SIMBA SC YAMNASA ELIAS MAGURI KUTOKA RUVU SHOOTING

July 31, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

KLABU ya Simba sc imemalizana na klabu ya Ruvu Shooting kuhusu kumsajili mshambuliaji wa maafande hao, Elias Maguri .
Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema wakati wa sikuu ya Eid El Fitri, Simba walipeleka ofa, wakakaa pamoja na kujadili na hatimaye kufikia makubaliano.
“Simba wamefuata taratibu zote, wamekuja kwetu,  kwasababu Maguri ana mkataba na sisi. Tumekubaliana na kilichobaki ni mchezaji mwenyewe kumalizana na Simba kwa maslahi binafsi,” alisema Masau.
Masau aliongeza kuwa kwasasa Maguri yupo kambini Ruvu Shooting na anasubiriwa na Simba ili wakafikie makubaliano binafsi ili asaini mkataba.
Maguri ni miongoni mwa washambuliaji waliokuwepo katika mipango ya kocha mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Awali Ruvu Shooting waliwashutumu Simba kutaka kufanya usajili wa kinyemela na kuwataka wafuate taratibu zote zinazotakiwa kwasababu wao wana haki zote za mchezaji.
Simba walifyata mkia na kuwafuata Shooting ambapo sasa wamefikia makubaliano baina ya pande zote mbili. Hata hivyo ada ya uhamisho ya Maguri haijawekwa wazi.

MARCIO MAXIMO KUANIKA WANANDINGA WA KOMBE LA KAGAME, OKWI, KIIZA, NIYONZIMA MAMBO MAGUMU!

July 31, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

KOCHA mkuu wa Yanga sc, Mbrazil, Marcio Maximo kesho anaweza kuwataja wachezaji atakaowatumia katika michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika mjini Kigali, Rwanda kuanzia Agosti 8 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema Maximo atazungumza na waandishi wa habari kesho baada ya mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar es salaam, hivyo anaweza kudokeza wachezaji atakoenda nao Rwanda.
“Kesho mwalimu ataongea  na waandishi wa habari, kwahiyo yawezekana akatoa dalili ya wachezaji gani anaweza kuwatumia  kombe la Kagame,” alisema Njovu.
“Hasa ukizingatia mwishoni mwa wiki timu nyingi za taifa zitakuwa na mechi, kwahiyo yawezekana wachezaji wengi wakawa hawajawasili, mpaka terehe ya safari yetu, hivyo mwalimu akashindwa kuwatumia.
Njovu alisema kwa vile michuano inaanza Agosti 8, wanajipanga kuondoka nchini Agosti 5, ingawa bado hawana uhakika.
Kuhusu mchezaji wa kigeni atayeachwa kati ya Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza na Haruna Niyonzima baada ya kusajiliwa kwa Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na Gleison Santos Santana ‘Jaja’,  Njovu alisema mpaka sasa mwalimu hajafikia mamuzi ya nani anapunguzwa.
“Mwalimu atathibitisha baada ya kuwaona wachezaji hawa wote wakifanya mazoezi pamoja na kuona ni kombinesheni ipi itamfaa, hapo ndipo ataamua ni mchezaji gani anaachwa, hata kama itasikitisha”

“Bado muda tunao, mwalimu anaweza kumtema mchezaji hata baada ya kombe la Kagame kwa maana ya kwamba atakuwa amepata muda mzuri wa kuwaona wachezaji hao”. Aliongeza Njovu.
MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

July 31, 2014

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika  Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika  Kusini Thabo Mbeki  akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika  Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoto na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati  ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

LHRC YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NUSU MWAKA KUANZIA JANUARY HADI JUNI 2014

July 31, 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo.
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe (kushoto), akisoma taarifa hiyo kwa wanahabari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni 2014 wanawake na wasichana 2878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
 
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
 
“Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633″ alisema Kijo -Bisimba.
 
Kijo-Bisimba alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akizungumzia kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya, maji, umeme, umeme na shule.
 
Alisema takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima.
 
Kuhusu kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono.
 
“Uwekezaji katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa” alisema Kijo-Bisimba.

NAIBU WAZIRI MAKALLA AKAGUA MIRADI YA VISIMA VYA MAJI MKURANGA

July 31, 2014

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
 Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
 Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth
Naibu Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.
 Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga leo.
Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji., ambapo  zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla
 Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.
 Mkandarasi wa mradi wa maji wa Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant  akitoa majibu ya ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa pampu kutoka Afrika Kusini.
Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI MKOANI ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI MKOANI ARUSHA

July 31, 2014


LiberatusSabasJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 
NDUGU WANAHABARI, MTAKUMBUKA KUWA WIKI MOJA ILIYOPITA JESHI LA POLISI LILITOA TAARIFA KWA UMMA JUU YA WATUHUMIWA SITA WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA TAREHE 07/07/2014 KATIKA MGAHAWA WA VAMA ULIOPO MAENEO YA VIWANJA VYA GYMKANA JIJINI ARUSHA.
TAARIFA HIYO ILIZUNGUMZIA PIA TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE ALIKUTWA NA MABOMU SABA YA KURUSHA KWA MKONO, RISASI SITA ZA BUNDUKI AINA YA SHOT-GUN PAMOJA NA UNGA WA BARUTI. TULIELEZA PIA KUWA OPERESHENI YA KUKAMATA WATUHUMIWA WENGINE KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ILIKUWA IKIENDELEA, NA KWAMBA WATUHUMIWA KADHAA WALIKUWA CHINI YA ULINZI WA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO.
KUTOKANA NA OPERESHENI HIYO ENDELEVU, WATUHUMIWA WENGINE KADHAA WAMEKWISHA KAMATWA NA KUHOJIWA, AMBAPO USHAHIDI ULIOKUSANYWA UMEBAINI KUWA  KATI YAO  WATUHUMIWA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAHUSIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA ULIPUAJI MABOMU NA KUMWAGIA WATU TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2012 HADI YALE YALIYOTOKEA KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI. WATUHUMIWA HAO WANATAZAMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 01/08/2014 KUUNGANA NA WENZAO WALIOKWISHA TANGULIA ILI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI. UFAFANUZI WA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA MATUKIO WALIYOHUSIKA NAYO NI KAMA IFUATAVYO:
WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI

July 31, 2014


PG4A7512 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A7500Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2014. Kulia ni Naibu  Balozi wa Ujerumani nchini, Hans Koeppel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UDA yatoa msaada wa shilingi milioni 15 kwa kanisa la Mt. Rita

UDA yatoa msaada wa shilingi milioni 15 kwa kanisa la Mt. Rita

July 31, 2014

St. RITA PIX 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase (kulia) kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita hivi karibuni. Picha na mpiga picha wetu.
St. RITA PIX 3
Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase(kulia) akionyesha hundi ya shilingi milioni 15 zilizotolewa na  Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mchango huo wa kampuni ulitolewa kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri kanisani hapo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija. Picha na mpiga picha wetu
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu   
MAENDELEO ya kijamii na kiuchumi yataweza kupatikana endapo tu kila mtu ataweza kutoa mchango wake kuwasaidia wale wanaohitaji msaada ili kubadilisha maisha yao na kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Simon Bulenganija wakati wa harambee ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, ambapo UDA ilichangia shilingi milioni 15.
“Watanzania wasisubiri mpaka makampuni makubwa yajitokeze na kutusaidia kubadilisha hali zetu za kiuchumi na mfumo wetu wa maisha. Mabadiliko yataweza kufikiwa tu endapo kila mmoja wetu ataweza kuchangia kwa nafasi yake kikamilifu. Makampuni yote makubwa na madogo na watu binafsi wenye uwezo wa kusaidia, wawashike mkono wale wanaohitaji msaada ili tuweze kuendelea pamoja,” alisema.
Bw. Simon Bulenganija alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni jitihada madhubuti zinazolenga katika upatikanaji wa maendeleo miongoni mwa watanzania wote.
Alisema kuwa shilingi milioni 15 zilizotolewa na UDA zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga jeki maendeleo ya kanisa hilo hususani katika ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na mradi wa ujenzi wa kanisa jipya.
“Japokuwa bado kampuni yetu ni kampuni changa ya kitanzania, tumeunda programu yetu ya shughuli za kijamii katika namna ya kwamba shughuli tunazojihusisha nazo, zitasaidia katika kutekeleza ajenda yetu yenye kaulimbiu “ukuaji wa kampuni yetu uwe sambamba na ukuaji wa kiuchumi wa jamii yetu”. Hii pia ni njia pekee ya kurudisha sehemu ya pato letu kwa jamii,” alisema Bw. Bulenganija.
Naye, Bw. Frederick Msumali, Mwenyekiti wa Kigango cha Mtakatifu Rita, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake na ushiriki wa Mkurugenzi wa UDA wakati wa shughuli hiyo ya harambee ambayo iliwezesha kanisa hilo kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60 zitakazotumika katika mradi huo.
“Tungependa kwa kiasi kikubwa kutoa shukrani zetu kwa mchango uliotolewa na UDA.  Msaada huu kwa kiasi kikubwa utasaidia kupiga jeki mradi wetu wa ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na ujenzi wa kanisa jipya utakaofanyika karibu na kanisa hili la sasa.
“Lakini pia, tunaishukuru UDA kama kampuni na Bw. Bulenganija mwenyewe kwa kuwa mgeni wetu rasmi. Mfano huu unahitaji kuigwa na makampuni mengine nchini,” alisema Bw. Msumali.

MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA IMEAMURU KUCHOMWA MOTO DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA BILION 1.8 ZILIZOKAMATWA MPAKANI TUNDUMA MWAKA 2010

July 31, 2014


Dawa hizo a kulevya zateketezwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi




Madawa hayo yakitumbukizwa katika tanuru la moto mkali
HOYCE TEMU AHAMASISHA WATANZANIA KUMPIGIA KURA MISS TANZANIA USA 2014 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MISS AFRIKA USA

HOYCE TEMU AHAMASISHA WATANZANIA KUMPIGIA KURA MISS TANZANIA USA 2014 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MISS AFRIKA USA

July 31, 2014

IMG-20140727-WA0011
Pichani ni Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu nchin Marekani.
Mpigie Kura Miss Tanzania USA, Joy Kalemera anayeshiriki kinyang'ayiro cha kumtafuta Miss Africa USA. Mtangazaji wa Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ambaye pia ni Miss Tanzania 1999 yupo nchini Marekani na amefanya mahojiano na mrembo huyo.
Usikose kuangalia marudio ya mahojiano hayo kwenye kipindi cha "Mimi na Tanzania" Jumamosi ya tarehe 2 August ,2014 Saa saba mchana katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.
IMG-20140727-WA0013
Miss Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.
Joy Kelemera
Namna ya kushiriki kumpigia kura moja kwa moja kwenye profile yake Bonyeza hapa utakuwa umeingia kwenye profile ya Joy Kalemera na bonyeza kitufe chenye alama ya mkono (sehemu iliyozungushiwa duara na wino mweusi) na moja kwa moja utakuwa umempigia kura Mtanzania mwenzetu anayeiwakilisha vyema nchini yetu kwenye kinyan'ganyito hicho.
NOTE: Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kila baada ya dakika mbili kwa kubofya sehemu ile ile.
Let us all wish her all the best! Ushindi wake ni wa Nchi! Piga Kura Sasa!
IMG-20140727-WA0014
Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.
IMG-20140727-WA0015
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi za madaha.