BENKI YA NBC YATOA MAFUNZO YA FEDHA KWA WACHEZAJI WA STAND UNITED

February 01, 2024

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC tawi la Shinyanga imetoa Elimu ya Fedha kwa Wachezaji wa Timu ya Stand United ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Alhamisi Februari 1,2024 katika Benki ya NBC tawi la Shinyanga yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha, kuimarisha ushirikiano na kufahamiana.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja amesema Benki ya NBC ambayo ni Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) na NBC Championship imewashauri wachezaji wa Stand United kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Benki hiyo ikiwemo Bima za afya na vyombo vya moto, mikopo pamoja na akaunti mbalimbali ikiwemo Akaunti ya Mshahara, Akaunti ya Kua Nasi, Akaunti ya Malengo, Akaunti ya NBC Direct na huduma za NBC Wakala.

Amewashauri wachezaji hao kujiwekea utamaduni kwa kujiwekea akiba na uwekezaji pamoja na kuwa na bima katika Benki ya NBC wanaposajiliwa na timu mbalimbali.

“Tumekutana hapa leo ili kutoa mafunzo ya huduma za kifedha kwa wachezaji wa Stand United ili kuimarisha mahusiano na timu hii, tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha tunatatua changamoto zinazoikabili timu hii.

Tunazo huduma nyingi za kifedha. Karibuni Benki ya NBC pia mfurahie njia mbadala za kupata huduma za kibenki ‘Benki Kidijitali na NBC’ bila ulazima wa kufika kwenye tawi kwa kupiga *150*55# au kupitia App ya NBC Kiganjani”,amesema Chagonja.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja.

Katika hatua nyingine amesema Benki ya NBC ina jumla ya matawi 57 nchi nzima, ATM 197 na zaidi ya mawakala 11,000 ikihudumia makundi matatu ya wateja wakiwemo watu binafsi, wateja wa kati na wateja wakubwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Stand United ya Mkoa wa Shinyanga inayoshiriki Ligi ya Championship, Stivian Antidius (Wenger) ameishukuru Benki ya NBC kwa kuwapatia elimu ya fedha wachezaji na viongozi wa timu hiyo huku akiiomba Benki hiyo kuisaidia kwa chochote timu hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa katika kipindi hiki ambacho wana mechi 13 mbele yao.

“Tunawashukuru sana NBC na wadhamini wetu Jambo kwa ushirikiano wanaotupatia, tunaomba wadau wengine katika mkoa wa Shinyanga na nje ya Shinyanga mjitokeze kutusaidia kwani tunakabiliwa na changamoto mbalimbali”,amesema Antidius

Nao washiriki wa mafunzo hayo, wameishukuru Benki ya NBC kwa kuwajali na kuwapata mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kuweka akiba na kuwekeza kupitia benki hiyo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja akizungumza wakati wa mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na Viongozi wa Stand United leo Alhamisi Februari 1,2024 katika Benki ya NBC Tawi la Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja akizungumza wakati wa mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na Viongozi wa Stand United

Mwenyekiti wa Stand United ya Mkoa wa Shinyanga inayoshiriki Ligi ya Championship, Stivian Antidius (Wenger) akiishukuru Benki ya NBC kwa kuwapatia elimu ya fedha wachezaji na viongozi wa timu hiyo

Mwenyekiti wa Stand United ya Mkoa wa Shinyanga inayoshiriki Ligi ya Championship, Stivian Antidius (Wenger) akiishukuru Benki ya NBC kwa kuwapatia elimu ya fedha wachezaji na viongozi wa timu hiyo
Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Regan Daud akielezea huduma za Kibenki zinazolewa katika Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Afisa Biashara Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Allen Myalla akielezea kuhusu Masuala ya Bima, Mikopo na Akaunti mbalimbali zinazopatikana katika Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Afisa Biashara Wateja wa Kati na Wakubwa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Carlos Kapinga akielezea kuhusu masuala ya Fedha wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United
Afisa Biashara Wateja wa Kati na Wakubwa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Carlos Kapinga akielezea kuhusu masuala ya Fedha na Mikopo inayotolewa na Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Mmoja wa wachezaji wa Stand United akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo
Mmoja wa wachezaji wa Stand United akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo
Mmoja wa wachezaji wa Stand United akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo
Wachezaji wa Stand United wakiwa katika benki ya NBC Tawi la Shinyanga

Mkuu wa Kitengo cha Michezo Jambo Fm, Chris Kakwaya akifuatilia matukio wakati wa mafunzo hayo 
Viongozi wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Viongozi na wachezaji wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Viongozi na wachezaji wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Viongozi na wachezaji wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Viongozi na wachezaji wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Picha ya kumbukumbu viongozi wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga na Viongozi , wachezaji wa Timu ya Stand United 

Picha ya kumbukumbu viongozi wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga na Viongozi , wachezaji wa Timu ya Stand United.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
MIL. 180 ZAKARABATI SHULE CHAKAVU KIBITI’ NDEJEMBI

MIL. 180 ZAKARABATI SHULE CHAKAVU KIBITI’ NDEJEMBI

February 01, 2024

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imepeleka Sh Milioni 180 kwa ajili ya ukarabati wa shule chakavu za msingi katika Jimbo la Kibiti mkoani Pwani ambapo jumla ya shule nne zitakarabatiwa ambazo ni Pongwe (Madarasa Matatu), Mchinga (Madarasa Mawili), Saninga (Madarasa Mawili) na Misimbo (Madarasa Mawili).

Mhe Ndejembi ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Mhe Twaha Mpembenwe aliyehoji ni lini Serikali itaanza ukarabati wa Shule Chakavu za Msingi Jimbo la Kibiti.

NORWAY KUKIJENGEA UWEZO KITUO CHA UBIA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI

NORWAY KUKIJENGEA UWEZO KITUO CHA UBIA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI

February 01, 2024

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akisalimiana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, walipokutana ofisini kwakwe jijini Dodoma kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, wakati akimsindikiza baada ya kukutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake jijini Dodoma, kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza katika kikao chake na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (watatu kulia) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes (wapili kushoto), walipokutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake jijini Dodoma, kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, akifafanua jambo katika kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes (wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania pamoja na ujumbe wa Tanzania (Wizara ya Fedha), baada ya kumalizika kwa Kikao chao, jijini Dodoma, ambapo katika kikao hicho walijadili kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na. Peter Haule, WF, Dodoma

Norway imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika kukijengea uwezo Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kuiwezesha sekta binafsi kushiriki kikamilifu kujenga Uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma, na Mhe. Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes, kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuona kuona sekta binafsi inashiriki katika kujenga Uchumi wa nchi, kutengeneza ajira kwa wananchi wakiwemo vijana na wanawake na kutengeneza vyanzo vipya vya kodi.

Aidha, Dkt. Nchemba alieleza kuwa, Norway imepiga hatua kubwa katika eneo la kodi na kuishauri nchi hiyo iangalie namna ya kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana ujuzi katika eneo hilo na masuala mengine ya kifedha.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa eneo hilo ni muhimu kwa Tanzania, ambapo ameiomba Norway ambayo imepiga hatua katika eneo hilo, kushirikiana na Tanzania ili iweze kupata vigezo muhimu vya kupatiwa fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya mabadiliko hayo.

Dkt. Nchemba ameishukuru Norway kwa mchango wake katika maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati, elimu, kilimo na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes, alisema kuwa Ushirikiano wa nchi hizo mbili umetimiza zaidi ya miaka 60, na katika kipindi hicho nchi yake imeshiriki katika maendeleo kwenye Sekta za miundombinu, nishati, kilimo, na pia imeshiriki katika uanzishwaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na imechangia kujenga mitambo ya umeme wa maji.

Alisema kuwa katika eneo la Kilimo, nchi yake inaadhimisha miaka 50 ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa kutoa ujuzi na pia imekuwa na mchango wa ujuzi katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha.

Mhe. Tone Tinnes, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kutoa kutoa ushirikiano katika kufanikisha mahitaji mapya ili kuharakisha maendeleo zaidi.

Alilitaja eneo mahususi ambalo nchi yake itashirikiana na Tanzania ni kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi jambo ambalo limekuwa na changamoto si tu kwa Tanzania nali pia Dunia nzima kwa ujumla, na kusisitiza kuwa kilimo kinatakiwa kutekelezwa kwa kuangalia athari ya mabadiliko ya Tabia nchi.