WAZIRI MBARAWA ALITAKA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI KUAANISHA GHARAMA ZA UJENZI WA MIRADI YAO

September 22, 2017
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku moja ya wadau wa sekta ya ujenzi iliyohusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam jana.

RAIS DK. SHEIN AFUNGUA WA MSIKITI MASJID JAAMIU ZINJIBAR -MAZIZINI

September 22, 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono Waislamu mbali mbali alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo,sambamba na  Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,"Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science" ambao   umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,"Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science" Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali  mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofuatana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,"Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science" wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Msikiti Masjid Jaamiu  Zinjibar baada ya kuufungua rasmi leo,ambao  umejengwa Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,"Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science" Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami wakati alipotembelea sehemu mbali mbali mara alipofungua Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea Shahada na Ufunguo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,"Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science" Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Msikiti Masjid Jaamiu  Zinjibar leo uliojengwa kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman katika maeneo ya Mazizini Wilaya Magharibi 'B" Mkoa wa Mjini Magharibi.

IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

September 22, 2017
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.


Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia), akifafanua jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa (aliyesimama), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji Majenzi na Msanifu Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.

Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.

“Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.

Ameongeza kuwa mapendekezo yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji wa miundombiu mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine zikiwemo za kilimo, nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa biashara na nchi nyingine za kikanda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ongezeko la miradi ya ujenzi imechangia Serikali kutafuta wataaalm waliofanya tafiti kwa ajili ya uboreshaji wa baraza hilo wataongeza tija na ufanisi wa sekta hii muhimu ya ujenzi kwa wadau, wananchi na Serikali.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la NCC  Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.

Sekta ya Ujenzi ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina mchango mkubwa kwa Pato la Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia asilimia 14 ya Pato la Taifa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MPINA AAGIZA KIWANDA CHA UNGA WA NGANO CHA AZANIA KUFANYA VIPIMO VYA VUMBI LA LITOKALO KIWANDANI HAPO

September 22, 2017
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akikagua mfereji wa maji katika kiwanda cha Chemi Cotext kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la kiwanda cha unga wa ngano cha Azania kilichopo Ubungo jijini Dar Es Salaam.

NA; EVELYN MKOKOI  - DAR ES SALAAM

Akiendelea na ziara yake ya ukaguzi na utekelezaji wa sheria ya Mazingira jijini Dar es Saalaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameagiza Baraza la taifa la Usimizi wa Mazingira NEMC kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa Ngano wa Azania, kupima kiwango cha ubora wa hewa inayoambatana na vumbi la unga wa ngano linalotoka kiwandani hapo baada ya shughuli za uzalishaji  na kwenda kwenye mazingira na makazi ya watu kana vinakidhi viwango vya kimazingira.

Mpina alisema kuwa baada ya matokeo hayo  yanayotegemewa kutoka baada ya wiki mbili, serikali ndiyo itakuwa kwenye hatua ya kusema jambo kwa wananchi pamoja na kiwanda.

“Baada ya matokea hayo sasa serikali inaweza kuwa na nafasi ya moja kwamoja kuchukua hatua kwa mwenye kiwanda ikiwa ni pamoja na kukitoza faini kwa mujibu wa sheria, na kama matokeo ya vumbi na kelele zitokazo kiwandani hapo yatakuwa ndani ya kiwango, sasa hatua itakayofuata ni yakuangalia mahusiano kati ya mwenye kiwanda na wakazi majirani wa eneo hilo. Alisema Mpina.”

Aidha Mpina aliongelea kufaanyika kwa taratibu za kujua kama suala la kiwanda hicho kuwa karibu na makazi ya watu ,  ni sahihi na kwa upande wa wananchi kuwa karibu na kiwanda  hususan kuwepo kwa nyumba kila baada ya hatua moja nalo ni sahihi.

Awali katika muendelezo wa ziara yake ya ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira jijini Dar es Salaaam, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Chemi  cotex kilichopo Mbezi Beach.

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI LA KAMPUNI YA MABATI ALAF DODOMA

September 22, 2017
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF  Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji  (roofing) wa Kampuni ya mabati  ALAF, Dipti Mohanty  akishuhudia ufunguzi huo.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148.

Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali  kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo  na  kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”.

Kufunguliwa kwa tawi hili  kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani.

Wateja kutoka Dodoma na Singida  sasa wataweza  kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF.

Tunauza  bidhaa zilizo tayari kwa matumizi kulingana na mahitaji ya mteja hasa mabati ya rangi  pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi na kiutaalamu.

Kwa sasa kiwanda chetu cha ALAF kina matawi manne Mbeya, Mwanza, Arusha na Dodoma.

Kuhusu kampuni ya ALAF
Kampuni ya ALAF ni sehemu ya kampuni ziliyoko chini ya Kampuni   ya SAFAL, kampuni inayoongoza bila mpinzani ktika utoaji wa bidhaa bora za uezekaji barani Afrika.Kampuni ya SAFAL inaendesha shughuli zake katika nchi 13 kuanzia mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

Tukiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika biashara, ALAF tunaongoza  katika uzalishaji  wa bidhaa za  uezekaji za chuma.Katika kuongezea bidhaa zake za upauaji, bidhaa za kitaalamu pia zinauzwa na ALAF kama misumari (fixtite fastener), steel pipes, na Hollow section pamoja na viambatanisho muhimu kwa uezekaji.

Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.
Wasilana nasi kwa namba hizi  Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560,  Dodoma - 0764 131442  na Mwanza 0682 808 080. 

Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited

WAFANYAKAZI WASHAURIWA KUPIMA AFYA MARA BAADA YA KUSTAAFU

September 22, 2017
Na: Lilian Lundo – MAELEZO Dodoma.

Wafanyakazi nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Eric Shitindi alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo Mjini Dodoma.

“Kumekuwa na mazoea kwa wafanyakazi kupima Afya pale tu wanapoajiriwa na kutotilia maanani upimaji afya zao mara wanapostaafu ili kujua ikiwa kazi wanazozifanya zimewaathiri kwa kiasi gani,” amesema Shitindi.

Ameendelea kwa kusema kuwa, upimaji wa afya mara baada ya kustaafu utasaidia watumishi kujua afya zao na ikiwa watakuwa wameathirika upitia kazi walizokuwa wakizifanya basi mwajiri atawajibika mkulipa fidia mtumishi huyo.

Aidha amesema kuwa licha ya juhudi za Serikali katika kusimamia Usalama na Afya maeneo mengi ya kazi sio ya kuridhisha kutokana na waajiri wengi kutokuzingatia sheria na kanuni mbalimbaliza Usalama na Afya.

Hivyo basi kutokana na waajiri hao kutofuata sheria na kanuni hizo kumesababisha maeneo mengi ya kazi kulalamikiwa kutokana na ukiukwaji wa sheria hizo.

Vile vile amesema kuwa baadhi ya waajiri na wafanyakazi wana uelewa mdogo  kuhusu kuzingatia maelekezo ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ikiwemo matumizi sahihi ya vifaa kinga.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema kuwa, wameamua kuandaa semina hiyo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini ili na wao wakatoe elimu hiyo kwa wafanyakazi wote nchini kutokana na wafanyakazi hao kutokuwa na uelewa mzuri juu ya masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ambapo aliwashauri wafanyakazi nchini kupima afya mara wanapostaafu ili kujihakikishia kama hawajaathirika na kazi walizokuwa wanafanya.Katikati ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule na Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda 
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule akiongea naViongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi, kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi na kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule (KUSHOTO) na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Jones Majura(KULIA) wakiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi baada ya ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi leo Mjini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma. PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO,DODOMA
CRC yazinduwa mradi wa utoaji huduma za msaada wa kisheria

CRC yazinduwa mradi wa utoaji huduma za msaada wa kisheria

September 22, 2017

Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo. 
Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.  
Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam. 
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada. 

KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni na Ubungo. 

Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria, mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa na kupungua.

 Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. 

Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri. "...wadau katika maeneo hayo mnatakiwa kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru," alisema Bi. Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao. 

Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye Kata ya Saranga. Alisema CRC itashirikiana na wadau katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru.  
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga). 
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga). 
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi Bi. Saida Mukhi. -- ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

TCRA WAENDESHA WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI NA KUZINDUA KAMPENI YA KUSISITIZA MATUMIZI BORA YA MITANNDAO YA KIJAMII-AWAMU YA PILI

September 22, 2017
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe akifungua rasmi warsha ya vyombo vya Habari Mtandaoni iliyo wahusisha Blogu na 'Online Tv' katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
 Bw. Thadeus Lingo kutoka TCRA akiendesha mada kuhusu Matumizi Salama ya Mitandao ya Kijamii
 Mwakilishi wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Maxence Melo akiwasilisha mada juu ya Maudhui ya Mtandaoni na Changamoto zake.
 Mratibu Msaidizi wa Polisi Joshua Mwangasa akitoa mada juu ya Hali ya Usalama Mtandaoni

 Mzee Abdul Ngarawa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka TCRA akitoa neno la Busara wakati wa warsha hiyo ambapo alisisitiza kuzingatia uzalendo umuhimu wa kutazama utu na staha ya mtu
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (Kushoto) akiongoza majadiliano kwa ujumla ambapo wadau walichangia mawazo na kuuliza maswali mbalimbali
Bwana Daniel Mbega Mmiliki wa Blogu ya Maendeleo Vijijini akichangia mawazo yake wakati wa warsha hiyo

 Bw. William Malecela Maarufu kwa jina la Le Mutuz mmiliki  Blogu ya Wananchi na Le Mutuz Tv Onine akichangia mambo mbalimbali na kutoa maoni yake wakati wa Warsha hiyo
 Mwenyekiti wa  Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Joachim Mushi (kulia) akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya waendesha wote wa mitandao kwa TCRA kuendesha warsha hiyo
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba pamoja na wadau wengine wakizindua Rasmi Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii awamu ya Pili ambapo Kauli mbiu inasema "Usinitumie Sitaki na Simtumii Mwengine Nitakuripoti"
 Baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. ValerieNdeneingo-Sia Msoka akitoa neno la kufunga wakati wa Warsha hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania

Na. Paschal Dotto-MAELEZO.
Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasiliano kwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzania kupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi uliobora.

Haya yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas Kilimbe  alipokua akihutubia hadhara ya wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii”  iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Katika hafla hiyo, Dkt. Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya mitandao kuwa makubwa.

“Sekta ya mawasiliano kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema Dkt.Kilimbe.

Aidha Dkt.Kilimbe alisema kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.

“Tuna jukumu zito na ni kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyo waandishi mitandaoni tumieni weledi  mkubwa kwa habari za maendeleo.”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.
Dkt.Kilimbe alisema kuwa katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa  kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.

Aidha Dkt. Kilimbe amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umilikajia wa vyombo hivyo kwa kuwahabarisha wananchi.

Naye mtoa mada na mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika katika kuhabarisha umma kwa njia hii.