Benki ya NMB Philbert Casmir akizungumzia wakati akielezea kampeni ya Mastabata –Halipoi leo kwenye viwanja vya Mkwakwani Mjini Tanga wakati wa uzinduzi wake kulia Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mastabata –Halipoi leo kwenye viwanja vya Mkwakwani Mjini Tanga
Watumishi wa Benki ya NMB Mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mastabata –Halipoi leo kwenye viwanja vya Mkwakwani Mjini Tanga.


Na Oscar Assenga,TANGA.

WANANCHI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuacha kutumia mifumo ya kizamani ikiwemo ya kutembea na fedha mifukoni badala yake watumie mifumo ya kibenki ya Master Card Qr kwani ndio njia salama na ya uhakika wa kuhifadhi fedha zao

Hatua hiyo inaeleza kwambaa itakuwa ni salama kwani itawaepusha wananchi hao na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kukutana nazo ikiwemo wizi

Wito huo ulitolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mastabata-Halipoi inayoendeshwa na Benki ya NMB kwenye Halfa iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.

Ambapo alisema wakitumia mifumo ya kibenki ya Master Card QR itawawezesha kuwa na usalama wa fedha zao ikiwemo kutokuchakaa haraka.

Alisema kwamba wananchi wakiwa na mwamko wa kufanya hivyo itawaepusha na kuharibika kwa fedha lakini pia kama nchi itasaidia kuondokana na kuingia gharama na ndio maana wanasistiza umuhimu wa kadi.

“Ndugu zangu leo tupo hapa kwenye uzinduzi wa kampeni hii ya Mastabata –Haipoi niwaambie huu ni mfumo salama na makini hivyo niwaase wana Tanga na watanzania tuuchangamkie”Alisema

Aidha aliwaeleza wakazi wa mkoa huo kutumia njia mbadala kwa ajili ya kufanya malipo kuna kuwa na faida nyingi hivyo niwapongeze benki ya NMB kwa kuja na ubunifu huu.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huo kuacha kutumia mifumo ya kizamani kutembea na fedha mfukoni ili kuepukana na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kukumbana nazo ikiwemo wizi.

Alisema kwa sababu unapotumia kadi kwa kufanya malipo Benki ya NMB haikuachi hivihivi bali inakupa na zawadi mbalimbali hivyo wananchi changamkieni fursa hiyo muhimu.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo,Mkuu wa Idara ya Kadi wa Benki ya NMB Philbert Casmir alisema kampeni hiyo ni kusisitiza matumizi ya kadi wanaoita mastabata haipoi.

Alisema ili kurudisha faida ya benki ya NMB kwa jamii kila mwaka mwishoni wanafanya kampeni hiyo kwa kushirikiana na wadau wao wa mastakadi kwa kufanya kampeni kubwa kutoa zawadi kemukemu.

Aidha alisema utoaji wa zawadi hizo unakwenda sambamba na kuhamasisha wateja wao kuachana na matumizi ya pesa taslimu badala yake watumie kadi kufanya miamala,manunuzi.

Alisema pia watumie simu zao kufanya manunuzi ambapo kampeni hiyo leo wameizinduliwa Tanga na ilianza mwaka 2018 na 2022 waliita mastabata kivyakovyako na leo wanaita mastabata haipo.

Philbert alisema kwamba kupitia kampeni hiyo benki ya NMB inaendelea kuhamasisha malipo ya njia kidigitali na kuachana na pesa taslimu kupitia hiyo watakuwa na droo ya kila wiki,mwezi na hatimaye fainali droo sasa hapa mnisikilize kwa umakin.

Hata hivyo alisema kwamba benki ya NMB wakishirikiana wenzao wa mastakadi wameandaa milioni 350 zawadi ambazo zitakuwa zikishindaniwa na wateja wao huku akieleza vigezo kwanza zawadi za kila wiki.

Ambapo alisema watakuwa na washindi 100,kila mmoja atashinda pesa taslimu 100,000 lakini watafanya zoezi akikuta mtu afanaya manujnuzi kwa kutuimia kadi palepele anapewa 50,000.
MAKONDA, RABIA ‘WARIPOTI’ KWA CHONGOLO, AWAPATIA RUNGU KUANZA KAZI

MAKONDA, RABIA ‘WARIPOTI’ KWA CHONGOLO, AWAPATIA RUNGU KUANZA KAZI

October 27, 2023



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Daniel Godfrey Chongolo amesema CCM iko salama na imara katika kusimamia misingi, shabaha na malengo yake, ikiwemo kuendelea kuwa daraja la kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na jinsi ambavyo CCM kinaendelea kuwatumikia wananchi kwa kuzisimamia Serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussein Ali Mwinyi, ambazo zimeendelea kutafsiri maelekezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kwa vitendo.

Ndugu Chongolo amesema hayo Alhamis, Oktoba 26, 2023, alipokutana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Ndugu Paul Christian Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdallah Hamid, walipofika ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya kuonana naye, kujitambulisha na kuanza kazi, baada ya kukabidhiwa ofisi zao rasmi na watangulizi wao.

Ndugu Chongolo aliwaelekeza Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Paul Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid, kuanza majukumu yao, wakitambua imani kubwa waliyopewa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndugu Dokta Samia Suluhu Hassan, kutumikia Chama kupitia nafasi hizo walizoteuliwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Chongolo amesema kuwa nafasi hizo mbili, Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ni mojawapo ya maeneo ya kimkakati ya CCM, hivyo wanapaswa kujua kuteuliwa kwao ni sehemu ya kuongeza chachu na kasi ya idara hizo kutekeleza malengo yaliyokusudiwa na CCM, katika kutumikia wananchi na kuzisimamia Serikali zote mbili za CCM.

“Karibuni sana. Hongereni sana kwa kuaminiwa na kuteuliwa. Ujio wenu utakuwa sehemu ya kuongeza kasi ya yale ambayo Chama tumekusudia. Uenezi na siasa ndiyo kila kitu. Mmeaminiwa na kuteuliwa kushika maeneo muhimu.

“Siasa (na Uhusiano wa Kimataifa) ni mojawapo ya core activities za Chama chetu. Kwa upande wa Itikadi na Uenezi ni core activity ya siasa yetu na imani ya Chama chetu. Hatuna mashaka na ninyi. Tunatarajia mtafanya makubwa kufikia malengo. Tuna maandalizi ya uchaguzi hapa, 2024 na 2025 (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu). Tuko kwenye reli…tuko kwenye track sahihi. Karibuni sana.”

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Chongolo, pia alitumia nafasi hiyo kuwatakia kila la heri katika majukumu yao na kuwaelekeza kuwa, baada ya kukabidhiwa ofisi zao na majukumu yao rasmi na watangulizi wao, waanze kazi mara moja, kwa kuwa hakuna muda wa kusubiria.

“Najua watu wetu wa Dar Es Salaam wamewaandalia mapokezi. Nawatakia mapokezi mema na kila la heri mnapoenda kuanza majukumu yenu rasmi. Na Gavu (Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu) atawasindikiza,” amesema Katibu Mkuu Chongolo.

Ndugu Makonda na Ndugu Hamid, waliteuliwa kushika nafasi hizo, hivi karibuni na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), iliyoketi katika kikao chake maalum chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndugu Dokta Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 22, 2023, jijini Dodoma.

Ndugu Paul Makonda aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema aliyeteuliwa kuwa Mshauri Ofisi ya Rais, Masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, ambapo Ndugu Rabia Abdallah Hamid aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.