NA MWANDISHI WETU,TANGA.
KATIBU
MKUU Kiongozi Balozi,Ombeni Sefue amewaonya watumishi wa serikali wenye tabia ya
kudanyanga katika masuala mbalimbali yakiwemo ya malipo madai yao kwa kuwataka
kuacha mara
moja kwani watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Sefue alitoa
wito huo wakati wa mkutano wake na watumishi wa sekretarieti ya mkoa na
taasisi za serikali mkoani Tanga ambapo alisema kuwa wapo baadhi ya watumishi
ambao wanafanya udanganyifu baada ya kulipwa madai yao na baadae kudai tena jambo
ambalo linaleta usumbufu mkubwa .
Amesema mara
nyingi watumishi hao wamekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa kuidanganya
serikali kwa kutaka kulipwa madai ambayo tayari yalikwisha kulipwa na mamlaka
husika hivyo kabla wao hawajafanya hivyo watashughulikiwa ili kuweza kukomesha
tabia hiyo.
“Tunashangaa sana tabia za baadhi ta
watumishi ambao sio waaminifu hasa katika masuala ya malipo kwa kudai mara
mbili licha ya kulipwa hivyo nataka niwaambie acheni mara moja jambo hilo kwani
mtakaobainika mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo “Alisema Sefue.
Akizungumzia
suala la watumishi wa serikali kujiingiza katika masuala ya siasa,Sefue alisema
watumishi wa kada hizo hawapaswi kufanya hivyo ikiwemo kuwaonya kuacha kufanya
hivyo mara moja kwa sababu watakuwa wamekiuka taratibu zilizopo kisheria.
Badala
yake aliwataka wafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na serikali iliyopo
madarakani lengo likiwa kuharakisha kasi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali
hapa nchini .
“Kama kuna watumishi wa serikali wanataka
kujiingiza kwenye siasa ni bora wakachagua moja waache kazi na kuendelea siasa
kwa kufuata taratibu zilizopo kisheria kwa sababu hawawezi kuchanganya vitu
viwili kwa wakati mmoja “Alisema Katibu Kiongozi.
Alisema
jambo hilo linasababisha wakati mwengine kuchukua muda mrefu kujiridhisha ili
kuweza kujua madai yaliyopo yaweze kulipwa badala ya kupokea madai na kulipa
kwa wakati kutokana na vitendo vya baadhi yao kufanya udanyanyifu kutokana na
kutaka kulipwa madai mara mbilimbili.