MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAPOKEZI YA MWILI WA SPIKA MSTAAFU MHE. SAMUEL SITTA

November 10, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Jeneza lenye mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta likiwa limebebwa na askari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan pamoja na  Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji akimfariji Mama
Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi na wananchi  katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini  Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.
 
Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa limeondokewa  kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi
wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi
utendaji wake.
Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya
Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga  na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baada ya
Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini leo mchana amepelekwa
nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho asubuhi viongozi na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika viwanja wa Karimjee jijini

WAZIRI KAIRUKI AKABIDHIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA KITAIFA YA KUJENGA NA KUKUZA MAADILI

November 10, 2016

                       Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG),Profesa Mussa Assad ,amesema kuwa kwa kipindi cha miaka kumi hadi kumi na tano iliyopita hapa nchini watanzania wengi wamekuwa waongo, hali iliyochangia kuongeza kwa ukosefu wa maadili.
Profesa Assad ameyasema hayo alipokuwa anafunga mkutano wa wandishi wa habari juu ya masuala ya maadhimisho ya siku ya maadili na utawala bora yatakayofanyika Desemba 10 mwaka huu.
“Ndani ya miaka 10 hadi 15 sasa,Watanzania wengi wamekuwa waongo sana kiasi cha kupoteza maadili na uaminifu kwani swala hili la uongo limeshamiiri sana katika matumizi ya simu kiasi cha kuathiri utendaji wetu wa kawaida katika kazi za kila siku”amesema Profesa Assad.
Amesema kuwa hata vyombo vingi vya habari hivi sasa vimeingia katika mpango huo wa kuongopa kwa kushindwa kuandika habri za kina na zilizofanyiwa utafiti ambao unatoa ushahidi wa moja kwa moja kwa jambo linalo andikwa.
 Amemaliza kwa kusema kuwa ni  vyema watu wakaanza kupunguza uongo kwenye simu na Maisha yao ya kila siku hili kuishi Maisha halisi yatakayowezesha kupunguza uovu 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akitoa utambulisho kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (katikati) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama Nyanduga.
Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama Nyanduga. akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC aomboleza msiba wa Spika Sitta

November 10, 2016


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri, Marehemu Samuel Sitta nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam leo.Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo ukitokea nchini Ujerumani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akisalimia na mmoja wa watoto wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri Marehemu Samuel Sitta baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu kutoa pole ya msiba huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri, Marehemu Samuel Sitta
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akisalimiana na mmoja wa waombolezaji wa msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri, Marehemu Samuel Sitta.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri, Marehemu Samuel Sitta.Picha na Hussein Makame, NEC

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE JOSEPH MUNGAI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

November 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ardhia Mhe. William Lukuvi alipowasili kuongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaamleo Novemba 10, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe.Isaya Charles Mwita alipowasili kuongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaamleo Novemba 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa alipowasili kuongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaamleo Novemba 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa alipowasili kuongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaamleo Novemba 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Kate Kamba  alipowasili kuongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaamleo Novemba 10, 2016
  Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Mze Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva na Mama Salma Kikwete leo Novemba 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Mze Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi John Kijazi 
  Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 10, 2016
  Sehemu ya waomboleszaji na wana familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 10, 2016

PAC YAISHAURI SERIKALI KUANZISHA MFUKO WA UWEKEZAJI.

November 10, 2016


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeishauri Serikali kuanzisha mfumo maalum wa uwekezaji ili fedha zitakazowekwa katika mfuko huo zitumike kama mtaji katika maeneo ambayo nchi inataka kuwekeza.

Ushauri huo umetolewa mjini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati hiyo iliyochambuliwa kwa kina juu ya changamoto, maombi na mapendekezo yatakayoiwezesha nchi kusonga mbele.

Mwenyekiti Mhe. Kaboyoka amesema kuwa ushauri huo umetolewa baada ya kukwama kwa baadhi ya miradi pamoja na shughuli nyingine za Serikali zinazofanywa ili kuwasaidia wananchi kutokana na ukosefu wa fedha za kufanyia shughuli hizo hivyo kuanzishwa kwa mfuko huo kutahakikisha faida ya uwekezaji inaonekana.

“Sisi kama kamati tunaishauri Serikali kuanzisha mfuko maalum wa uwekezaji kwani utaisaidia Serikali kupata fedha za kufanyia maendeleo na kupata mitaji ya kuwekeza sehemu mbalimbali ili kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa na watanzania wanaiona faida ya uwekezaji”, alisema Mhe. Kaboyoka.

Mhe. Kaboyoka aliongeza kuwa kamati hiyo imependekeza kuwa mfuko huo uanzishwe chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kutumia mfumo wa kubakisha mapato kwa sababu ofisi hiyo ndiyo ina mamlaka ya kugawa fedha za Serikali kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Aidha, taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imebaini kuwa pamoja na kuwa Idara ya Uhamiaji imeweka usimamizi wa utoaji wa viza katika Makao Makuu ya Idara, kwenye Balozi pamoja na maeneo ya mipaka ya nchi lakini mfumo wa kutoa viza kwa wageni wanaowasili nchini hauna mawasiliano mazuri.

Kukosekana kwa mawasiliano hayo kunasababisha mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali yanayotakiwa kukusanywa kutokana na utoaji wa viza hivyo kamati pia imeiomba Serikali kukamilisha haraka mradi wa Uhamiaji Mtandao (E- Migration) ili kuboresha njia za ukusanyaji wa mapato katika Idara hiyo.

Kwa upande wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliyowasilishwa Bungeni hapo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vedasto Ngombale Mwiru ambaye ameelezea matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Umma katika Serikali za Mitaa pamoja na ushauri wa kamati hiyo katika kuhakikisha tatizo hilo linakoma.

Mhe. Ngombale Mwiru ameeleza kuwa Kamati imebaini udhaifu wa watendaji wa Halmashauri mbalimbali nchini katika usimamizi wa mikataba ya utekelezaji wa maendeleo unaopelekea miradi hiyo kuchelewa kukamilika, kukamilika kwa kiwango cha chini au kutokukamilika kabisa.

“Kulingana na taarifa hiyo, kamati imezishauri Halmashauri zote nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili iweze kukamilika kwa wakati na kutumika kama ilivyo kusudiwa”, alisema Mhe.Ngombale Mwiru.

Ameongeza kuwa kumekuwa na tatizo katika Halmashauri hizo la kutotenga asilimia 10 ya fedha za mapato kutoka katika vyanzo vya ndani kwa ajili ya mfuko wa wanawake na vijana ambapo kuna baadhi ya Halmashauri hazijawasilisha michango hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu.

Kutokana na tatizo hilo, Kamati imetoa agizo kwa Halmashauri zote kuandika barua ya kuthibitisha kulipa madeni hayo pia kuelezea mipango watakayotumia katika kutekeleza ulipaji huo.

Pia Kamati imeishauri Serikali kuleta Bungeni Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Maendeleo ya wanawake na vijana ili iwe sheria ambayo itatekelezwa kwa lazima hivyo kuendelea kuinua maisha ya wanawake na vijana kama ilivyokusudiwa.

Baada ya kamati zote mbili kuwasilisha taarifa hizo mbele ya Bunge,sasa ni zamu ya wabunge kujadili kwa kina masuala yaliyozungumziwa katika taarifa hizo kwa kutoa maoni yao na kuishauri Serikali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza katika matumizi ya fedha kwa kuyapatia ufumbuzi ili yasijirudie katika taarifa zijazo.
BOT YASITISHA KUWEKA DHAHABU KAMA HAZINA YA RASILIMALI ZA KIGENI.

BOT YASITISHA KUWEKA DHAHABU KAMA HAZINA YA RASILIMALI ZA KIGENI.

November 10, 2016
jiatu
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
 
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.
 
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.
 
Mhe. Kijaji amesema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.
 
“Katika kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.
 
Naibu Waziri huyo ametoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.
  
Mhe. Kijaji amefafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.
 
Aidha, Mhe. Kijazi amesema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo.

MOTO MKUBWA WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

November 10, 2016
Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.
 Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari
 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa 
Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika
 Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa.
Baadhi ya wataalam wa kuzima moto wakiwa wanaendelea na juhudi za kutazama maeneo ambayo moto unawaka zaidi ili kuuzima
 Moja ya Gari la zima moto likiwa linawahi eneo la Tukio kusaidia kuzima moto
Zima moto wakiendelea na shughuli ya kuhakikisha moto unazimika katika Bohali hilo
 Moto ukiendelea kuteketeza Bohari hilo lililokuwa la kuhifadhia mataili
 Pamoja na watu kupewa tahadhali ya Moto mkubwa uliokuwa unawaka lakini bado walikuwa wakiongezeka kushuhudia tukio hilo.
 Katika juhudi za kuhakikisha moto huo unazimika kabisa magari ya kila aina yanayobeba maji yalichukuliwa kuongeza nguvu za kuzima moto huo.
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa kabisa katika eneo ambalo moto ulikuwa unawaka
 Mmoja wa wafanyakazi wa Bohari hilo Shaban Salum akielezea kwa ufupi kile alichokiona wakati moto huo unaanza kuwaka mida ya saa sita mchana
 Magari ya zimamoto na mengine ambayo ni ya kubebea maji yakiwa katika eneo la Bohali la 7 General kuhakikisha wanashirikiana kumaliza moto huo
 Umati wa watu  wakiwa katika eneo hilo la Bohari wakiendelea kushuhudia Tukio hilo
 Watu wengine wakiwa wamekaa Jirani kabisa na Moto huo bila wasiwasi wakishuhudia tukio hilo la Moto.

Taarifa kamili itakuja kutoka Jeshi la Polisi

Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za mikoa

DC CHUNYA AAGIZA TOZO ZOTE ZA VIJIJI NA MALISASILI KUINGIZWA KATIKA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI

November 10, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa


Na Mwandishi wetu,Chunya

Mkuu wa Wilaya ya Chunya  Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na zinaonekana kwenye taarifa ya mapato na matumizi.

Aidha ameitaka halmashauri kuingiza  takwimu halisi za mazao yote yanayo toka katika maeneo ya vijiji husika.

Agizo hilo, amelitoa leo  baada ya kutembelea  na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazoendelea katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha shilingi milioni 900.

Amesema, licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia kubwa  ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi ipasavyo kutokana na kukithiri kwa njia za panya.

“Serikali inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo kwa  mfumo bora wa ufutiliaji wa mazao hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika Wilaya na halmashauri yenyewe,”amesema.

Hata hivyo, amesema nguvu kubwa iliyopo sasa ni kudhibiti njia zote za panya hasa katika eneo la Shoga ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na wafanyabiashara wasio waaminifu.