UNESCO KUPITIA READ INTERNATIONAL WATOA MSAADA WA VITABU VYA SAYANSI KWA SHULE YA SEKONDARI MWEDO ARUMERU

UNESCO KUPITIA READ INTERNATIONAL WATOA MSAADA WA VITABU VYA SAYANSI KWA SHULE YA SEKONDARI MWEDO ARUMERU

August 11, 2014

DSC_0019 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya Sayansi wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia vitabu hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.
Meijo alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
DSC_0026 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Aidha alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa kutoa mifugo yao.
“Changamoto kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji na umeme wa kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa mitihani yao kwa kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa wanafunzi hao” alisema Meijo.
Ameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka ilikuweza kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia kusaidiwa upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa msaada huo wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa ufaulu shuleni hapo.
DSC_0037 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al Amin.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na Wizara ya Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu wenu kama wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika ujenzi wa taifa.
Bw. Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule hiyo kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa ajili ya masomo.
Shule hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
DSC_0041 
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana ya Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
DSC_0057 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0065 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba hiyo kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes.
DSC_0162
DSC_0101 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla ya kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa “Software” ya kisasa zaidi na kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba hiyo.
DSC_0141 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na Mwalimu wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
DSC_0129 
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
DSC_0386 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) na fisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y sekondari ya wasichana MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi shuleni hapo Bw. Edickiel Mturi.
DSC_0231 
Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu shuleni hapo.
DSC_0248 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu.
DSC_0308 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0313 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo, Martha Sengeruan.
DSC_0315Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
DSC_0332
DSC_0356 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 LAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI MWANZA.

August 11, 2014

Nyota wa  muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho  la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki.
 Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. 
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Diamond
na Ney wa Mitego wakioneshana umwamba wa kuwateka mashabiki kila mmoja
kwa staili yake,huku miluzi na Shangwe ikiwa imtawala ndani ya uwanja.
 Mmoja
wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva
Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa
jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia
mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba
jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki.
.
 Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa kupitia wimbo wake mpya wa Ole Themba akiwa chini ya Kampuni mpya ya No Fake Zone,Linah Sanga akitumbuiza mbele ya maelfu ya
wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi
kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa
CCM Kirumba lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la
Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la
Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la
Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Wasanii wa kundi la Tanikando Group kutoka Igoma, Mwanza nao
wakionesha umahiri wao kupamba onesho la muziki la Serengeti fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa CCM Kirumba jijini humo na kuhudhuriwa na maelfu ya wapenzi na washabiki wa tamasha hilo.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakishangilia baada ya kukongwa na burudani wakati wa tamasha la
Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki. 
 Sehemu ya Wasanii wa bongofleva waliofanya vyema katika tamasha la Fiesta 2014 kupitia shindano la Serengeti fiesta 2014 Supa Nyota.
 Msanii wa bongofleva anaekuja kwa kasi katika mchakato wa kuchanganya nyimbo za asili na za kizazi kipya kutoka Bukoba,BK Sande akiimba wimbo wake mpya uitwa OMWANA mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Hivi ndivyo wakazi wa jiji Mwanza walivyojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
 Msanii wa Bongofleva kutoka Mo Music akiimba jukwaani
 Utulivu ulikuwepo wa kutosha ndani ya tamasha la Fiesta 2014 huku umati mkubwa ukishuhudia uzinduzi wa tamasha hilo jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba,mwishoni mwa wiki.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young  De, akifanya vitu vyake ndani
ya Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa tamasha la Serengeti fiesta
2014, lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini  Mwanza.
 Umakini na mitambo ya kutosha kuwapa burudani isiyo nakikomo kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
Wakata Mikaa Chege na Themba wakishambulia jukwaa la fiesta
   Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakishangilia baada ya kukongwa na burudani wakati wa tamasha la
Serengeri fiesta lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki,tamasha hilo wiki hii litaendelea katika miji ya Bukoba na kahama.
 Pichani kushoto ni Msanii kutoka ndani ya jiji la Mwanza.Young killer akiwa na msanii mwanzake amkimpa tafu kulishambulia jukwaa vilivyo
 Wadau wakuu wa tamasha hilo wakifurahia jambo
 Msanii wa bongo fleva, Mr Blue akikonga nyoyo za umati wa wakazi wa
Jiji la Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kirumba katika tamasha
la Serengeti fiesta mwishoni mwa wiki ndani ya uwanaja wa ccm kirumba.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la
Serengeri fiesta lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki,tamasha hilo wiki hii litaendelea katika miji ya Bukoba na kahama.
 Vijana wa Mkubwa Fella,Yamoto Band wakilishambulia jukwaa.
 Mkamua ngoma wa Diamond,Romyjons akifanya vitu vyake wakati Diamond akitumbuiza jukwaani.PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA