WATANZANIA WALIVYOTUIA FURSA YA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFANYA BIASHARA NA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.

September 01, 2016
Wafanyabiashara wa tikiti maji wakitumia tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali kuuza matunda hayo kwa wananchi waliofika katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa Jua. 
Wafanyabiashara wa Mchele wao pia hawakubaki nyuma wakatumia fursa hiyo kuuza Mchele kwa wananchi waliofika kushuhdia tukio hilo.
Mama lishe pia hawaubaki nyuma kuhakikisha wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo .
Benki ya NMB pia walitoa huduma ya kufungua Akaunti kwa wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yaiendelea katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Amosi Makala akizungumza juu ya fursa za kiuchumi zilizojitokeza kutokana na tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Songe Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa akizungumza na wananchi waliofika katika eneo hilo kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA ,Pascal Sheluetete akizungumza na wanahabari ambapo shirika hilo limetangaza kufungua lango la Ikoga kwa ajili ya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa upande wa Bonde la Ihefu.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa walipokutana kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makala,(katikati) ,Mkuu wa Mkoa wa Songwe ,Chiku Galawa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete wakitizama tukio la kupatwa kwa jua ka kutumia miwani maalumu za kutizamia.
Hatua ya mwanzo ya tukio la kupatwa kwa jua ,baada ya mwezi kuanza kupita mbele ya Jua na kuanza kuzuia mwanga usifike katika uso wa Dunia.
Mwezi ukiwa umebakiza kipande kidogo wakati ukipita mbele ya jua.
Mwezi ukiwa katikati ya jua na kutengeneza kipete.
Mwezi ukiwa umeanza safari  ya kuliachia jua.
Baadhi ya wananchi wakitizama tukio hilo .
Wengine walilazimika kutumia miwani maalumu kwa ajili ya kuchomea vyuma kutizama tukio hilo. 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali ,Mbeya.

WAZEE WATAKA USHIRIKI WA WAZI KATIKA SERA NA MIPANGO YA MAENDELEO

September 01, 2016
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akiongoza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za ESRF kufungua warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)  iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati). Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha na Mkurugenzi Mkazi Msaidizi wa Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Smart Daniel (wa pili kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)  iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Jukwaa la Wazee Tanzania, Samson Msemembo (85) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo wazee katika vituo vya huduma za afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii Bw.Rabikira Mushi kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida waliopo meza kuu.
 Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Oswald Mashindano akizungumzia nafasi ya wazee katika sera ya kitaifa kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros akishiriki kutoa maoni kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)  iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros.
  Mshauri wa Masuala ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Magharibi wa Shirika la Help Age International, Roseline Kihumba akizungumzia hali ya uzee na wazee duniani na ushirikishwaji wa wazee katika maendeleo endelevu kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)  iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akichangia mada kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)  iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
 Mkurugenzi wa Mtandao wa Watu Waishio na Virusi vya Ukimwi Tanzania (SHDEPHA), Joseph Katto akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi na VVU katika kupata huduma mbalimbali nchini kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki waliohudhuria warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa ESRF wakati wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International
 Picha ya pamoja

Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuhakikisha kwamba kunakuwapo na ushirikishaji wa wazi wa wazee katika sera na mipango ya maendeleo.
Aidha imetakiwa kutoa nafasi kwa wazee katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo, jamii na mazingira.
Kauli hizo zimetolewa na washiriki  wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ,SDGs ambayo imeingizwa katika mipango ya maendeleo ya taifa.
Wakiongozwa na mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu mbalimbali kama Dk Oswald Mashindano, Danford Sango,  Ahmed Makbel, Dk. Ntuli Kapologwe washiriki walisema kwamba ingawa Tanzania ina sera nzuri kuhusu wazee utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na kukosekana kwa utashi.
Aidha walisema kwamba kukosekana kwa sheria ya wazee kunawafanya wazee hao kunyanyasika hasa katika masulaa ya kiuchumi na kiafya.
Joseph Kato (62) ambaye alisema kwamba amekuwa akiishi na UKIMWI tangu ujana wake hadi sasa ameingia rasmi katika rika la wazee, anasema kwamba sera za nchi hasa za afya haiztoa umuhimu kwa magonjwa kama Ukimwi.
Aidha alisema kwamba wazee wakiwa na afya zao wamekuwa wakipuuzwa katika suala la uchumi kwani ukiwa unaishi na Virusi vya Ukimwi ukienda benki hupewi mikopo na pia ukiwa mzee hupewi mikopo.
Alisema kama sera ni kuhakikisha hakuna anayeachwa katika safari za utekelezaji wa maendeleo endelevu ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba wazee hawanyanyaswi na wanasaidiwa kuwezeshwa kiuchumi.
Mshiriki mwingine aliyejitambulisha kama Mama Koku alisema kwamba ngazi za chini za utekelezaji zimekuwa hazitoi kipaumbele kwa wazee japo serikali kuu katika mipango yake imeonesha nini kinachotakiwa kufanywa na kila mmoja katika nafasi ya kuhudumia wazee.
Alisema upo mkakati wa mwaka 2007 hadi 2025 ambao umeonesha utekelezaji wa huduma kwa makundi tete lakini wakurugenzi wa halmashauri hawaweki wazee kama kipaumbele chao wakisingizia serikali kuu.
Hata hivyo amesema wakati umefika kwa serikali kufuatilia mkakati huo kwa lengo la kuwabana wahusika ili kipaumbele kwa wazee kiwepo.
Amesema maofisa mipango wengi wanakwepa kuweka kipaumbele kwa dai kuwa fedha wanazoletewa ukomo wake hauruhusu kuwaingiza wazee huku wengine wakidanganya kwamba serikali kuu ndio imeondoa msaada kwa wazee.
Naye Ishaka Msigwa kutoka Ruvuma alisema kwamba tatizo kubwa la kuhudumia wazee sio sera kwani ipo ila dhamira ndio haipo. Alisema wazee wanataabika sana katika suala la uchumi na kwamba ipo haja sheria ya wazee ikatungwa ili kuwasaidia kuondokana na adha ya kukataliwa wakati wa kutafuta mikopo ya kuwainua kiuchumi.
Alisema asilimia 50 ya mayatima wanakaa na wazee vijijini na kitendo cha kuwanyima ushiriki wa uwezeshaji unawatesa.
Pamoja na malalamiko hayo ya wazee  ambayo yalijikita katika kuwa na kipato cha uhakika na suala la upatikanaji wa matibabu, serikali ilisema imekamilisha utaratibu wa utoaji wa pensheni kwa wazee Tanzania bara na kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji wake.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akifungua warsha hiyo kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) alisema hata hivyo serikali itaanza kutoa posho hizo kwa wazee wa miaka 70  kwenda juu na badae watashuka hadi katika umri unaokubalika.
Alisema wamejifunza kutoka Zanzibar na wanaona hapo ni eneo jema la kuanzia.
Aidha alisema kwamba bado anaendelea na juhudi zake za kutaka sheria ya wazee itungwe kwa kuwa ipo sera inayohusu wazee.
Kwa hesabu za karibuni Tanzania inawezee zaidi ya milioni 2.
Pamoja na kuzungumzia suala la malipo ya pensheni ambapo alisema suala hilo kwa sasa lipo Hazina, waziri huyo alirejea msisitizo wake wa kutaka wazee watibiwe bila malipo.
Alisema serikali ya awamu ya tano ni serikali ya utekelezaji na kwamba suala la tiba bure kwa wazee ni suala la sera na wala si utashi.
Akizungumza kwa kina masuala yanayogusa wazee kama yalivyotolewa kwa sauti na mzee Samson Msemembo (85), Waziri Ummy alisema kwamba serikali inatambua changamoto zinazowakumba wazee na itazifanyia kazi kuhakikisha kwamba zinapatiwa majibu.
Mzee Msemembo kutoka Jukwaa la wazee Tanzania, alisema kwamba wazee wamekuwa wakinyanyasika katika sekta ya afya na uchumi wakibaguliwa na kunyimwa fursa za kuishi kwa furaha.
Akizungumza kuhusu kero zilizoelezwa katika warsha hiyo iliyoendeshwa kwa pamoja katika Taasisi za Tafiti za Kiuchumi na Kijamii nchini (ESRF) na taasisi ya kimataifa ya kusaidia wazee Help Age, Waziri Ummy alisema serikali inataka wazee wawe na  kipato cha uhakika na kupewa matibabu.
Amesema hakubaliani na suala la wazee kukosa matibabu na kutaka wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha kwamba wazee wanaingizwa katika mfumo wa matibabu wa CHF au wanapewa kadi maalumu ya matibabu bure.
Alisema kwamba haingii akilini kuona kwamba wazee sita katika watu 100 wanakosa kutibiwa kwa dai la kukosekana kwa fedha wakati sera zipo zinazotaka watibiwe bure.
Akizungumzia tatizo  la Hospitali ya Taifa Muhimbili kutotibia wazee alisema kwamba atalishughulikia tatizo hilo kwani haliingii akilini mwake:“Watumishi, vifaa, kila kitu ni cha serikali inakuaje wazee wasitibiwe” alihoji Waziri Ummy .
Akizungumzia suala la kukuza uchumi wa wazee alisema kwamba atamwandikia barua Rais Magufuli ili aweze kutoa agizo la asilimia 2 katika mapato ya ndani ya halmashauri kuchochea uchumi kwa wazee.
Alisema kuna asilimia 5  zimetengwa kwa vijana na wanawake pia 5 na haoni sababu zisitengwe asilimia 2 kwa ajili ya wazee.
Katika warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba warsha hiyo imelenga kusaidia wadau mbalimbali kutambua masuala ya wazee katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za chini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU UMETANGAZA KUTOA MILIONI 100 KWA AJILI YA MADAWATI MKOA WA GEITA

September 01, 2016
Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita

    
Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.

      Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita

Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu  Umetoa Tsh 100m/- kwa Ajili ya Madawati ya Shule Mkoani Geita. 


 Akitangaza kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika  Desire Park Mjini Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu  Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu  imebarikiwa kuwa  karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita.

“ Hivyo basi tulipopokea  mwaliko kutoka  kwa Mkuu wa wilaya ya  Nyang’wale  kuhusu kampeni ya leo  ya madawati tumeamua kwamba japokuwa  miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona kuna umuhimu  wa kufanya hivyo  mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila.

"Hivyo basi  siku ya leo tunajitolea  kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya kampeni  za mikoa inayolenga kuondoa  upungufu wa  madawati 70,000.”aliongeza Kasitila.

 Elias aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini  ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia imetumia  takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja  ambayo inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000.

 Mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu wa  Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo.

 Akiwahutubia  washika dau waliokuwa  Desire park Naibu Waziri Jafo  alisema “Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu  kuhusiana na mwitikio ambao nimeushuhudia leo  ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita kuorodhesha washika dau wote waliochangia  leo na kuwasilisha orodha hiyo kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa kuiondolea Geita uhaba wa madawati.”

 Katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi alijitolea kuchangia  fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya kampeni hiyo.

MBUNGE MUFINDI KASKAZINI MAHMOUD MGIMWA ATOA MSAADA WA AMBULACE JIMBONI KWAKE

September 01, 2016


 MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
 MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni

SHINDANO LA OZONA MISS LAKE ZONE 2016 LAZINDULIWA RASMI JIJINI MWANZA.

September 01, 2016
Shindano la Ulimbwende la "Ozona Miss Lake Zone 2016" linaloshirikisha Walimbwende 18 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa limezinduliwa rasmi hii leo Jijini Mwanza.

Shindano hilo litakalofanyika jumamosi Septemba 10,2016 katika Ukumbi wa Rock City Mall, limeandaliwa na Flora Promotions na kupewa nguvu na wadhamini mbalimbali akiwemo mdhamini mkuu, Kampuni ya vipodozi ya Ozona ambayo imetoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa mshindi wa kwanza.

Katika picha, kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ozona, Dr.Thobias Mkina, akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo ambapo kushoto ni Mkurugenzi wa Flora Promotions, Flora Lauwo.
Na BMG
Wadau mbalimbali Ozona Miss Lake Zone wakiwa kwenye uzinduzi wa shindano hilo hii leo
Wadau mbalimbali Ozona Miss Lake Zone wakiwa kwenye uzinduzi wa shindano hilo hii leo
Mkurugenzi wa Flora Promotions, Flora Lauwo, akiteta jambo kwenye uzinduzi wa shindano la Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Mzee wa Masauti, Christian Bella pamoja na Mchekeshaji Erick Omond wanatarajiwa kuungana na watumbuizaji wengine pamoja na wadau wengine kwenye kufanikisha Usiku wa Ozona Miss Lake Zone 2016.