MKE WA WAZIRI MKUU AZINDUA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

June 01, 2015
 Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .
Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu. Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya LuvTouch Manjano
Touch. 
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bongo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda. 
wageni walikwa
wageni Waalikwa waliungana na Mama Shear kumuunga Mkono Mwanamke Mwenzao aliyepiga Hatua kubwa na Kuanzisha Taasisi ya Kumwezesha Mwanamke wa Kitanzania
NHIF YAENDELEA NA MPANGO WAKE WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA KATIKA MIKOA YA PEMBEZONI.

NHIF YAENDELEA NA MPANGO WAKE WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA KATIKA MIKOA YA PEMBEZONI.

June 01, 2015

1 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Ali akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua mpango wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa,
2
2. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Raphael Mwamoto, akitoa maelezo kuhusu mpango wa Madaktari Bingwa wanaopelekwa mikoani na Mfuko huo.
3
Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakisubiri huduma za madaktari Bingwa,
4
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Bingwa baada ya kuzindua rasmi huduma ya madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara,
…………………………………………………………………………………………….
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF unaendelea na mpango wake wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa. Mpango huo pia unalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko katika hospitali za mikoani ambao watafanya kazi pamoja na madaktari bingwa hao. Madaktari waliokwenda Mtwara ni pamoja na wagonjwa ya akinamama,m magonjwa ya ndani, bingwa wa upasuaji na bingwa wa dawa za usingizi. Zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku sita.
Akizindua zoezi hilo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mtwara kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ili kuujengea uwezo zaidi Mfuko huo kupeleka huduma za kibingwa katika mikoa mingi zaidi.

TAASISI YA UTT-PID CHINI YA WIZARA YA FEDHA YAPANUA BARABARA ENEO LA MRADI WA VIWANJA LINDI

June 01, 2015
 Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Baada ya kupima na kufanikiwa kuuza viwanja zaidi ya 2,500 katika fukwe za Mabano na Mmongo kwa ushirikiano na Manispaa ya Lindi, Mradi huo umeingia katika hatua ya upanuzi wa barabara kuu na za mitaa ndani ya mradi ambapo kwa ushirikiano huo zaidi ya Shilingi Billion 1 zinatarajiwa kutumika mpaka kukamilika kwake.
Mradi huo mkubwa zaidi nchini katika upimaji wa viwanja Manispaa ya Lindi ulifadhiliwa na Taasisi ya UTT-PID utekelezaji wake ulianza mapema mwaka 2013 na sasa uaandaji wa hati kwa wanunuzi upo katika hatua ya mwisho baada ya kila mteja wa kiwanja kufanikiwa kuweka saini kwa hati zao katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwenyewe.
 Uchongaji wa hatua za awali wa Barabara ukiendelea katika eneo la Mradi. Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kukamilika kabla ya wanunuzi kuuanza ujenzi wa makazi yao katika eneo la mradi.
Uwekezaji huo ukiendelea pia Taasisi hiyo kwa ushirikiano huo na Halmashauri ya Lindi inatarajia kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa upimaji viwanja katika fukwe hizo ambapo zaidi ya viwanja elfu tano vitapimwa na kuuza kwa wananchi wote. Utekelezaji wa awamu ya pili bado upo kwenye hatua za awali na unatarajia kuuanza ndani ya mwaka huu 2015.
 Viwanja vya Mabano na Mmongo vipo katika fukwe nzuri na vikipata upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi.
Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
 Upanuzi huu wa barabara utafanyika mpaka kwenye fukwe kuwapa nafasi wakazi wa eneo husika kutembelea maeneo ya fukwe hizo
Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).

STARS KUINGIA KAMBINI LEO

June 01, 2015
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).

Kikosi kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.

Taifa Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wachezaji waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.

Msafara wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na viongozi .

Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa  kuchezwa Juni 14, 2015 katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.

Wakati huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.

Kufuatia kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5, Juni 2015 kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.

Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda Ethiopia kisha nchini  Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  
 
Rais Kikwete ampongeza Mzee Mwinyi kwa kutimiza miaka 90

Rais Kikwete ampongeza Mzee Mwinyi kwa kutimiza miaka 90

June 01, 2015

1
Rais Mstaafu awamu ya Pili Alhaji Hassan Mwinyi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ambapo jana alitimiza umri wa miaka 90.Sherehe hiyo ilifanyika katika hoteli ya Sea Cliff na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
2
.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa kutimiza miaka 90 wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwake iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mkewe Mama Siti Mwinyi.
3 4
Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na familia yake watoto na wajukuu zake wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ambapo alitimiza umri wa miaka 90 jana katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaa.
 Marais wakiwa katika aazungumzo ya amani Burundi Dar es salaam jana

Marais wakiwa katika aazungumzo ya amani Burundi Dar es salaam jana

June 01, 2015
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo juu ya mzozo wa Burundi jana.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
3
ais Dkt.Jakaya Mrisho  Kikwete  akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt.Nksazana Dlamini Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo ya amani ya Burundi jana
4
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha Ikulu  marais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini na Rais Yoweri Museveni wakati wa mkutano wa wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliohusu mazungumzo ya amani ya Burundi jana.
5 6 7
Marais wakiwa katika mazungumzo ya amani ya burundi Ikulu jijini Dar es salaam jana.
Tigo yadhamini Mnazi Mkinda

Tigo yadhamini Mnazi Mkinda

June 01, 2015


TIG1 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tigo John Wanyancha akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Mnazi Mkinda lenye lengo la kuendeleza vipaji kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Wilayani Ilala,  tamasha hilo linategemewa kufanyika Juni 2-3 mwaka huu, kushoto kwake ni Afisa Elimu wa Wilaya ya Ilala Bi Elizabeth Thomas.
TIG3 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tigo John Wanyancha akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Mnazi Mkinda lenye lengo la kuendeleza vipaji kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Wilayani Ilala,  tamasha hilo linategemewa kufanyika Juni 2-3 mwaka huu.
TIG4 
Baadhi ya Walimu na wageni waliofika kushuhudia uzinduzi wa tamasha la Mnazi Mkinda litakalofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 2 na 3 Juni, wakimsikiliza kwa makini Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tigo Bwana John Wanyancha.
TIG5 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tigo John Wanyancha akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Mnazi Mkinda lenye lengo la kuendeleza vipaji kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Wilayani Ilala,  tamasha hilo linategemewa kufanyika Juni 2-3 mwaka huu, kushoto kwake ni Afisa Elimu wa Wilaya ya Ilala Bi Elizabeth Thomas, wa kwanza kushoto ni mratibu wa Tamasha hilo Haroun Kinega.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA ALIPOFUNGUA MAONYESHO YA TANO YA SEKTA YA MAKAZI 2015

June 01, 2015
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya tano ya Sekta ya Makazi kwa mwaka 2015 Dar es Salaam yaliyomalizika jana. Kutoka kushoto ni Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege, Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula waandaaji wa maonyesho hayo, Ofisa Masoko wa EAG Group, Helen Mangare na Richard Ryaganda, Ofisa Masoko wa EAG Group.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua maonyesho hayo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula (katikati), akiteta jambo na DC Makonda (kushoto) na Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege.
Ofisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (N.H.C), Vicent Ngaile (kulia), akimuelekeza jambo DC Makonda baada ya kutembelea banda la shirika hilo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco Village, Ahzari Marik (kulia), alipotembelea banda la kampuni hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masaimara Gardening, Murwa Kihore Simindei (kulia), akizungumza na DC Makonda alipotembelea banda lao.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ivan Amulike (wa pili kushoto), akimuelekeza jambo DC Makonda katika maonyesho hayo. Wa nne kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Tumaini Iddi Setumbi na kushoto Ofisa Ardhi, Brenda Kuringe
Tigo Yafungua Duka Lililokarabatiwa Jijini Arusha

Tigo Yafungua Duka Lililokarabatiwa Jijini Arusha

June 01, 2015

du1
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe.Christopher Kangoye akikata utepe kuzindua Tawi la Kampuni ya Tigo mjini Arusha,wanaoshuhudia kulia ni Meneja huduma kwa wateja Tigo Kanda ya Kaskazini, Gwamaka Mwakilembe na kushoto ni Mwangaza Matotola, Meneja wa Ubora wa huduma kwa Wateja Tigo.
du2
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe.Christopher Kangoye akangalia bidhaa zilizomo ndani ya Duka la Tigo mara baada ya kuzindua duka hilo, kulia kwake anayetoa maelekezo ni Meneja huduma kwa wateja Tigo Kanda ya Kaskazini, Gwamaka Mwakilembe.
du3
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe.Christopher Kangoye akibadilishana mawazo na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
du4
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa wilaya.
du5
Meneja wa Mifumo ya Kibiashara na Mawasiliano wa Tigo Bi. Halima Kasoro akimkabidhi zawadi Afisa Mtendaji wa Temi Jijini Arusha Bi. Irene Joshua Ndosi wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo.
du6
Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja wa Tigo Bi Mwangaza Matotola akimkabidhi zawadi Afisa Mtendaji wa Levolosi Jijini Arusha Bi.Ester Maganza wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo.
du8
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe.Christopher Kangoye (katikati) akipokea zawadi toka kwa Mwangaza Mtotola na Halima Kasoro