January 05, 2014

Sunday, January 5, 2014

AZAM YAFUZU ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA TUSKER 1-0

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kuwa timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali za Kombe la Mapinduzi, baada ya usiku huu kuifunga Tusker ya Kenya bao 1-0, katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
 Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche baada ya kuchukua pasi ya Waziri Salum.
Mfungaji wa bao pekee la Azam leo, Kipre Tchetche akimtoka beki wa Tusker anayejaribu kulala kuokoa mpira
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Kipre Tchetche kulia baada ya kufunga bao muhimu leo Amaan

Tusker ndiyo waliouanza mchezo huo kwa kasi na kupeleka mashambulizi langoni mwa Azam kwa takriban dakika 10, lakini baada ya hapo vijana wa Joseph Marius Omog wakazinduka na kuanza kuwapeleka Wakenya.

DULLAH WA MICHANO SASA KAZI MOJA.

January 05, 2014
WASANII WANAOUNDA KUNDI LA AKILI MUSIC TEAM WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA LEO,DULLA WA MICHANO,MORRIS,D.DOCTOR,VALENTAIN,KIDANI,MWANDEI, DAN TOUCH PRODUCER,JOJO,SMART BUSINESS NA TSETSEFLY.
MSANII DULAH WA MICHANO WA TATU KUTOKA KUSHOTO AKIFURAHIA JAMBO NA WASANII WENZAKE MARA BAADA YA KUMALIZA KUREKODI WIMBO WAO MPYA LEO.
January 05, 2014

STEVE NYERERE AWA MWENYEKITI MPYA WA BONGO MOVIE

IMEWEKWA JANUARI 6.

  Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu Mwenyekiti wa Bongo Movie,Dk Cheni akiwashukuru wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama hicho

Katibu Mkuu wa Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.

DULLAH WA MICHANO:TUMEPANIA KUENDELEZA MZIKI WA BONGO FLEVA MKOANI TANGA.

January 05, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Mkoani Tanga,Ally Khamisi "Dullah wa Michano"apania kuendelea mziki wa kizazi kipya mkoani hapa kwa kuwakutanisha wasanii hao lengo likiwa kuinua vipaji vyao.

Dulla wa Michano (Pichani Juu)alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na TANGA RAHA ambapo alisema bila jitihada na sapoti kubwa kwa wasanii ikiwemo kushirikiana mziki huo hauwezi kufika mbali hivyo lazima wasanii wakubali kuwa na mshikamano ili kuweza kuleta mapinduzi katika tasnia hiyo.


Michano ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake  "NAZEEKA"aliomshirikisha  kaka yake SELLE wa MICHANO amsema ana matumaini makubwa utafanya vizuri kama nyengine zilizopita ambavyo pia zinaendelea kuubamba mziki wa bongo fleva hapa nchini.

Wimbo huo aliurekodia kwenye studio za DIVA TALENT inayomilikiwa na MESEN SELECTA ambapo ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimemtambulisha sana kwenye mziki huo ambao umeonekana kuwa na wapenzi wengi hapa nchini.

Akizungumzia mziki huo,alisema mziki wa bongofleva unalipa kilichobakia ni watu kuwa makini na kujitambua wanapaswa kufanya nini ili kuweza kuendana na ushindani.

 "Kama unavyojua mziki wa sasa unalipa tofauti na miaka ya nyuma hivyo wasanii wanapaswa kutumia umakini mkubwa hasa wakati wanapokuwa wakitunga mashairi yao na sio kukurupuka kitendo ambacho kinawapeleka kushuka badala ya kupiga hatua za kimaendeleo "Alisema Dulla wa Michano.

Aidha aliwataka watangazaji na watayarishaji wa mziki huo kuwapa nafasi wasanii wachanga ili nao waweze kuonyesha vipaji vyao badala ya kuwabania kwani kufanya hivyo kunapeleka kushuka mziki huo.
January 05, 2014

BOBAN ARIPOTI COASTAL UNION TANGA.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Coastal Union yenye maskani jijini Tanga, Haruna Moshi ‘Boban’, ameripoti mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanzania Bara.

Haruna Moshi Boban pichani.
Kuripoti kwa Boban kunashusha presha kutoka kwa wadau wa timu hiyo wanaosema kuwa kiungo huyo amekuwa mtovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti kambini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa timu ya Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa Boban aliafiki kujiunga na wenzake mapema wiki hii ili kuendelea na mazoezi ya pamoja.

DC DENDEGO AONGOZA BONANZA LA KUKUZA VIPAJI JIJINI TANGA.

January 05, 2014
 Na Burhan Yakub,Tanga.
Vijana wa mjini hapa jumamosi walionyesha vipaji vyao vya uchezaji michezo mbalimbali, uimbaji ,uchezaji muziki na kuendesha
pikipiki katika bonanza la kukuza vipaji lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi  Majani Mapana Jijini Tanga.

Bonanza hilo lililoratibiwa na diwani wa kaya ya Nguvumali,Selebosi Mustafa ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima
Dendego lilifanyika kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ambalo kwa mujibu wa melezo ya Selebos itakuwa ikifanyika kila jumamosi kwa kipindi cha miezi sita mfulizo ilikuwa ni soka ambayo zilichezwa mara tano,netboli nne,mchezo wa wavu mara tatu,kuvuta kamba wanawake na wanaume na kufukuza kuku.

BREAKING NEWS: BOTI YA MV KILIMANJARO II KUTOKA PEMBA KUELEKEA UNGUJA YANUSURIKA KUZAMA

January 05, 2014
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema boti ya Kilimanjaro 2 iliyokuwa ikitoka Pemba kuelekea Ugunja inasemekana imepingwa na dhoruba kali na kunusurika kuzama, inadaiwa kuna vifo vimetokea. 
 
Ukweli ni kwamba wimbi kubwa liliipiga boat na kusababisha hali ya tafrani. Nimetoka kuongea na mamlaka ya bandari sasa hivi na boat iko njiani inakuja unguja iko maeneo ya Beit ras sasa hivi. Haijazama  na iliondoka na abiria watu wazima 269, watoto 60 na mabaharia 8 wote wako salama.

Wimbi kubwa liliipiga likachukua mabegi na baadhi ya life jackets. Injini za boat zilizima, ilibidi watulie kwa muda kuona kama wimbi lilichukua na baadhi ya abiria lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeachwa.

Nakumbuka mamlaka ya hali ya hewa walitoa tahadhari kuhusu mchafuko wa bahari hizi siku.
 
Tunamshukuru mungu kwa kuepusha hili janga.

CHANZO: JAMII FORUM NA CLOUDS FM
January 05, 2014

*RAIS KIKWETE AFUNGUA HOSPITALI YA KMKM KIBWENI, ZANZIBAR JANA
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar jana Desemba 4, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar.
Askari wakakamavu wa kike wa KMKM wakiwa wamesimama kumlaki Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alipowasili kwa a ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar. PICHA NA IKULU