ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

February 25, 2016

● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi .
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao.
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
MAB4
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
MAB5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
MAB6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
MAB7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
MAB8
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
MAB9
Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
MAB10
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bibi Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
MAB11
Baraza la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.
MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA MAKAMPUNIYA PEPSI, COCACOLA NA AZAMCOLA

MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA MAKAMPUNIYA PEPSI, COCACOLA NA AZAMCOLA

February 25, 2016

we1
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola- SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia  kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto   ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we3
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto   ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we4
we6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto  Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni  Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana   baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji  baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza.  Kulia    ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu awataka Mawazi kuzingatia Maadili

Waziri Mkuu awataka Mawazi kuzingatia Maadili

February 25, 2016

1
Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa,Majaliwa akizungumza na mawaziri na manaibu waziri wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
2
Waziri ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
4
Kamishna Tume ya Maadili kwa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu salome Kaganda akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
5
Baadhi ya Mawaziri na manaibu Waziri wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda ikiwa ni ishara ya kuonesha uzalendo kwa nchi kabla ya kuanza semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
7
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi Virginia Blaser akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe huku mawazili wengine wakisililiza mazungumzo hayo.
8
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimsikiliza  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. JumanneMaghembe kabla ya kuanza kwa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam katikati ni Waziri ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
9
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza jambo pamoja na mawaziri wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam ,kulia ni  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Uratibu, Bunge,Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama(Kulia na katikati ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi.
10
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Hamad Masauni  kushoto  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina huku mawazili wengine wakupitia makabrasha yao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
11
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo kwa mawaziri na manaibu iliyotolewa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewaasa Mawaziri na Manaibu Waziri kuzingatia sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma kwani maadili ni nyenzo  kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimi wa Majaliwa ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya Maadili kwa Mawaziri na Manaibu Waziri inayolenga kuwajengea uwezo mkubwa yanamna kiongozi wa utumishi wa umma anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake bila kukiuka maadili.
“Chimbuko la Maadili ya Utumishi wa Umma ulianza tangu siku nyingi na umekuwa ukitajwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika Katiba ya nchi ya mwaka 1977, Sheria za Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishiwa Umma,”alisemaMajaliwa.
Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo WaziriMkuu alisisitiza kuwa Semina hiyo siyo semina elekezi kwa viongozi hao kama jinsi imekuwa ikijadiliwa katika mitandao ya kijamii, bali ni semina inayolenga kutoa mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya Uadilifu na mada katika semina hiyo zitahusu masuala ya maadili tuu.
Kwa upande wa Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma amesema semina ya maaadili kwa viongozi ni jukumu la Sekretariati ya maadili kuandaa kwani hiyo ni sehemu ya majukumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma na wao ndiyo wenye wajibu wakuhakikisha viongozi wa utumishi wa umma wanazingatia maadili.
“Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma inamamlaka ya kufanya uchunguzi kwa kiongozi yoyote wa umma atakayesikika kukiuka maadili kama kiapo cha ahadi za uadilifu kinavyosema,”alisema Jaji Mstaafu Salome.
Aidha Kamishna wa Maadili huyo aliendelea kusema Ofisi ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya rasimali fedha ambapo wanazaidi ya miaka mitatu wameshindwa kufanya uhakiki wa mali za viongozi pamoja na uchunguzi kutokana na changamoto hiyo.
Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na Shirika la USAID.

Ofisi ya Uhusiano, Kitengo cha Masoko TANESCO aelimisha umma kuhusu usalama na ubaya wa wizi wa umeme

February 25, 2016

 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA NJIRO,
waliohudhuria kwenye mafunzo ya usalama na wizi wa umeme wa kwanza (Kushoto) ni
Afisa Huduma kwa wateja Bw. Juma Msuya.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Veta kilichopo Oljoro mkoani Arusha
akiuliza swali kwa wataalamu wa TANESCO katika mafunzo hayo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Oldonyo Sambu Mkoani Arusha wakiwa na zawadi zao walizopewa na wataalam wa TANESCO kama zawadi za kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kujibu na kuuliza
maswali, kushoto ni Afisa Mahusiano na Wateja Mkoa wa Arusha Bw.Fred
Mbavai.
 Baadhi ya wanafunziwa Shule ya Msingi Mbweni ya jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kuwapokea
wataalam kutoka TANESCO kwa ajili ya kupokea elimu kuhusu masuala mbalimbali ya umeme.
  Afisa Masoko  Bi. Jenifer Mgendi kutoka Shirika la Umeme (TANESCO)     akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu maswali vizuri wakati wa utoaji elimu ya masuala ya umeme, katika Shule ya Msingi Tandika ya
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisukuru ya jijini Dar es Salaam, wakishangilia zawadi walizopewa wakati wa wataalam kutoka TANESCO walipotoa elimu ya masuala ya umeme. Katikati ni Afisa Uhusiano Bi.salama
Kasamalu.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ATETA NA WAFANYABIASHARA MKOA WA ARUSHA,WAAHIDI KUUNGA MKONO SERIKALI

February 25, 2016

 
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango akizungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Arusha leo katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa na kuwakumbusha wajibu wao kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu na Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja.
Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja akijibu hoja za wafanyabiashara mkoa wa Arusha huku Waziri wa Fedha na Mipango,Philip Mpango akifatilia kwa makini . 
Mfanyabiashara wa Usafirishaji ambaye ni Katibu wa Wamiliki wa magari ya abiria mkoa wa Arusha na Kilimanjaro(AKIBOA)Roken Adolf akiuliza maswali na kutoa maoni ya wanachama wenzake.
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha nguo na bidhaa mbalimbali cha A to Z,Anuj Shah akizungumza namna mlolongo wa nyingi unavyowakera wawekezaji wa ndani.
Mkurugeni wa taasisi kilele inayohusika na kilimo cha mbogamboga na matunda ya TAHA,Jackline Mkindi aliiomba serikali kuweka mazingira mazuri na kupunguza kodi ili kuwezesha ndege za mizigo kutoa huduma zao hapa nchi badala ya kusafirisha mazao yao kupitia nchi ya Kenya.
Mkurugenzi wa Kibo Guides and Tanganyika Wildernes Camps akizungumza kwenye mkutano huo ambao aliiomba serikali kuwabana wafanyabiashara wa utalii wanaokwepa kodi.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Ernest Kahindi,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Francis Miti na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Omary Kwaang’ wakifatilia miongoni mwa maafisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo.
Wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali waliohudhudia mkutano huo
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com,Arusha
ACTIONAID NA NORAD WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA UBORESHWAJI ELIMU NCHINI

ACTIONAID NA NORAD WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA UBORESHWAJI ELIMU NCHINI

February 25, 2016
IMG_3912
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog).
Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu.
Alisema ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya shule ya msingi ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa kupata elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.
“Elimu bora inataka kuwepo kwa uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa kila jambo kama ni uniform, kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na mengine yote yatimizwe,
“Ukitaka elimu bora lazima ujue inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka kuongeza fursa kwa wanafunzi kwa kuanzia shule za msingi na zaidi tunaangalia vijijini,” alisema Dkt. Lwaitama.
Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ana furaha kuona mradi huo unafanyika kwa maendeleo ya baadae ya Tanzania.
Alisema Norway itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini katika kusaidia vijana kupata elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya ufundi ili kuweza kuongeza wasomi ambao watasaidia ukuaji wa uchumi nchini.
“Nina furaha kuona mradi ambao utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae kwa Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na ushirikiano wa Norway na Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na Tanzania inaushirikiano mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.
Kwa upande wa Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alisema kupitia Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2) inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kujielimisha na kusoma ngazi zote za elimu hadi anapoamua kuacha kuendelea kusoma na hivyo mradi huo utasaidia watanzania kupata haki yao ya kikatiba.
Mradi huo unataraji kufanyika katika wilaya za Kilwa na Singida na utakuwa wa miaka mitatu ambao unataraji kuzifikia shule 60, 30 kwa kila wilaya.
Aidha unataraji kuwafikia wanafunzi wa kiume 7,758 na wakike 8,474 kwa wilaya ya Singida na Kilwa kuwafikia wanafunzi wa kiume 6,607 na wakike 6,546 lakini pia walimu 287 kwa Singida na 290 kwa Kilwa.
IMG_3943
Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
IMG_3946IMG_3953
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ActionAid, Josaphat Mshighati akitoa maelezo kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
IMG_3957Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
IMG_3963
Mshereheshaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Jovina Nawenzake akisherehesha wadau wa sekta ya elimu waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_4012
Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akielezea kuhusu sera ya elimu inayotumika nchini na mipango waliyonayo ili kuiboresha zaidi.
IMG_4016
Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akielezea kuhusu haki ya elimu kwa watanzania.
IMG_4037
Samwely Mkwatwa kwa niaba ya AAT akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia ukujuaji wa elimu Tanzania.
IMG_4043
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.
IMG_4084
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization). Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.
IMG_4097
Baadhi ya wahuzuriaji waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization) iliyoandaliwa na Shirika la ActionAid.
IMG_4116
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akizindua taarifa kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
IMG_4121
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akimkabidhi taarifa ya mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
IMG_4124 IMG_4127
Kwa pamoja wakionyesha taarifa hiyo kwa wahudhuriaji wa warsha hiyo.
IMG_4147
Watekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), wakisaini mikataba na mwongozaji wa mradi huo.
IMG_4158
Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Patrick Ezekiel akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia kuinua elimu nchini.
IMG_4168
Mratibu Mkuu wa TEN/MET nchini, Cathlee Sakwambo akitoa neno la ufungaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
IMG_4182
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.