ZIARA YA IGP MANGU NCHINI RWANDA

March 05, 2017
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto),  na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakibadilishana hati ya makubaliano yenye mkakati wa kuhakikisha nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda, zinakuwa salama hususan maeneo ya mipakani na hata kwenye barabara zote zinazotumiwa na wafanyabiashara, IGP Mangu, pamoja na ujumbe wake amefanya ziara ya kikazi nchini humo jana.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda 
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (mbele kushoto) akitoa neno mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, pamoja na ujumbe alioongozana nao nchini humo jana, katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akimsikiliza mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, akitoaneno mbele ya  wajumbe kutoka Tanzania (hawapo pichani) IGP Mangu, yupo nchini Rwanda, kwa ziara ya siku moja  yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akimsikiliza mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, akitoa neno mbele ya  wajumbe kutoka Tanzania (hawapo pichani) IGP Mangu, yupo nchini Rwanda, kwa ziara ya siku moja  yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, mara baada ya kuitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda (Picha zote na Demetrius Njimbwi- Jeshi la Polisi Tanzania)

RAIS AHUTUBIA WANANCHI WA MTWARA KATIKA VIWANJA VYA MASHUJAA MKOANI MTWARA

March 05, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mtwara katika siku ya mwisho wa ziara yake katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara.
Wananchi wa Mtwara wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mtwara mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mtwara mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara-PICHA NA IKULU

AFISA MAENDELEO JIJI LA TANGA AFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE LA JIJIN HILO AWATAKA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI KUJIPATIA MAENDELEO

March 05, 2017
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akifungua kongamano la Wanawake Jijini Tanga ambalo lilikuwa na lengo kuu la kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa wanawake ikiwemo fursa za kiuchumi sambamba na kupambana na dawa za kulevya kwa jamii lililofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga leo
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi  wa pili kutoka kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa wakati wa kongamano la wanawake Jijini Tanga kuelekea siku ya wanawake dunia kushoto ni Rehema na Yahaya Seumbe ambaye ni Afisa kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii kwenye Jiji la Tanga wakifuatilia kongamano hilo.
 Baadhi ya Wakina wanawake jijini Tanga  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo
 Sehemu ya Umati wa wanawake wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo la wanawake wa Jiji la Tanga kuelekea siku ya wanawake Dunia ambapo kilele chake itakuwa ni Machi 8 mwaka huu
 Baadhi ya waandishi wa habari jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo wa kwanza kulia ni Burhan Yakub wa gazeti la Mwananchi,Bertha Mwambele wa TBC TV na Sussan Uhinga wa Clous TV

 Sehemu ya wakina wanawake Jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano la wanawake kuelekea siku ya wanawake ambapo kilele chake ni Machi 8 mwaka huu
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia Machi 8 mwaka huu mara baada ya kufungua kongamano la wanawake Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga baada ya kumalizika kwa kongamano hilo ambapo alisema kuelekea siku ya wanawake kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii

NAMAINGO YATOA ELIMU BURE WAKAZI DAR KUHUSU UJASIRIAMALI

March 05, 2017
 Mkurugenzi wa Taasisi  ya Namaingo Business Agency Tanzania Limited, Ubwa Ibrahim akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Ukonga, Dar es Salaam jana. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Aliwapiga msasa kuhusu ufugaji wa kisasa wa kuku,sungura, samaki pamoja na kilimo biashara pia na jinsi ya kuwaunganisha na taasisi za kifedha na serikali ili kuwarahisishia kupata mikopo ya kuendeleza miradi. Pia aliwafundisha jinsi ya kupata masoko ya bidhaa zao.
 Bi Ubwa Ibrahim akihojiwa na vyombo vya habari baada ya semina hiyo

















MAKAMBA ATOA TAAFIFA YA OPERESHENI MAALUM YA UTEKELEZAJI WA KUSITISHA, UZALISHAJI, USAMBAZAJI, UUZAJI NA MATUMIZI YA POMBE KALI KATIKA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI (VIROBA)

MAKAMBA ATOA TAAFIFA YA OPERESHENI MAALUM YA UTEKELEZAJI WA KUSITISHA, UZALISHAJI, USAMBAZAJI, UUZAJI NA MATUMIZI YA POMBE KALI KATIKA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI (VIROBA)

March 05, 2017
JANU1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba). Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi
JANU2
Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alipozungumza nao na kutoa matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba).
……………………………………………………………………………
Kama mnavyofahamu unywaji wa pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, ajali na vifo zivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizi, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. Madhara haya ndiyo yaliyopelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kutoa tamko tarehe 16 Februari, 2017 akiwa Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha uzalishaji, usambazaji,  uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) kuanzia tarehe 1 Machi 2017; Baadaye tarehe 20/2/2017 na tarehe 28/2/2017 nilitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu ufuatiliaji wa agizo hilo.
Ili kutekeleza kwa ufanisi agizo hili serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuratibu Operesheni Maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya serikali na kuchukua hatua stahiki.
Kikosi Kazi hicho kiko chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, na kinajumuisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango,  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.
Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote  kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na  Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya.  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).
Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu operesheni maalum  katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii ilitokana na kuwepo  kwa viwanda vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets)  ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.
Kikosi Kazi maalum katika Operesheni hii  tulikielekeza kufanya yafuatayo:-
RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE PIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE PIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

March 05, 2017
DAN1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili kiwandani hapo kwa ajili  ya kuzindua magari 580 ya kusafirisha saruji nchini.
DAN2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumkabidhi barua ya malalamiko kutoka kwa madereva wanaolalamikia utoaji wa ajira hizo kiwandani hapo.
DAN4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja hivyo vya kiwanda cha Dangote kabla kuzindua magari 580 ya kiwanda hicho yatakayosafirisha saruji nchini.
DAN5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
DAN6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kukagua kiwanda chake cha Saruji mkoani Mtwara.
DAN7
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani Mtwara.
DAN9
Rais Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki huyo wa Kiwanda akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari hayo 580.
DAN10
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.