MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAUPONGEZA MGODI WA BUZWAGI

June 03, 2016
  Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi huo.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo.
  Afisa mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba wakati wa ziara hiyo.
  Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Marco Peter katika eneo la uchimbaji.
  Shimo ambalo shughuli za uchimbaji hufanyika kama linavyoonekana.
   Eneo maalumu la kusagia mawe kabla ya kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu.
Madiwani pamoja na wataalamu kutoka halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga picha mbele ya moja ya mitambo inayotumika kusomba mawe mgodini hapo.
  Meneja Uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi Rodney Burgess (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama.
  Wataalamu wa halmashauri ya mji wa Kahama wakiwa katika kituo cha kupozea umeme, kituo ambacho kinaelezwa kuwa kitatumika pia kufunga kifaa maalumu kilichonunuliwa na Mgodi wa Buzwagi ambacho kitawawezesha wananchi wa Kahama na viunga vyake kuweza kupata umeme wa uhakika.
  Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Magesa Magesa akiteta jambo na Katibu wa Mbunge wa Kahama mjini, Abdul Mpei wakati wa ziara ya madiwani ambayo pia ilihusisha wataalamu kutoka halmashauri.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Kahama wakati wa kuhitimisha ziara yao walipotembelea Mgodi huo.
  Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba (Kulia) akiwa na mwenyekiti wa ya wilaya ya Kahama, Abeli Shija wakimsikiliza Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakati alipokuwa anazungumza na madiwani baada ya ziara yao.
  Picha ya pamoja baina ya madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wataalamu wa halmashauri hiyo pamoja na maofisa wa Mgodi wa Buzwagi.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.


Madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.



Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.

 

“Kwa niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za kisasa ” alisema Shija.



Mwenyekiti huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji wa huo.

 

Akijibu ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na kukifunga.

 

“Kifaa kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa uhakika.” Alisema Mwaipopo.

 

Ziara hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo, walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za mazingira na uchimbaji na  kulifanya eneo hilo kuwa salama zaidi.

Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua ukweli.



Mwisho.

NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016 YATAKAYOFANYIKA KESHO KUTWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR E SALAAM

June 03, 2016
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
 Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
 Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
 Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.
Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.

Dotto Mwaibale

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, 
 zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

"Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.

Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

"Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

"Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.

Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.

TIMU YA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA YAIADHIBU TIMU MGODI WA BUZWAGI.

June 03, 2016
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akisalimiana na Mwamuzi wa kirafiki kati ya timu ya soka ya Mgodi wa Buzwagi na timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama,mchezo uliopigwa kama sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Mgodi wa Buzwagi kabla ya kuanza kwa mchezo,nyuma yake ni  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama kabla ya kuanza kwa mchezo,nyuma yake ni  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo.
Vikosi vya timu ya Mgodi wa Buzwagi na  kile cha Hosptali ya wilaya ya Kahama wakisalimia kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Moja ya Hekaheka langoni mwa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakati wa mchezo wa kirafiki uliolenga kujenga mahusiano baina ya mgodi huo na wnanchi wanaozunguka eneo la mgodi huo.
Kombe lililoandaliwa mahususi kwa mshindi wa mchezoo huo wa kirafiki .
Wachezaji wa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakisalimiana na viongozi mara baada ya kumalizika kwa mcheoz wa kirafiki ambapo timu ya Hospitali wilaya ya Kahama iliibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 .
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo akikabidhi kombe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kahama,Anderson Msumba aliyeongozana na nahodha wa timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama.
Wachezaji wa timu ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kombe ilipoichapa timu ya Mgodi wa Buzwagi mabao 2 kwa 1.
Baadhii ya wananchi wakifuatilia zoezi la utoaji kombe kwa washindi hao.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.

RC AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WILAYA YA PANGANI,AZINDUA JENGO LA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MWERA WILAYANI HUMO

June 03, 2016
MKUU WA MKOA WA TANGA,MH.MARTINE SHIGELLA AKIZUNDUA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI (OPERATING THEATRE) KATIKA KITUO CHA AFYA MWERA LEO IJUMAA  JUNE 3 WA KWANZA KULIA NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA ESTERINA KILASI

 KULIA NI MGANGA MFAWIDI WA KITUO CHA AFYA CHA MWERA WILAYANI PANGANI DR.MADARAKA RAPHAEL AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA TANGA,MH.,MARTINE SHIGELLA WAKATI ALIPOTEMBELE UJENZI HUO KUSHOTO NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA PANGANI,
MH.MKUU WA MKOA WA TANGA,MARTINE SHIGELLA AKISOMA JIWE LA MSINGI WA PILI KULIA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA MHANDISI ZENA SAID

MKUU WA MKOA WA TANGA,MH MARTINE SHIGELLA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA
BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MKUU WA MKOA WA TANGA,MH,MARTINE SHIGELLA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NAO LEO

KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA TANGA,MH,MARTINE SHIGELLA AKIVUKA NG'AMBO YA PILI YA PANGANI KWA KUTUMIA KIVUKO LEO WA MBELE YAKE NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI,MH,ESTERIA KILASI


MKUU WA MKOA WA TANGA,MH.MARTINE SHIGELLA KATIKATI AKIINGIA  KWENYE KIVUKO CHA MTO PANGANI KUSHOTO KWAKE NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI,ESTERIA KILASI AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA NA KULIA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,MHANDISI ZENA SAID