WAZIRI JAFO AONGOZA KAMPENI YA UPANDA MITI ZAIDI YA 450 SHULE YA DAR ES SALAAM GIRLS SEC.

March 15, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Suleiman Jafo,ametoa pongezi kwa wanafunzi wa shule ya wasichana Dar es salaam Sekondari kupanda miche ya miti zaidi ya 450 katika eneo la shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Ubungo.

Kuelekea miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo ameongoza zoezi la upandaji miti zaidi ya Mia tano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam.

Pongezi hizo amezitoa leo Machi 15,2024, alipotembelea shuleni hapo kuhamasisha kampeni yake ya upandaji miti ambapo amesema kila mtu anawajibu wa kupanda miti hivyo basi wameona ni vyema kushirikisha wanafunzi wote nchini kufanya zoezi hilo lidumu kuwa endelevu katika vizazi vyao.

Aidha Dkt,Jafo amewashukuru mawakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa juhudi zao za kuzalisha miche ya miti kwa ajili ya kupanda nchini ili kuondokana na adha ya mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea kupungua kwa mvua na kuongezeka kwa kina Cha bahari.

"Tumeshuhudia dunia nzima joto linaongezeka ambapo joto hili linasababisha athari kubwa katika maisha ya wanadamu na viumbe mbalimbali lakini sehemu nyingine ukame umeshamiri,mvua ambazo hazina utaratibu zinasababisha mafuriko"Dkt,Jafo amesema

Amesema uharibifu wa mazingira umesababisha changamoto ya uchumi,umeme kukatika kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha kwa ajili ya uzalishaji wa umeme,jambo ambalo limeibua upungufu wa uzalishaji nishati hiyo.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa katika maelezo ya nchi na ilani ya chama cha mapinduzi imeagiza kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka kwa lengo la kupanda miti zaidi ya milioni 200 katika halmashauri zote ambapo katika taasisi za serikali wanafunzi kushiriki kufanya zoezi hilo.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule hiyo ya wasichana.

Kampeni hiyo ya upandaji miti imefadhiliwa na Benki ya NMB ambao wamekuwa wadau wakubwa wa Uhifadhi wa mazingira nchini,ambapo wanachama wa chama Tawala (CCM),Mabarozi wa mazingira,Pamoja na Mawakala wa huduma za misitu(TFS) wamehudhuria katika tukio hilo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiongoza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Dar es Salaam kupanda miti zaidi ya 450 katika utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati Waziri Jafo alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule hiyo na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 leo Machi 15,2024.



Baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 kwenye shule hiyo leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akitoa cheti cha shukrani kwa baadhi ya wadau wa mazingira katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti katika shule hiyo leo Machi 15,2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

TAMWA ZNZ Yawashukuru Wadau Kufanikisha Zoezi La Utoaji Tuzo Kwa Waandishi Wa Habari 2024.

March 15, 2024

 


MKURUGENZI Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ kwa niaba ya ZAFELA na PEGAO ametoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia kufanikisha hafla ya utoaji tuzo kwa waandishi wa habari iliyofanyika Jumamosi, Machi 9, 2024, katika Ukumbi wa SHAA mjini Unguja.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko ofisi za TAMWA ZNZ Tunguu, Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, Dkt. Mzuri Issa ametoa pongezi kwa waandishi wote waliowasilisha kazi zao kwa ajili ya kushiriki tunzo za umahiri wa waandishi wa habari za wanawake na uongozi.

Tuzo hizo zilitolewa katika vipengele vinne tofauti ikiwemo Radio Jamii, Radio za kitaifa, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo habari zilizowasilishwa zilikua zikiangazia maeneo mbalimbali ya kupigania haki za wanawake na mabadiliko.

Washindi wa tuzo hizo walizawadiwa zawadi ya vyeti, ngao pamoja na fedha taslim ambapo mshindi wa jumla ni Amina Masoud aliyezawadiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tatu za Kitanzania, ikionesha kutambuliwa kwa mchango wake wa kipekee katika tasnia hiyo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Jaji Mkuu wa Tuzo hizo Dkt. Abdalla Mohammed Juma alisema waandishi wa habari wanawake wameonesha muamko mkubwa katika kuwasilisha kazi zao ambapo katika waandishi wote walioleta kazi wanawake walikua ni 379.

Dkt. Abdalla aliongeza kuwa kazi hiyo ya kuwatafuta washindi wameifanya kwa uadilifu mkubwa kuhakikisha washindi waliopatikana ni wale waliowasilisha kazi zenye ubora.

“Kazi tuliyopewa tumeifanya kwa uadilifu mkubwa, na kama kuna mapungufu ni sisi majaji tunayabeba mapungufu hayo kwa asilimia 100”, Dr. Abdalla Mohammed alisema Jaji.

Bi Nasra Mohammed, mwandishi wa habari mkongwe ambae pia alikua ni miongni mwa majaji amewahimiza waandishi kuandika kazi zao katika viwango vya juu ili kuweza kuisaidia jamii katika masuala hayo ya takwimu.

"Sisi waandishi wa habari tufanye kazi kwa bora na zenye viwango kila siku ili kuweza kuipasha jamii taarifa sahihi zilizoshiba na kuleta tija katika jamii." Alisema Bi Nasra

Mwisho Dkt Mzuri alitoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kuandika habari zinazohusiana na wanawake, ikiwa ni pamoja na changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa nafasi za uongozi.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika kwa tuzo hizi, na kwa mwaka huu kumekua na ongezeko kubwa la idadi ya kazi zilizowasilishwa ambapo jumla ya kazi 529 kutoka vyombo vya habari mbalimbali Zanzibar ziliwasilishwa.

Tuzo hizi zinafanyika ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi ambao unatekelezwa na TAMWA ZNZ, ZAFELA na PEGAO kwa ushirikiano mkubwa na ubalozi wa Norway ambapo Kaulimbiu ya Tuzo hizi ni "Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake" inayoakisi dhamira endelevu ya waandishi wa habari kuongeza sauti za wanawake na kuchangia katika maendeleo yao.

MADEREVA WA MABUS YAENDAYO MIKOANI WAPATIWA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO

March 15, 2024


Na Mwamvua Mwinyi,MBEZI Machi 15

Hii ni wiki ya maadhimisho ya Ugonjwa wa Shinikizo la macho au Presha ya Macho duniani ambapo hospitali ya CCBRT,kwa kushirikiana na hospitali ya Barrack PolisI Kilwa Road na halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, wameadhimisha kwa kutoa huduma ya upimaji macho kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kunusuru uoni wa macho yao kutokana na kazi muhimu wanayoifanya.

Pia huduma hii inatolewa kwa mtu yoyote anayefika kituoni hapo ambapo tangu kuanza kwa zoezi hilo la wiki moja tarehe 12.3.2024 zaidi ya watu 400 walikuwa wamepatiwa huduma.

Ugonjwa wa presha ya macho unatajwa na wataalamu wa afya ya macho duniani kuwa wa kwanza kusababisha upofu usiotibika duniani.





BARRICK YAJITOSA KUTOA HAMASA NA MOTISHA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NCHINI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

March 15, 2024

 

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akiwa na wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika somo la hisabati muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi za laptop kutoka Barrick.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Franklin Rwezimula (kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa kwa niaba ya kampuni.
Mmoja wa wasichana waliofanya vizuri katika somo la hisabati, kutoka sekondari akipongezwa baada ya kupokea zawadi la Laptop kutoka Barrick
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani Morogoro walishiriki katika maadhimisho hayo
Wanafunzi wakishiriki kujibu maswali ya chemshabongo katika hafla hiyo.
---
Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini, imedhamini madhimisho ya Siku ya Hisabati Duniani ambapo kwa hapa nchini yalifanyika mkoani Morogoro kwa kuandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania ambacho kinashirikiana na Serikali kuongeza ufaulu wa masomo ya hisabati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

Kwenye kilele cha maadhimisho hayo , Barrick ilieleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia

Pia imedhamiria kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kutoa wito kwa wasichana kujiamini na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika hafla hiyo wanafunzi wa kike watatu waliofanya vizuri katika somo la hisabati lililoandaliwa na Chama cha Hisabati nchini mwaka jana walizawadiwa na laptop za kisasa kila mmoja na kampuni ya Barrick .Wanafunzi hao wanatokea katika sekondari za Lumumba-Zanzibar,Canosa na Marian.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk.Franklin Rwezimula, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, alisema Serikali inaendeea kufanya mikakati mbalimbali kuhakikisha ufaulu wa somo la hesabu na masomo mengine ya sayansi unaongezeka na aliwapongeza wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za Serikali katika kufanikisha suala hili.