HUBERT KAIRUKI KUJENGA KITUO KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA UJAUZITO

February 04, 2018
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano iliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya muasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4, 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu. Na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG. Katika kuadhimisha miaka 19 ya kumbukizi ya Marehemu Profesa Hubert Kairuki, Shirika la afya na elimu la Kairuki limejipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone amesema kuwa maadhimisho hayo yaliyoanza tokea Februari 1-6, 2018 jambo kubwa wamejipanga kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida huko Bunju jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ali Hapi. "Kumekuwa na matatizo hasa ya ukosefu wa vituo vya kuwasaidia watu wenye matatizo ya uzazi jambo linalotupa msukumo wa kuanza ujenzi huu, kwa sasa tupo katika hatua za mwisho tupate kibali tuanza ujenzi maana sisi tumeshajipanga na tumeshazalisha wataalamu wa kutosha," alisema Prof. Mgone. Professa Mgone amesema kukamilika kwa kituo hicho kitakuwa msaada mkubwa maana mpaka sasa hospitali ya Hubert Kairuki imekuwa chachu katika utoaji wa huduma ya afya ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 700. Aliongeza kuwa mbali na ujenzi wa kituo hicho wanatarajia kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto huko Bunju ili kuendeleza kuokoa vifo vya akinamama na watoto hasa waliombali na huduma. Jambo lingine ambalo wanalifanya katika maadhimisho hayo ni kutoa huduma za afya bure kwa kipindi cha kuanzia Februari 1-6, 2018  kwenye Hospitali ya Kairuki, pia wanajitolea damu kwa hiari ili kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu. Vile vile wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki watashiriki katika shindano la kujipima ujuzi juu ya mambo mbalimbali katika taaluma ya afya, maswali ya ufahamu kuhusu Tanzania, maisha ya mhasisi Marehemu Prof. Kairuki, Jiografia na jamii kiujumla. Mwisho wa kilele cha maadhimisho hayo kutafanyika mhadhara wa kitaaluma utakaoendeshwa na Professa Malise Kaisi juu ya mada 'Maono ya Prof. Hubert Kairuki yanayodumu': Umuhimu wake katika utoaji wa huduma za afya barani Afrika. Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) limasimamia Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) ambapo muasisi wake ni marehemu Hubert Clement Mwombeki Kairuki aliyezaliwa Juni 24, 1940 Bukoba mkoani Kagera. Mnamo Machi 17, 1987 muasisi huyo alianzisha hospitali ya TAG Mikocheni na mwaka 1992 aliibadilisha jina na kuitwa Mission Mikocheni hospitali ambayo kwa sasa inaitwa Kairuki Hospitali. Mwaka 1997, Prof. Kairuki alianzisha Mikocheni International University na baadae miaka 2 kupita alifariki dunia Februari 6, 1999 na chuo kikabadilishwa kuwa Hubert Kairuki Memorial Univesity. Wakati hospitali inaanzishwa ilikuwa walikuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wa nje 200 na wagonjwa wa ndani 30 kwa siku na kwasasa hospitali inauwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje 700 kwa siku na wagonjwa 150 wa ndani ambapo wakati muasisi anafariki chuo kilikuwa na wanafunzi 30 katika fani ya udaktari na uuguzi kwasasa chuo kinatakribani wanafunzi 1509.

TATUMZUKA YACHANGIA VIFAA VYA SHULE NA MATANKI YA MAJI WILAYA YA UBUNGO.

February 04, 2018
 Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo akizungumza na Waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu wilaya hiyo kupokea msaada wa baadhi ya vifaa Vya shule,kama vile Madawati 25,Vitabu 131 pamoja Matanki makubwa mawili  ya kuhifadhia maji kutoka kwa wachezeshaji wa Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka.Kulia ni Mwakilishi wa TatuMzuka,Bi Patronela. Mkumbo alisema kuwa wamepewa msaada wa vifaa hivyo kutokana na mkazi wa wilaya hiyo ya Ubungo,aitwaye Catherine Tryphone kushinda kitita cha Milioni 60 kupitia mchezo huo wa TatuMzuka.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi Vitabu 131 kwa ajili ya shule za Wilaya hiyo kwa  Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya  hiyo,Ally Juma Ally akishuhudia tukio hilo.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi madawati 25 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo,Ally Juma Ally,pichani kati anaeshuhudia ni Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo.Pichani nyuma kulia ni moja ya tanki lililokabidhiwa kwa viongozi hao wa Serikali.

POLEPOLE AMNADI MTULIA KWA KISHINDO KATIKA KATA YA MUZIMUNI, MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

February 04, 2018
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akitema cheche wakati akimnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Maulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akimnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Maulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akiingia kumnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Maulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Wananchi na wana CCM wakitimua vumbi kumlaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole , alipowasili kwenye viwanja vya Mtambani, kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Kinondoni  Maulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akimsalimia Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni baada ya kuwasili kumnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Mulid Mtulia (wa pili kushoto) katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni katibu wa CCm mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akimsalimia mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba baada ya kuwasili kumnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Mulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole na viongozi wengine wa meza kuu wakishangilia baada ya kuwasili, kumnadi Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Mulid Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya taida (NEC) ya CCM Humphrety Polepole akisaini kitabu cha wageni baada ya kuketi
 Mwenyekiti wa zamani wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Londa akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani kusalimia
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate kamba akimkaribisha Ndugu Polepole jukwaani baada ya kuhutubia
 Ndugu Polepole akitamba jukwaani kabla ya kumwita jukwaani Ndugu Mtulia kumnadi
 Polepole akimnadi Mtulia kwa wananchi
 Mtulia na Polepole wakionyesha furaha jukwaani wakati wakishangiliwa na wananchi
 "Ukishachaguliwa hawa wananchi wasaidie sana kutatua matatizo yao, maana wanakuamini na wanaaiamini CCM ndiyo maana watakuchagua" akasema Polepole kumwambia Mtulia (kushoto)

 " Na utatutuzi wa matatizo ya wanancho kwako utakuwa rahisi ukitumia Ilani hii ya CCM, maana kila kitu kimo humu" akaongeza Ndugu Polepole kumwambia Ndugu Mtulia kabla ya kumkabidhi kitabu hicho cha Ilani ya CCM ya 2015-2020
 Wananchi na wana CCM wakilipuka kwa nderemo wakati Ndugu Polepole akimnadi Mtulia
 Ndugu Polepole akimpongeza Mtulia baada ya kumkabidhi Ilani hiyo
 Kisha akamuasa zaidi
 Wananchi wakizidi kushangilia kwa vifijo
 Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni Said Mulid Mtulia akiomba kura katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanayika leo katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Muzimuni, Magomeni jijini Dar es Salaam, leo.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WANA CCM MUHEZA WAADHIMISHA MIAKA 41 KWA KUSHRIKI MSARAGAMBO WA UJENZI WA HOSPITALI

February 04, 2018
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Desderia Haule kushoto wakishirikiana na wananchi na wanachama wa chama hicho kushiriki msaragambo wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo 
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Desderia Haule kushoto wakiwa na mashepe wakishirikiana na wananchi na wanachama wa chama hicho kubeba kukoto kwa ajili ya ujenzi  ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo 
 Sehemu ya wananchi wakishriki kwenye zoezi la kubeba maji kwa ajili ya kushiriki Msaragambo wa Ujeniz wa Hospitali ya wilaya ya Muheza
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu kushoto akishusha ndoo iliyokuwa na zege kwa ajili ya kusambazwa kwenye msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambapo Mwenyekiti huyo aliwaongoza wanachama wa chama hicho kushiriki kwenye msaragambo huo
 Sehemu ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakishiriki kwenye kuchanganya zege
Sehemu ya wana CCM na wananchi wakishirikiana kubeba zege tayari kuimwaga kwenye msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza wakati waliposhiriki Msaragambo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA KUSIMIKWA KWA ASKOFU MKUU WA TANO WA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM LEO

February 04, 2018
Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo leo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018

 Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt Jacob Chimeledya  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Willim Mkapa akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu Mhe Augustino Ramadhani akipiga kinanda kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli wakikomunika kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   akiongea machache baada ya kushiriki  katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimsihi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya kuketi kwenya kiti alichoandaliwa yeye wakati wa kupiga  picha za pamoja wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya na viongozi wengine  wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

Picha na IKULU

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA YAKE KOREA KUSINI

February 04, 2018
 Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea Kusini. Viongozi hao wawili walikutana kwenye ofisi za Benki hiyo Jijini Seoul Korea Kusini wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu ya Waziri Mahiga nchini humo.
  Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na ujumbe wake kwenye mazungumzo na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI).
 Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI). Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Mheshimiwa Matilda Masuka.
 Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI). Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Mheshimiwa Matilda Masuka.
 Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na ujumbe wake kwenye mazungumzo na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI)
Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimkabidhi zawadi ya majani ya chain a kahawa za Tanzania Bw. Choi Jong-won, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Dong Myeong ya Korea Kusini.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA NCHINI KOREA KUSINI, AAHIDI USHIRIKIANO WENYE TIJA KWA MAENDELEO YA WANANCHI WOTE
                                                                                                                                                                                                                                                                                
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameahidi kusimamia uimarishwaji wa uhusiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ili wananchi wa pande zote mbili wapate manufaa.

Waziri Mahiga ameyasema hayo alipokuwa anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ambapo siku ya mwisho aliitumia kikamilifu kukutana na taasisi za umma za biashara na viwanda, Benki ya Exim ya Korea pamoja na makampuni binafsi yanayojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.

Amesema kuwa miaka 25 ya kwanza ya uhusiano wetu na Jamhuri ya Korea ilijikita kwenye kuweka misingi imara ya uhusiano wa kidiplomasia ambapo nchi zetu zilikuwa zinajiimarisha kama mataifa huru. “Sasa ni wakati wa kushamiri kiuchumi tuone sekta binafsi zinavyoshiriki katika kukuza uchumi, wananchi wa Tanzania waje kwa wingi nchini Korea kujifunza masuala ya teknolojia, uhandisi na hata usanifu na ubunifu. Huu ndio uhusiano wenye tija kwa mataifa yetu”. Mheshimiwa Waziri alisema.

Akizungumza na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea, Mheshimiwa Mahiga mbali na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa mikopo na misaada nchini Tanzania, Waziri Mahiga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli sasa imejikita kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ujenzi wa viwanda ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu. Kwasasa Benki hiyo inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na maji mikoa mbalimbali ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mahiga alifafanua kuwa ajenda ya Mheshimiwa Magufuli ya viwanda, haiwezi kukamilika bila kuwa na miundombinu ya msingi kama vile uzalishaji wa umeme wa kutosha na ukuaji wa sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambapo Korea Kusini ni wabobezi kwenye masuala hayo.

Alitumia fursa hiyo kumkaribisha Bw. Chang na timu yake kwenda Tanzania kufanya tathmini ya miradi tunayoshirikiana nao, lakini pia miradi mipya kwenye sekta ya uchukuzi kama ujenzi wa Standard Railway Gauge “SRG” kutoka Isaka hadi Kigali, n.k. ambayo ni miradi ya kipaumbele kwa sasa kwa taifa letu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Chang alisifu utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli, na Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania na kusema kuwa utendaji kazi wa aina hii ni wa kupigiwa mfano barani Afrika, na umekuja wakati muafaka tunapoingia kwenye hatua nyingine ya uhusiano wa kiuchumi baina ya nchi zetu mbili. Aidha aliongeza kuwa, wakati umefika sasa wa kufanya kazi, nay eye yuko tayari kufanya kazi na Tanzania kwani Serikali yake, imetoa kipaumbele kwa nchi hii.

Korea Exim Bank ni taasisi ya Serikali inayosimamia mikopo na misaada ya Jamhuri ya Korea inayotoa kwa nchi nyingine. Katika kipindi cha miaka minne (tangu 2016 hadi 2020), Korea Kusini kupitia taasisi hiyo, imeongeza mikopo ya maendeleo kwa bara la Afrika kwa asilimia 20. Uamuzi wa Serikali iliyokuwa madarakani mwaka 2016 wa kuichagua Tanzania kupokea kiasi kikubwa cha msaada huo kuliko nchi nyingine ya Afrika, umeendelezwa na Serikali iliyopo sasa madarakani ya Mheshimiwa Moon Jae-in, Rais wa Jamhuri ya Korea.

Ujumbe wa Mheshimiwa Augustine Mahiga pia ulikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Judong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Korea (Korea Chamber of Commerce and Industries KCCI), ambapo Waziri Mahiga aliwasisitiza kuja Dar es salaam kuangalia fursa zilizopo ili kuwashawishi wanachama wao kutafuta bidhaa na masoko nchini Tanzania.

Akielezea umuhimu wa KCCI kuzuru Tanzania na kujifunza soko la biashara, Bw. Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE aliyeongozana na ujumbe wa Mheshimiwa Waziri Mahiga, alisema njia nzuri ya kupata picha halisi ni kupitia Maonesho ya Biashara ya Saba Saba. Hivyo alitumia fursa hiyo kualika ujumbe wa KCCI kushiriki kwenye maonesho ya 42 yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Juni – 10 Julai, 2018.

Kabla ya kuhitimisha ziara yake, Mheshimiwa Mahiga pia alikutana na kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa makampuni ya DOHWA, ambao wamejikita kwenye ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya reli n.k. Makampuni mengine ni KORAIL, STX Engine, KTMI & STX Offshore pamoja na GS E&C, ambao wote wameonesha nia ya kuwekeza au kufanya biashara nchini Tanzania. Ujumbe mkuu kwa taasisi na makampuni hayo ulikua ni kupanua fursa za ushirikiano wa biaashara na uwekezaji, ubadilishanaji wa ujuzi na ujengaji uwezo wa wafanyakazi ambao ndio nguvu kazi ya taifa letu.

Pamoja na kuzungumza na makampuni ya umma na sekta binafsi yaliyoorodheshwa hapo juu, ziara ya Mheshimiwa Augustine Mahiga, ilimuwezesha kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kwanza la Biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ambapo alihutubia mamia ya wafanyabiashara wa Korea kuhusu utayari wa Tanzania kushirikiana na nchi hiyo kibiashara.

Mkutano huo uliopewa kauli mbiu ya “Eplore Tanzania” ulifuatiwa na mikutano midogo midogo iliyowakutanisha baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Korea Kusini ili kuangalia kwa ukaribu maeneo ya ushirikiano. Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kusini nchini Tanzania wameazimia kuendeleza makongamano hayo ya kila mwaka ili kuwa na ushirikiano wa karikiano wa karibu wa kibiashara kwa mataifa hayo mawili kwa maendeleo ya wananchi wote. 

Wajumbe wengine walioongozana na Mheshimiwa Waziri Mahiga nao walipata fursa ya kuhutubia hadhara hiyo kuhusu Tanzania ambapo Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Investment Centre alitoa utangulizi kuhusu uwekezaji Tanzania; Kanali (mstaafu) Joseph Simbakalia, Mkurugenzi Mkuu wa EPZA alizungumzia maeneo ya kipaumbele kwenye maeneo maalum ya uwekezaji nchini Tanzania. Naye Bi. Nasriya Nassor, Mkurugenzi wa Biashara wa Taasisi ya Uwekezaji Zanzibar alitoa taarifa fupi kuhusu Zanzibar kama kivutio cha utalii ndani ya Tanzania na eneo linalopendelewa na watalii wengi duniani.

Jamhuri ya Korea, kama inavyojulikana rasmi na Umoja wa Mataifa, ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri zaidi duniani kiuchumi kwa sasa. Viashiria vya uchumi vinaonyesha uchumi wa nchi hiyo utaendelea kukua kwa viwango kutokana na jitihada za dhati za viongozi wa nchi hiyo za kufuta kabisa umaskini kwa wananchi wao. Kwa sasa wastani wa pato kwa mtu “per capital income” inakadiriwa kuwa zaidi ya US$ 34,000, ukilinganisha na US$ 22,670 mwaka 2012. Baada ya vita ya Korea kwenye miaka ya mwanzo ya 1950, nchi ya Korea Kusini ilikua maskini kuliko nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania ambapo wastani wa pato kwa mtu ilikua na US$67.

Mheshimiwa Mahiga anatarajiwa kurejea nyumbani baada yakuhitimisha ziara hiyo aliyosema italeta faida sio tu kwa wafanyabiashara, ila kwa jamii kwa ujumla. Nchi hii ni tajiri sana kiuchumi; lakini utajiri wake mkubwa pia uko kwenye taaluma ya rasilimali watu, hivyo kwa Tanzania kufanikiwa kufungua ubalozi hapa, sasa tumefungua milango ya ushirikiano wa karibu, kuliko ilivyokuwa mwanzo. Tuchangamke tuige mfano wa uchapa kazi wao, na sisi tutaondoka kwenye umasikini Waziri Mahiga alisema kwa umaliza, kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon, uliopo mjini Seoul, Jamhuri ya Korea.

-Mwisho-

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Seoul, Korea Kusini,
3 Februari 2018.