TAARIFA KUSOGEZWA MBELE TAREHE YA KURUDISHA FOMU ZA UCHAGUZI TBF

December 22, 2017



RAIS KARIA KUKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO

December 22, 2017


Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27,2017.
Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.
Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.
Taarifa zaidi za mkutano huo wa Rais Karia na Wahariri,mahali utakapofanyika pamoja na mualiko utatolewa kwa vyombo vya habari.
Huu ni mkutano wa kwanza wa Rais Karia na Wahariri wa habari za Michezo tokea ameingia madarakani.
Rais Karia aliingia madarakani August 12, 2017 kwenye uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ambao pia uliwaingiza madarakani Michael Wambura kwenye nafasi ya makamu wa Rais.
Wajumbe wa kamati ya utendaji waliongia madarakani kwenye uchaguzi huo ni pamoja na
Kanda namba 13 Dar es Salaam
Lameck Nyambaya
Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga
Khalid Abdallah
Kanda No 11 Pwani na Morogoro
Francis Ndulane
Kanda Namba 10 Dodoma na Singida 
Mohamed Aden
Kanda Namba 9 Lindi na Mtwara
Dunstan Mkundi
Kanda namba 8 Njombe na Ruvuma
James Mhagama
Kanda namba 7 Mbeya na Iringa
Elias Mwanjala
Kanda Namba 6 Katavi na Rukwa
Kenneth Pesambili
Kanda namba 5 Kigoma na Tabora
Issa Bukuku
Kanda namba 4 Arusha na Manyara
Sarah Chao
Kanda namba 3 Shinyanga, Simiyu
Mbasha Matutu
Kanda namba 2 Mara, Mwanza
Vedastus Lufano
Kanda namba 1 Kagera, Geita
Salum Chama

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF
Desemba 22,2017

DC SENYAMULE AFUNGUA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI, DINI NA WASIMAMIZI MPANGO WA PETS

December 22, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) waliohudhuria semina iliyofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Na Kajunason/MMG.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa mpango wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) kuwa na uadilifu katika kufiatilia matumizi ya fedha za serikali. Hayo ameyazungumza leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo uliowakutanisha viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) uliofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Mhe. Senyamule alisema ni vyema watendaji hao wakafuata misingi imara itakayowezesha serikali kujua ni wapi wanamatumizi mabovu ya fedha katika halmashauli. Aliagiza halmashauri kushirikiana kwa karibu na watu hao kwani kazi wanayoifanya ni ya halmashauri, hasa ukaguzi na mipango. "Idara ya ukaguzi ina watumishi 3 tu wanaohitaji kukagua kila kitu, sio rahisi wakidhi kwa wakati; lazima tuwashirikishe wadau wa PETS ili taarifa zao ziwe ni moja ya misingi ya ufuatiliaji kwa halmashauri," alisema Mhe. Senyamule. Pamoja na yote Mhe. Senyamule aliomba CCT kuongeza idadi ya kata wanazofanyia kazi kutoka 11 hadi zote 34 zilizopo kwa sasa. -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

SHAKA ATEMA NYONGO,ASEMA YUPO TAYARI KUWAJIBIKA IWAPO ITABAINIKA AMEFANYA UFISADI

December 22, 2017
Na Said Mwishehe,blogu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Shaka Hamdu Shaka amesema yupo tayari kuwajibika iwapo itabainika anefanya ufisaidi wa aina yoyote katika utendaji wake kwenye nafasi aliyonayo sasa.

Shaka ametoa kauli hiyo kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam leo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Kheir James Denis ambaye amepokelewa rasmi na kutambulishwa kwa vijana wa mkoa huo.

Amesema katika nafasi hiyo amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kutetea mali za umoja huo na kwa bahati mbaya hatua hiyo imemfanya apigwe vita na kumkwamisha.Amesema chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Dk.John Magufuli ataendelea kusimama imara kusimamia rasilimali za umoja huo na hatarudi nyuma.

Amesema amekuwa katika mazingira magumu yanayotokana na kupigwa na ikafika mahali baadhi ya watu wakaanza kumzushia mambo ambayo hayana ukweli wowote.Ametumia nafasi kueleza wazi yupo tayari kuchunguzwa na kuwa tayari kuwajibika iwapo itabainika ameshiriki kufuja mali za umoja huo."Nimeshambuliwa na kupigwa vita kwasababu tu ya kuwa na msimamo thabiti wa kusimamia mali za jumuiya na maadili.

" Naomba niseme leo hii ni siku ya historia kwangu kwani nimetoa la moyoni ambalo nimekuwa nalo muda mrefu,nimeshambuliwa na kupigwa vita bila sababu.Niseme nipo tayari kuwajibika kama nitabainika kufanya ufisadi kwa kutumia bafasi yangu,"amesema Shaka.

Amesema katika kusimamia mali za umoja huo amebaini kuliwa kwa zaidi ya Sh milioni 250 katika mabanda ya maduka ya biashara eneo la Ukumbi wa Vija a Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuliwa fedha hizo wakaamua kusimamisha shughuli za kibiashara na kinachoendelea kwa sasa ni kubomoa eneo hilo na kujengwa jengo la kitega uchumi ambalo litaingizia fedha umoja huo.

Ameelezea namna ambavyo amekuwa akitiwa moyo na Rais Magufuli na kufafanua hatarudi nyuma atashirikiana na mwenyekiti wa umoja huo taifa kuusimamia umoja huo.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

December 22, 2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.

Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani,alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .

“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema Makamu wa Rais.Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.

Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo  za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.

Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiandaa mti wake kabla ya kuupanda mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti  mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya kampeni ya kupanda miti  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WANAFUNZI SHULE ZA SEKONDARI IRINGA KUNUFAIKA NA ELIMU YA MASOMO YA SAYANSI

December 22, 2017
Wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya iringa kunufaika na elimu ya masomo ya sayansi kutokana na kuandaliwa kambi maalumu kwa ajili ya kuwafindisha kutoka kwa walimu waliobobea katika masomo hayo kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Ofisi ya mbunge wa viti maalum Ritta Kabati imeandaa mpango wa kuwaongezea elimua wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya Iringa kwa kuanzisha kambi ya masomo ya sanyasi itakayo kuwa inafanyika bure kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Akizungumza na Nuru fm Dicksoni Kawovela ambaye ni mratibu wa miradi ya jamii kutoka ofisi ya mbunge RITTA KABATI amesema kuwa wameamua kuja na mpango huo kwa lengo la kuinua elimu ya sayansi kwa wanafunzzi wa shule za sekondari hapa manispaa.

Aidha Kawovela amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa na manufaa kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wanahudhuria masomo haya ambayo yatakuwa yanatolewa bure.

Kawovela amewaka wazazi wa wanafunzi kuwaruhusu watoto wao kwenda kwenye makambi hayo ili waongezewe uwezo katika masomo ya sayansi.

Hata hiyo Kawovela alisema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania