TUTAENDELEZA UTALII WA PICHA KATIKA PORI LA AKIBA BURIGI - DK. KIGWANGALLA, WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

March 02, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Twiga katika fukwe za ziwa Burigi ndani ya Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera.
Baadhi ya Twiga wanaopatikana katika Pori la Akiba Burigi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Malmlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata kuhusu mipango mbalimbali ya mamlaka hiyo kuendeleza utalii katika Pori la Akiba Burigi alipotembelea pori hilo jana mkoani Kagera.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari fukwe ya ziwa Burigi kwa kutumia darubuni alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka ngazi kwa ajili ya kukagua fukwe za ziwa Burigi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki kusukuma boti iingie kwenye maji kwa ajili ya kunza ziara ya kukagua fukwe za ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga kasia tayari  kwa kwa kuanza Safari ya boti kwa ajili ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. 
Ndege aina mbalimbali pia ni kivutio katika pori hilo.
Viboko nao wanapatikana katika pori hilo ndani ya ziwa Burigi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti baada ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti baada ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi.
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na watumishi wa Pori la Akiba Burigi.
Picha ya pamoja. (Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Malisili na Utalii)

MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO NA TATO WAAZIMIA KUSHIRIKIANA KUKUZA UTALII NCHINI

March 02, 2018


Katibu Mtendaji wa TATO, Siriri Akko akichangia mada katika kikao kazi hicho juu ya maazimio ya kuondoa kero na changamoto wakutanazo watoa huduma za utalii nchini


Katibu Mtendaji wa TATO, Siriri Akko akiainisha baadhi ya changamoto wanazokutana nazo wanachama wa TATO katika hifadhi ya Ngorongoro na kuomba uongozi wa NCAA kuwaondolea kero hizo ili kukuza utalii nchini na wanaomsikiliza kwa makini ni naibu mhifadhi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Assangye Bangu nabaadhi ya  viongozi wa NCAA kutoka idara ya uhasibu na teknolojia ya mawasiliano 


naibu mhifadhi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Assangye Bangu kushoto akizungumza na mwanachama wa chama cha mawakala wa utalii mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika hotel ya NEW ARUSHA.

Add caption

Baadhi ya wadau na wanachama wa cham cha mawakala wa utalii yaani Tanzania Association of Tour Operators wakimsikiliza kwa makini naibu mhifadhi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Assangye Bangu juu ya suluhisho la changamoto zilizopo geti kuu la kuingia hifadhi ya Ngorongoro



Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Chama cha Mawakala wa Utalii(TATO), wamefikia makubaliano ya  kuondoa vikwazo baina yao na hivyo kushirikiana katika kukuza utalii hapa nchini.

Makubaliano hayo, yalifikiwa jana katika kikao  kazi kilichofanyika Arusha katika hotel ya New Arusha,   baina  viongozi NCAA,TATO na  Kampuni za Utalii  ambazo hivi karibuni zilitajwa kuwa huenda zingezuiwa kuingiza watalii katika hifadhi ya Ngorongoro.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu mhifadhi wa NCAA anayeshughulikia Huduma za Shirika  Asangye Bangu alisema,NCAA imejipanga kuboresha huduma kwa watalii na kuondoa changamoto zinazowakabili wenye makampuni ya Utalii.

"Kikao chetu kimekwenda vizuri, NCAA tutaendelea kuboresha mifumo ya malipo, kuboresha mawasiliano baina yetu na mawakala wa utalii lakini pia kutatua changamoto kadhaa, ikiwepo barabara ndani ya hifadhi"alisema

Alisema katika kukabiliana na kero ya barabara, NCAA inatarajiwa mwezi wa nane mwaka huu, kuanza ujenzi wa barabara ya kutoka geti la kuingia Ngorongoro hadi geti la kuingia Serengeti yenye urefu wa kilomita 83 kwa kuweka tabaka gumu juu.

"hii ni kero ya muda mrefu ya makampuni ya Utalii lakini sasa Shirika la umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO)limetukubalia kuijenga barabara hii na ikikamilika tunaimani barabara itadumu kwa zaidi ya miaka 40"alisema

Awali Katibu Mtendaji wa TATO, Siriri Akko alisema, katika siku za karibuni kuliibuka taarifa za kuwachanganya baadhi ya wanachama wao juu ya kuzuiwa kuingia ngorongoro kupeleka watalii.
Hata hivyo, alisema baada ya kupata maelezo kutoka NCAA wamefikia makubaliano ambayo lengo lake ni kuboresha sekta ya utalii nchini na pia kuondoa changamoto zinazowakabili.
"kikao chetu kimekwenda vizuri na ile hofu ya kampuni kuzuiwa sasa haipo na tunaimani kampuni zote zitafuata sheria na taratibu za kufanya biashara ya utalii hapa nchini"alisema

Akizungumza katika kikao hicho,Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii wa Shidolya, Lazaro Mafie alisema ni muhimu kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara baina ya NCAA na makampuni ya utalii ili kutatua kero.
Mafie alisema wao kama wamiliki wa makampuni ya Utalii, wateja wao ni watalii sawa na NCAA ambayo uwepo wao unategemea watalii hivyo ni lazima kuwepo na mawasiliano mazuri baina yao.
"kuna changamoto kadhaa ambazo tunakabiliana nazo lakini tunaimani sasa zitafanyiwa kazi ili kuboresha sekta ya utalii hapa nchini"alisema.

JUKWAA LA WANAWAKE SOMANGILA, KIGAMBONI, LAZINDULIWA LEO, ANGEL AKILIMALI AWATAKA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUZALISHA BIDHAA BORA KUKIDHI SOKO

March 02, 2018
Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Wanawake wajasriliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo  Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani katika soko.

Alivishauri vikundi vya wanawake wajasiriamali kwenda kuomba mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye mikopo ya riba nafuu.

Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.
 Wanawake wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kaya ya Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa uhuru FM Angel Akilimali (kulia) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Jukwaa hilo wakati wakipokea maandamano ya Wanawake wajasiriliamali kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo, leo
 Viongozi wa Vikundi mbalimbali vya Wanawake Wajasili na Jukwaa la Wanawake wakiwa tayari kupokea maandamano ya wanawake Wajasiriamali. Kushoto ni Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM angel Akilimali akipunga mikono
 Viongozi wakimwayamwaya kupokea maandamano hayo 
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.
 Diwani wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Francis Chihi (kulia) akionyesha umahiri wa kusakata muziki pamoja na Kinamama wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo, leo
 Mwanamke Mjasiriamali wa kutengeneza vifaa vya ujenzi Amina Zakumera (kushoto) akimpatia maelezo ya utaalam wake Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali (Wapili kulia) alipokuwa akikagua bidhaa za Wanawake wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wanawake wa Kata ya somangila, Kigamboni, leo 
 Angel Akilimali akipata maelezo kuhusu bidhaa za mwanamke Mjarismali  Winifrida Jafari (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somanga, Kigamboni leo. Wapili kushoto ni Mjasiriamali Joha Amour wa Joha Fashion.

 Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto)
 Angel Akilimali (kushoto) akimuuliza Mwanamke Mjasiriamali jinsi anavyotengeneza bidhaa zake.
 Angel Akilimali na Diwani Chichi wakinywa togwa kwenye banda la maonyesho la Mwanamke Mjasiriamali, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni. 
 Wanawake wajasriamali wa Kata ya Somangila wakijimwayamwaya kucheza muziki kufurahia uzinduzi wa Jukwaa lao, leo
 Mtendaji wa Kata ya Somangila Munna Msafiri akitambulisha viongozi wa vikundi mbalimbali na Jukwaa la wanawake kutoka maeneo mbalimbali
 Viongozi wa Majukwaa ya Wanawake kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Kigamboni wakitambulishwa
 Diwani wa Kata ya Somangila Ndugu Chichi akifanya harambee ya uchangiaji wa fedha kutunisha mfuko wa Jukwaa la wanawake katika kata yake.
 Mkuu wa Polisi Kata ya Somangila Mwakila Chile akizungumza baada ya kutambulishwa na Diwani Chichi
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akiungana na Wanawake wajasiriamali kusakata muziki wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akicheza ngoma na msanii wa kikundi cha Vijana wa Somangila wakati wa Sherehe hizo za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila 
 Mgeni rasmi katika Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya somangila Kigamboni Angel Akilimali akifurahia vijana walivyokuwa wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
 Kijana akiwa kihwa chini miguu juu, tena hewani wakati akicheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
 Wasani wa kikundi cha sanaa cha Vijana wa Smangila wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
 Mgeni rasmi katika sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, Angel Akilimali akinadi kiatu alipoendesha mnada wa vitu mbalimbali vya wanawake wajasriamali wakati wa sherehe hizo
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akikitazama kwa makini kiatu hicho baada ya kukubali kukinunua kwa sh 50,000
 Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo
  Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo
 Angel Akilimali akipongezwa na MC katika sherehe hizo
 Angel Akilimali akiwa na mtunza Fedha wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kigamboni Pili Doto mwishoni wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake kata ya Somangila
 Angel Akilimali (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa New Life Queen Bahati mwishoni mwa sherehe hizo
 Angel Akilimali akiwa na baadhi ya Wanawake wajasiriamali
Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la wanawake Kata ya Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Angel Akilimali akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jukwaa hilo katika kata mbalimbali za Kigamboni na Viongozi wa vikundi vya Wanawake wajasiriamali wa kata hiyo baada ya uzinduz leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO