TIB CORPORATE BANK KTK JUKWAA LA BIASHARA TANGA

August 18, 2017
 Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe kulia akilakiwa na wajumbe wa Jukwaa hilo wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TSN Dokta Jimmy Yonazi wanne kushoto ni MD wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege na wakwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.



TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara ,Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta maendeleo.
 
TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali KTK Mkoa wa tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities).
 
TIB Corporate Bank  inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati,dhamana za kibenki( bank guarantee),ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni,uwekezaji katika hati fungani,( treasury bills & Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka
  
Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.

Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.

UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA RADIO ZA KIJAMII VYA MAMILIONI

August 18, 2017
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini,Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.
Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

VIDEO: TAZAMA MAANDALIZI YA IKUNGI ELIMU CUP 2017 SINGIDA.

August 18, 2017
Fundi akichomelea vyuma kwa ajili ya kufunga nyavu ikiwa ni marekebisho ya mwisho katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi, wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu ya Ikundi Elimu Cup 2017 wilayani Ikungi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.

Na George Binagi, BMG
Mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali kutoka Kata 28 wilayani Ikungi yakilenga kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa elimu kushiriki katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo uhaba wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo vya shule.

Hii ni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu kuteuliwa kuwa mlezi wa mfuko wa elimu wilayani humo na hivyo kuamua kuanzisha michuano hiyo ili kuleta chachu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuchangia masuala ya kielimu.

Jumamosi timu ya soka ya Ikungi United na inakuwa ikimenyana na timu ya Puma ambapo mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Katika mchezo huo wa awali timu ya madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Elias Tarimo.

Ufunguzi wa mashindano hayo utatanguliwa na shughuli ya ufyatuaji matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imetakiwa kufyatua matofali yasiyopungua 10,000 ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu na vyoo vya shule.
Mwl.Seth Raban Mwakalasya ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya ligi ya ligi ya soka ya Ikungi Elimu Cup 2017 yanayotarajiwa kuanza katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jumamosi Agosti 19 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi.
Timu ya soka ya Ikungi United Sports Club ikifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club wakifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club watamenyana na timu ya Puma katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Ikungi Elimu Cup 2017
Timu ya Ikungi United Sports Club ikiwa kwenye mazoezi hii leo jioni
Nahodha wa timu ya Ikungi United Sports Club, Lazaro John Francis (pichani) amesema maandalizi yao yako vizuri na kwamba michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 itakuwa na ushindani mkubwa hivyo wapenzi wa soka wategemee soka la kuvutia kwenye michuano hiyo
Kocha wa timu ya soka ya Ikungi United Sports Club, Danny Ayoub amesema kikosi chake kimejipanga vyema na kwamba michuano itaweza kuiwezesha timu yake kusonga mbele kimichezo nchini ikifuata nyayo za kaka zao Singida United.
Kikosi cha Ikungi United Sports Club kikiwa kwenye tathmini fupi baada ya mazoezi ya hii leo jioni
Kocha wa kikosi cha Ikungi United Sports Club akitoa tathmini fupi baada ya mazoezi ya timu hiyo jioni ya leo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo michuano hiyo itafunguliwa jumamosi Agosti 19,2017 huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.
  Dk. Kigwangalla aanza ziara ya kikazi Arusha

Dk. Kigwangalla aanza ziara ya kikazi Arusha

August 18, 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB),mapema leo Agosti 17,2017 amefanya ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo Mkoani hapa. Dk.Kigwangalla ametembelea Kituo cha Afya Kaloleni, kituo cha Afya Levolosi, kituo cha Afya Ngarenaro, Kituo cha Afya Daraja Mbili, Kituo cha afya Mkonoo na Kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya . Akizungumza wakati wa kutoa maagizo kwenye vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V.Timothi Wonanji na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe na viongozi wengine wa mkoa akiwemo kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi kuhakikisha wanatatua changamoto za Afya ikiwemo ukosefu wa vyumba vya upasuaji na ukosefu wa vitendanishi katika mashine za vipimo vya maabara. "Mnavyo vituo vya Afya 7. Mnahitaji kuwekeza zaidi ili mnunue vifaa vya Maabara na kufanyia ukarabati hivyo vilivyopo. Kuna vifaa vya maabara vya kisasa ambavyo ni ‘portable’ na havina gharana kubwa. Tunataka mtenge fedha za kutosha ili kuimarisha sekta ya Afya" aliagiza Dk Kigwangalla. Aidha akitoa agizo wakati kukagua kituo cha Afya Daraja Mbili ameagiza mara moja jengo la Chumba cha Upasuaji cha kituo hicho kianze kazi ndani ya wiki mbili na upasuaji ufanyike ikiwemo wataalamu kuwapo hapo muda wote. "Naagiza ndani ya wiki mbili. Huduma za upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho kila kitu , vifaa vingi na vya kutosha na jengo zuri la kisasa" alisema, Dk Kigwangalla. Katika hatua nyingine Dk.Kigwangalla ameagiza kituo cha Afya Kaloleni kuhakikisha wanajenga wodi ya akina mama na kukamilisha maboresho ya Chumba cha upasuaji. "Hiki kituo hakina hadhi ya kuwa Kituo cha Afya. Ni sawa na Zahanati tu maana kama hakuna huduma muhimu za upasuaji na wodi ya wazazi, nahitaji kuona munakamilisha mara moja" alieleza Dk. kigwangalla. Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameweza kukagua sehemu za Maabara, wodi za wazazi na vyumba vya upasuaji pamoja na maeneo mbalimbali ya hospitali kuona utendaji wa kazi muhimu na namna ya utoaji wa huduma zinazotolea katika Jiji la Arusha. Mbali na kukagua vituo hivyo vya Arusha, Dk. Kigwangalla pia ameweza kutembelea baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya Afya kwenye maeneo hayo ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya Kaloleni namna watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani ya kituo hicho cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema leo Agosti 17,2017 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.

Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya Levolosi juu ya uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo

Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro

Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe.

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akiwa katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi

Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.

Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni.

Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari

Dk. Kigwangalla akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Rebecca Mongi wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya

DR.DALLO OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI

August 18, 2017



Na Woinde Shizza,Arusha



Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa  na chama hicho.



Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na  tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyeji



Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa  katika uchaguzi  kwa mujibu wa kanuni ya  muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010



Alisema kuwa yeye binafsi ajawaoana watu hao wanaodaiwa ni waganga wa kienyeji na usahili  ulienda vizuri na k atika kipindi hichi  uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .



“nasema kwakweli ili swala na mgombea  wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona ila ukweli napenda kuchukua nafasi hiii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote Yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuinta kikao kama jambo ni gumu sana pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dr,Dallo

Alizitaja baadhi yakanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na  nyingi 



Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobaki



Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi

SABABU ZA KUANZA 'KU-BLOGU' KUHUSU SEHEMU UNAZOTEMBELEA

August 18, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Miongoni mwa tasnia zinazokua kwa kasi sasa hivi nchini Tanzania ni uandishi wa mtandaoni au blogu. Kuenea na ukuaji wa matumizi ya mtandao wa intaneti kumepelekea watu waliokuwa wanatamani kuingia kwenye tasnia ya uandishi kufungua blogu zao mitandaoni.
Blogu zinatoa fursa kubwa kwa watu mbalimbali wanaopenda uandishi kuandika masuala mbalimbali juu ya mada tofauti na kuwashirikisha wasomaji wao kwa njia ya mtandao. Jumia Travel ingependa kukufungua macho kwamba miongoni mwa masuala ambayo mpaka sasa hayajaangaziwa kwa kiasi kikubwa ni pamoja na vivutio vilivyopo sehemu tofauti za nchi ya Tanzania. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache za kuanza kuandika na kuwashirikisha wasomaji wako juu ya maeneo tofauti unayoyatembelea.

WAZIRI JENISTA, NAIBU WAZIRI DKT. KALEMANI WAZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME VIJINI REA III KWA KUGAWA VIFAA VYA UMEME TAYARI (READY BOARD MKOANI RUVUMA

August 18, 2017


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),  kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi, Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali nchini


NA MWANDISHI WETU SONGEA.
KAMPENI ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti 16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amezindua  mradi huo kwenye kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.
Katika hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).
“Kifaa hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye ziara hiyo.
Hali kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.
Alisema, tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.
“Jambo la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)” alifafanua Bi. Muhaji.