WAZIRI MKUU MPYA KASSIM MAJALIWA KASSIM AAPISHWA LEO IKULU YA CHAMWINO DODOMA

WAZIRI MKUU MPYA KASSIM MAJALIWA KASSIM AAPISHWA LEO IKULU YA CHAMWINO DODOMA

November 20, 2015

maj1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimuapisha Kassim Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, hafla ya kiapo ilifanyika leo Ikulu ya Chamwino Mkoa wa Dodoma ]Picha na Ikulu.]
maj2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim  baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, hafla ya kiapo ilifanyika leo Ikulu ya Chamwino Mkoa wa Dodoma ]Picha na Ikulu.]
maj3
Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]
maj4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]
maj5
Makamo wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]
maj6
Viongozi wa Wakuu wa majeshi ya  Ulinzi pamoja na Viongozi mbali mbali waalikwa wakiwa katika hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu Mpya wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim leo katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma,[Picha na Ikulu.]
maj7
Watoto wa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim wakimshuhudia  Baba yao akiapishwa na  leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]
maj8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (watatu kushoto mstari wa nyuma) baada ya kuapishwa rasmi leo katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma,[Picha na Ikulu.]
maj9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (kulia) baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]
maj10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wabunge mbali mbali leo wakati waliposherehekea kwa kuapishwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim   na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ANOGESHA MAHAFALI YA 10 YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM LEO.

November 20, 2015

 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila akielezea mafanikio ya chuo.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Benard Nyoni, aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila na  Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Godfrey Nchimbi aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MASO), Elias Kumanya. 
 Wahitimu wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza waliofanya vizuri katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
 Meza kuu ilivyokuwa ikionekana kwenye mahafali hayo.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto),  na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Evelyne Makalla katika mahafali hayo.

SHEREHE ZA KUAPISHWA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TANO VIWANJA VYA IKULU NDOGO CHAMWINO MJINI DODOMA

November 20, 2015

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimkabidhi nyaraka za Serikali baada ya kumwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpongeza Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015.
Rais Dkt. John Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, baada ya kuapishwa Waziri huyo Mkuu kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Chamwino mjini Dodoma leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mtoto Majaliwa mtoto wa Waziri Mkuu mpya kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya Wabunge wapya wa bunge la 11, walipokutana kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20, 2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Peramiho, Mhe Jenister Mhagama, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akimpongezwa na mkewe baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi, Asham Abdallah Juma, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele , kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge Mchengerwa kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti maalum Kaskazini Unguja, Angela Malembeka, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR

SERIKALI ZA MITAA ZAONGEZA MAPATO KUPITIA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

November 20, 2015

 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bi. Rebecca Kwandu akifurahia jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam wakati akiwaeleza mafanikio ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki katika mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCIS). Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA wa ofisi hiyo Bw. Mtani Yangwe na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
 Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Mtani Yangwe akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam namna mfumo wa wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki unavyorahisisha ulipaji wa kodi mbalimbali kwa kuhusisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na mifumo ya kibenki. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu.
 Afisa Msimamizi wa Fedha Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Dar es Salaam kuhusu mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuondokana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu.
 Mhasibu wa Mfumo wa Mapato Jiji la Arusha Bw. Prosper Mlacha akiwaeleza waandishi wa habari leo Dar es Salaam kuhusu ongezeko la mapato katika jiji la Arusha kutokana na matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (LGRCIS) ambapo kwa mwaka 2014/2015 zimekusanywa bilioni 10.7.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO)

Na Georgina Misama.
SERIKALI imeboresha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki katika mamlaka za serikali za mitaa.

Hayo yamesemwa na msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu leo jijini Dar es salaam.

Bi Rebecca amesema kuwa TAMISEMI imekuwa ikiendelea kwa nyakati tofauti kufanya maboresho mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kuzisaidia mamlaka hizo katika kuongeza mapato ya ndani na kuondokana na uteuzi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.

“Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI iliamua kuanzisha mfuko wa Local Governement Collection Information System (LGRCIS) baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa nyakati tofauti na zilionyesha kuwa hakukuwa na mfumo wowote wa kielektroniki kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Halmashauri” alifafanua Bi. Rebecca.

Mbali na hayo Msemaji huyo alisema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya kuanzishwa kwa mfumo wa LGRCIS ni pamoja na kupata taarifa za walipa kodi wa mamlaka za serikali za mitaa na kuhifadhiwa kwa usahihi katika kanzi data ya mfumo.

“ Kupata takwimu sahihi ya vyanzo vya mapato na kufanya usuluhishi kati ya kilichokusanywa na kilichotarajiwa kukusanywa, kuongeza mapato kwa kasi zaidi kwa kuwa na uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu, kuweka uwazi na uwajibikija katika makusanyo ya mapato,na kuhimarisha ulipaji miamala ya kodi na tozo itakayofanywa na walipakodi” aliongeza Bi Rebecca.

Pia alisema kuwa matarajio ya TAMISEMI ni kuwa mfumo wa LGRCIS utaleta mabadiliko makubwa katika Halmashaurina kuachana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu.

Hata hivyo teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo fikra za watumiaji wa mfumo wa walipakodi kubadili mazoea.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NCHINI KUTEMBEA WAGENI WA KIMATAIFA MAKUMBUSHO YA TAIFA

November 20, 2015

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye ukumbi wa Sanaa, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Michoro ya Mapangoni kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi Agnes Gidna.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Chimbuko la mwanadamu kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Amandus Kweka. Fuvu lilipo kulia kwenye sanduku lililo nakshiwa na dhahabu ni la Zinjanthropus lililo gunduliwa zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyo pita huko Ngorongoro Oldvuvai kwenye miaka ya 1959. 
Balozi Mulamula akiagana na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure baada ya kumaliza kuitembelea Makumbushi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akitembezwa kujionea miundombinu ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.


Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeridhishwa na huduma mbali mbali zinazo tolewa na Makumbusho ya Taifa kwa wageni mbali mbali wanao tembelea Makumbusho hizo ili kujionea na kujifunza mambo mbali mbali yanayo huyu Tanzania.

Akiwa kwenye ziara ya kimafunzo katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mukamula amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuitumia Makumbusho za Taifa ili kutoa elimu kwa wageni mbali mbali wanaotembelea Tanzania.

Ameongeza kuwa Wizara yake hupokea wageni wengi wa kimataifa wanaokuja kwa shughui za kiserikali hivyo ofisi yake itafanya utaratibu wa kuhakikisha wageni hao wanatembelea makumbusho kwa maana ndio sehemu pekee wanapo weza kuifahamu Tanzania kwa muda mfupi bila kuizunguka nchi yote.

“Nimekuja mwenye kujionea na kujifunza huduma mnazo toa hapa, ili nijiridhishe kwanza kabla ofisi yangu haijaanza kuwaleta wageni hapa, kiukweli nimeridhishwa sana na huduma yenu na licha ya kujifunza nimeona vipo vivutio vingi vinaweza kuwavutia wageni wa kiserikali na kujifunza kupitia vitu hivi, hongereni sana” Alisema Balozi Mulamula.

Akimshukuru Balozi Mulamula kwa kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure alisema kuwa amependezwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuona umuhimu wa kuitumia Makumbusho kama Mwalimu Mwelekelezi wa Mambo yanayo thaminiwa na watanzania

“Viongozi wetu wa kubwa wakienda kikazi nchi za wenzetu, wakifika huko hutembezwa Makumbusho, ili kuwafanya wasiondoke bila kuzifahamu hizo nchi kihistoria na hata kimaendeleo ya kisayansi na teknolojia, vivyo hivyo wanapokuja hapa nchini wanapaswa kutembezwa Makumbusho ili wapate sura sahihi ya nchi yetu” Aliongeza Bw Bufure.

Mkurugenzi huyo wa Makumbusho ametoa  wito kwa Wizara zote za Serikali, Taasisi za watu binafsi na Watanzania kwa ujumla wenye kutembelewa na wageni kutoka nje ya Tanzania kuwa na Utamaduni wa kuwatembeza wageni wao Makumbusho ili kujifunza mambo ya Tanzania.

BOMOA BOMOA YA MANISPAA YAENDELEA MBEZI BICHI (BLOCK K) JIJINI DAR

November 20, 2015

Manispaa ya wilaya ya Kinondoni kushirikiana na Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakiwa wameweka tangazo lao katika ukuta wa uzio wakimaanisha eneo hilo lisitumike kwa maana ya maeneo ya wazi.
mmmm










  Nyumba nyingine eneo hilo nayo ikisubili kubomolewa na manispaa ya Kinondoni. 
 Ubomoaji ukiendelea.   
Familia ya nyumba inayotakiwa kubomolewa na manispaa wakitoa dhamani za ndani ili kupisha ubomoaji.







 Ubomoaji ukiendelea katika maeneo ya Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam.
 Wazee wa kazi wakiwa katia geti la nyumba inayotakiwa kubomolewa  maeneo ya mtaa wa  Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
 Ubomoaji wa uzio wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kubisha hodi na kutokufunguliwa.
Uzio umebomolewa na watu wakiwa ndani kwaajili ya ubomoaji wa nyumba hiyo ambayo imejengwa maeneo ambayo ni ya wazi.
Magari yakiwa ndani ya nyumba inatotakiwa kubomolewa.
 Magari ya kitolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba maeneo ya  Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
Wenyeji wa nyumba ambayo imeanza kubomolewa uzio wakitoa vitu ndani ili kupisha ubomoaji wa nyumba hiyo.
 
 Wakazi wa nyumba nyeupe inayobomolewa wakitoka nje ya nyumba baada ya kuanza kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.


 Wananchi wakihamisha vitu kupisha bomoabomoa.
 
Wananchi waangalia jinsi manispaa inavyobomoa nyumba Mbezi bichi jijini Dar es Salaam leo
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.